Wednesday, December 12, 2012

SITAISAHAU facebook------ 16


MTUNZI: Emmy John P.

MAWASILIANO: 0654 960040

SEHEMU YA KUMI NA SITA

...
Ule ujumbe ulioonekana katika akaunti yangu, ulinishtua sana. Sasa sikuwa na ujanja tena nikafikia hatua ya kukubali kuwa yamenishinda na ninatakiwa kumshirikisha mtu mzigo huu.
Kitu cha kwanza niliiondoa akaunti yangu ya facebook katika matumizi ‘deactivation’. Sikuhitaji tena kuwa katika mtandao huo. Baada ya hatua hiyo nikaandika barua ya kuomba ruhusa ya kutofanya mitihani hiyo iliyokuwa mbele yangu pale chuoni.
Kwa kuwa nilikuwa nafahamika sikupata usumbufu nikapewa ruhusa hiyo upesi. Nikaamua kufunga safari kuelekea nyumbani. Lengo kuu likiwa kumueleza mama kila kitu kilichonitokea na kutishia uhai wangu. Sikuwa na ujanja mwingine.
Usiku nilikuwa nimetingwa katika kujiandaa. Ni Maria pekee ambaye nilimueleza kuwa nitasafiri, na wakati huo alikuwa akinisaidia kufungasha mabegi yangu. Tayari kwa siku inayofuata.
Ilikuwa saa sita kasoro dakika kadhaa. Nilitulia nikamtazama Maria na yeye akanitazama mimi. Kisha kila mmoja akageuka na kutilia maanani kile kinachosikika. Mlango ulikuwa unagongwa.
Hakika ni palepale katika nyumba yangu niliyokuwa naishi.
Nani huyu muda huu? Nilimuuliza Maria kana kwamba yeye alikuwa anamfahamu aliyepo mlangoni.
Maria hakuwa na cha kunijibu.

Nikiwa nimemshika mkono Maria tuliufikia malango, tukaulizia ni nani? Hakujibu. Tukauliza tena!! Kimyaa!!
Kila mmoja akamshikia mwenzake kwa nguvu sana!!
Ghafla mlango ukabamizwa kwa nguvu sana.
Mungu wangu!! Watakuwa majambazi! Nilihisi.
Kabla sijajua nini cha kufanya, mlango ulisukumwa bila kutoa kelele ukafunguka.
Waaa!!
Ghafla pakawa giza. Nikasukumwa kando na mikono ya baridi sana. Nikajaribu kupiga kelele sauti haikutoka. Nikajaribu tena sikuweza kabisa. Kisha nikasikia mlio mkubwa. Kisha kama gunia la mahindi kitu kikatua chini huku kikipiga kelele. Ilikuwa sauti ya Maria.
Kama vile haitoshi nikashikwa tena na yule mtu mwenye mikono ya baridi. Akaanza kuniburuza. Moja kwa moja hadi chumbani kwangu.
Akaninyanyua akanitupa kitandani.
Nikajaribu tena kupiga kelele sauti haikutoka.
Mara taa ikawashwa!! Chumba kikang’ara.
Ana kwa ana na mtu ninayemfahamu!!
Ni yule niliyemuandikia barua ya kuomba kuacha kazi!!
Dokta Davis mbele yangu!!
Alikuwa amevalia suti nyeupe. Na hakuwa akitabasamu!!
Nikajaribu kuzungumza, sikuweza!! Akacheka, nikamsikia.

“Isabela……” aliponiita, nikajaribu kuitika sauti ikatoka.
Maajabu haya!!
“Milioni thelathini, mama yako mzazi, ama wewe!” alinieleza kwa utaratibu.
Sikumuelewa. Nadhani hata yeye aliitambua hali hiyo.
“Ni hivi..hadi sasa umetumia shilingi hizo…sasa unatakiwa kabla sikjaweka saini yangu katika barua yako kuhalalisha wewe kuacha kazi nahitaji ufanye maamuzi. Nakupa wiki moja tu!! Uwe umerejesha pesa hizo, ama mama yako akae mbali nawe maisha yako yote na mwisho ni uchaguzi ujitoe wewe kwa usiku mmoja!!”
“Usiku mmoja?” nilijiuliza. Ikawa tena kama ananisikia.
“Usiku mmoja wewe na mimi na kisha nitakuacha huru na uamuzi wako wa kuamua kuacha kazi. Ole wako umueleze mtu…nitachukua maamuzi ambayo hautaamini”
Sikuamini kama maneno hayo yanatoka kinywani mwa mtu huyu. Na ameweza vipi kufika Tanzania bila kunieleza. Mbaya zaidi amekuja nyumbani kwangu usiku mnene.
Kabla sijamjibu lolote. Alizima taa. Kisha nikasikia mlango unafungwa. Nikaendelea kutulia kama nilivyo huku naogopa.
Nilidhani yupo jirani na eneo lile. Sikuthubutu kusimama. Baada ya dakika kadhaa nikasikia hatua zikijongea kuja katika mlango wa chumba changu.
Anarudi! Niliwaza nikaendelea kutulia. Jasho likilowanisha shuka zangu.
Taa ikawashwa. Kwa ncha za macho nikamtazama aliyepo mbele yangu. Alikuwa ni Maria. Uso wake ukiwa umevimba.
“Bela…nimeanguka mwenzako.” Alianza kunieleza. Nikageuka kumtazama huku nikipatwa na hisia za kumwoga.
“Mh!! Mbona hivyo Bela. Kimekusibu nini?” aliniuliza.
Sikuwa na cha kumjibu. Nilibaki kushangaa. Maana niliamini na yeye amemuona dokta Davis lakini hakuonekana kujua lolote.
Nilitamani sana kumueleza lakini hofu ya onyo la Dokta ilinitawala. Maria akanisogelea akanikumbatia. Nikahesabu alama kadhaa za vidole katika shavu lake. Huenda kabla ya kuanguka alipigwa kofi.

