MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI.
MAHALI: DAR ES SALAAM.
SIMU: 0718 069 269
Kwa kiasi fulani nikauhisi moyo wangu kuingia katika hali fulani hivi, najua wale ambao waliwahi kuwasiliana na wasichana kwa zaidi ya dakika themanini watakuwa wamekwishawahi kukutana na hali hii. Alikuwa msichana ambaye alikuwa wazi na wala hakutaka kujificha chochote kile. Aliniona kumvutia sana.
MIMI: Asante sana japokuwa najiona kuwa mtu wa kawaida sana.
MSICHANA: Wa kawaida? Labda kwako mwenyewe. Hivi nikuulize swali la kizushi?
MIMI: Uliza tu.
MSICHANA: Una msichana?
MIMI: Yeah! Ninao.
MSICHANA: Unao?
MIMI: Ndio.
MSICHANA: Wangapi?
MIMI: Wengi tu.
MSICHANA: Kama wangapi?
MIMI: Ngoja kwanza. 1, 2, 3, 4. Kwa sasa ninao hao tu japokuwa wa 5 na wa 6 nipo kwenye process za mwisho.
MSICHANA: Sawa. Hongera.
MIMI: Asante.
MSICHANA: (Kimyaaaaa)
Kila wakati nilikuwa mtu wa kupenda sana utani pasipo kugundua kwamba wakati mwingine utani wangu unaweza kuniletea mambo mabaya. Nilikuwa nimeongea nae hayo yote kama sehemu ya utani, nikahisi tu kwamba alikuwa amekasirika japokuwa hakutaka kuongelea hilo. Hakunitumia meseji, alibaki kimya kwa muda wa dakika ishirini, nikashindwa kuvumilia, nikamtumia meseji.
MIMI: Mbona kimya tena?
MSICHANA: Nipo bize.
MIMI: Bize? Ubize wa nini tena?
MSICHANA: Hautakiwi kujua.
MIMI: Ok.
Tayari nilikwishaona kwamba nimeharibu, nilichokifanya, nami nikajidai kukaa kimya, si unajua mwanaume hautakiwi kuonyesha udhaifu kirahisi namna hiyo. Nilikuwa nikiumia sana kukaa kimya japokuwa nilikuwa nikijikaza kisabuni sana. Nikamtumia meseji.
MIMI: Nimechoka.
MSICHANA: Eehh! Umechoka kufanya nini tena?
MIMI: Kuwa...ok!
MSICHANA: Kuwa muwazi bhana.
MIMI: Nimechoka kuwa online. Nadhani natakiwa kusaign out mpaka wiki ipite ndio nirudi tena.
MSICHANA: Kwa nini tena?
MIMI: Sioni umuhimu wa kuwa online.
MSICHANA: Kivipi?
MIMI: Kwa sababu hautaki kuchati nami. Umekaa kimya sana.
MSICHANA:Napenda amani Nyemo.
MIMI: Nafahamu hilo. Ila unamaanisha nini?
MSICHANA: Huwa sipendi kuchati na mtu mwenye wasichana wengi.
MIMI: Hahaha! Nilikuwa nakuzingua bwana. Unadhani naweza kuwa na wanawake wote hao. Utani tu, naomba unizoee wangu.
MSICHANA: Poa
MIMI: Unafanya nini?
MSICHANA: Nipo chumbani. Peke yangu huku kwa mbali wimbo wa Westlife ukisikika.
MIMI: Wimbo gani?
MSICHANA: As love as my witness. Unaujua.
MIMI: Yeah.
Akakaa kimya tena. Kwa wakati huo kidogo nikaanza kujisikia amani. Muda wote nikawa bize kusikilizia meseji yake, ghafla meseji ikaingia, meseji hii ilikuwa imeambatana na picha moja nzuri, alikuwa amepiga akiwa kitandani huku juu akiwa wazi na nguo yake ya ndani ndio ambayo ilikuwa mwilini mwake.
MSICHANA: Umeionaje picha hiyo?
MIMI: Mmmh
MSICHANA; Kuna tatizo.
MIMI: Hapana. Ila......una nyingine tena unitumie?
MSICHANA: Subiri
Akaanza kunitumia picha nyingi nyingi, picha zote zilikuwa zinanichanganya tu, nilikuwa nikiweweseka tu.
MSICHANA: Na wewe nitumie zako.
MIMI: Poa.
Hapo ndipo nilipoanza kujipiga picha na simu yangu. Nilijipiga picha zaidi ya kumi huku na mimi nikiwa nimevaa boksa tu. Nilipomaliza, nikawasha bluetooth na kisha kuziweka kwenye kompyuta na kisha kumtumia.
MSICHANA: Unavutia sana. Naomba tufanye kitu kimoja.
MIMI: Kitu gani?
MSICHANA: Nitumie namba ya simu, nataka tufanye kitu fulani usiku.
MIMI: Kitu gani?
MSICHANA: Mapenzi kupitia maongezi simuni.
MIMI: Mmmh!
MSICHANA: Mbona unaguna? Haujawahi kufanya hivyo?
MIMI: Nimewahi. Tena zaidi ya mara ishirini tena ikiwa zaidi ya masaa sita simuni.
MIMI: basi naomba tufanye hivyo.
Hapo nikabaki kimya, nikaanza kujifikiria kama ilikuwa vizuri kumtumia namba ya simu au la. Alikuwa akitamani sana tufanye ngono simuni jambo ambalo nilijua lilikuwa na matatizo sana kisaikolojia. Hata kabla sijajua nifanye nini, meseji yake ikaingia, nikawa na shauku ya kuifungua. Nikaifungua haraka haraka.
Nikaifungua ile meseji, kwa wakati huu meseji ile ilikuwa imekusanya maneno mazuri ya mapenzi. Nilikuwa nikiziangalia kwa kuzisoma moja baada ya nyingine. Hazikuwa meseji ngeni kwangu, nilikwishawahi kuziona mara kibao.
MIMI: Unaonekana unapenda sana mahusiano ya kimapenzi pamoja nami?
MSICHANA: Ndio. Nimetokea kuvutiwa nawe.
MIMI: Hahaha! Unataka nianze kuwindwa na bunduki mitaani.
MSICHANA: Kwa nini?
MIMI: Mvulana wako.
MSICHANA: Hahahahaha
MIMI: Unacheka unaona mazuri?
MSICHANA: Mbona unakuwa muoga hivyo? Yaani unamuogopa hadi mwanaume mwenzako
MIMI: Si kwamba namuogopa, hapana, naogopa bunduki.
MSICHANA: Hahahaha! Hapana bwana. Siko kwenye mahusiano, nilikuwa na mpenzi ila tumeachana.
MIMI: Chanzo nini?
MSICHANA: Alikuwa anadate na rafiki yangu mmoja hivi.
MIMI: Pole sana.
MSICHANA: Asante sana. Vipi kuhusu wewe?
Hapo nikabaki kimya kwa muda. Kichwa changu kilikuwa kikifikiri kwa haraka sana. Hii ilimaanisha kwamba kama ningemwambia nina msichana, kwanza angeumia halafu ndio ingekuwa mwisho wangu na
yeye kuchati. Huku nikiwa najifikiria nini cha kujibu, mara meseji yake ikaingia.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment