Tuesday, October 6, 2015

THE PAINFUL TRUTH 6

 RIWAYA: PAINFUL TRUTH (UKWELI WENYE KUUMA)
MTUNZI: Nyemo Chilongani
MAWASILIANO: 0718 06 92 69

SEHEMU YA SITA

Bwana Brown alionekana kuchanganyikiwa mara baada ya kuyasikia maneno yale ambayo alikuwa ameambiwa na kijana wake, Wayne. Kitu cha kwanza akazirudisha kumbukumbu nyuma na kuanza kukumbuka kama kuna siku yoyote Wayne alikuwa ametembea na msichana na kumpa mimba lakini hakupata jibu.
Hakuelewa ni mtoto gani ambaye Wayne alikuwa amemzungumzia mahali hapo. Akakiinua kichwa chake kutoka karibu na Wayne na kisha kuyapeleka macho yake usoni kwa mke wake, Bi Lydia. Uso wa Bwana Brown ulionyesha waziwazi kwamba ulikuwa umetawaliwa na maswali mengi, akaanza kupiga hatua na kumfuata mke wake.
“Vipi?” Bi Lydia aliuliza huku akionekana kuwa na hamu ya kutaka kufahamu kitu.
“Anamtaka mtoto wake” Bwana Brown alimjibu.
“Mtoto gani?”
“Sijui”
“Kwani katika kipindi ambacho alipata ajali, Kristen alikuwa mjauzito?” Bi Lydia aliuliza.
“Hapana”
“Sasa mtoto gani anayemtaka?”
“Hata mimi mwenyewe nashangaa. Ila nafikiri atakuwa hajakaa sawa, si unajua mishipa yake ya fahamu ndio inaanza kurudi katika hali yake”
“Inawezekana”
Hakukuwa na mtu ambaye alijisumbua kufuatilia maneno ambayo alikuwa ameyaongea Wayne kwani walijua kwamba akili yake wala haikuwa imekaa sawa. Daktari mmoja na manesi wawili wakaingia ndani ya chumba kile na kisha kuwataka Bwana Brown na Bi Lydia kutoka ndani ya chumba kile kwa ajili ya kuanza kazi yao.
Kila siku Wayne alikuwa akiwaambia maneno yale yale kwamba alikuwa akitaka kumuona mtoto wake. Maneno yale yakaendelea kuwashtua kupita kawaida kitu kilichowapelekea kuanza kufuatilia. Walifuatilia kwa muda wa mwezi mmoja lakini hawakufanikiwa kujua mtoto ambaye Wayne alikuwa akimzungumzia.
Hali ya Wayne ilikuwa ikizidi kutengemaa kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele. Kutokana na fedha nyingi ambazo alikuwa nazo Bwana Brown, madaktari kutoka katika hospitali kubwa wakaanza kuingia ndani ya hospitali ile kwa ajili ya kumtibia Wayne.
Miezi tisa ikakatika na ndipo hali ya Wayne ikarudi kabisa ila mwili wake ulikuwa na tofauti kubwa sana. Alichokifanya daktari ni kuwaita wazazi wake ndani ya ofisi yake na kisha kuanza kuongea nao huku kila mmoja akionekana kuyafurahia maendeleo ya Wayne.
“Tunamshukuru Mungu kwa kuwa Wayne anaendelea vizuri” Dokta aliwaambia huku akiyaweka vizuri miwani yake pamoja na kulichukua faili kubwa ambalo lilikuwa juu ya meza yake.
“Hata sisi tunashukuru” Bwana Brown alimwambia daktari huku akiwa amemshika mkono mkewe pale vitini walipokuwa wamekaa.
“Kuna mambo mawili ambayo yametokea katika mwili wake. Kwanza ninasikitika kuwaambia kwamba mtoto wenu Wayne hatoweza kutembea tena. Miguu yake pale ilipo ilikuwa imesagika kidogo. Katika kipindi chote tulikuwa tukiangaika nayo. Namshukuru Mungu kwamba tulifanikiwa kwa asilimia themanini kwani kama tungeshindwa kabisa, haina budi tungeikata miguu yake” Daktari aliwaambia.
Kila mmoja akaonekana kushtuka, maneno ambayo alikuwa ameyaongea daktari yalionekana kuwagusa kupita kawaida, walimwangalia daktari mara mbili mbili kana kwamba yeye ndeye ambaye alikuwa amesababisha yale yote.
“Ila tunashuru kwamba ni mzima” Bi Lydia alimwambia daktari.
“Jambo la pili ni kwamba tuligundua kwamba mtoto wenu amekatika mshipa mkubwa ambao unawezesha uume wake kusimama. Mshipa ule haufanyi kazi tena, kwa maana hiyo mtoto wenu hatoweza kusimamisha uume wake tena jambo ambalo halitoweza kumpa mtoto katika maisha yake yaliyobakia” Daktari aliwaambia.
Taarifa hiyo ndio ambayo ilionekana kumshtua zaidi kila mmoja. Wakamwangalia daktari kwa macho yaliyojawa na mshtuko, hawakuonekana kukiamini kile ambacho daktari alikuwa amekiongea mbele yao. Kwa mtoto wao Wayne kukosa uwezo wa kuwa na mtoto kulionekana kuwakosesha raha, waliyaona maisha yake kujaa giza huko mbeleni.
Hawakujua Wayne angeishi katika maisha gani, kutokutembea na kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake yalionekana kuwa matatizo makubwa ambayo yalikuwa yameupata mwili wake. Bi Lydia akashindwa kujizuia, akainamisha kichwa chake chini, alipokiinua, machozi yalikuwa yakimtoka.
Ni kweli kwamba walikuwa na mtoto mwingine, huyu alikuwa akiitwa Esther, lakini kwa upande wao walikuwa na mapenzi ya kweli kwa Wayne. Hata kama Esther angepata watoto kumi lakini furaha yao isingekamilika bila Wayne kutokuwa na mtoto.
Hawakujua ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya, kukubaliana na matokeo yale ikaonekana kuwa kazi kubwa sana mioyoni mwao. Walichokifanya mara baada ya kutoka ndani ya hospitali ile ni kuanza kuwasiliana na madaktari waliokuwa wakubwa zaidi kutoka katika nchi mbalimbali.
Wayne akaanza kusafirishwa na kupelekwa katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kulitatua tatizo lile ambalo alikuwa nalo mwilini. Walitembea zaidi ya nchi kumi duniani tena kwa madktari mabingwa ambao walikuwa na uwezo mkubwa lakini kote huko hawakufanikiwa kabisa jambo lililowafanya kurudi nchini Marekani.
Wote wakakubaliana na matokeo. Wayne akaanza maisha mapya ya kuwa mlemavu wa miguu yake. Kila siku waandishi wa habari walikuwa wakielekea ndani ya nyumba hiyo na kuanza kuongea na Wayne ambaye siku zote hakuonekana kuwa na furaha.
Kitu ambacho alikuwa akitaka kuwaambia wazazi wake ni kuhusu Happy, msichana wa Kitanzania ambaye alimuacha akiwa mjauzito. Hakutaka kufanya haraka katika kuwaaambia hilo kwani aliamini kwamba ni lazima apate muda wa kutulia kabla ya kuongea kitu chochote kile.
Siku ziliendelea kukatika lakini Wayne hakuongea kitu chochote kile kwa wazazi wake. Kila siku alikuwa akijitahidi kutafuta njia mbalimbali za kumuwezesha kuwasiliana na Happy lakini ilishindikana kabisa. Miezi miwili ikakatika na ndipo hapo Wayne alipoamua kuwaita wazazi wake na kuanza kuongea nao.
“Nahitaji kwenda Tanzania” Wayne aliwaambia.
“Kuna nini?”
“Hapana. Ninahitaji tu kwenda Tanzania” Wayne aliwaambia.
“Hali yako si nzuri kusafiri masafa marefu. Tuambie kitu chochote kijana wetu tutakufanyia ila si kukuruhusu kuelekea nchini Tanzania” Bwana Brown alimwambia Wayne.
“Maisha yangu yametawaliwa na majonzi, kila siku nilikuwa nikikaa nikimfikiria msichana mmoja ambaye nilikutana nae katika mazingira ya kutatanisha na kumfanyia kitu ambacho kimekaa na kuniumiza moyoni” Wayne alisema huku akianza kulengwa na machozi.
Kila mmoja alikuwa kimya akimwangalia Wayne, maneno ambayo aliyaongea yalikuwa yamewagusa mioyoni mwao lakini pia yalikuwa yamewachanganya kupita kiasi. Wayne akaonekana kuwa na kitu kizito ambacho alikuwa akitaka kuwaambia kwa wakati huo.
“Unatuchanganya” Bwana Brown alimwambia.
“Nafahamu kama mmechanganyikwa na maneno yangu ila ninahitaji kwenda nchini Tanzania kuonana na Happy” Wayne aliwaambia. Wote wakaonekana kushtuka zaidi.
“Happy! Ndiye nani huyo?” Bi Lydia aliuliza kwa mshtuko.
“Msichana niliyemuacha akiwa na ujauzito wangu” Wayne alijibu.
Kwa mshtuko ambao walikuwa wameupata mioyoni mwao, walijihisi kwamba muda wowote ule wangeweza kuzimia. Maneno yale yaliwachanganya zaidi kuliko hata maneno mengine ambayo walikuwa wameyasikia kutoka kwa Wayne.
Wakamwangalia Wayne na kuanza kumsoma saikolojia yake kuona kwamba alikuwa akitania au alikuwa akimaanisha kile ambacho alikuwa akikiongea. Wayne alionekana kumaanisha. Jina la Happy ndilo ambalo lilizua mjadala mkubwa vichwani mwao, wakatamani kumfahamu huyo Happy, mbali na huyo, pia walitaka kufahamu kuhusu huo ujauzito.
“Umesemaje?” Bwana Brown aliuliza huku akionekana kuwa na mshtuko uliojaa furaha.
Hapo ndipo Wayne akaanza kuwaadithia kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika safari yake ya kwanza ya kitalii kuelekea nchini Tanzania miaka sita iliyopita. Hakuficha kitu chochote kile, alikuwa wazi kwa kila kitu ambacho alikuwa amekifanya kipindi kile.
Bwana Brown na mkewe, Bi Lydia wakaonekana kushtuka kwa furaha, hawakuamini kama kijana wao alikuwa na uwezekano wa kuwa na mtoto ambaye alikuwa nchini Tanzania. Wakajikuta wakisimama na kukumbatiana, machozi ya furaha yakaanza kuwatoka.
“Msifurahi kwa sasa mpaka pale ambapo mtakapomuona mtoto wangu mbele ya macho yenu. Hamuwezi kujua kwamba labda Happy alipata matatizo na mimba kutoka au hata mtoto kufariki” Wayne aliwaambia.
“Ni lazima nisafiri kuelekea huko Tanzania. Ni lazima nikamchukue mjukuu wangu” Bwana Brown alisema huku akionekana kuwa na furaha.
“Nami pia ninataka kwenda huko. Ninataka kumuona mjukuu wangu” Wayne aliwaambia.
“Wewe pumzika nyumbani. Tutakwambia kila kitu kitakachojili” Bwana Brown alimwambia Wayne.
Hakukuwa na cha kuchelewa, kwa haraka haraka viza zikaandaliwa na baada ya siku mbili safari ikaanza. Ndani ya ndege, Bwana Brown na mkewe, Bi Lydia walikuwa wakizungumzia kuhusu mtoto huyo ambaye walikuwa wakielekea kumuona nchini Tanzania.
Sala zao bado zilikuwa zikiendelea mioyo mwao kwa kumuomba Mungu awe Amemlinda mtoto yule mpaka katika kipindi ambacho watamchukua na kumpeleka kwa baba yake. Waliiona ndege ikienda kwa mwendo wa taratibu sana, walitamani wapotee kama wachawi na kujikuta ndani ya nyumba hiyo ambayo walikuwa wameelekezwa.
Mara baada ya ndege kutua katika uwanja wa Mwl Julius Nyerere, wakatoka nje ambako wakaomba kupelekwa katika ofisi za shirika la ndege la Precious Airlines na kukata tiketi ya ndege tayari kwa ajili ya kuelekea jijini Arusha.
Kutokana na kutokuwa na wasafiri wengi siku hiyo, wakapata ndege na saa tisa jioni safari ikaanza. Walichukua dakika arobaini na tano mpaka ndege kuanza kutua katika uwanja wa KIA ambapo wakaanza kuelekea katika moja ya hoteli ya nyota tano ya Jupiter iliyokuwa hapo Arusha.
Wakapata chumba na kutulia. Wakatoa ramani ambayo walikuwa wamechorewa na Wayne na kisha kuanza kuiangalia vizuri. Kila mmoja akaonekana kuridhika, ramani ya kuelekea nyumbani kwa Bi Selina ilionekana kueleweka vichwani mwao.
Siku iliyofuata asubuhi na mapema safari ya kuelekea nyumbani kwa shangazi yake Happy, Bi Selina ikaanza. Walikuwa wakiifuatilia ramani ile kama jinsi ilivyokuwa imeelekeza. Walipata tabu sana kutokana na nyumba nyingi kujengwa na hata mazingira kuwa tofauti sana, mwisho wa siku wakafanikiwa kuiona nyumba hiyo.
Wakaanza kuugonga mlango na baada ya muda fulani, mwanamke mmoja aliyekuwa na nywele zilizoanza kupatwa na mvi akafungua mlango, alikuwa Bi Selina. Wakajitambulisha kwake, wakaonekana kueleweka.
“Mmmhh!”
“Mbona umeguna?” Bwana Brown aliliza.
“Sidhani kama Happy atakubali kuonana nanyi” Bi Selina aliwaambia.
Hapo ndipo walipoanza safari ya kuelekea Machame. Njia nzima Bwana Brown na mkewe walikuwa wakijitahidi kuuliza maswali mengi kuhusu mjukuu wao lakini Bi Selina hakutaka kujibu chochote kile. Wakaingia ndani ya daladala, Bwana Brown hakujali kama alikuwa tajiri mkubwa, kitu ambacho alikuwa akikijali kwa wakati huo ni kumuona mjukuu wake tu.
Wakaanza kuingia katika eneo la nyumba ya mzee Lyimo. Bi Selina akaanza kuufuata mlango na kisha kuugonga, baada ya muda, Bi Vanessa akaufungua mlango ule. Wazungu ambao walikuwa wakionekana mbele yake hakuwa akiwafahamu lakini akaonekana kuhisi kitu fulani. Baada ya salamu, akawakaribisha ndani.
Maongezi yakaanzia hapo huku nae mzee Lyimo akiwa pembeni. Bwana Brown alijitahidi kujielezea kwamba alikuwa nani na alikuwa amefuata kitu gani mahali hapo. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa amemuelewa, walionekana kupinga kupita kawaida.
Kila walipokuwa wakikumbuka siku ambayo Wayne alikuwa amekuja hapo na kisha kuondoka kwa hasira mara baada ya kuambiwa kwamba Happy alikuwa mjauzito waliona hakukuwa na sababu za kuwakubalia ombi lao.
“Amechukua miaka sita na huu unakwenda kuwa mwaka wa saba, hajawahi kumjulia hali mtoto wake, mbaya zaidi alikataa mimba na kusema kwamba si ya kwake, iweje leo anakuja kudai mtoto? Hata kama ni mahakamani tutakwenda lakini Andy atabaki kuwa kwetu” Mzee Lyimo aliwaambia huku akionekana kukasirika.
Hapo ndipo Bwana Brown alipoanza kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimtokea katika maisha ya Wayne toka katika kipindi kile alichokuwa amepata ajali na kulazwa kitandani kwa muda wa miaka sita. Wote wakaonekana kushtuka, hasira ambazo walikuwa nazo zikaonekana kupotea.
“Hapo alipo hawezi hata kutembea. Na kamwe hatoweza kutembea katika maisha yake” Bwana Brown aliwaambia.
“Furaha pekee ambayo imebaki kwake ni kumuona mtoto wake tu. Nafikiri ataweza kufanya jambo lolote baya kama tu hatutarudi na kile ambacho amekitarajia” Bi Lydia aliwaambia.
Habari za kupata ajali kwa Wayne zikaonekana kuwa mpya kwao, ni kweli kwamba Wayne alikuwa ameikataa mimba ile lakini katika upande wao mwingine wa moyo walijua kwamba kama asingepata ajali basi angekuwa amekwishafika nyumbani hapo siku nyingi.
Alichokifanya Bi Vanessa ni kuinuka na kuelekea chumbani kwa Happy ambaye alikuwa amelala. Ile kuufungua mlango, Andy akatoka huku akikimbilia pale sebuleni na kumfuata mzee Lyimo na kuishika miguu yake.
“Babu atata mma” Andy alisema katika lafudhi ya kitoto.
Bwana Brown na mkewe hawakuamini mara macho yao yalipotua kwa Andy. Andy alikuwa amefanana kwa kila kitu na mtoto wao, Wayne. Wote wakaonekana kufarijika, wakajikuta wakitokwa na machozi ya furaha.
“Ndiye yeye. Mwangalie alivyofanana na baba yake” Bi Lydia alisema huku akitamani kumfuata Andy na kumkumbatia.
Wala hazikupita dakika nyingi, Happy akatokea sebuleni hapo akiongozana na mama yake. Macho yake yakatua kwa Bwana Brown na Bi Lydia ambao macho yao bado yalikuwa yakimwangalia Andy. Alichokifanya Happy ni kumfuata mtoto wake, Andy kumchukua na kumpakata.
Mazungumzo yakaanza upya, walielezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha ya Andy mara baada ya kuondoka nchini Tanzania na kuelekea nchini Marekani. Tofauti na matarajio yao, Happy alikuwa akitabasamu muda wote ambao alikuwa akielezewa kuhusu Wayne.
“Hayo ndio malipo. Hivyo ndivyo Mungu alivyotaka iwe. Andy ni mtoto asiyekuwa na baba. Nafikiri huyo Wayne ambaye amewatuma mje kumchukua si yule Wayne ambaye nini baba yake. Kama mlivyokuja na ndivyo ninavyotaka muondoke. Mtakapomuona, naomba mmwambie kwamba baba yake Andy alikwishafariki hata kabla Andy hajazaliwa. Mtakapoona haelewi naomba mmwambie kwamba Andy alifariki kwa ugonjwa wa Tete kuwanga ambao ulikuwa umemsumbua sana utotoni” Happy alisema.
Bila kutarajia, Happy akajikuta akianza kutokwa na machozi, uwepo wa Bwana Brown na mkewe ulionekana kumkumbusha mbali sana tangu kipindi cha kwanza ambacho alikutana na Andy. Kamwe hakutaka kumuona mwanaume huyo, alikuwa akimchukia kupita kiasi. Ilikuwa ni afadhali kukutana na shetani angempenda kuliko kukutana na mwanaume ambaye alikuwa ameikimbia mimba yake.
“SITAKI KUONANA NAE WALA MTOTO WANGU KWENDA POPOTE” Happy alisema na kisha kuingia chumbani kwake pamoja na mtoto wake, Andy.
Walijaribu kuugonga mlango lakini wala mlango haukufunguliwa. Bwana Brown na mkewe wakakaa mahali hapo huku wakimtaka mzee Lyimo na Bi Vanessa waongee na Happy lakini hilo nalo halikuwezekana kwani Happy alikuwa amejifungia mlango na wala hakukuwa na dalili za kuufungua.
“NIMESEMA SITAKI....SITAKI....SITAKI......SITAKI...”Sauti ya Happy ilisikika kwa nguvu masikioni mwao.

Je nini kitaendelea?
Je Happy ataendelea na msimamo wake huo?
Je uamuzi gani atauchukua Wayne baada ya kusikika kwamba Happy amekataa kumtoa mtoto?
Itaendelea.


Thursday, April 11, 2013

FACEBOOK CHATTIN (SEASON TWO) -------------1MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI.
MAHALI: DAR ES SALAAM.
SIMU: 0718 069 269

...
Unaikumbuka ile Season One niliyoandika kuhusiana mimi na msichana yule wa kishua? Leo hii nakuja na Season two ambayo itakuwa kali zaidi ya ile season one iliyopita. TWENDE PAMOJA.

Najisikia nimechoka sana huku laptop ikiwa mapajani mwangu na nimeunganisha na internet nikicheki updates za facebook, macho yangu yanakuwa mazito, natamani kulala lakini ghafla naliona jina, jina zuri la msichana mmoja hivi, jina la msichana ambaye nilikuwa namtaka kila siku toka kipindi kile alichokuwa akikaa mtaani kwetu. Ghafla uchovu wote ukanitoka, naanza kumwangalia, ndiye yeye, ndiye yeye kabisa kwani nilikuwa nimemtumia friend request jana tu, leo kanikubali kuwa rafiki yake, halafu yupo online.

Kwanza nasita kumpa hi, hii ni kwa sababu katika kipindi ambacho alikuwa akiishi mtaani kwetu, alikuwa akiringa sana kutokana na urembo wake, nilikuwa nimemtaka mahusiano ya kimapenzi zaidi ya mara saba, zote alinipiga mbavuni. Leo hii, huyu msichana Dorcas kanikubalia urafiki, lazima nianze upya mpaka anikubalie bila kujua mimi ndiye yule yule ambaye alikuwa akinikataa sana. Kwa kuwa katika kipindi hicho nilikuwa ninatumia a.k.a ya jina langu kama BROTHER PRINCE, hakuweza kunitambua. Ninamfuata na kumpa hi

MIMI: Mambo mrembo! (Nilimsalimia kwa kujiamini)
DORCAS: Poa. Mzima Brother?
MIMI: Nipo poa sana. Asante sana.
DORCAS: Asante ya nini tena? (Aliuliza huku nikiona kabisa swali lake dizaini kama lilikuja na tabasamu pana)
MIMI: Kwa kunikubalia urafiki. Nimefurahi sana.
DORCAS: Usijali Brother.

Kwanza hapo nikakaa kimya, sikujua ilitakiwa niendelee vipi na mawasiliano nae, kwa dakika kadhaa, vidole vyangu vikabaki kwenye keyboard ya laptop bila kuandika chochote kile. Kuna kitu nikatokea kukikumbuka, nikaona ngoja kwanza niende kuangalia picha zake.
Asikwambie mtu, alikuwa Dorcas yule yule, msichana ambaye alinifanya niwe kama chizi mtaani kwetu, msichana ambaye alinifanya niumwe na mbu sana vichochoroni, msichana ambaye alinifanya niwe namsubiria sana kumsindikiza shuleni kwao huku nikiwa radhi nichelewe shuleni kwetu.

MIMI: Dorcas......! (Niliita kwa mwandiko wa kioga)
DORCAS (Baada ya dakika mbili): Abeeee.
MIMI: Upo bize sana?
DORCAS: Sio sana. Ila kwa nini umeuliza hivyo?
MIMI: Nimeona nimekuandikia meseji halafu unanijibu baada ya dakika mbili kupita. Kweli haki hii jamani?
DORCAS:Samahani. Unajua ninachati na watu wengi ndio maana.
MIMI: Au kwa sababu mimi ni mgeni kwako?
DORCAS: Hapana jamaniiiii. Nisamehe basi.
MIMI: Usijali. Naweza kukuuliza swali moja la kizushi?
DORCAS: Swali gani?
MIMI: Lakini haujanijibu.
DORCAS: Sawa. Uliza.
MIMI: Unaishi wapi?
DORCAS: Jamani ndio swali gani tena hilo. Si kila kitu nimeandika kwenye profile langu uangalie.
MIMI: Ninatamani sana kufanya hivyo. Mtu anapouliza swali hili si kwamba siwezi kuangalia, hapana. Internet zetu kwa sisi tunaotumia simu huwa hazina kasi kabisa na ndio maana nimeona bora nikuulize tu.
DORCAS: Kwa hiyo hapo unatumia simu?
MIMI: Yeah! (Nilidanganya)
DORCAS: Mmmh!
MIMI: Mbona unaguna?
DORCAS:Nakuona online.
MIMI: Hilo si tatizo. Natumia Opera Min mpya. Naomba unijibu.
DORCAS: Naishi Magomeni.
MIMI: Ila si unafahamu kama ni kubwa sana.
DORCAS: Nipo Mapipa.
MIMI: Sawa. Nashukuru kwa kukufahamu. Naomba tuwe tunachati kila tunapokutana online.
DORCAS: Usijali. Karibu sana.
MIMI: Poa.
DORCAS: Na wewe unaishi wapi?
MIMI: Naishi Manzese Midizini (Nilidanganya kwani ningesema kweli, angehisi kitu).
DORCAS: Owkey. Unasoma?
MIMI: Nimekwishamaliza kidato cha sita (Nilidanganya tena)
DORCAS: Shule gani?”
MIMI: Makongo.
DORCAS: Hongera.
MIMI: Asante. Wewe unasoma?
DORCAS: Nasoma kidato cha tano ila mwezi wa pili mwishoni naingia kidato cha sita.
MIMI: Nawe hongera sana.
DORCAS: Asante. Naomba nikuulize swali jingine.
MIMI: Uliza tu.
DORCAS: Mbona haujaweka picha yoyote ile?