Siku iliyofuata nilitakiwa kusafiri. Maria aliwahi sana kuniamsha lakini sikuwa na uwezo tena wa kusafiri. Onyo la Davis kuwa iwapo nitamwambia mtu yeyote atafanya anachojua.
Niliunda sababu kadhaa nikafanikiwa kumshawishi Maria kuachana na safari hiyo. Alishangaa lakini hakuwa na jinsi maana msafiri nilikuwa ni mimi.
Siku ya pili hiyo zikasalia siku tano Dokta afanye yake aliyoyaahidi.
Bado sikuwa nimepata jibu sahihi la kumpa. Milioni alizonitajia kwa kweli sikuwa nazo hata nusu yake. Kumuondoa mama yangu katika uso wa dunia ni jambo ambalo sikutaka kulisikia.
Kulala na mimi usiku mzima. Lilikuwa ni sawa na tukio la kubakwa kwa hiari. Udhalilishaji!!
Nikajilaani kumuamini sana Davis. Majuto yakaninyanyasa.

Bila kumuaga Maria, niliamua kutoweka pale nyumbani kwangu na kwenda kupanga katika nyumba ya kulala wageni. Maeneo ya Igoma.
Nilizima simu yangu! Siku zikazidi kukatika na sasa ilikuwa imesalia siku moja ya mimi kutamka jibu langu.

Nikaiwasha simu yangu!! Nikaitafuta namba ya Davis. Nikafungua sehemu ya ujumbe nikamtumia.
USIKU MMOJA MIMI NA WEWE. Nitakueleza wapi nipo uje!!

Ujumbe ukapokelewa! Lakini haukujibiwa!!

****

Siku ya tukio ikafika!! Nilikuwa najaribu kumpigia simu Dokta huyu wa maajabu nimuelekeze wapi nipo lakini simu yake haikuwa inapatikana. Nilijaribu tena na tena bado hali ilikuwa ileile.
Hofu ikanitawala! Huenda Davis ameamua kufanya anachojua yeye. Vipi kama ameamua kumtokomeza mama yangu!! Nilianza kulia baada ya kufikiria hayo.
Nikiwa katika kulia simu ya chumbani ilianza kuita.
Nikaitazama kisha nikaipokea.
“Kuna mgeni wako..”
“Mgeni?”
“Anaitwa Davis.” Sauti ya muhudumu ilinijibu.

Kulisikia jina hilo tu. Nikakurupuka kutoka kitan]dani bila kujua ni wapi ninakimbilia. Nilikuwa naogopa sana jambo ambalo lilikuwa linakuja mbele yangu. Kufanya mapenzi bila hiari na kiumbe cha ajabu sana.
Haya yote niliyataka mwenyewe!! Sasa nikaanza kuhisi kuwa Davis hakuwa mtu mzuri kwangu!!
Davis ni MCHAWI!!!
Naenda kufanya mapenzi na mchawi!!
Ghafla nikaijiwa na kumbukumbuku za chapa ya shetani 666, niulipokumbuka hili nikakumbuka na mshahara wangu ulikuwa una hizi namba, hata simu ya Osmani nayo ina 666, Davis aliwahi kunitumia nauli nayo ilikuwa na 666 na sasa nipo katika chumba namba 66 namsubiri huyu mfalme wa 666
Hapana! Hapana! Niliipinga nafsi yangu. Na sasa nilikuwa nimeamua kumkimbia mchawi huyu. Kuikimbia chapa ya shetani!!!
Nikiwa najiandaa kukimbia
.Mlango ukafunguliwa!!!

NANI AMEUFUNGUA MLANGO!!!
JE ISABELA ATAIKIMBIA CHAPA HII 666.
Kama akiikimbia je ndo anaruhusu MAMA YAKE afe!! NANI KAMA MAMA???

ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Recent Posts