Monday, April 1, 2013

RIWAYA: WASALIMIE KUZIMU-------1


MTUNZI: Hussein Wamaywa

SIMU: 0755 697335

SEHEMU YA KWANZA

...
Utangulizi

Miaka kadhaa iliyopita, mtu mmoja mtanashati mwenye kiu ya uwendawazimu wa ngono Aitwae Promota Halfan Kigundo alianzisha mashindano ya urembo aliyoyaita Miss Temeke Akademia.

Lengo lake lilikuwa kufanya mapenzi na wasichana wote wataokaojitokeza kupigania taji hilo. Kweli, anafaulu kufanya nao mapenzi na katika hilo, Husna mmoja wa washiriki anapata mimba na kujitoa mashindanoni mapema.

Siku chache kabla ya fainali, rafikie Danny Masimango anamshauri amwingize mashindanoni Nasra Alwatan Dafu (Binti wa kiarabu anayechungwa na baba yake kama malighafi) ili aweze kufanya nae mapenzi kwa kuwa alikuwa mzuri sana.

Halfan anaupokea ushauri huo na kumuingiza mashindanoni, na kwa mbinu za hali ya juu anafaulu kumtongoza, kufanya nae mapenzi na kumjaza mimba pasipo kujua kwamba Nasra anaye mchumba aitwae Saadan huko Oman. Mchumba aliyetafutiwa na baba yake Alwatan Dafu ingawa si chaguo hasa la Nasra.

Siku ya fainali za mashindano ya Miss Temeke Academia, Nasra anajifungua ukumbini watoto mapacha baada ya kunyakua taji. Kitendo kinachowakasirisha wasichana waliotoa penzi kwa Halfan, wanaamua kutoa siri, Halfan anapokea kipigo kutoka kwa mashabiki na wananchi wenye hasira.

Alwatan Dafu, baba yake na Nasra anamshtaki Halfan kwa kuanzisha mashindano ya urembo ya udanganyifu yenye lengo la kuwaharibia maisha wasichana akiwemo Mwanae Nasra. Kwa kutumia nguvu ya fedha, Alwatan Dafu anafaulu kufanya hatia zimuelemee Halfan, hatimaye anafungwa miaka thelathini na kazi ngumu!

Ambacho hakukijua Mzee Alwatan Dafu ni kuwa mwanae Nasra alikuwa amekufa ameoza kwa Promota Halfan. Alimpenda mno, alimpenda kupita kiasi…! Je Nasra alichukua hatua gani baadae?

Tafadhali endelea na simulizi hii ya kusisimua ya raha na karaha za mapenzi inayoletwa kwako na Hussein Wamaywa, Mtunzi wa zama zetu!


GEREZANI UKONGA, DSM

Ni saa kumi jioni. Hali ya gereza alilofungwa Halfan inaanza kupata uhai, baada ya upweke wa kutisha uliolikumba toka nyakati za asubuhi.
Halfani mwenyewe anakuwa mmoja kati ya watu wanaolipa uhai gereza hili. Ndio kwanza amerejea yeye na wenzake wakitoka kufanya kazi ngumu walizopewa, kutimiza sehemu ya adhabu yao ya kifungo.
Pamoja na kuchoka, haoni vibaya kusafisha eneo lake la kulalia. Wenzake kadhaa anaolala nao katika chumba hicho kidogo, bado hawajafika.
Ukweli hali ni mbaya sana na ukimuona Halfani wa sasa utamsikitikia. Hakuwa Halfani yule yule Promota anayetisha kwa ukwasi na kipenzi cha warembo, aliondokea kuwa Halfani mwingine mwenye uchovu uliozidia ukomo.
Rangi yake maji ya kunde ilishatoweka kitambo na nafasi yake kuchukuliwa na weusi wa ukungu usiopendeza hata kidogo. Ukungu huo ulitiwa nakshi na vipele vikubwavikubwa vilivyoizingira sehemu kubwa ya mwili na uso wake.
Hali yake kiafya ilisikitisha. Kunawiri kulishaondoka dhahiri, akabakia amekondeana vifupa mbalimbali vilijitokeza hapa na pale katika mwili wake. Nywele alizozoea kuzinyoa katika mtindo unaopendeza sasa zilinyolewa rafu rafu na wafungwa wenzake kwa wembe na kitana. Hakuwa na mkasi wala mashine.
Mikono tayari ilishatengeneza ngozi ya kujitetea kutokana na kazi ngumu alizokuwa akizifanya kila kukicha. Gerezani ilikuwa ngangari tu, ule ‘umayai mayai’ aliokuwa nao uraiani ulishaanza kufutika hata katika kichwa chake.
Na miguu yake iliyozowea kutinga mitwango ya nguvu, sasa ilikuwa imeanza kuzoea uzito wa ‘kata mbuga’ zenye unene wa kutisha pengine kuliko ule wa viatu vingi vya wamasai.
Mbali ya nguo zake kuwa chafu kupindukia. Promota Halfani pia alishaizoea harufu mbaya iliyozalishwa na mwili wake, chumba chao wachilia mbali ile inayozalishwa na wafungwa wenzake.
Hakuwa na sabuni na kukaa muda mrefu bila kuoga kilikuwa kimeshakuwa kitu cha kawaida kwao. Naam! Huu ulikuwa mkondo mpya wa maisha ya Halfani ndani ya gereza la Ukonga badala ya ule wa uraiani.
Ulikuwa mkondo mbaya unaochusha na kuudhi, mkondo mbaya wanaomtoa mtu thamani, mkondo mbaya unaomuua mtu haraka zaidi kisaikolojia na kiaikolojia. Mkondo mbaya usiofaa kutumiwa hata na washenzi wa tabia. Ulikuwa mkondo mbaya… mbaya unaokiuka haki za kibinadamu katika kila sekta wale waliowahi kufika jela wananipata vilivyo.
Ndugu yangu kama hujafika jela omba Mungu wako akusaidie uendelee kuisoma hivyo hivyo magazetini na vitabuni. Jela sio Duniani ni Jehanamu! Pengine hata kuzimu kuna afadhali, maisha ni yabisi na moto toka unaingia mpaka unatoka.
Alipomaliza kusafisha Halfan alitoka nje, ambako aliwakuta wenzie wako katika foleni ya chakula. Foleni ilikuwa ndefu iliyotembea taratibu sana lakini hakuchoka kusubiri. Naam angechoka angekula wapi? Akaendelea kusubiri.
Ghafla muujiza ukaja.
Geofrey akaja na chakula sahani mbili, sahani moja na akimgawia Halfan! Msaada wa mashaka. Halfan akaukataa kistaarabu akimwambia
“Ahsante nashukuru, nami naenda kuchukua chakula changu!”
“Pokea fala wewe!” Geofrey akaunguruma. “Usiwe mjinga, ukifika msosi utakuwa umekwisha foleni ndefu!” Geofrey akalazimisha.
“Poa! Ni mpaka hapo utakaokwisha!”
“Ndo kusema ushakuwa mwenyeji sio? Ushajifunza ubishi na ujeuri? Sasa nasema hivi…” Akaweka chakula chini na kumsogelea Halfan “Utachukua!”
Halfan hakuwahi hata kujibu alishtukia sare yake chafu ikikusanywa kusanywa pale kifuani kwake, akavutwa pembeni na kuondolewa kwenye foleni halafu akaanza kutikiswa.
Hakukubali nae akamdaka mashati, wakatikisana!
Wakati Halfan akiendelea kujitetea Nyapara Pongwe akatokea na kumfokea Geofrey. Geofrey akachana na Halfani, akanyanyua pleti zake alizokuwa ameziweka chini na kutokomea.
Halfani akarekebisha shati yake iliyoongezwa na michuzi ya maharage iliyokuwa imetapakaa katika mikono ya Geofrey na kurudi katika foleni ya kwenda kuchukua chakula.
Geofrey au Jofu au Gideon ni mmoja kati ya wafungwa wanaolala chumba kimoja na Halfan. Kuikataa ofa ya Jofu, Halfan hakuwa amefanya makosa. Alijua kabisa ofa hiyo ingemletea matatizo baadae hususani usiku .
Ndiyo! Alipofika hapa kwa mara ya kwanza, alizoea kupokea pokea vitu hovyo toka kwa wafungwa wenzake. Siku walipokuja kumdai malipo ya misaada hiyo kwa staili ya sodoma, ndipo alipotia akili kichwani.
Alipotia ngumu kutoa malipo hayo, ukawa mwanzo wa uhasama kati yake na wafungwa wenzake hasa Geofrey.
Uhasama ambao mara kadhaa ulishampatia vipigo vya haja ambapo kimoja kati ya vipigo hivyo, kilimpelekea alazwe hospitali kwa matibabu zaidi. Kuanzia hapo amekuwa mzoefu na hata awe na tatizo la namna gani, ofa ya mtu hapokei!
Hatimaye akafika mbele na kupatiwa ugali uliokuwa na sehemu kubwa ya makoko meusi na manene. Alipolalamika kwa mpishi, akaishia kufyonzwa na kutazamwa kwa jicho kali kabla hajaambiwa awapishe wengine upesi.
Akasogea mbele na kuwekewa mchuzi mwingi na maharage kidogo. Wadudu walionekana waziwazi katika unga wa dona na maharagwe mabovu. Hii haikumsikitisha Halfan mabaye tayari alishaizoea. Naam! Miaka miwili na nusu aliyoishi humo haikuwa haba.
Akasogea pembeni, maji ya kunawa wala ya kunywa hayakuwepo! Akaipangusa mikono katika sare chafu na kuanza kula! Alikila chakula kile vizuri sana.
Akanawa kwa kutumia sare zake tena na kurudisha vyombo. Kiu ilimsumbua kweli kweli, lakini nani wa kumpa maji? Akajitia kuisahahu.
Juu ya maradhi, hilo walishamuachia Mungu kila mwezi wafungwa ‘walikuwa wanaondoka’ kutokana na homa za matumbo. Matumbo ya kuhara na kudhalilika na yanapotokea magonjwa ya milipuko hali huwa mbaya zaidi.
Baada heka heka za chakula kumalizika Halfani akarudi katika eneo lake, akanyoosha kigunia kidogo chakavu na kulala juu yake, mawazo mbalimbali yakapita kichwani mwake.
Alikumbua siku za mwanzo mwanzo, wafungwa walipomdharau na kumcheka pale alipowaeleza kosa lililomfanya afungwe. Kwamba alikuwa anapenda sana uroda. Akaandaa mashindano ya urembo, akawapitia warembo wote, akashitakiwa na mzazi wa mrembo mshindi ndio akafungwa.
Kuanzia pale Halfan akawa amejifunza kitu kimoja muhimu, kwamba ili uheshimike huko gerezani hupaswi kusema nilibaka au nilimtia mimba mwanafunzi n.k.
Bali unapaswa kusema ‘nilibugi stepu wakati tukiteka gari!’ ‘tulikuwa tumevamia benki’ n.k. Makosa hayo ndiyo wafungwa wanayoyahusudu.
Kwa ujumla mawazo yalikuwa mengi kichwani mwake, na yalikatizwa kila mara wakati wafungwa walipokuwa wakiingia mmoja baaya ya mwingine kuungana nae katika matayarisho ya kuiaga siku hiyo.
Mpaka usingizi unamchukua, tayari idadi kubwa ya wafungwa anaolala nao walishaingia na kuchukua nafasi zao…