Swali hilo likanifanya kukaa kimya kwa muda fulani, halikuwa swali gumu kabisa na pia nilikuwa na picha nyingi sana kwenye mashine yangu ila yeye ndiye alikuwa miongoni mwa watu ambao sikutaka waone picha yangu yoyote ile. Kumbuka kwamba Dorcas nilikuwa nikimtaka toka alipokuwa akiishi mtaani kwetu Tandale, tena katika mara zote ambazo nilikuwa nikimtaka, alinikataa sana kiasi ambacho mpaka nikachoka. Leo hii Dorcas alikuwa hapa, ninachati nae moja kwa moja kupitia inbox. Sikuwa tayari kwa kipindi hicho kuweka picha zangu, nilitaka zibaki zile zile za wasanii wa Wamarekani.

DORCAS: Mbona kimya Brother?
MIMI: Sina picha. Ninatamani sana niweke picha ila tatizo simu yangu haina kamera. Ila usijali, ndani ya siku mbili, utaziona picha zangu.
DORCAS: Sawa. Nakwenda kulala. Tutachati kesho Brother Mungu akipenda.
MIMI: Mungu anapenda labda wewe usipende tu.
DORCAS: Hahaha!
MIMI: Huo ndio ukweli.
DORCAS: Basi sawa mimi nakwenda kulala.
MIMI: Usijali. Wape hi wote.
DORCAS: Wa kina nani?
MIMI: Utakaowaota.
DORCAS: Na kama nikikuota wewe?
MIMI: Nipe Hi tu. Ila kumbuka kwamba ukiniota, nami nitakuota, na kama tukiotana basi hiyo inamaanisha tumemisiana.
DORCAS: Hahaha! Una maneno Brother.
MIMI: Napenda kuongea tu. Ila usijali. Usiku mwema Dory.
DORCAS: Nawe pia (Akaenda offline)

Kuanzia hapo nikawa na amani. Muda wote nilikuwa nikishukuru sana kwa Mungu kwa sababu alikuwa amenipa uwezo mkubwa sana wa kuandika kiasi ambacho uwezo ule nilikuwa nautumia kwenye chatting kiasi ambacho ulionekana kuwa mzuri sana.
Huyu Dorcas nilikuwa namtaka sana, tena nilikuwa namtaka kuliko wasichana wote. Japokuwa zamani alikuwa akinikataa lakini nilikuwa nimekwishaapa kwa marafiki zangu kwamba ilikuwa ni lazima nimpate. Wengi walinicheka kidharau kwa kuniona najisumbua, hata alipohama nilichekwa sana kwa kuonwa kwamba sikuwa nimekamilisha lengo langu.
Leo hii, vita vya chini chini vimeanza, vita ambavyo sitotaka kuwaambia marafiki zangu mpaka pale ambapo ningekamilisha ‘mission’ yangu na kuwa nae. Hebu jifikirie kwanza, Dorcas angetoka vipi? Angeweza kuanzia wapi kunikataa na wakati nilikuwa na maneno mengi ya kuandika? Sikuona angetokea wapi, ila kama atanikubali, siku ya kuonana sijui ingekuaje kama atagundua kwamba ni mimi atafanyaje? Ila hiyo sio ishu, ishu kubwa ni kumfanya aangukie kimapenzi kwenye mikono yangu iliyo salama juu ya maisha yake......thats all.

MIMI: (Nikalog out na kulala huku nikisubiri kesho nianze pale nilipoishia)


Itaendelea kesho.

Tuesday, April 9, 2013

FACEBOOK CHATTING============== 5

 

 MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI.

MAHALI: DAR ES SALAAM.

SIMU: 0718 069 269
MSICHANA: Ndio najiandaa mpenzi. Unataka nivae mavazi gani?
MIMI: Vyovyote tu. Ila sipendelei kukuona ukivaa suruali.
MSICHANA: Kwa nini?
MIMI: Sina sababu.
MSICHANA: Basi usijali. Nitavaa gauni moja zuri sana ambazlo nilinunuliwa na baba katika moja ya maduka makubwa jijini New York. Nitakuja nalo huko.
MIMI: Poa. Wewe njoo tu mpenzi.
MSICHANA: Ili uwahi, naomba ufanye kitu kimoja.
MIMI: Kipi?
MSICHANA: Kodi bajaji na hela nitalipia mimi huku.
MIMI: Poa. Ila usiniingize choo cha kike.
MSICHANA: Usijali mpenzi.

Nikaanza kujiandaa kwa haraka sana, japokuwa toka nizaliwe sikuwahi kufika mapema sehemu ya appointment ila siku hiyo nilitaka kufika mapema sana. Nilipomaliza kujiandaa, nikaanza kwenda kwenye maegesho ya madereva wa mabajaji ambako nikamuita rafiki yangu ambaye alikuwa akiendesha bajaji moja.

MIMI: Sikiliza Moody, nataka unipeleke Slipway. Kiasi gani?
MOODY: Du! Unakwenda kufanya nini tena?
MIMI: Achana na hayo. Kiasi gani?
MOODY: Elfu kumi.
MIMI: Poa. Ila naomba tufanye kitu kimoja.
MOODY: Kitu gani?
MIMI: Tukifika kule, sema gharama ni shilingi elfu ishirini na tano. Umesikia?
MOODY: Poa. Kwani kuna mtu anakulipia?
MIMI: Yeah! Mtoto fulani wa kishua.
MOODY: Poa jembe. Ingia twende.

Nikaingia ndani ya bajaji na safari ya kuelekea Slipway kuanza. Ndani ya bajaji bado nilikuwa nikiendelea kuchati nae huku akiniambia kwamba amekwishafika na ni mimi tu ndiye nilikuwa nikisubiriwa.

MIMI: Sasa hiyo elfu ishirini na tano, yako elfu kumi na yangu elfu kumi na tano. Nitaifuata baadae nikitoka kuonana nae. Umenielewa?
MOODY: Du! Yaani hata hauniongezi kwa mchongo ninaoucheza?
MIMI: Nikuongeze nini hapo? Kwanza bei yenyewe tu umenibamiza. Halafu kama ningetaka si ningechukua daladala kwa nauli ya shilingi mia tatu na ningefika Msasani ningepiga kwa mguu mpaka Slipway.
MOODY: Dah! Poa bwana. Mara ya kwanza nilitaka kushangaa eti unakodi bajaji. Mtoto wa uswahilini akodi bajaji!
MIMI: Ndio hivyo bwana. Yaani hapa najiona kupata zali sana.

Safari ilikuwa ikiendelea zaidi na zaidi mpaka tulipofika Slipway. Gari nzuri na ya kifahari ilikuwa imepaki nje. Mara msichana yule akateremka. Nikajikuta nikianza kutetemeka kupita kawaida, sikuamini, sikuamini kama duniani kulikuwa na msichana mzuri namna ile. Nilibaki kimya nikimwangalia kwa mshangao. SI mimi tu, hata Moody alikuwa akionekana kushangaa. Uzuri wa msichana yule ulinishtua kupita kawaida.

MSICHANA: Vipi mpenzi?
MIMI: Poa
MSICHANA: Ngoja nimlipe dereva.

Akaanza kuisogeea bajaji na kisha kumlipa Moody gharama zake. Sikutaka kuzubaa, nami nikaelekea pale pale kuona anamlipa kiasi gani ili baadae Moody asije akanigeuka. Nikaona wekundu wawili na elfu tano wakitoka kwenye pochi yake, nikaona kwa ushahidi ule Moody asingeweza kunizika.
Tukatoka hapo na kuelekea ndani. Ingawa mule ndani kulikuwa na warembo wengi lakini mbele ya msichana yule wote walionekana kuwa si kitu. Tukatafuta sehemu na kukaa. Vinywaji na chakula vikaagizwa na kuanza kula.

MSICHANA: Tukitoka hapa nataka twende tukapumzike kwenye chumba chochote kile.
MIMI: Sawa. Ila jina lako hasa ni nani manake naona kwenye facebook unatumia jina la Precious Angel.
MSICHANA: Naitwa Angeline.
MIMI: Ok!

Tukala na kuanza kwenda katika sehemu iliyokuwa na vyumba na kuchukua chumba kimoja. Tulipoingia ndani, akaanza kuvua nguo zake na mimi kuvua zangu. Akajilaza kitandani huku akiniangalia kwa macho ya kurembua. Nami sikutaka kuchelewa, ninaanza kumsogelea. Nikaanza kumwangalia usoni.

GIDEON: Nyemo....Nyemo...Nyemo...amka.

Ilikuwa ni sauti ya kaka yangu ambayo ilikuwa ikisikika kwa mbali huku akiugonga mlango wa chumbani kwangu. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo nilivyozidi kuisikia sauti ile. Ghafla nikaamka kutoka usingizini. Mungu wangu! Kumbe matukio yote yale ambayo yalikuwa yakiendelea ilikuwa ni ndoto. Nikaamka, nikabaki kimya kitandani, sikuamini.

MIMI: Ndoto! Mungu wangu! Kumbe ilikuwa ndoto! Damn!

Nikasimama na kwenda kuufungua mlango wa chumbani kwangu, kaka yangu, Gideon alikuwa amesimama mlangoni. Nilikuwa nimechukia kupita kawaida.

GIDEON: Rafiki yako amekuja kukuulizia.
MIMI: Nani?
GIDEON: George Iron Mosenya
MIMI: Aaaggghhh! Kwa nini usingengoja hata kwa dakika moja.
GIDEON: Kuna nini?
MIMI: Dah! Nilikuwa chumbani. Tena kila kitu kikiwa kwenye hatua ya mwisho kaka.
GIDEON: Mbona sikuelewi.
MIMI: Naomba modem yangu kwanza.

Gideon akanipa modem yangu na kisha kuanza kurudi chumbani. Nikachukua laptop ambayo ilikuwa juu ya dressing table, nikaiwasha na kisha kuchomeka modem ile, nikaoganisha na internet na kufungua mtandao wa Facebook.

MIMI: Anaitwa Angeline.

Nikaanza kuwaangalia marafiki zangu wote huku nikimtafuta huyo msichana mwenye jina la Angeline. Sikuwa na rafiki huyo kabisa kitu kilichonipelekea kuanza kulitafuta. Majina yote yalikuja lakini hakukuwa na msichana yule, sura zao zilionekana kuwa tofauti kabisa na msichana yule mrembo. Sikutaka kuishia hapo, nikaanza kwenda kwenye akaunti zangu zote, twitter, myspace, beareshare, yahoo messenger lakini kote huko hakukuwa na msichana huyo.

MIMI: Mungu wangu! Kumbe alikuwa msichana wa ndoto! Kumbe nilikuwa nikiota. Ndoto....Ndoto! Kumbe ilikuwa ni ndoto! Nazichukia ndoto.

Nilijisemea huku nikionekana kukata tamaa. Sura ya msichana huyo bado itaendelea kubaki katika akili yangu, alikuwa ni msichana mzuri ambaye kila ninapowaangalia wasichana wote, hakukuwa na msichana ambaye alikuwa mzuri kama yeye. Miaka miwili imepita tangu niote ndoto hiyo lakini kamwe sura ya msichana huyo haikuweza kuondoka kichwani mwangu, nilikuwa namkumbuka kwa kila kitu. Nimejaribu kwa muda mrefu sana kumtafuta kwenye mtandao wa facebook lakini wala sijafanikiwa kumuona. Angeline....Angeline ataendelea kubaki kwenye akili yangu, nitaendelea kumkumbuka kila siku.

N:B. Hadithi hii ni ya kutunga, haihusiani na tukio lolote. Asanteni kwa kunifuatilia kutoka mwanzo hadi mwisho. Kama kweli ulitokea kuipenda hadithi hii, naomba uniambie kwa kutumia LIKE yako na kama una chochote cha kusema, unaweza kucomment pia.

MWISHO

Je umeifurahia na mwisho kukuchekesha?
Basi LIKE.

LIKE zikiwa nyingi kama 300. Kesho naanza na CACEBOOK CHATTING SEASON 2.

Monday, April 8, 2013

RIWAYA: PAINFUL TRUTH (UKWELI WENYE KUUMA)

 MTUNZI: Nyemo Chilongani

MAWASILIANO: 0718 06 92 69


SEHEMU YA TANO

Happy alionekana kuchanganyikiwa, hakuamini kama kweli Wayne alikuwa akitoka chumbani kwake huku akionekana kuwa na hasira mara tu alipothubutu kumwambia kuhusiana na ule ujauzito ambao alikuwa nao. Mshtuko mkubwa ukampata moyoni mwake hali iliyompelekea kuinuka pale kitandani na kuanza kumfuata Wayne.
Wayne alikuwa akitembea kwa mwendo wa haraka haraka, Happy akajitahidi kukimbia kumfuata huku akiita lakini Wayne hakugeuka nyuma. Happy hakutaka kuendelea kumfuata Wayne, akasimama na kisha kuanza kulia.
Tukio lile ambalo lilikuwa limetokea lilikuwa limemuumiza moyoni mwake zaidi ya tukio lolote ambalo liliwahi kutokea maishani mwake. Akaanza kupiga hatua kurudi nyumbani kwao, macho yake yalikuwa yakitoa machozi mfululizo.
Mama yake na shangazi yake wakaonekana kushangaa, hawakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea mpaka Wayne kutoka chumbani mule na kuondoka huku akionekana kubadilika. Hapo ndipo Happy alipoamua kuwaambia kile ambacho kilikuwa kimetokea.
“Yaani amekataa mimba yake?” Bi Vanessa aliuliza huku akionekana kushtuka.
Happy hakujibu kitu, bado alikuwa akiendelea kulia mfululizo. Alihisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa na ncha kali ambacho kilikuwa kimeuchoma moyo wake. Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya ili siku moja Wayne aamini kwamba mtoto yule alikuwa wake.
Happy akarudi chumbani na kujifungia, siku hiyo wala hakutaka kuongea na mtu yeyote yule, alikuwa akilia kwa uchungu. Kuna wakati alikuwa akinyamaza, ila kila alipokuwa akiliangalia tumbo lake, akaanza kulia zaidi na zaidi.
Mpaka katika kipindi ambacho mzee Lyimo alikuwa akitoka shambani na kuingia hapo nyumbani, bado Happy alikuwa amejifungia chumbani kwake. Alipopewa taarifa juu ya kilichoendelea, mzee Lyimo akaanza kupiga hatua kuufuata mlango wa kuingia chumbani kwa Happy.
Mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, akaanza kugonga lakini wala haukufunguliwa kitu ambacho kilimfanya kuanza kuliita jina la Happy huku akiendelea kugonga. Hazikupita hata dakika nyingi, Happy akafungua mlango na mzee Lyimo kuingia.
Macho ya Happy yalikuwa mekundu huku yakiwa yamevimba hali iliyoonyesha kwamba alikuwa amelia kwa muda mrefu sana. Mzee Lyimo akakaa kitandani na kuanza kuongea nae. Moyo wa mzee Lyimo ulimuuma zaidi, kamwe hakutarajia kama mzungu Wayne angeweza kuikataa mimba ile.
“Haiwezekani. Ameikataa?” Mzee Lyimo aliuliza huku akionekana kutokuamini.
“Ndio. Ameikataa” Happy alijibu.
Mzee Lyimo akasimama na kutoka nje ya chumba kile. Akauona mwili wake ukiwa umekufa ganzi kabisa. Hakuaamini kile ambacho alikuwa amekisikia kutoka kwa Happy, alitamani akutane na Wayne na kuongea nae ili aone kama alikuwa na ujasiri wa kuukataa ule ujauzito mbele ya macho yake.
Baada ya hapo, maisha ya Happy yakaendelea kama kawaida ingawa muda mwingi alikuwa akitawaliwa na huzuni. Alikuwa akijitahidi kula vyakula vizuri ambavyo vilikuwa vikimpa afya bora yeye pamoja na mtoto.
Mara kwa mara alikuwa akihudhuria kliniki kama ambavyo madaktari walivyotaka afanye. Kamwe hakulala katika kitanda kisichokuwa na neti, alikuwa akiyalinda maisha yake na ya mtoto wake ambaye alikuwa tumboni.
Ingawa ilikuwa ni vigumu sana lakini akaamua kujisahaulisha kuhusu Wayne, akaamua kuishi maisha yake peke yake, hakutamani kabisa kumuona Wayne mbele ya macho yake, alionekana kumchukia kuliko kiumbe chochote duniani.
Miezi tisa ikatimia na ndipo Happy akajifungulia shambani katika kipindi ambacho alikuwa akilima pamoja na wazazi wake hatua iliyowapelekea kumpeleka hospitalini.
Happy alikuwa amelala juu ya kitanda ndani ya chumba kimoja katika hospitali ya KCMC iliyokuwa Moshi mjini. Bado hakuwa ameongea kitu chochote kile. Dripu moja baada ya nyingine zilikuwa zikiingiza maji katika mishipa yake.
Happy alikuja kufumbua macho yake baada ya masaa nane kupita. Akayapeleka macho yake huku na kule, yakatua katika nyuso za wazazi wake. Tabasamu likaanza kuonekana usoni mwake. Mzee Lyimo na Bi Vanessa wakaanza kupiga hata kumfuata.
“Mtoto wangu yuko wapi?” Happy aliuliza kwa sauti ya chini.
“Kimaro. Tulikuja nae hapa. Amewekwa katika chumba maalumu” Mzee Lyimo alijibu.
“Silitaki jina hilo baba. Sitaki mtoto wangu aitwe Kimaro” Happy alisema kwa sauti ya chini.
“Sawa binti yangu. Unataka aitwe nani?”
“Aitwe Andy” Happy alijibu.
“Kwa hiyo aitwe Andy Wayne?”
“Hapana. Aitwe Andy Ryn. Hili ni jina la babu yake. Sitaki achukue jina la baba yake” Happy alisema.
Hicho ndicho kilichoamuliwa. Jina likawa limekwishapatikana. Baada ya siku mbili, Happy akaruhusiwa kurudi nyumbani. Kila wakati alikuwa pembeni ya mtoto wake, watu mitaani walikuwa wakishangaa namna mtoto yule alivyokuwa mweupe.
Afya yake ilikuwa bora hata zaidi ya watoto wengine ambao walikuwa wamezaliwa mitaani hapo. Happy alimthamini sana mtoto wake hata zaidi ya alivyojithamini yeye mwenye. Miezi ikakatika, Andy Ryn akaanza kujifunza kutembea.
Katika kila hatua ambayo alikuwa akiifikia, Happy alionekana kuwa na furaha. Ila kamwe hakuweza kumsahau Wayne kwani kadri alivyokuwa akimwangalia Andy, alifanana sana na baba yake. Mpaka katika kipindi hicho hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea katika maisha ya Wayne katika kipindi ambacho alikuwa ameondoka na kuelekea nchini Marekani.
Mwaka wa kwanza ukapita, wa pili ukaingia na kupita, Wayne hakuwa ameonekana kabisa mbele ya macho yake. Mwaka wa tatu ukaingia na kupita na mwaka wa nne kuingia. Hapo ndipo Happy akaamua kumuanzisha Andy katika shule ya chekechea iliyokuwa hapo Machame.
“Atakuwa na akili kama za mama yake” Happy alijisemea huku akimvarisha Andy nguo tayari kwa kumuanzisha shule.
Katika kipindi ambacho Happy alikuwa akiingia shuleni hapo pamoja na mtoto wake, walimu wote wakaonekana kushangaa, mtoto wa Happy alionekana kuwa tofauti kabisa. Alikuwa ni mzungu kwa asilimia themanini huku ishirini zilizobaki akiwa amechukua asili ya mama yake.
Andy akaanza kusoma katika shule hiyo. Kwa siku ya kwanza tu aliyofika shuleni hapo, uwezo wake ulijionyesha wazi. Ingawa alikuwa na umri mdogo lakini alikuwa na uwezo mkubwa sana kiasi ambacho kila mwalimu alikuwa akishangaa.
“Mmmh! Huyu mtoto ni wa maajabu nini?” Mwalimu Nuru alimuuliza mwalimu Leonila ambaye nae alikuwa akishangaa tu.
“Wala sijui. Ila uwezo wake unanishangaza sana. Nimewahi kufundisha watoto zaidi ya elfu tano katika shule hii, lakini mtoto huyu ameonekana kuwa wa kipekee sana” Mwalimu Leonila alimjibu mwalimu Nuru.
Mwaka wa tano na wa sita ukaingia. Andy akaanzishwa darasa la kwanza katika shule ya Machame Primary School. Kila mwanafunzi alikuwa akimshangaa, hawakuwahi kumuona mtoto wa kizungu akiwa anasoma katika shule kama ile.
Maswali mengi yalikuwa yakimiminika vichwani mwa walimu wa shule hiyo asili halisi ya mtoto huyo. Kila mmoja alikuwa akiongea lake. Mpaka amefikisha miaka sita, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifahamu kama Andy alikuwa mtoto wa Wayne ambaye alikuwa ameikataa mimba yake kipindi cha miaka sita iliyopita.
****
Ilikuwa ni taarifa mbaya ambayo ilikuwa imesikika masikioni mwa Bwana Brown na mkewe, Bi Lydia. Waliiangalia simu ile ya mezani ambayo ilikuwa imepigwa na kupewa taarifa ile ya ajali mbaya huku wakionekana kutokuyaamini masikio yao.
Wakaonekana kuchanganyikiwa, wote walijiona kuwa kwenye ndoto iliyojaa huzuni ambapo baada ya muda wangeshtuka kutoka usingizini na kumuona Wayne akiendelea kujiandaa na harusi pamoja na mchumba wake, Kristen.
Hiyo haikuwa ndoto, lilikuwa ni tukio halisi ambalo lilikuwa limetokea katika maisha yao. Walichokifanya ni kuondoka na kuelekea katika hospitali ya Jackson Heights ambayo walikuwa wameelekezwa iliyokuwa katika mji wa Albertson hapo hapo jijini New York.
Gari likafunga breki ndani ya eneo la hospitali ile, wote wakateremka na kuanza kuelekea ndani ya hospitali hiyo kubwa. Waandishi wengi wa habari walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kupiga picha na kuandika kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea kwani tukio lile la ajaili lilikuwa limegusa hisia za watu wengi nchini Marekani.
Bwana Brown na mkewe wakaingia ndani ya jengo lile huku wakipigwa picha na waandishi wale waliokusanyika katika eneo la hospitali ile. Breki ya kwanza ilikuwa ni nje ya chumba cha wagonjwa mahututi ambacho alikuwa amelazwa Wayne.
Wote wawili wakajikuta wakitokwa na machozi hasa mara baada ya kuuangalia mlango wa chumba kile kilichoonekana kutisha. Wakakaa vitini huku bado machozi yakiendelea kuwatoka. Walitakiwa kusubiri mahali hapo mpaka pale ambapo wangeruhusiwa kuingia ndani ya chumba hicho kwa ajili ya kumuona mtoto wao.
Masaa yalikatika lakini hakukuwa na yeyote ambaye alikuwa ameruhusiwa kuingia, nao hawakutaka kuondoka mahali hapo, waliendelea kusubiri zaidi na zaidi. Usiku ukaingia na hata asubuhi kufika lakini bado hawakuruhusiwa zaidi ya madaktari kupishana mlangoni.
Hali ya Wayne ilionekana kuwa mbaya kiasi ambacho akatolewa chumbani akiwa juu ya machela na kisha kuanza kupelekwa katika hospitali ya St’ Albert ambayo ilikuwa kubwa sana nchini Marekani. Hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuifuatilia machela ile huku Bi Lydia akilia kama mtoto.
Katika maisha yao walikuwa wamepitia katika hali ngumu sana lakini kwa wakati huo, hali hiyo ndio ilikuwa ikionekana kuwa ngumu zaidi katika maisha yao. Wayne akapakizwa ndani ya helkopta ya hospitali ile na kisha kuanza kupelekwa katika hospitali ya St’ Albert huku dripu zikining’inia.
Bwana Brown na mkewe, Bi Lydia wakaingia katika gari lao na kisha kuanza kuelekea katika hospitali hiyo iliyokuwa katika mji wa RockVile uliokuwa karibu na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa John F Kennedy.
Ni ndani ya dakika mia moja wakawa wamekwishafika katika eneo la hospitali hiyo. Wakateremka na kuanza kuingia ndani ya jengo la hospital hiyo. Kama kulia walikuwa wamelia sana na kama macho yao kuvimba yalikuwa yamevimba sana.
Miili yao ilikuwa ikitetemeka kupita kawaida, tayari hali ya wasiwasi ilikuwa imewashika, walikuwa wakiogopa kupita kawaida, waliona kwamba muda wowote ule wangeweza kumpoteza mtoto wao ambaye walikuwa wakimpenda sana hata zaidi ya walivyokuwa wakimpenda mtoto wao mwingine, Esther.
Mara baada ya oparesheni ya kuwekewa ngozi nyingine kufanyika ndani ya chumba maalumu na ndipo wakaruhusiwa kuingia ndani ya chumba kile. Hawakutakiwa kupiga kelele zozote zile kwa kuhofia kuleta matatizo mengine zaidi.
Wayne alikuwa kitandani kimya, dripu zilikuwa zikiendelea kuingiza maji mwilini mwake huku mashine ya hewa ya Oksijeni ikiwa imeziba mdomo na pua yake. Wote wakashindwa kuvumilia, hali ambayo ilionekana kwa mtoto wao ikaonekana kuwatisha, wakaanza kulia.
Hayo ndio yalikuwa maisha ya Wayne. Ajali ilionekana kubadili maisha yake kabisa. Ila kila siku wazazi wake walikuwa wakimshukuru Mungu kwa kumnusuru mtoto wao kutokana na Kristen kufariki pale pale. Wayne akaonekana kuwa na bahati katika maisha yake.
Miezi ilikatika lakini Wayne hakufumbua macho yake. Mwaka wa kwanza ukakatika, wa pili ukafuata. Mwaka wa tatu ukaingia, wa nne na hata wa tano ukaingia, bado alikuwa amefumba macho yake vile vile.
Mishipa yake ya fahamu ilikuwa imelegea sana kutokana na ajali ile kumletea matatizo na ilikuwa imechukua muda mrefu sana mpaka kukaa sawa. Waliamini kwamba ni lazima kuna siku Wayne angekuja kufumbua macho iwapo tu kama mishipa ile ya fahamu ingekaa sawa.
Kama kulia, wazazi wake walilia sana. Katika kipindi cha miaka mitano, kila siku walikuwa wakifika hospitali hapo huku wakiwa na mtoto wao, Esther ambaye alikuwa na majonzi zaidi ya wote. Maisha ya kitandani bado yalikuwa yakiendelea kwa Wayne.
Mwaka wa sita ukaingia na siku kumi na mbili, Wayne akayafumbua macho yake. Manesi hawakuamini kile ambacho walikuwa wamekiona, walichokifanya ni kwenda kumuita daktari ambaye alifika mahali hapo na kumwangalia Wayne.
“Glory to Almight God (Utukufu kwa Mungu Mkuu)” Dokta Carthebert alisema huku akiinyoosha mikono yake juu.
Walichokifanya ni kuwapigia simu wazazi wake ambao walifika mahali hapo huku wakiwa na furaha kupita kawaida. Kitendo cha mtoto wao kufumbua macho kilionekana kuwafurahisha kupita kawaida. Wakaanza kumshukuru Mungu kwa jambo kuu ambalo alikuwa amelifanya katika maisha ya mtoto wao, Wayne.
Japokuwa Wayne alikuwa amefumbua macho lakini hakuweza kuongea kitu chochote kile kitandani pale. Kumbukumbu zake zikaanza kurudi upya, akaanza kukumbuka kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea siku ile alipopata ajali.
Alitamani kuongea kitu lakini hakuweza kuufumbua mdomo wake kabisa. Miezi sita ikakatika na ndipo Wayne alipoanza kufumbua mdomo wake na kuanza kuongea. Madaktari wakaonekana kuwa na furaha, walichokifanya ni kuwapigia simu wazazi wake na kuwapa taarifa.
Bwana Brown na Bi Lydia wakafika hospitalini hapo huku wakionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Taarifa walizoambiwa kwamba Wayne alikuwa amefumbua mdomo wake na kuongea zilikuwa zimewapa faraja.
Wakaingia ndani ya chumba kile na macho yao kutua kwa mtoto wao, Wayne. Wote wakajikuta wakitoa tabasamu pana. Wayne alikuwa akiongea vitu fulani kwa sauti ya chini kabisa hali iliyomfanya Bwana Brown kumsogelea na kulipeleka sikio lake karibu na mdomo wa Wayne.
“Say something my son (Ongea kitu chochote kijana wangu)” Bwana Brown alisema huku akitabasamu.
“I want my kid....I want to see my kid (Ninamtaka mtoto wangu.... Ninataka kumuona mtoto wangu)” Wayne alisema maneno yaliyomfanya Bwana Brown kushangaa.


