MTUNZI: EmmyJohn Pearson
MAWASILIANO: 0654 960040
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
...
Mayowe yakatawala, akinamama wakiwa wamesahau watoto wao na wanaume nao
wakiwasahau wake zao sasa kila mmoja alikuwa akiipigania nafsi yake.
Sikuwa katika umoja na akina Jesca tena! Hapa sasa kila mwenye macho
hakungoja kuambiwa tazama!!
Makaburi yale mawili yaliendelea kufuka ule moshi wa rangi ya dhahabu.
Wenyeji wa kijiji kile walikuwa katika taharuki kubwa sana huku wakizungumzia juu ya kukasirika kwa mizimu.
Nani sasa aliyeikasirisha? Walijiuliza.
Vilio vilisikika tena kutokea gizani. Watu wakakimbilia huko.
Waliporejea ilikuwa taarifa ya mama mmoja aliyekuwa anakimbia
ameshambuliwa na kitu kisichofahamika na hatamaniki tena. Amekufa!!
Hali ikatulia kwa muda. Akajitokeza mzee mmoja wa makamo akitembea kwa kutumia mkongojo.
Huyu hakuogopeshwa hata kidogo na hali iliyokuwa inaendelea. Alisimama
mbele ya kunndi na kuanza kusema anachokifahamu, alielezea historia fupi
ya makaburi ya Kiyeyeu na majanga yanayotokea iwapo wazee wale
waliolala katika makaburi yale wakikerwa na jambo. Hapa sasa akafikia
kusema kuwa kuna mtu mmoja katika msafara alikuwa ameikasilisha mizimu!!
Ni lazima abaki ili kuwanusuru wenzake. Kama akiendelea mbele basi
litatokea balaa kubwa zaidi ya hili. Alizungumza kwa sauti ya juu na
kila mmoja aliweza kusikia. Sauti yake na umri wake vilikuwa vitu viwili
tofauti!!
“Hivyo kama unajua una lolote la kuikera mizimu hii ni
heri ubaki nyuma kuwanusuru wenzako.” Alizungumza kisha akatuachia
mtihani wa kuamua aidha kujitokeza ama la!
Maneno yake niliamini
kabisa yalikuwa yanamlenga John. Nilijisikia uchungu sana, John
alitakiwa kubaki nyuma. Yaani harakati zangu zote hizo zinaishia hapa!!
Niliumia sana.
Niliangaza huku na huko. Sikumuona John!! Nilitaka kumuita lakini niliamini kuwa hawezi kunisikia.
Kimya kilitawala akisubiriwa mtu huyo ambaye ameikera mizimu aweze kujitoa kundini. Hakuna aliyejitokeza.
Mzee akaendelea kusubiri!! Bado hakujitokeza mtu yeyote.
Kimya kilikatishwa na sauti ya mwanaume akipiga mayowe. Tukageuka nyuma
kumtazama. Alikuwa amejishika shingo yake huku akipiga kelele. Mara
damu zikaanza kumtoka puani, masikioni na mdomoni. Badala ya kumsaidia
kila mtu akawa anamuogopa!!
Hatimaye akaanguka na kutulia tuli! Alikuwa amekata roho!!
Kina mama wakapiga kelele sana, wanaume wakabaki kushangaa.
Yule mzee wa kimila akaipaza tena sauti yake, “Kama asipojitokeza mtu huyu majanga yataongezeka. Mizimu inakasirika.”
Sasa watu wakaanza kusemezana huku wakisisitizana kuwa mtu huyu
ajitokeze ili mizimu itulie. Bado hakuweza kujitokeza mtu yeyote.
Zikaanza kutolewa hirizi miilini mwa watu, lakini yule mzee wa kimila akapinga kuwa hizo ndio tatizo.
Waliokuwa na dawa za kienyeji wakatoa. Bado haikuwa tiba.
Kiza kinene kikatanda kama dalili ya mvua. Mwanga mkali ukamulika bila kutoa kelele. Watu watatu wakasalimia na ardhi.
Ilikuwa radi!! Na walikuwa maiti tayari.
Roho ikaniuma sana, nikajiona mimi ndiye muhusika. Nikatamani John
atokezee nimtangaze kuwa ndiye chanzo. Lakini John hakuwepo tena!!