* * *
Baada ya kutambulishana mikono ilianza kutambaa hapa na pale katika miili, kila mmoja katika mwili wa mwenzake. Shania Njenje alikuwa hodari kweli katika shughuli hii.
Alitembeza mikono yake laini kwenye sehemu muhimu za Halfan huku Halfan nae kiuoga uoga akifanya vivyo hivyo kwake. Alihisi mikono yake iliyojaa sugu ikiuchubua mwili wa Shania, lakini sauti iliyokuwa ikitoka kwa Shania ilidhihirisha ni raha kiasi gani aliyokuwa akiipata. Hili likampa Halfani mori wa kuendelea.
Na alimtesa kweli kwani alihakikisha anaipeleka mikono katika sehemu ambazo zitamfanya ajihisi kusisimka wakati wote. Shania alipandisha na kushusha pumzi mithili ya anayemaliza mbio ndefu za marathon.
Nguo zikawa nzito kupindukia. Ilikuwa ni hiyari yake alivyoomba Halfan aifungue zipu ya nguo yake na Halfan akalitekeleza hilo. Baada ya zipu, vikafuatia vishikizo vya sidiria vilivyoyaacha matiti mazuri ya Shania yakiwa nje. Yalikuwa matiti mazuri ambayo Halfan hakuwahi kuyaona
Hata Nasra hakuwa na matiti kama haya! Akawaza moyoni kabla hajayabugia kwa pupa bila kuyameza, akamuacha Shania akitabasamu na kumalizia nguo zilizobakia mwilini mwake tahamaki alibaki kama alivyozaliwa.
Halfan akapagwa na kutopewa baada ya kuona kitovu murua na zile sehemu hatari za Shania, zilizozungukwa na cheni aghali za dhahabu. Hali ikabadilika mzee mzima aliyehifadhiwa mahala akaanza kumsumbua.
Ikawa vurugu mtindo mmoja mmoja.
“Where is the master bed room?” Halfan akauliza kichovu, ulevi wa ashki ukionekana dhahiri katika macho yake, midomo ikijaza mate huku koromeo likifanya kazi ya kuyameza bila kuchoka.
“Kushoto kwako! Mbele kidogo kutoka hapa” Shania akasema puani. Yeye pia alikuwa hoi bin taaban kama Halfan. Ashki, uchu na matamanio vikimkaanga vibaya.
Halfan akamnyanyua kwa kumchota. Alishazoea kubeba miti mizito, magogo na mabanzi ya mbao, kwake Shania alikuwa mwepezi kama ubua! Akampakata mikononi hadi kitandani huku mchezo wa kupapasana ukiendelea Shania akaita “Promota?”
“Naam!” Halfan akaitika.
“Je?” Akauliza “Unanipenda kweli?”
“Huniamini?!” Akasita na kuuliza, “Ndiyo ninakupenda. Ninakupenda kupita kiasi!”
“Muongo! Wala hunipendi!”
“Eti unasema?” Halfan akashtuka na kumtumbulia macho Shania.
“Endelea!” Shania akahimiza. “Kwani huwezi kujibu huku ukiendelea kunipapasa”.
“Hapana naweza!” Halfan akajibu akiendelea na utundu wake
“Kwa nini unasema hivyo?” Akasaili baadae.
“Kwa nini ulininyima ushiriki katika shindano lako la Miss Temeke Academia?
“Sikukunyima baby! Nafasi zilikuwa zimejaa! Nisingeweza kuongeza warembo, wengine wasingenielewa hasa ukizingatia kuwa niliwapata baada ya mchujo mkali. Niko katika matayarisho mengine naandaa Miss Tanzania Academia! Haki ya nani lazima ulivae taji hilo.
“Muongo, Halfan! Tena muongo mkubwa! Mimi na Nasra nani aliyechelewa zaidi? Mbona Nasra ulimpa nafasi au kwa vile yeye ni Suriama?”
Halfan akakwama kwa muda kabla ya kujibalaguza. “Kwani na wewe unahitaji sana zawadi ya gari? Mbona magari mazuri unayo mengi tu? Ona hili jumba la kifahari ulilonalo, achana na vitu vidogo vidogo! Tuangalie mapenzi yetu kwanza”.
