Monday, April 1, 2013

RIWAYA: MREMBO ALIYEPOTEA------------1

 

MTUNZI: Andrew Carlos

MAWASILIANO: 0713133633

SEHEMU YA KWANZA

...
Umati wa waumini wa dini ya kikristo ulikuwa unaendelea kumiminika katika kanisa kubwa la Mtakatifu John. Shangwe kubwa ziliendelea kusambaa ndani ya kanisa hilo ikiwa ni msisitizo kwamba waumini wake wameguswa sana na mahubiri yaliokuwa yakiendelea ndani ya kanisa ambayo yalikuwa yakitolewa na mchungaji Joseph. Mmoja wa waumini katika kanisa hilo alikuwa ni Majaliwa na mkewe Juliana. Japokuwa alikuwa ni fundi mabomba na kila siku alitakiwa awe anafanya kazi hata kama ni jumapili, lakini kwake Majaliwa haikuwa hivyo kutokana na kuheshimu sana siku ya jumapili. Aliitenga kama siku muhimu maishani mwake na ya kutubu dhambi zake zote. Upole na ucheshi aliokuwa nao Majaliwa ulizidi kumuongezea marafiki kila kukicha ikiwa ni kanisani mpaka mtaani alipokuwa akiishi.
Tatizo kubwa lililokuwa likimuandama Majaliwa ni juu ya mtoto. Pamoja na umri wake kufikia miaka thelathini na tano lakini bado alikuwa hajabahatika kupata hata mtoto mmoja. Alihangaika yeye na mke wake kwenda karibu kila hospitali kujaribu kuangalia pengine mmoja wapo anamatatizo lakini karibu kila hospitali waliyoenda jibu lilikuwa ni hilo hilo kuwa wana uwezo wa kupata mtoto ila kinachotakiwa ni kuvuta subira na kuomba sana kwa mwenyezi Mungu. Ndani ya miezi takribani mitatu tayari mke wa Majaliwa alikuwa ameshanasa ujauzito. Furaha ya ajabu ikamtawala Majaliwa na mkewe Juliana na kuamini kile kilio alichokuwa akikililia kila siku sasa kimepata ufumbuzi.
Hakutaka hata kumwacha mke wake abaki nyumbani peke yake mpaka atakapojifungua. Kutokana na kuwa na kipato kidogo alichokuwa akikiingiza kupitia kazi yake ya ufundi mabomba hakikutosha hata kutafuta msichana wa kazi japokuwa pia ilikuwa ni tatizo kubwa kwake kwanza sehemu aliyokuwa amepanga ni ya chumba kimoja. Majaliwa akaendelea kuwa bega kwa bega mkewe mpaka alipofikisha miezi tisa ambayo mke wa Majaliwa alizidiwa na uchungu wa mara kwa mara.
“Mume wangu? sijisikii vizuri nakuomba nisidie kunyanyuka hapa!”
Aliongea mke wa Majaliwa huku uchungu ukizidi kumzidia hali iliyomfanya Majaliwa atafute usafiri na kumkimbiza hospitali haraka. Woga uliochanganyana na kutetemeka mara kwa mara ukamfanya ajihisi kama mkojo unamtiririka kupitia suruali aliyokuwa amevaa. Muda wote alishikilia mikono yake kwa nguvu nje ya hospitali huku kila muda akionesha ishara kama ngumi juu kwa kusali na kuomba mkewe ajifungue salama hapo hospitali. Jasho jembamba likaendelea kumteremka kupitia kwenye kola ya shati lake huku dhahiri likionesha vifungo kupishana sababu ya haraka aliokuwa nayo ya kumuwaisha mkewe hospitali. Kila mlango wa wodini ulipofunguliwa Majaliwa alikuwa akitetemeka nakuona kama analetewa majibu juu ya maendeleo ya mkewe huko ndani. Hatimaye ndani ya muda mchache akatoka daktari aliyevaliwa mavazi makubwa meupe huku mikononi mwake akilishikilia karatasi na kalamu.
“Wewe ndio Majaliwa?”
“Ndio mimi dokta, dokta?”
Majaliwa aliitikia kwa kutetemeka huku akiendelea kumtolea macho yule dokta.
“Twende ofisini kwangu?”
Majaliwa akaongozana na yule daktari mpaka ofisini kwake kisha akamkalisha kwenye kiti na maongezi yakaendelea.
“Kwanza kabisa nikupe hongera mzee mwenzangu!!”
Majaliwa hakutaka kabisa kuamini yale maneno kutoka kwa yule daktari, kwanza akahisi ni ndoto aliyokuwa akiiota kila siku halafu akizinduka inayeyuka. Akajaribu kufumba macho nakufumbua ili kuamini kwamba anachokiona na kukisikia ni kweli kabisa na hayo maneno yanayotoka kwa daktari aliyekuwa amemuita mpaka ofisini kwake au la!
“Kwahiyo dokta?, embu niambie mke wangu kajifungua mtoto wa kike au wakiume maana natamani kumuona wee acha tu!!”
“Anhaa!, umefanikiwa kupata mtoto wa kike bwana Majaliwa”
“Oohh!! Ashukuliwe Mungu, apewe sifa baba yetu aliye Mbinguni, nasema asante sana Mungu umejibu maombi Baba, ulisema kwako hakuna lishindwalo chini ya dunia Baba”
Majaliwa akajisahau kabisa kama tayari yupo katika himaya ya hospitali. Akadhania yupo kanisani tena alijihisi yupo kwenye kipindi cha maombi. Akaanza kushukuru taratibu lakini hali ilivyozidi ukichanganya na furaha aliokuwa nayo Majaliwa akajikuta akiitoa sauti kubwa na kali mule ofisini mwa daktari hali iliyomfanya daktari amuondoe ampeleke mpaka alipo mke wake ajionee mtoto wake. Majaliwa alipofika na hapo wodini hali ikamzidia akaanza kutangaza neno la Mungu huku kelele akiziachia karibu wodi nzima kwa kulitaja neno la Mungu na kushukuru kupata mtoto wa kike. Majaliwa akabaki kuwa kama kituko pia kama kivutio katika ile wodi ya wakinamama.

*****

Ndani ya miaka kumi na nne hali ya Majaliwa ilikuwa imeshabadilika. Hakuwa Majaliwa tena kwani alitambulika kama baba Alice kutokana na yule mtoto aliyempata. Ule ulokole aliokuwa nao kipindi cha nyuma kabla ya kumpata Alice sasa ukawa haupo tena. Majaliwa alibadilika sana na haikujilkana haswa kipi kilichofanya akabadilika. Mama Alice na Alice walikuwa na kazi ya ziada juu ya kumfanya baba Alice abadilike lakini hali ikawa pale pale. Ulevi wa pombe za kienyeji ulikuwa umeshamuathiri halmashauri ya kichwa chake. Kurudi kwake usiku wa manane na kuanza kutukana ovyo mitaani na hata kuamsha majirani waliolala kwa kuwaporomoshea matusi mengine ya nguoni kilikuwa ni kitendo kilichomsononesha sana mama Alice na Alice kwa ujumla. Ile kazi ya ufundi mabomba ambayo ilimsaidia Alice japo kumaliza darasa la saba, baba Alice akawa ameachana nayo huku akiamini kazi ya kuuza na kukaanga samaki aliokuwa akiifanya mama Alice itawasaidia. Akajifariji kwa kuomba kwa ndugu jamaa na marafiki na akizipata ni kukimbilia kilabuni kunywa pombe za kienyeji.
Siku moja usiku wa sana baba Alice alikuwa ametoka kunywa pombe zake na alipofika kwake alichukuwa kipande cha kuni ambayo mama Alice uvitunza ndani kwa ajili ya kukaangia samaki zake. Bila ya kuwa na sababu zozote za msingi baba Alice aliingia mpaka chumbani kwake huku mkononi mwake akiwa na ukuni mkubwa nakuanza kumpiga nao mama Alice kwa nguvu zote. Mama Alice akajitahidi japo kujikomboa lakini haikuwezekana huku baba Alice akimnyamazisha kwa kumnyoshea ishara ya kumnyamzisha kwa vidole mdomoni. Maumivu makali aliokuwa anaendelea kuyapata mama Alice yakamfanya atafute upenyo na kukimbia huku akielekea nje kusikojulikana.
Ndani ya wiki hali ikazidi kuwa mbaya kwa Alice kutokana na kutoelewa mama yake alipoelekea toka mara ya mwisho apate kipigo kutoka kwa baba yake. Alice akaendelea kukaanga na kuuza samaki huku akiamini mama yake atarudi tu. Hali ya baba yake nayo ikaendelea hivyo hivyo ya kilevi japokuwa siku nyngine alikuwa akirudi kwake akiwa amepooza na wala hajanywa. Alice akajitahidi sana kumpenda baba yake kwa kuwa aliamini dhahiri yeye ni mtoto pekee kutoka kwa baba na mama yake hivyo inabidi awapende kwa hali yeyote.
Siku moja usiku kwenye muda wa saa tatu usiku baba Alice aliwahi kurudi kwenye mizunguko yake na hali yake ilikuwa si kilevi kama ilivyozoeleka. Alimkuta alice kishamtayarishia chakula cha jioni hivyo alipofika akatengewa akala na kisha akaelekea kulala. Ilimchukuwa masaa matatu tu baba Alice alikurupuka usiku sana akaenda kuwasha mshumaa kisha akasogea hadi maeneo alipokuwepo Alice amelala. Akamwangalia mtoto wake Alice kwa masikitiko kisha akavua zipu ya suruali yake na baada ya hapo akavua nguo zake zote na kubaki mtupu. Usingizi mkali uliokuwa umempitia Alice ukichanganya na pilika pilika alizokuwa nazo siku nzima za kuandaa samaki na kuwakaanga pia kutengeneza chakula zilimfanya alale fofofo. Baba Alice alivyomaliza kuvua nguo zake zote akamsogelea Alice kwa ukaribu. Akaanza kumvua gauni lake nakubakiwa uchi kama alivyozaliwa. Baada ya hapo baba Alice akaanza kufanya tendo la kujamiiana na mtoto wake tena huku akitumia nguvu zake zote.
“Mamaaa nakufaaa?”
Alice akashtuka kutoka usingizini huku jasho likimtoka akimtazama baba yake ambaye bado alikuwa juu ya kifua chake huku akiendelea kumbaka. Machozi yakaanza kumtiririka Alice. Maumivu makali aliokuwa anaendelea kuyapata kupitia sehemu zake za siri yalizidi kumuumiza akili yake. Baba alice akamtishia kwamba endapo atapiga kelele atamchoma na moto kupitia ule mshumaa. Alice alikuwa bikra ambayo alitamani sana siku moja mume atakayekuja kumuoa ndio aitoe lakini tayari baba yake akawa ameshaitoa na kumsababishia maumivu makali.
“Nakupenda mwananagu Alice!!”
Aliongea baba Alice huku akimwambia Alice kwa kumbusu kifuani mwake.
Alice akachukuwa mikono yake na kumsogeza baba yake kutoka juu ya kifua chake lakini haikuwezekana. Kwanza baba Alice alizidi kuwa mkali kama mbogo huku akiendelea kufanya mapenzi na Alice hali iliyomfanya kuendelea kupata maumivu. Machozi ya uchungu yakaendelea kumwagika Alice pale kitandani, hasira kali ni kati ya vitu ambavyo baba Alice alivigundua lakini kutokana na hamu aliokuwa nayo ilimbidi kufanya hivyo. Baba Alice alipomaliza kufanya mapenzi na Alice akairudishia suruali yake vizuri kisha akazima ule mshumaa nakuelekea kwenye kitanda chake tayari kwa kulala. Usiku wote ukawa ni mkubwa kwa Alice kwa sababu ya mambo makubwa mawili. Kwanza kabisa kitendo cha kuingiliwa na baba yake mzazi na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri. Na pili ni kumtoa bikra yake aliyokuwa ameitunza kwa muda mrefu.

******


***NINI kilimsibu MAJALIWA hadi kubadilika kiasi hicho??
MKE WAKE amekimbilia wapi…..na je ALICE aliyebakwa ataishi vipi na baba yake???

ITAENDELEA KESH

No comments:

Post a Comment

Recent Posts