Vile vifo vya radi ya ghafla vilimshtua kidogo yule mzee.
Mara akabadilika sura na kuwa kama aliyekasirika!!
Akatoa amri ya watu kujipanga msitari. Amri ikasikilizwa. Wanaume na
wanawake mstari mmoja, mistari ilipopangwa ndipo nilimuona John. Na yeye
alikuwa amepanga mstari. Akaanza kupita na kufanya kile anachokijua
mwenyewe. Alimfikia John, na yeye akamuona akamshika mkono. Ina maana
John anaonekana? Nilijiuliza.
Nikiwa katika hali ya mashaka ya
kila kinachoendelea. Mara yule mzee mkongwe alinifikia, alikuwa
anatabasamu, mgongo wake uliopinda ulimfanya awe ameinama na kuwa mfupi
sana!!
“Shkamoo babu.” Nilimsalimia.
“Marahaba mjukuu wangu.” Alinijibu kwa ukarimu sana.
Kisha akanishika mkono.
Alipofanya hivyo kwa wasafiri wengine hakutumia muda mrefu, lakini kwangu ni kama alitumia sekunde nyingi.
“Unaitwa nani binti.”
“Isabela!!”
“Nani alikwambia unaitwa Isabela.” Aliniuliza huku akinitazama usoni.
“Naitwa Isabela mzee.” Nilitaharuki kutokana na maswali ya mzee huyu.
“Hilo sio jina lako binti.”
“Sio jina langu?”
“Na litakugharimu sana na kuwaumikza wengine katika maisha yako.” Kauli nzito za mzee huyu zilinishangaza.
Isabela sio jina langu? Ni miaka zaidi ya ishirini tangu nipewe jina
hilo. Sasa leo ananiambia kuwa hilo sio jina langu? Maajabu haya.
“Hautaendelea na safari hii…kuwaepusha wenzako na mabalaa yasiyowahusu.”
Alininong’oneza. Nikahisi ubaridi ukinipenya mwilini, mapigo ya moyo
yakapungua kasi. Nikakata tamaa.
Mimi tena? Sio John!! Maajabu haya.
“Kama unao upendo waruhusu wenzako waende zao. Janga lako haliwahusu
hata kidogo.” Alinisihi. Nikatikisa kichwa kukubali. Huku nikiamini kwa
asilimia kadhaa kuwa tatizo ni John na yule mzee hajui kitu.
Mzee
akawatangazia watu kuwa tatizo limekwisha. Na kweli nilipokubali tu
waondoke zao. Nilipogeuka makaburini. Ule ukungu haukuwepo tena.
Abiria wakaingia katika basi lile la ziada lililokuja kutuchukua.
Tofauti na mawazo yangu. Kuwa John atazuia basi lisiondoke baada ya
yeye pia kuwa mmoja kati ya abiria. Haikuwa hivyo. Basi liliwaka vyema.
Na kutoweka!!
Ilikuwa usiku mnene lakini kinyume na taratibu za
usafiri Tanzania, basi lile lilisafiri usiku. Hayakusikika malalamiko ya
kubanana tena. Kila mmoja alitaka kutoweka eneo lile. Hata madereva na
makondakta wote walikuwa waoga.
Nilibaki na yule babu!!! Akina
Samson, Jesca, na Jenipher walitaka kubaki na mimi lakini kwa maneno ya
yule babu kuwa mzigo wangu hauwahusu. Niliwaruhusu waende zao huku
nikiwapatia pesa nyingine ya ziada.
“Nendeni mkautangaze ushuhuda
huu popote pale. Msifiche hata moja lililotokea. Hata kama sitafika huko
mtakapokuwa. Naamini sisi ni washindi.” Niliwaeleza. Wakalia kwa
uchungu. Samson akagoma kabisa kuondoka lakini hatimaye alikubali
kuondoka.
Nilibaki na mzee yule tukizungumza. Alinieleza juu
ya jina langu. Akadai kuwa hakuwa akijua nilikuwa naitwa nani lakini
Isabela halikuwa jina langu.
“Rejea nyumbani ukalitafute jina lako.