Je ni nini kitaendelea?
Je Wayne ataweza kumuona mtoto wake?
Je wazazi wataweza kufahamu Andy anamzungumzia mtoto yupi?
Itaendelea

RIWAYA: WASALIMIE KUZIMU---------------- 5


MTUNZI: Hussein Wamaywa

SIMU: 0755 697335


SEHEMU YA TANO

Kwa yakini hakuna, hakuna kwa maana ya watu wanaojua kupenda, natumai ushujua naongelea nini!” Akahitimisha. Nasra akatikisa kichwa kukubaliana nae. Akasema.
“Ni kweli uyasemayo baba. Saadan ana moyo wa peke yake! Lakini mimi…..” Akasita na kumtupia jicho baba yake. Alitaka kusema ‘simpendi kabisa!’ macho ya Alwatan Dafu ndiyo yaliyombadilihia uelekeo wa maongezi.
“Lakini mimi simjui fika! Nahitaji kumjua kwanza baba pengine inawezekana yeye akawa mbaya zaidi kuliko wote uliowataja. Inawezekana anajifanya Simba mwenda pole ili ale nyama! Huwezi kujua baba!”
“Inawezekana wala sio uongo, wala sikatai utabiri wako. Lakini pamoja na yote bado sijaelewa unataka kuniambia nini? Ujue sitaki kabisa kuusikia upuuzi wa Halfan!”
“Swali zuri Daddy! Nataka kwenda Oman kwa Saadan. Nikakae walau mwezi mmoja, miwili au miattu! Nione hali halisi ya maisha ya kule, nimjue vilivyo, naamini nikirudi hapa nitakuwa nimerejea na tarehe ya harusi!”
“Good Nasra. Ndio sababu nakupenda Nasra. Wewe ni msichana wa ajabu. Ninajivunia hilo, I love you Nasra!” Baba Nasra akishangilia kwa vigelegele “Sasa umeamua jambo la busara kuliko yote uliyowahi kuamua katika maisha yako!” Akainuka na kuingia ndani, akarudi na vitabu vitatu vyenye majalada ya plastiki.
“Hizi ni Passport zenu aliniachia Saadan siku chache kabla ya kuondoka. Ni wewe tu kuamua uondoke lini! Sawa mwanangu? Juu ya nauli usiofu aliacha fedha za kutosha tu.
“Sawa baba, lakini naomba kitu kimoja tu ukifanya hicho utanihakikishia ni kiasi gani unanipenda na kunithamini.
“Kuwa huru na usema unachotaka.”
“Ni juu ya Halfan!” Alwatan akakunja uso.
“Najua ni kiasi gani ninakukera na kukuudhi kila ninapotaja jina hili. Lakini baba wewe ni mtu mzima sasa. Na ugomvi wako na yeye ulishamiri wakati ule nilipomkataa Saadan, lakini sasa nimeshamkubali! Sioni kama kuna haja ya ugomvi tena. Halafu ujue hata kama mimba ile iliingia kwa bahati mbaya, lakini ndo tayari watoto wameshazaliwa na hatuwezi kuwaangamiza au kumsusIa!
Hivyo tutake tusitake tumeshaunga undugu na Halfan, ingawa ninaolewa kwingine! Ingawa nitakuwa nimeolewa tayari; Halfan kama Halfan ataendelea kuwa mzazi mwenzangu forever! Na wewe lazima umuheshimu kama mkweo! Kama Saadan.
Naomba upunguze chuki dhidi yake na ikiwezekana muondoleane uhasama baina yenu. Please baba, temeni mate chini Shetani apite!
Alwatan Dafu akafikiria kwa muda na kushusha pumzi. “Nitafikiria ‘I mean’ nitajitahidi kufanya uliyoinambia. Hakuna haja ya uhasama, aghalabu maelewano huwa ni bora zaidi kuliko mifarakano. Nitajitahidi mwanangu!”
“Good baba! Very Good!” Ikawa zamu ya Nasra kufurahi.
“Sasa unaweza kwenda kazini baba, nakutakia kazi njema yenye afya, furaha na bashasha!” Nasra akahitimisha kwa kumkumbatia na kumbusu baba yake.
“Na wewe pia, nakutakia mapumziko mema hapa nyumabni unatarajia kuondoka lini?”
“Nafikiri wiki ijayo, lakini natarajia kushauriana na mama juu ya siku nzuri ya kuondoka!” Akajibu wakiachiana. Alwatan Dafu akienda kazini. Nasra akirudi chumbani kwake!”
Kwisha kazi yake! Kila mmoja kwa upande wake aliwaza hivyo. Walikuwa wamewezana! Hawakurofautiana sana na ile hadithi ya mjanja mjanjuzi.
Chumbani hakukukalika. Nasra akatoka mbio mpaka kwa mama yake, akafika anamkumbatia kwa nguvu huku machozi ya furaha yakimtoka “Thank you mama, Thank you. Nashukuru sana kwa ushauri wako mzuri”
“Enhe nipe habari mwanangu, mambo yamekwendaje?”
“Imekuwa rahisi nisivyotegemea, yaani kama kumsukuma Mlevi vile!” akamueleza mama yake kila kitu. Mama mtu akabaki mdomo wazi kwa ujasiri wa mwanae.
“Sasa …?” Alikuwa mama Nasra “Sasa unaweza kufanya mambo yako taratibu kabisa bila usumbufu wowote ule!” Baadae walipanga tarehe ya safari kuwa ingekuwa wiki mbili zijazo.
Jioni Dafu aliporudi akapewa habari hizo na kuzidi kufurahia. Siku zikasogea. Na kadiri muda ulivyozidi ndivyo hali ya Romota, mtoto mdogo wa Nasra ; pacha wa Promota ilivyozidi kuwa mbaya kiafya.
Walimpeleka hospitali hii na ile bila mafanikio. Siku ya safari ilipowadia bado hali ya Romota ilikuwa haijakaa sawa. Wakaiahirisha na kumpigia simu Saadan na kumueleza sababu za kuiahirisha safari ya Nasra.
Miezi michache baadae hali ya Romota ilizorota zaidi, ikawa mbaya kupindukia, hatimaye akafariki dunia. Nasra alilia mno kumlilia mwanae kiasi cha kupoteza fahamu mara kadhaa.
Habari za msiba wa mototo wa Nasra zilitambaa na kufika mbali zaidi. Siku mbili baadae watu walikuwa wamefurika nyumbani kwao. Saadan nae alikuwepo.
Wakazika na kumaliza matanga. Siku chache za kumfariji mfiwa zikakatika. Hatimaye Nasra akakubali kuwa kazi ya mungu haina makosa. Miezi michache baadae waliondoka na Saadan pamoja na Promota na kuelekea Omani!
Ilikuwa safari ndefu na ya ajabu kwa Nasra ambaye hakuwahi kupanda ndege kabla. Alijifunza mengi na vingi njiani. Mpaka wanafika Oman, tayari alishaelimika vya kutosha!


* * *
Husemwa na kuimbwa kwamba mtaka cha uvunguni sharti ainame, mwombaji sharti mikono iwe nyuma na pengine haraka haraka haina baraka.
Misemo nahau na methali zinazokwenda sambamba na ile ya subra yavuta kheri huleta kilicho mbali, ilitumika haswa kutekeleza matakwa ya Nasra Alwatan Dafu.
Badala ya mwezi mmoja au miwili aliyokuwa ameipangilia, aliishi miezi mingi zaidi. Na ili kuweka mazingira mazuri ya kuondoa mizengwe, kauzibe na ukuta katika mioyo ya ndugu wa Saadan, Nasra na Saadan walikubaliana kumfanya Promota kuwa mtoto wa Saadan.
Ingawa rangi na matendo ya Promota vilikuwa beni beni na hali ya Saadan, Nasra na Saadan walijitia hawalioni hilo. Ndugu nao hali kadhalika, wengine wakadai kitanda hakizai haramu!
Saadan aliyekuwa mcha-Mungu kupindukia, aliwasha ngaza daadhi ya ndugu zake pale alipokubali kuwa ‘alimuingilia’ Nasra bila kufunga ndoa. Na mara zote alipoulizwa ni kwa nini alifanya hivyo, jibu lake lilikuwa moja tu, “Ibilisi jamani!”
Wengi kama siyo wote walimpokea Nasra vizuri. Na baadhi walikuwa wacheshi kama yeye mwenyewe. Na vile lugha ya kiarabu Nasra aliifahamu vizuri, hakuwa na shida katika mawasiliano.
Ajabu ni kwamba kwa kipindi chote alichokuwa Oman, Nasra hakumruhusu Saadan kuukurubia katika mwili wake.
Lakini vitendo vidogo vidogo kama kuiruhusu miili yao ikaribiane, kukumbatiana na pia kubusiana; Nasra alishindwa kuvizuia na kumruhusu Saadan afanye hivyo mara nyingi tu katika mwili wake.
Noor, mtoto wa kiume anayemfuata Saadan ndiye kidogo aliyeonekana kutokubaliana na ulaghai kwamba Promota alikuwa mtoto wa kaka yake. Yeye alitamka wazi kuwa Saadan amepigwa bao la kisigino na wabongo!
Huyu alikuwa kero kwao lakini kwa kuwa familia nzima ilimuona kama ambaye hajatulia, hakuna aliyezitilia maanani kauli zake ambazo zilikuwa kama msumari wa moto katika donda bichi la moyo wa Saadan.
Hali hii na lile la kupigwa marufuku asiusogelee mkate wa siagi wa Nasra, vilimuathiri sana. Lakini kwa vile moyo wake ulishatua kwa Nasra, na wenyewe wanasema ‘muhitaji ni khanithi;’ Saadan aliyameza haya kwa machungu makali na maumivu yasiyo na mfano.
Hatimaye siku ilifika, siku ya kuondoka kwa Nasra. Ilikuwa siku ngumu kwa Saadan ambaye moyo wake ulikuwa ukipata faraja kumuona Nasra pembeni yake kila wakati.
Wakiwa Air port pamwe na ndugu zao, Saadan alishindwa kabisa kuyazuia machozi yaliyotiririka mashavuni baada ya kufanya vurugu za mwaka katika macho yake. Hili likamgusa Nasra.
Akamchukua Saadan na kusogea nae pembeni. Huku naye machozi ambayo nilishindwa kung’amua mara moja kuwa ni ya furaha au uchungu yakimtoka;
Akamkumbatia kwa nguvu na kwa mara ya kwanza akampiga busu la kinywa. “Saadan! Naamini unanipenda mimi kuliko kitu kingine chochote. Na ninataka kukuahidi kitu kimoja. Kwamba amini sasa Nasra bint Dafu ataolewa na Saadan peke yake!
Kujizuia na kuzizuia tamaa za mwili wako kwangu ingawa mara nyingi tumeondakea kupewa ‘one room’, juu ya kitanda kimoja tukiwa kama bibi na bwana harusi mtarajiwa, kumenifanya niamini kwamba upendo wako kwangu haumaananishi tamaa za kimwili tu;
Bali umekwenda mbali zaidi. Ndivyo mapenzi ya kweli yanavyotakiwa kuwa! Umenionyesha kwamba unanipenda kwa dhati. Sioni kwa nini nisikupe tumaini. Nakupenda Saadan!” Nasra alinong’ona taratibu akiwa juu ya kifua cha Saadan. Saadan akafarijika. Kwa kila hali ilikuwa habari njema kwake.
Akafaulu kufuta machozi na kubaki akimtazama Nasra kwa matamanio. “Sasa kama unalitambua hilo ni kwa nini basi unasita nisilete washenga kwenu waje kuulipa mahari uwe wangu wa milele, tutenganishwe na kifo?”
“Sisiti kwa nia mbaya dia, mambo mazuri hayataki haraka. Fanya taratibu, pole pole. Utaona matokeo yake na unaweza kuona mambo yanakuwa vipi!
Mara ya kwanza nilikwambia nitakuja Oman. Na tayari nimetiza ahadi! Hiyo pekee inatosha kukuonyesha kwamba Nasra sio mtu wa kupoteza miadi! Ni mtu ambaye akiahidi anatimiza.
Naelewa kwamba ahadi ni deni na shuruti uitimize. Amini ahadi niliyotoa kwako itatimia. Jambo la muhimu ni subira tu hata hivyo nataka unihakikishie kwamba mdogo wako Noor hatambughudhi mwanangu endapo tutafunga ndoa!”
“Nakuahidi hatombughuddhi! Tone moja la damu kamwe haliwezi kuchafua maji ya mto au bahari. Nitamdhibiti istoshe ndugu wote wanamjua kuwa hajatulia.”
“No! tena hao wasiotulia ndio wabaya kwa kuumbuana. Maana akishtukia ishu tu, hakai kimya. Bahati nzuri au mbaya watu hawa wasiotulia hufikia wakati wakatoa mawazo ambayo waliotulia hushindwa hata kuyafikilia wachilia mbali kuyatoa. Mfano kama hili sio siri kanifanya nionekane Malaya na tapeli!”
“Usifadhaike mpenzi! Nakuahidi tutaishi raha mustarehe!”
Wakaachana pale wasafiri waliposikia tangazo lililowahitaji kuingia ndani ya ndege upesi Nasra akawaaga ‘wifi’ zake, ‘shemeji zake’ ‘wakwe zake’ na hata marafiki zake.
Akawaacha na nyuso zilizojaa simanzi na huzuri, akavuta hatua kuijongelea ndege mwanae Promota akiwa kifuani mwake Naam! Dakika kumi baadae alikuwa hewani.

* * *
Watu waliojitokeza kumpokea nyumbani Tanzania walikuwa wachache sana. Baba yake, mama yake na wafanyakazi wao kadhaa wa ndani. Pengine waliokuwa wageni ni washiriki wenzake wa Miss Temeke Academia ambao walishika nafasi ya pili na ya tatu.
Labda kilichomfurahisha ni kile kitendo cha wazazi wake kuja kumpokea na gari yake ya ushindi Caddilac. Wakajipakia garini na msafara wa kuelekea nyumbani kwa Alwatan Dafu ikaanza.
Nyumbani kwao kulikuwa na sherehe kubwa ikimsubiri. Nusura Nasra aanguke kwa Mshutuko alioupata. Akajumuika na wenzake wakasherehekea kurudi kwake. Wakala kunywa na kucheza muziki.
Sherehe ilipokwisha washiriki wenzake wa urembo waliondoka na kumuacha jioni akiteta na wazazi wake, ambao walikuwa wanahitaji kusikia mengi kutoka kwake.
Kwanza aliwaoongopea mengi kuhusu Saadan na Oman na mipango yao ya ndoa ambayo ilipangwa kufanyika mwaka mmoja baadae. Halafu akahitimisha kwa kuwapa zawadi zao alizotoka nazo ukweni.
Alwatan Dafu alikaribia kupasua kwa furaha. “Kwa nini mipango yenu ya ndoa mmeiweka mbali hivyo?” Alwatan akashindwa kujizuia.
“Kusomana baba, unajua Kusomana tabia sio kazi ndogo. Ni kazi isiyohitaji papara ili maamuzi yatakayofikiwa yasijekuwa na majuto baadae. Ni vizuri kufikiri kabla ya kutenda.”
“Sasa mnasomanaje na hali mko beni beni kama mbingu na ardhi? Mmoja Afrika, mwingine Asia! Inawezekana kweli?!”
Kwa nini isiwezekane baba? Huu ni mwanzo tu kuna wakati yeye atakuja huku na tutaishi kwa kipindi furani. Na kuna wakati tunaweza kusafiri na kwenda kuishi nje. Tutafanya mambo kadiri tutavyoona. Subira tu ndiyo inayohitajika.
“Oke! Whatever you like, I’m ready to listen you! (vyovyote mpendavyo ninawasikiliza nyie!)
“Good Baba! Ninajivunia kuwa wewe ni baba yangu!” kauli hii ilimuacha Alwatan Dafu akitabasamu, kabla hajambusu mwanae na kumtakia usiku mwema. Kisha akaingia ndani kulala.
Akawaacha mtu na mama yake wakiteta kwa nafasi. Hapo ndipo Nasra alipomueleza mama yake ukweli halisi ulivyo, vile alivyohisi na mipango yake ya baadae ambayo ilikuwa tofauti na mbali kabisa na Saadan.
“Mh! Mtoto una hatari wewe! Haki ya Mungu sijaona!” Mama yake akasema kwa kicheko mwisho wa maelezo ya Nasra. “Nataka kumuonyesha baba kuwa yeye akiujua huu, wenzie tunaujua ule.
Naomba nikushukuru tu kwa vile wazo lako la kwenda Oman limeniweka huru. Na tena ninaamini kuwa sasa nitaweza kuitumia Caddilac yangu. Naomba unifanye mpango wa kuipata kadi yake! Akaomba.
“Nitakufanyia mwanangu! Iko katika droo ya baba yako. Kumbuka furaha yangu inakuja pale unapokuwa na furaha nitakupatia!“ Na kweli alimpatia siku mbili zilizofuata.
“Thanks mama! I won’t stop loving you!” Nasra akashukuru wakati akiipokea kadi hiyo. Akiwa na funguo na kadi ile tena sasa akiwa na uhuru wa kufanya atakalo na kwenda atakako tena katika wakati atakao (isipokuwa usiku) Nasra alijihisi kama aliyetua mzigo mzito baada ya kazi ngumu! Alifurahia kuona akimiliki gari yake mwenyewe.
Ni hapo alipoamua kumpeleka mwanae katika shule za awali. Na taratibu ubongo wa Promota, mwanae pekee aliyesalia, ukaanza kunolewa…


***NASRA anaendelea na mkakati wake babkubwa....kimya kimya bila mzee wake kujua...SAADAN amedanganyika anahisi anapendwa kweli....
nini kitafuata???

ITAENDELEA KESHO

FACEBOOK CHATTING------- 4

MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI.

MAHALI: DAR ES SALAAM.

SIMU: 0718 069 269
MSICHANA: Tayari.
MIMI: Safi sana. Itegeshe mike ya Hearphone yako karibu na mdomo. Ipe mikono yako uhuru. Wakati mwingine, unaweza kufumba macho. Itulize akili yako kabisa, achana na kufikiri mambo mengine. Isikilize sauti yangu kwa makini, nitakwenda kuongea maneno mengi, yanayotakiwa kufanya na wewe, fanya kama nitakavyokwambia. Hakikisha umelala chali. Umesikia mpenzi.
MSICHANA: (Huku sauti yake ikianza kubadilika na kuwa ya chini) Sawa.
MIMI: Tunakwenda kuanza mchezo huu. Mchezo huu utaanzia mwilini mwako, nitakwenda kuitembelea kila sehemu yako ya mwili. Kumbuka kwamba mikono yako ndio mimi kwa sasa. Hakuna maswali, tulia na niache nifanye kazi yangu.
MSICHANA: Sawa mpenzi.
MIMI: Tunakwenda kuanza mchezo wetu. Tunaanzia kifuani kushuka chini.
MSICHANA; Sawa.

Kuanzia hapo, mchezo ulivyochezwa hautoweza kuelezwa sana kwa sababu ya matumizi ya facebook kutumiwa hadi na watoto walio chini ya miaka 18. Usiulize maswali wala usibishe. Kuna watoto wengi huku mtaani kwetu ambao ni marafiki zangu na wote wanaisoma post hii. Sitoelezea sana mchezo huu kwani sitotaka kuiharibu saikolojia yao, ufahamu nilio nao kwenye mchezo huu acha ubaki kuwa wangu tu, sitaki kuibiwa maujuzi kabisa. Kila mtu anatakiwa kuucheza mchezo huu kwa kutumia ujuzi wake na si kuiba ujuzi kutoka kwangu kwani unaweza kumuua hata binti wa watu na kuniletea matatizo.

NB: Watoto wengi, sehemu hiyo inakatishwa kidogo na wala haitoelezewa kwa kina.


Mchezo uliendelea zaidi na zaidi, kila wakati nilikuwa namsikia akipumua kwa nguvu huku akilalamikalalamika. Bado nilikuwa nikiendelea kama kawaida. Dakika kumi zikapita, niliendelea kuongea nae, dakika ishirini zikapita, nusu saa na hadi saa moja, bado alikuwa akilalamikalalamika tu.

MSICHANA: Stooooooooooopppppp (Aliitoa sauti yake kimahaba)
MIMI: Nini tena?
MSICHANA: Stooooooopppp mpenzi. Aaaaggggghhhhh! Naomba nipumzike.
MIMI: Mbona unaomba kupumzika tena na wakati bado masaa kama matatu hivi?
MSICHANA: Utaniua. Nimeshindwa kujizuia mpenzi.
MIMI: Poleeeee
MSICHANA: Asante. Ngoja nikaoge kwanza.
MIMI: Vipi tena?
MSICHANA: Umenichafua.
MIMI: Hahahaha! Nimekuchafua au umejichafua?
MSICHANA: Umenichafua. Haukumbuki ulisema uwe mikono yangu?
MIMI: Ok! Nimekuelewa. Ukitoka huko naomba ulale. Mimi mwenyewe nimejichafua pia. Nakwenda kuoga, sitokuwa na nguvu ya kuendelea. Acha nilale kwanza mpaka kesho. Usiku mwema.
MSICHANA: Nawe mpia mpenzi (Bado sauti yake ilikuwa ikisikika kimahaba)

Nikabaki nikicheka sana, sikuamini kama msichana yule hakutaka kuendelea kuucheza mchezo ule na wakati ndio kwanza tulikuwa tumetumia dakika sitini tu. Nikaenda kuoga na kisha kurudi kitandani. Sikutaka kuwasha simu yangu kwani nilijua kwa namna moja au nyingine angenitafuta tu.
Kesho, nikaanza kuelekea chuoni. Akili yangu nikaituliza huku ikionekana kama kutokukumbuka kitu chote kilichotokea. Saa tano na nusu nikawasha simu yangu na kukutana na meseji zake tano.

MSICHANA: *Usiku wa jana umekuwa usiku wa kukumbuka sana kwangu.
*Nilikuwa nikilalamika mpaka mama akasikia na kuamua kuja chumbani kwangu. Sijui amejua nilichokuwa nimekifanya kwani asubuhi alikuwa akiniangalia kwa jicho la wasiwasi sana.
* Kama mchezo wenyewe upo vile, sijui itakuwaje. Unaonekana kuwa mchezo mzuri lakini uliojaa hatari.
* Ingawa niliwahi kuucheza mchezo ule lakini jana ilikuwa balaa. Yaani kama ni mpira basi nimekutana na timu inayokimbiza muda wote.
* Mbona upo kimya mpenzi? Naomba ukizipokea meseji hizi nijibu chochote ili niwe na furaha. Leo sijaenda shule kabisa kwa kuogopa kutokuelewa darasani. Nimesingizia naumwa. Yote kwa ajili yako. Nakupenda mpenzi. Nakupenda My Only Nyemo.

Nilibaki nikicheka sana. Msichana ambaye ilikuwa imepita siku moja tu tangu tuanze uhusiano wa kimapenzi alikuwa amechanganyikiwa sana. Mahusiano yetu yakawa yamechangamka sana kana kwamba yalikuwa yameanza miezi sita iliyopita.

MIMI: Usijali mpenzi. Mchezo ule unahitaji sana maandalizi. Wengi wanashindwa kuucheza kwa sababu tu huwa wanakurupuka. Mimi kama mimi huwa ninakwenda hatua kwa hatua mpaka mwisho. Najiamini, ninafanya kazi zangu kwa uhakika mpenzi.
MSICHANA: Una tabia mbaya sana. Mbona haukunijibu toka asubuhi nilipokutumia meseji zile?
MIMI: Nilikuwa darasani baby. Hadi hapa bado nipo darasani.
MSICHANA: Umejifunza wapi mchezo ule?
MIMI: Nyumbani.
MSICHANA: Mmmh! Una hatari wewe!
MIMI: Hatari ya nini tena?
MSICHANA: Ungeweza kuniua last night. Yaani kuna kipindi nilikuwa naona viungo vyote vikiishiwa nguvu.
MIMI: Poleeeee
MSICHANA: Asante mpenzi.
MIMI: Naomba leo tucheze tena.
MSICHANA: Sitaki. Sitaki tena kucheza, utaniua jamani. Jana nilikuwa nahema juu juu kama nakata roho vile.
MIMI: Polee sana. Ila ndio ukubwa huo.
MSICHANA: Au ulitaka kunitoa usichana wangu?
MIMI: Kwani unao?
MSICHANA: Ndio
MIMI: Mmmh! Kweli hatari. Unanishangaza sana.
MSICHANA: Kwa nini?
MIMI: Ulidumu na mpenzi wako kwa muda gani?
MSICHANA: Kwa miaka miwili.
MIMI: Hamkufanya kitu chochote kile?
MSICHANA: Ndio.
MIMI: Alikuwa na chembechembe za ushoga nini?
MSICHANA: Hahahaha! Kwa nini unasema hivyo?
MIMI: Inawezekana. Miaka miwili halafu kimya. Haiwezekani, kuna jambo hapo nyuma ya pazia.
MSICHANA: Inawezekana.
MIMI: Hivi una miaka mingapi?
MSICHANA: Kumi na nane.
MIMI: Hahahaha! Unafaa kuliwa wewe. Umeshaiva mpenzi. Inabidi nikutungue kutoka mtini. Umeiva vizuri kabisa.
MSICHANA: Hahahaha! Una maneno wewe
MIMI: Hayo ndio maneno tunayopenda kuyatumia huku kwetu. Miaka kumi na nane mkubwa sana, tena sana. Kama ungekuwa huku kwetu ungekuwa unatafutiwa mume.
MSICHANA: Ningekuwa natafutiwa mume?
MIMI: Ndio. Tungekuwa tunakula pilau sasa hivi.
MSICHANA: Hahahaha! Sawa bwana. Ila inakubidi uwe na shabaha ya kulitungua tunda lililoiva.
MIMI: Shabaha ninayo tena kubwa sana. Nikiona kama nakukosa, nitakupandia uko uko mtini. Hahahaha!
MSICHANA: Una visa sana Mpenzi.
MIMI: Usijali. Lecturer anaingia. Kama vipi tutaendelea kuchati baadae.
MSICHANA: Poa. Nakupenda mpenzi.
MIMI: Nakupenda pia.

Msichana yule alionekana kuwa msumbufu sana, muda wote alikuwa akinitumia meseji za mapenzi lakini sikumjibu hata moja, muda wote nilikuwa nikimfuatilia lecturer alivyokuwa akifundisha. Muda wa kutoka ulipofika, sikutaka kumshtua, nikarudi nyumbani na kujilaza kitandani.

MIMI: Nipo nyumbani.
MSICHANA: Namshukuru Mungu umerudi nyumbani salama. Kuna kitu nilikuwa nakifikiria mpenzi.
MIMI: Kitu gani?
MSICHANA: Unaonaje tukionana somewhere?
MIMI: Lini?
MSICHANA: kesho.
MIMI: Haitowezekana kabisa.
MSICHANA: Kwa nini mpenzi?
MIMI: Labda tufanye weekend.
MSICHANA: Okey! Ila naomba tuonane mpenzi.
MIMI: Usijali.

Baada ya hapo, mawasiliano yalikuwa yakiendelea kila siku, alitamani sana kuonana nami lakini nilikuwa bize sana mpaka pale ilipofika weekeend ambapo tulipanga sehemu ya kukutania.

MIMI: Umesema wapi?
MSICHANA: Slipway.
MIMI: Du! Sipajui bwana.
MSICHANA: Acha kunitania mpenzi. Ila usijali, nitakuelekeza.
MIMI: Poa.

Baada ya hapo akaanza kunielekeza. Si kwamba nilikuwa sipajui kweli Slipway ila kwa wakati huu nilikuwa nikitaka kucheza na akili yake tu. Nilitaka afahamu kwamba mimi nilikuwa mtoto wa uswahilini na hata sehemu nyingi za kuenjoy hasa za watu waliokuwa na uwezo fulani nilikuwa sina uhitaji wa kupafahamu.
Nikafikiria kwa haraka haraka, sehemu ile ilikuwa haiendeki kwa daladala hivyo kama ningependa daladala ya Msasani na kwenda huko, ungekuwa mwendo mrefu kidogo. Sikuonekana kujali, kukutana na msichana wangu ndicho kitu pekee ambacho nilikuwa nikikihitaji.
Asubuhi ya Jumamosi tukaanza kuchati kwa sms hata kabla hatujaonana.Itaendelea

Sunday, April 7, 2013

RIWAYA: PAINFUL TRUTH (UKWELI WENYE KUUMA)============ 4

 

