MTUNZI: INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
SIMU: 0713 59 35 46/0755 04 05 20
SEHEMU YA KWANZA
ALIPOCHEKA, alipendeza. Tabasamu lake zuri, tabasamu linaloshawishi na kusisimua, huwafanya watu hususan wanawake, wamsogelee na kumsalimia. Baadhi ya wanawake hao husisimkwa miili pindi tu waisikiapo sauti yake. Alikuwa na sauti ya kipekee, sauti iliyogusa hisia zao na kuamsha gharika la maraha kwenye michipuo ya fahamu zao.
Alikuwa ni kijana wa kiume, mwenye sura ya ucheshi na macho ya upole. Hakuwa mwoga wa kutazamana na mtu, lakini hakupenda kutazamana na mwanamume mwenzake. Kwake, macho ya mwanamume mwenzake yalikuwa na kitu asichokijua, kitu kisichopendeza.
Hali hiyo ilikuwa kwa wanaume tu, siyo kwa macho ya wanawake. Aliyapenda macho ya wanawake na ilipotokea akakutanisha macho na kiumbe yeyote wa kike, katu hakuyabandua macho yake. Ndani ya mboni za mwanamke yeyote kulikuwa na kitu fulani kisichoelezeka, lakini kilichomvutia na kumsisimua.
*****
ALIPOZALIWA wazazi wake walimpa jina la Maftah, jina ambalo baada ya miaka kadhaa lilipotea na kuzaliwa kwa jina jingine, Kiwembe, ambalo alipachikwa kutokana na yale ayapendayo na ayatendayo, yale aliyokwishayageuza sheria badala ya kawaida.
Ni katika kitongoji cha Ujiji mjini Kigoma ambako Kiwembe alizaliwa. Wazazi wake walikuwa na nyumba katika Kata ya Kasingirima, na katika ndoa yao walibahatika kupata mtoto mmoja tu, huyo Kiwembe.
Kiwembe hakubahatika kufaidi vilivyo malezi ya baba na mama. Mwaka 1978 mji wa Kigoma ulitikiswa na maradhi ya kipindupindu, maradhi yaliyowakumba wakazi wengi, na wengi wao wakafariki dunia. Wazazi wa Kiwembe walikuwa miongoni mwa waliofariki kwa maradhi hayo. Walimwacha Kiwembe akiwa na umri wa miaka kumi na miwili.
Mzigo wa kumlea mtoto Kiwembe ulihamia kwa mama yake mdogo ambaye aliishi mtaa wa tatu kutoka kwao Kiwembe. Hayakuwa maisha yaliyostahili kwa mtoto wa rika la Kiwembe. Huyo mama yake mdogo hakujali kuwa Kiwembe kala nini au kama anahudhuria masomo ipasavyo. Hivyo, mara nyingi Kiwembe akawa anazurura mitaani.
Akiwa ni mtoto ambaye alijaaliwa kukua harakaharaka, Kiwembe alikadiriwa na wengi kuwa ana umri wa miaka kumi na minane au ishirini.
Ni umbo lake hilo kubwa ndilo lililomfanya Mama Kadala wa mtaa wa pili amtazame mtoto wa watu kwa macho yenye kila dalili ya njaa dhidi yake. Mama huyo aliyekuwa na umri wa kutosha kuwazaa akina Kiwembe wengine kama watatu, hakuwa mtu wa kujali eti huyu ni kijana aliyekwishabalehe au bado.
Alichopenda yeye ni ‘kupakata dogodogo.’ Na baada ya kumwona mtoto Kiwembe akiwa hana uangalizi mkubwa, akaamua kumwinda taratibu. Jimama hilo tipwatipwa likawa haliishi kujipitishapitisha jirani alikoishi mtoto Kiwembe.
Jimama hilo lilimpenda Kiwembe na likawa tayari kufanya jambo lolote na mtoto huyo potelea mbali hayo matokeo yake yatakavyokuwa. Na hata kama matokeo hayo yatakuwa ya kumfedhehesha, hakujali. Aliapa kuwa ni lazima ‘aanguke naye kisahani.’
Ndipo ikaja siku ambayo Kiwembe alijikuta akiingia kwenye anga za Mama Kadala. Walikutana njiani, saa 12 jioni, Mama Kadala akamwomba Kiwembe msaada wa kumbebea kijifurushi kidogo hadi kwake. Kilikuwa kijifurushi kilichosheheni vitunguu, nyanya na vikorombwezo vingine vya kutayarishia mboga.
Kiwembe hakuwa na hiyana, kwa heshima zote akamsaidia mama huyo mzigo huo mdogo hadi kwake. Ni hicho alichokihitaji mama huyo asiyejua soni au heshima ni kitu gani.
“Karibu Kiwembe,” Mama Kadala alisema huku akimtazama Kiwembe kwa macho yaliyoongezwa utaalamu wa kutazama kimapenzi.
Umri wa Kiwembe haukuwa wa kumfanya aweze kutambua kuwa Mama Kadala ana maana gani kumtazama kwa namna ile. Yeye alitii ile ‘karibu’ kwa kuingia na kijifurushi kile hadi ndani na kukitua sebuleni
Hapo Mama Kadala akavuta kigoda na kumkabidhi Kiwembe kisha naye akavuta kingine na kujibweteka puu!
Wakatazamana.
Ukaaji wa Mama Kadala ukampeleka mbali kimawazo mtoto Kiwembe. Akazidi kumkodolea macho jinsi alivyokuwa ameketi pale kwenye kigoda; kiti kidogo cha jikoni. Alionyesha kushangaza mama huyo jinsi alivyokaa huku tako moja tu likiwa limekijaza kigoda kile, tako jingine likiwa kando, kama vile likining’inia.
Jimama la nguvu!
Jimama tipwatipwa!
Ndiyo, Mama Kadala alikuwa amejaaliwa umbo kubwa na teketeke, umbo jeupe, lililonawiri na kunang’anika. Kwa ukubwa wa umbo lile, alionyesha dhahiri kuwa anakionea tu kigoda kile. Lakini yeye hakujali wala hakukihurumia. Alianza kutayarisha mlo huku wakiwa hapohapo, uso kwa uso na mtoto Kiwembe.
Mama Kadala akazidi kuchuchumia na kukifanya kile kitenge alichojifunga mwilini mwake kianze kuuachia wazi mwili kutokana na hekaheka za mwiko na sufuria. Wala hakujali Mama Kadala, kwamba yule mtoto anamkodolea macho.
Zaidi, alijiachia kwa uwazi, labda akitaka mtoto huyo akishuhudie kile anachosikia au ambacho aliwahi kukisikia. Mama mtu mzima huyo hakujali kuwa macho ya mtoto Kiwembe hayakuwa na pazia. Yeye aliithamini ile methali isemayo “MTOTO USIYEMZAA NI MKUBWA MWENZIO…”
Ni ile nguo pekee, ndogo, laini ya ndani ndiyo iliyomkinga na macho ya Kiwembe, asione vyote. ‘Sukari ndani, sukari nje!’ Lakini macho ya Kiwembe yalikuwa shahidi wa yote, yakaona kisichostahili kuonwa.
Punde Mama Kadala aliuachia mwiko ule, akashika sehemu ya pindo la kitenge alichojifunga, akajipangusa jasho usoni. Kitendo hicho kilimfanya awe mtupu, kama aliyedhamiria kumuumbua mtoto wa mwenzie.
Macho ya Kiwembe yalitazama kwa ukomo wa fahamu zake. Akayatembeza macho hayo taratibu, kutoka kwenye unyayo wa mama yule, unyayo uliokolea hina, akayapeleka hadi kwenye shina la mapaja; alichokiona hapo akakiundia taswira isiyoelezeka wala kueleweka akilini mwake. Akahisi ibilisi akimnyemelea kichwani. Kizunguzungu kikamvaa ghafla.
Fahamu zikamtoka!
Alizinduka muda mrefu baadaye, usiku ukiwa umeshaingia. Akajikuta kalala kwenye kitanda cha Mama Kadala, mwenzi wake katika kitanda hicho akiwa ni yuleyule Mama Kadala, na wote wakiwa tupu kama walivyozaliwa, wamejifunika shuka moja!
“Haa! Mama Kadala! Hapana! Unaniwangia Mama Kadala,” Kiwembe alinong’ona kwa sauti iliyoonyesha woga. Akakurupuka kutoka, hakuweza.
“Tulia…tulia mtoto…tulia mtoto mzuri,” Mama Kadala alimbembeleza huku akimkumbatia na kumpapasapapasa. “Tulia, usihofu… wasiwasi wa nini?”
Kiwembe akaishiwa kauli. Na huo ukawa mwanzo wa kijana mdogo, Kiwembe kulijua penzi. Tangu siku hiyo penzi lao likawa penzi la siri. Siri ikawa siri hadi siku alipojikuta akibalehe kifuani pa Mama Kadala, mwanamke mwenye mwili mkubwa, asiye na haya wala staha.
Wakazidi kupendana. Kiwembe akapikiwa ‘wali wa tako moja na chai ya maandazi ya sukari ndani, sukari nje’ na michuzi ya mapaja wazi. Ujiji ikamfanya mtoto Kiwembe abalehe kabla ya wakati!
*****
“UNAUMWA?”
“Hapana, siumwi.”
Kwa ujumla hata yeye mwenyewe alishangaa, kipi kilimchanganya hata ashindwe kula? Kama ni mpunga uko shamba, kuulima hawezi, lakini akiuhitaji anaupata. Mchele uko kwenye ungo, ukipepetwa na kuchaguliwa chuya, kisha ukapikwa, ukaiva, basi ndio huo unaoitwa “wali.” Na sasa wali huo ndiyo ulikuwa umepakuliwa, umo ndani ya sahani pale mezani. Kijiko anacho, vipi ashindwe kula? Badala yake kaduwaa, msichana mrembo wa rika lake akiwa mbele yake akimhimiza kula.
Tangu abalehe, mawazo yake yote yako kwenye mapenzi tu. Kila akifikiriacho ni mapenzi.
“Kula basi jamani, mbona huli?” alihimizwa tena. Lakini bado hakufanya kitu. Badala yake aliunyanyua uso na kumtazama msichana huyo mdogo na mwenye mvuto mkali. Akamtazama kwa haya kidogo.
“Kwani unaumwa?” msichana aliuliza tena. Kisha akaongeza, “Pole basi ka’unaumwa.”
“Mmmh!Hapana, siumwi,” Kiwembe alijitahidi kuipata sauti yake. “Ni wewe tu ndiye unipaye maradhi. Naamini mtoto mzuri kama wewe ndiye chanzo cha maradhi niuguayo. Sura yako na umbo lako ndivyo vinavyonifanya nipate hamu ya kustarehe na wewe. Tafadhali…”
Alikipa uzito kila alichokitamka. Kinywa kilitamka, sauti ikaghani, macho yakasihi na mikono ikashawishi alipokuwa akilitomasatomasa bega la Sharifa, mtoto wa Mama Kadala.
Kiwembe alizidiwa na kiwango cha matamanio hata akashindwa kujizuia. Akatamani penzi kila wakati. Penzi la Mama Kadala likawa halitoshi, penzi la usiku kwa usiku. Mchana kutwa Mama Kadala hushinda kwenye biashara zake za ‘mama lishe.’
