Friday, April 5, 2013

FACEBOOK CHATTING ----------------1

 MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI.

MAHALI: DAR ES SALAAM.

SIMU: 0718 069 269MSICHANA: Mambo Nyemo.
MIMI: Poa. Mzima?
MSICHANA: Mzima wa afya. Unafanya nini?
MIMI: Nachati na friends pamoja na kuangalia muvi kwa kuibia.
MSICHANA: Hata mimi nachati pia. Muvi gani hiyo unayoangalia kwa kuibia?
MIMI: Message in the Bottle.
MSICHANA: Mmmh!
MIMI: Mbona mguno tena?
MSICHANA: Hiyo muvi mpya?
MIMI: hapana. Toka mwaka 1999.
MSICHANA: Na mimi nataka nije kuangalia. Nakaribishwa?
MIMI: Duh! Poa. Karibu.
MSICHANA: Hahahaha! Inaelekea u kijana mcheshi sana.
MIMI: Kitu gani kimekufanya kuhisi hivyo?
MSICHANA: Basi tu. Nimejirubuni kusema hivyo.
MIMI: Yeah! Hivyo ndivyo nilivyo.
MSICHANA: Unaishi wapi?
MIMI: Tanzania.
MSICHANA: Yeah! Najua. Ila sehemu gani?
MIMI: Dar es Salaam.
MSICHANA: Nafahamu. Ila Dar es Salaam kubwa sana.
MIMI: Naishi Tandale. Unapajua?
MSICHANA: Huwa ninapita tu na gari mara chache chache.
MIMI: Okey. Thats gud then.

Ukimya unatawala kati yangu na yake kwa dakika kama tano hivi, mara nasikia kamlio ka meseji kanalia, ninapoangalia, naona ni yeye. Naifungua na kuisoma.

MSICHANA: Samahani kwa kukaa kimya, nilikuwa nimekwenda kununua Chill souce dukani. Nimefurahi kuchati nawe kwa sasa. Nakwenda kupika mara moja. Tunaweza kuendelea kuchati baadae?
MIMI: Usijali.
MSICHANA: Utakuwa online?
MIMI: Nafikiri kwa sababu sina pa kwenda.
MSICHANA: Poa basi, baadae kidogo.
MIMI: Poa.

Baada ya hapo anakwenda offline. SIkuonekana kujali, sikujua kwa nini msichana huyu alikuwa ameonekana kuwa karibu sana na mimi kwa kipindi hiki kichache, nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza, nikawa navuta subira mpaka katika kipindi ambachoatarudi tena online. Nikawa na hamu kumuona akirudi online na kumuuliza baadhi ya maswali ambayo yalianza kuja kwa haraka sana kichwani.

Nilikuwa na presha sana juu ya msichana huyu ambaye nilitoka kuchati muda uliopita. Niliporudi online, nikamkuta. Hata kabla sijamtumia meseji, akaniwahi.

MSICHANA: Naona umerudi.
MIMI: Yeah.
MSICHANA: Nimekumiss.
MIMI: (Kimya)
MSICHANA: Mbona haujibu chochote jamani?
MIMI: Sasa ulitaka nijibu vipi hapo?
MSICHANA: Kwamba na wewe pia umenimiss.
MIMI: Sasa kama sijakumiss jamani?
MSICHANA: Dah! Aya yaishe. Nilikuwa online muda mrefu kidogo, nilikuwa nakusubiria tu. Nilikuwa nimekwishaboreka, bora umerudi.
MIMI: Usijali. Nipo hapa kwa sasa.
MSICHANA: Kuna swali lolote ungependa kuniuliza?
MIMI: Yeah! Tena mengi tu.
MSICHANA: Kama yapi?
MIMI: Unaishi wapi?
MSICHANA: Mbezi.
MIMI: Unajua kama zimegawanyika sehemu mbili?
MSICHANA: Yeah! Nipo ya huku Beach.
MIMI: Ok! Unasoma au unafanya kazi?
MSICHANA: Nasoma sekondari.
MIMI: Wapi?
MSICHANA: St' Mary.
MIMI: Ok! Unaishi na nani?
MSICHANA: Na wazazi wangu. Baba yangu mfanyabiashara na mama yangu ni mhasibu pale BoT.
MIMI: Unasemaje?
MSICHANA: Kwani haujasikia jamani au unanifanyia makusudi tu.
MIMI: Sawa. Nimekuelewa. Hivi ni kitu gani ambacho kimekupelekea kupenda kuchati nami na wakati ni jana tu ndio tulianza urafiki?
MSICHANA: Kwa mara ya kwanza niliweza kukuona pale nilipoingizwa kwenye kundi lako la hadithi na rafiki yangu. Japokuwa sicomment wala kulike lakini nimependa sana hadithi zako. Huwa ninapenda sana kuzisoma huku nikiwa kitandani.
MIMI: Sawa. Usijali.
MSICHANA: Hivi itawezekana kuendelea kuchati hata kipindi ambacho hatupo online?
MIMI: Kivipi? (Niliuliza japokuwa nilifahamu alimaanisha nini?)
MSICHANA: Simuni.
MIMI: Kwa hiyo unamaanisha unataka namba ya simu?
MSICHANA: Ndio. Ila kama hautojali wangu.
MIMI: Hapana. Hapa facebook kunatosha sana.
MSICHANA: Ila ningependa kuisikia sauti yako wangu.
MIMI: Usijali, tutaweza kutumia skype pale utakapohitaji kuisikia sauti yangu, tena hadi kuniona utaniona huko.
MSICHANA: Jamaniiiii
MIMI: Kweli tena.
MSICHANA: Sawa.

Ghafla akakaa kimya, sikutaka kuchelewa, nilichokifanya ni kuanza kupitia picha zake. Mungu wangu! Kwanza nikajuta kwa nini nilimnyima namba ya simu, alikuwa msichana mzuri sana ambaye kwa mwanaume lijali kama mimi basi asingekubali kumuacha.

Mara nikaanza kupokea notification kwamba alikuwa akiLIKE picha zangu, yaani ilikuwa kama kero, kila wakati anaLIKE...analike.

MSICHANA: Nimevutiwa na picha zako. Na nimevutiwa na wewe pia.

Aliniambia maneno ambayo yalinichanganya.


Itaendelea

No comments:

Post a Comment

Recent Posts