MTUNZI: Nyemo Chilongani

MAWASILIANO: 0718 06 92 69


SEHEMU YA NNE

Maisha ya Happy hayakuwa na furaha tena hali iliyompelekea kuondoka nyumbani kwa shangazi yake na kurudi nyumbani kwao Machame. Kichwa chake kilikuwa kikifikiria kuhusu mimba ambayo alikuwa nayo, hakujua ni kitu gani ambacho angekifanya mpaka kuanza kuwaeleza wazazi wake kuhusiana na mimba ile.
Moyo wake ulikuwa ukimuuma, akaanza kumchukia Wayne ambaye alikuwa amempa ujauzito ule na kisha kuondoka kurudi nchini Marekani. Alijiona kuwa mpweke, akakosa amani kabisa.
Mpaka katika kipindi ambacho alikuwa akiingia nyumbani kwao, Happy alikuwa akilia tu. Wazazi wake, Mzee Lyimo na Bi Vanessa wakabaki wakimshangaa Happy, hawakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikimliza binti yao katika kipindi hicho.
Kila walipojaribu kumuuliza Happy kitu ambacho kilikuwa kimetokea, alikuwa kimya, hakutaka kuwaambia wazazi wake kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika kipindi ambacho alikuwa jijini Arusha. Alibaki kimya, siri ya kwamba alikuwa mjauzito ikabakia moyoni mwake.
Siku zikakatika mpaka katika kipindi ambacho matokeo ya kidato cha nne yalipotangazwa. Happy alikuwa amefanya vizuri sana zaidi ya wanafunzi wote wa Machame Girls Secondary School. Matokeo hayo yaliinua furaha kwa wazazi wake,
Kitu kilichowashangaza ni pale walipompa Happy matokeo yale. Badala ya Happy kuwa na furaha hata zaidi ya wao waliyokuwa nayo, akaanza kulia kwa uchungu. Kitendo kile kikaonekana kuwashangaza wazazi wake jambo ambalo liliwapelekea kumuuliza sababu ilikuwa nini. Happy hakutaka kuongea kitu chochote kile, tayari wazzi wake wakajua kwamba kulikuwa na tatizo limetokea.
“Kaongee nae. Nadhani ana tatizo” Mzee Lyimo alimwabia mkewe.
Bi Vanessa hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kuanza kuelekea chumbani kwa Happy na kuanza kuongea nae. Alichukua saa moja kuongea nae lakini Happy hakuwa tayari kuufungua mdomo kueleza ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea.
Bi Vanessa alitumia ujuzi wake wote na hatimae Happy kumwambia ukweli. Bi Vanessa akaonekana kama mtu aliyechanganyikiwa, hakuonekana kuyaamini maneno yale, alimwangalia binti yake mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini.
“Una mimba?” Bi Vanessa aliuliza huku akionekana kutokuamini.
“Ndio” Happy aijibu huku akiangalia chini.
“Ya nani?”
“Wayne”
“Ndiye nani?”
“Mvulana mmoja hivi”
“Anakaa wapi? Hapa hapa Machame au Arusha?” Bi Vanessa aliuliza.
“Anakaa Marekani”
“Marekani!”
“Ndio”
Bi Vanessa hakutaka kubaki ndani ya chumba hicho, alichokifanya ni kutoka na kisha kwenda kumwambia mumewe, mzee Lyimo.
Mzee Lyimo akaonekana kuchanganyikiwa, hasira zikaanza kumshika, akaanza kuondoka kumfuata Happy chumbani kwake. Alipoingia tu, akajikuta hasira zake zote zikipotea haa mara baada ya kuyaona machozi ya Happy ambayo yalikuwa yakimtoka mfululizo.
Mzee Lyimo akaanza kupiga hatua kumfuata Happy pale kitandani alipokuwa na kisha kukaa karibu nae. Moyo wake ukaonekana kuumia, alijua kwamba alitumia kiasi kikubwa sana cha fedha kumsomesha Happy mpaka kufikia hatua hiyo ambayo alikuwa mefikia, kupata ujauzito hata kabla hajaendelea na masomo kulionekana kumuumiza.
Alijua fika kwamba kumchapa Happy au kumfukuza nyumbani isingekuwa suluhisho la kile ambacho kilikuwa kimetokea, aliona kuwa na umuhimu wa kuwa pamoja na Happy na kumfariji katika hali ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho.
“Wayne ndiye nani?” Mzee Lyimo aliuliza japokuwa alikuwa ameambiwa kila kitu na mkewe.
“Mwanaume kutoka Marekani” Happy alijibu.
“Ni mzungu?”
“Ndio” Happy alijibu.
Mzee Lyimo akaonekana kukosa nguvu, alichokifanya ni kuinuka mahali hapo na kwenda nje. Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, kupata ujauzito kwa Happy kulionekana kumnyima furaha kabisa.
Huo ndio ukawa mwisho wa Happy kusoma, hakuendelea tena na elimu, akawa msichana wa kukaa nyumbani na kuwasaidia wazazi wake kazi mbalimbali hasa shambani. Miezi ilikuwa ikiendelea kukatika, Happy alikuwa akiutunza ujauzito wake huku wazazi wake wakimpa kila msaada ambao alikuwa akiuhitaji.
Dalili zote za kuwa mjamzito zikaanza kuonekana, akaanza kutapika mfululizo huku akipoteza hamu ya kula. Muda mwingi alikuwa akijisikia uchovu hali iliyompelekea kulala. Mpaka miezi mitano inatimia, hali ya ujauzito ikaanza kuonekana waziwazi.
Happy alikuwa amelala chumbani kwake huku pembeni yake kukiwa na maembe mabichi pamoja na udongo. Hivyo ndivyo vilikuwa vitu ambavyo alikuwa akipenda sana kuvitumia kila siku. Mara mama yake akaingia chumbani humo, uso wake ulikuwa umejaa tabaamu pana.
Maswali mfululizo yakaanza kujikusanya kichwani mwa Happy, hakujua sababu iliympelekea mama yake kuwa na tabasamu namna ile. Akainuka kitandani na kukaa. Mama yake akaja na kukaa pembeni yake huku tabasamu likiendelea kuonekana usoni mwake.
“Kuna nini?” Happy aliuliza.
“Amekuja” Bi Vanessa alijibu.
“Nani?”
“Wayne. Yupo nje anakusubiri” Bi Vanessa alimwambia Happy.
Badala ya kuonyesha furaha, Happy akaanza kutokwa na machozi. Hali ile ilionekana kumshangaza mama yake ambaye akaamua kuanza kumbembeleza. Alipoona Happy amenyamaza, akatoka chumbani mule na moja kwa moja kwenda kumuita Wayne ambaye alikuwa nje ya nyumba lle.
Ni ndani ya sekunde kumi tu, mlang wa chubani ukafunguliwa na Wayne kuingia ndani. Usowa Wayne ukaonekana kuwa na furaha mara baada ya kumuona Happy kwa mara nyingine tena. Huku akionekana kuwa na tabaamu pana, akakaa kitandani pale.
Happy akashindwa kuvumilia, akajikuta akimsogelea Wayne na kumkumbatia kwa furaha huku machozi yakiendelea kumtoka. Wayne akaipitisha mikono yake na kumkumbatia. Walikaa katika hali hiyo kwa dakika mbili, Wayne akayapeleka macho yake usoni mwa Happy, akaonekana kufarijika.
“Nimekukumbuka mpenzi” Wayne alimwambia Happy.
“Nimekukumbuka pia” Happy alijibu.
Furaha ya Wayne ikaonekana kurudi moyoni mwake, tayari alikuwa amekwishasahau kama alikuwa amemuacha Kristen hotelini. Alikaa pamoja na Happy kwa muda wa masaa mawili na ndipo walipoanza kupiga stori.
“Mbona ulikimbia chumbani siku ile?” Wayne alimuuliza Happy.
“Nilikuwa nikiogopa, kuna kitu nilikuwa nimekikumbuka” Happy alijibu.
“Kitu gani?”
“Kwamba nilikuwa katika siku zangu za kupata mimba” Happy alitoa jibu ambalo likaonekana kumshtua Wayne.
“Unasemaje?”
“Nilikuwa katika siku zangu za kupata mimba. Hapa unaponiona, nina ujauzito wako” Happy alimwambia Wayne.
Wayne akaonekana kushtuka, akamwangalia vizuri Happy, akaipandisha blauzi ambayo alikuwa ameivaa na kisha kuliangalia tumbolake, aliona mabadiliko makubwa lakini cha ajabu katika kipindi ambacho alikuwa akifanya nae mapenzi hakuyaona mabadilko hayo.
Wayne akaonekana kubadilika, wasiwasi ukaanza kuonekana machoni mwake, hakuamini kama alikuwa amempa ujauzito msichana wa kiafrika, akamwangalia Happy huku dhahiri uso wake ukionekana kuukataa ujauzito ule.
Wayne akainuka, akaanza kuvaa nguo zake na kuufungua mlango, kilichoendelea mahali hapo ni kuondoka huku akiwa kama mtu aliyechanganyikiwa. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kukifanya, moyo wake haukuwa tayari kukubali kama alikuwa amempa mimba msichana wa Kiafrika.
“Haiwezekani. Ile sio mimba yangu. Siwezi kumpa mimba msichana wa Kiafrika” Wayne alisema katika kipindi ambacho alikuwa akielekea kituoni huku akiwaacha watu nyumbani pale wakiwa hawaelewi ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea ndani ya chumba kile.
Wayne alifika hotelini baada ya saa moja. Kristen alikuwa na wasiwasi akimsubiri. Japokuwa Kristen alionekana kuwa na wasiwasi lakini hakuuliza kitu chochote kile. Tayari Wayne alikuwa amebadilika, uso wake ukaonekana kuwa na hasira kupita kawaida, kitendo cha kumpa mimba msichana wa Kiafrika kilionekana kumuumiza.
“Kuna nini?” Kristen alijikuta akiuliza.
“Tuondoke. Inatupasa turudi nyumbani haraka iwezekanavyo” Wayne alimwambia Kristen.
“Unasemaje? Mbona ni maamuzi ya haraka namna hiyo?”
“Ndio hivyo. Nakuomba usiulize kitu Kristen. Nimechanganyikiwa baada ya kusikia kwamba marafiki zangu kutoka Uingereza wameelekea Marekani tayari kwa kuhudhuria harusi yetu” Wayne alidanganya.
“Harusi gani? Mbona unaonekana kama umechanganyikiwa?”
“Ni lazima tufunge harusi haraka iwezekanavyo. Huo ni uamuzi ambao nimejiwekea. Najua ni uamuzi ulioamuliwa kwa haraka sana. Haina jinsi mpenzi. Wiki ijayo ni lazima tufunge ndoa” Wayne alimwambia Kristen.
Ni kweli. Ulikuwa ni uamuzi wa haraka sana, Wayne alionekana kuchanganyikiwa. Taarifa za ujauzito ambazo alikuwa amepewa zilionekana kumchanganganya kupita kawaida. Siku mbili zilizofuata, wakasafiri na kurudi tena nchini Marekani ambako huko mipango ya harusi ikaanza kufanyika.
Kila kitu kilikuwa kimepangwa kwa haraka haraka sana hali ambayo ilikuwa ikimshangaza kila mtu. Vyombo vya habari vikaanza kutangaza harusi kubwa ambayo ilitarajiwa kufanyika wiki ijayo. Kila mtu akawa na hamu ya kuiangalia harusi hiyo kwenye televisheni.
“Ni bora nioe ili nimsahau Happy. Haiwezekani kuzaa na msichana wa Kiafrika” Wayne alisema.
Kitu walichokifanya ni kuanza safari ya kuelekea Elmon, mji mdogo uliokuwa pembeni mwa jiji la New York kwa ajili ya kuwaona babu na bibi wa mchumba wake, Kristen kwa ajili ya kuwapa taarifa kile ambacho kilikuwa kinataka kutokea.
Ndani ya gari walikuwa wawili tu, Wayne na Kristen. Wayne ndiye ambaye alikuwa ameshikilia usukani, alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi sana kwani alihitaji wafike katika mji huo haraka iwezekanavyo.
Bado kichwa chake hakikuwa sawa, muda wote alikuwa akimfikiria Happy na ujauzito ule ambao alikuwa nao. Mara kwa mara alikuwa akipiga usukani ule kuonyesha ni kwa jinsi gani alikuwa amechanganyikiwa.
“Happy.....haiwezekani...” Wayne alijikuta akisema kwa sauti kubwa iliyosikiwa na Kristen.
“Umesemaje?” Kristen aliuliza.
“Nini?” Wayne nae aliuliza.
“Nimekusikia umeongea kitu”
“Kitu gani?” Wayne aliuliza.
Bado Wayne alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi hadi kutokukiona kibao ambacho kilimtaka kuendesha gari kwa mwendo wa taratibu kutokana na matengenezo ya barabara. Ghafla, mbele yake akaona gari kubwa likichimba barabara ile huku mainjiania wakitoa malelekezo kwa dereva wa gari lile kubwa la kutengeneza barabara.
Kutokana na mwendo mkali ambao walikuwa nao, ikawa ngumu kufunga breki na gari kusimama. Gari lao ambalo lilikuwa katika mwendo wa kasi likalivamia gari lile kubwa lililokuwa likitengeneza barabara.
Mlio mkubwa ukasikika, Kristen akarushwa kutoka ndani ya gari mpaka nje na kukibamiza kichwa chake katika chuma kikubwa cha gari lile lililokuwa likitengeneza barabara ile. Na Wayne akarushwa mpaka nje, akaburuzika katika marabara ile, sehemu kubwa ya ngozi yake tumboni ikabaki barabarani.
Ilikuwa ni ajali kubwa ambayo wala haikuwa na moyo kuitazama. Gari lao lilikuwa limebondeka, milango ya mbele haikuwa ikionekana kabisa, yaani gari lilikuwa limebaki nusu tu kuanzia milango ya nyuma.

Je nini kitaendelea?
Je huo ndio mwisho wa Kristen na Wayne?
Je nini kitaendelea katika maisha ya Happy?
Itaendelea.

Recent Posts