Na hapo nyumbani hushinda Kiwembe na Sharifa, peke yao! Sasa Kiwembe anahofia nini ilhali alishagundua kuwa hata Sharifa mwenyewe anamtamani? Kiwembe hakuisahau ile siku ambayo Sharifa alimwingilia chumbani wakati kajipumzisha kitandani. Sharifa aliingia huku kajifunga kanga moja tu maungoni bila nguo nyingine.
Umbo lake lililotoa taswira ivutiayo, lilikuwa likitikisika kwa namna ambayo Kiwembe alisisimkwa mwili. Na hata walipokutanisha macho, Kiwembe aliona kitu, zaidi ya utazamaji wa kawaida katika mboni za macho ya Sharifa.
Hata hivyo Sharifa alijitia kutafuta kitu ambacho Kiwembe hakukijua kisha akatoka huku makalio yake yakitikisika kwa nguvu na kuwa kivutio kingine akilini mwa Kiwembe.
Akilini mwa Kiwembe vitendo vile vya Sharifa ulikuwa ni uchokozi wa dhahiri. Kumbe Sharifa alifikiria nini ilhali alitambua fika kuwa yeye, Kiwembe, kijana ambaye hawajapishana sana kwa rika, ni mpenzi wa mama yake?
Siku hiyo ya majaribu ya Sharifa, Kiwembe alitaka amtamkie bayana hitaji lake, na kama angekataa, angembaka. Lakini mtoto wa kiume alijitahidi kumzuia shetani wake huku akijifariji kuwa ipo siku ataumia naye. Na huenda siku yenyewe ndiyo hii. Kiwembe aliamini hivyo.
Moyo ulikuwa wamdunda Sharifa. Hakujua afanye nini na huyo mpenzi wa mama yake. Maneno ambayo Kiwembe alikuwa amemwambia muda mfupi uliopita yalikuwa yakielea kichwani mwake na kumzulia utata usiotatulika.
“Lakini…lakini wewe si ni baba wewe?” Sharifa alijikuta akitokwa na maneno hayo. Hakuwa na neno jingine la kujitetea. Alikuwa kama anayepima uzito wa jambo lenyewe. Hata kauli yake, hata sauti yake vyote vilikuwa dhaifu, vikiwa havina nguvu wala punje ya upinzani.
“Sikatai,” Kiwembe alisema. “Lakini pamoja na hayo, haya si nd’o mageuzi yenyewe? Na hizo stori za “baba…baba” achana nazo. Hebu tazama umri nilionao, na alionao mama yako. Mimi ni mtu wa kufaa kuwa bwana’ake? Inakuingia akilini wewe? Achana na umbea wa waswahili, umbea usiojenga bali kubomoa. Sharifa, wewe ndiye saizi yangu. Wewe ndiye halali yangu kabisa! Cheki hata maumbo yetu yanavyoshabihiana.”
Sharifa alilainika kama mboga ya bamia. Akakamatwa kiuno na kuvutiwa kwenye kitanda cha mama yake. Wakashiriki dhahama. Naam, hawakujua ni ngoma ipi waliyocheza pale kitandani. Kama ni sindimba, basi ilikuwa sindimba kweli. Kama ni Mduara basi ulikuwa ni Mduara halisi. Kama ni Mugongomugongo, ilitisha. Chumbani kwa Mama Kadala, kitandani kwa Mama Kadala, na mtoto wa Mama Kadala!
Kiwembe! Kabalehe kwenye kifua cha Mama Kadala, na sasa anafanya mazoezi kwenye mwili wa mtoto wa Mama Kadala! Kwenye kitanda kilekile!
Huo ulikuwa ni mwanzo tu, mwanzo uliofungua ukurasa mpya wa uhusiano baina yao. Penzi likawanogea. Awali ilikuwa ni siri, siri iliyofichika, lakini hatimaye minong’ono ikaanza kuzagaa mitaani. Siri hiyo ilianza kufichuka.
KIWEMBE kaanza kumnyoa mama sasa anahamia kwa mtoto…vipi mama mtu akijua….
No comments:
Post a Comment