“Siyo gari Promota! Nataka umaarufu!! Kuwa na fedha ni kitu kimoja wakati umaarufu ni kitu kingine. Nataka watanzania wajue Shania ‘Twain’ Njenje ni nani katika nchi hii!”
Halfan akacheka Shania pia akacheka pamoja nae.
“Hilo tu? Au kuna jingine?
“Hilo kwanza, mengine baadae!” Akanong’ona.
“Hesabu umepata nimeshakwambia sasa ninaandaa Miss Tanzania Academia! Tena nitakushirikisha katika uratibu twende pamoja. Achana na Miss Temeke, nani anamjua Miss Temeke Academia? Nakupandisha chati baab–kubwa upo mapenzi?” Shania akakenua.
“Ndiyo sababu nilikuuliza kama unanipenda Halfani?”
“Kuliko unavyoweza kufikiria Shania!”
“Yaani! Naomba unipende kama ulivyokuwa ukimpenda Nasra, nakuhakikishia mimi sitakuwa kama yeye. Sitakuwa sababu ya kukufanya ufungwe, sitakuponza Halfan wangu sitakutelekeza... sita… sita… what do you do? Go on my love!” Akahimiza na kuendelea.
“Angalia mimi ninavyokupenda Halfani nimetumia pesa zangu kuhonga ili kukutoa kule jehanamu” Nasra hakuja hata siku moja! Hakuja walau kukupa hata pole.
Wakati kutoka anapoishi mpaka gereza ulilofungwa nauli ya basi ni shilingi mia tatu tu. Hivi Nasra alikuwa akikupenda kweli au alitaka ile Caddilac yako tu?
Masikini Halfan, angalia ulivyo… angalia ulivyo…!” Akashindwa kuendelea ni dhahiri aliumia moyoni, muda ukapita wakiendelea kupapasana.
“Naomba uniahidi kitu kimoja…” Shania akakurupuka tena ”Kwamba hutamrudia Nasra tena na utanipenda kama ulivyokuwa ukimpenda Nasra!
“Nakuahidi!”
“That is very good! Sasa nitakuonyesha nini maana ya mapenzi njoo sasa. Come on baby! Huku miguu akiitandaza vizuri nusu amefunga macho nusu ameyafungua; Shania alimruhusu Halfan atue kunakohusika.
Halfan akajivuta na kutua sawia kama kipanga. Shania akafumba macho na kuufaidi uhodari wa Halfan. Raha timilifu ikiutawala moyo wake, katu hakutaka kuuonyesha mashangao wake dhahiri.
Ndiyo! Aliona sio vyema kustaajabu ya Musa kabla ya yale ya Firauni. Huku wakipokezana pumzi, wote waliruhusu shughuli pevu kufanyika pale kitandani. Shania alipoona Halfan anataka kumzidi kete akasimamia pambano.
Akamuomba Promota asimamie, Halfan akatii kisha akamueleza kwa mikono kwamba akae akaanza! Halafu Shania akajiandaa kuyakalia mapaja ya Promota Halfan akiwa na lengo moja tu kupakatwa…!

* * *

Ni ile mikono yenye nguvu iliyokuwa imembana kiunoni kwa nguvu ndiyo iliyomshitua na kumuondoa toka katika njozi hiyo tamu aliyokuwa akiiota, alipogeuka nyuma akakuta jamaa linataka kumbaka.
Halfan akakurupuka baada ya kuhisi nini kinataka kuendelea hata hivyo juhudi zake za kutaka kujinasua zilikwama baada ya kujikuta amedhibitiwa vizuri na jamaa yule.Hakutaka kukubali kirahisi akakunja mkono upesi na kuachia kipepsi kilichotua sawia shingoni mwa jamaa. Akainuka na kuliacha likigugumia kwa maumivu.

***PROMOTA umalaya unamfikisha gerezani…uraiani ameacha mtoto….nini hatma yake gerezani???
Na kwa nini inaitwa WASALIMIE KUZIMU???
Usikose walau kipande kimoja cha riwaya hii ya kusisimua itakuwa ikikujia kila mchana hapa hapa uwanja wa simulizi……

ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Recent Posts