Jina lako limepotea ama limefichwa. Na ukiendelea kuamini kuwa wewe ni
Isabela basi maisha yako yatakuwa ya tabu sana. Utawatesa wenzako nawe
utateseka sana.” Alinieleza yule babu.
“Unaweza kwenda kupumzika nyumbani kwangu. Kesho upatafute nyumbani kwenu. Ukalitafute jina lako.”
Tuliongozana na yule mzee hadi nyumbani kwake. Hapo tulipokelewa na mbwa wengi sana waliomlaki bwana huyu kwa furaha.
Wahehe na mbwa!! Niliwaza.
******
Nililala katika mkeka. Ni kama nililala kwa sekunde kadhaa hatimaye pakapambazuka.
Mzee akaniamsha, akanisihi sana nihakikishe Napata jina langu halisi na hapo nitaendelea na maisha yangu vizuri.
“Jina langu ni nani?” nilijiuliza kwa sauti akanisikia.
“|Hata mimi silijui lakini ni lazima ulipate ili kuzikwepa laana za
ukoo wako. Fuatilia historia yako vyema mwanzo hadi mwisho. Historia ya
kweli ipo kwa mama…kamuulize mama yako. Wewe ni nani? Lakini
nakukumbusha kuwa wewe sio Isabela”
Mzee alinisindikiza hadi njia ya mabasi.
“Usizungumze na mtu yeyote, kwa usalama wako na abiria wenzako.”
Alifanya kunisemesha kwa sauti hafifu. Nikamsikia na kumwelewa.
Basi likapita. Nikapanda!! Mzee alinilipia nauli huku akichukua fursa ya kuzungumza na kondakta.
Safari ya kurejea Makambako. Safari ya kwenda kulitafuta jina langu. Jina lililopotea.
Kaka aliyekuwa pembeni yangu alikuwa anaongea maneno mengi sana. Lakini sikuwa namjibu chochote.
Hatimaye tukaifikia Makambako!! Nikashuka garini nikaikanyaga ardhi ya
Makambako kwa huzuni sana!! Hatua kwa hatua nikaanza kuelekea nyumbani.
*****
Mwanamke wa makamo ambaye sasa mvi zilikikaribia kichwa chake chote
alikuwa anafagia uwanja. Alikuwa akiimba nyimbo anazozijua yeye huku
akionekana kuzifurahia. Nilimtazama kwa makini. Nikatamani ningekuwa
nimekuja kwa mazuri huenda ningemshtua kisha tukacheka wote. Lakini
nilikuwa nimekuja kwa mengine magumu sana.
Huyu alikuwa ni mwalimu Nchimbi. Mama yangu mzazi.
Nikanyemelea. Akashtuka akageuka.
“Belaaa….Belaaa mwanangu.” Akautupa ufagio, akanikimbilia,
akanikumbatia kwa nguvu. Joto lake likaupenya mwili wangu ulio dfhaifu.
Nikaamini kuwa nilikuwa nimemkumbuka sana. Chozi likanitoka.
Nikamkumbatia kwa nguvu zaidi.
“Karibu mwanangu…mbaya wewe..yaani kimya kimya au uliongea na Suzi..wabaya sana nyie.” Alilalamika nikajilazimisha kutabasamu.
Tuliingia ndani. Tukafanya mazungumzo ya hapa na pale. Hadi
tulipokatishwa na nyimbo nyingine kutoka kwa mlevi. Huyu alikuwa baba
yangu mzazi. Asubuhi sana alikuwa anatokea kilabuni.
Sijui alilala huko? Nilimuuliza mama./
“Hamna sema ameamkia huko.”
“We Helena wewe…Aaah!! Suzy..inaq maana haunioni uje kunipokea…si ku
hizi hamsalimii watu!!” alizungumza kilevi. Macho yake hayakumwezesha
kujua iwapo mimi ni Isabela.
Akapita akiacha nyuma harufu ya pombe kali. Akaingia chumbani.
Baada ya kelele za hapa na pale akasikika akikoroma!!!
Nilijikaza sana na sasa nikaamua kumueleza mama kilichonileta pale nyumbani.
“Mama hivi hili jina la Isabela ni nani alinitungia.”
“Mbona wauliza hivyo mwanangu.”
“Nipe jibu mama..ama ukoo wangu ni upi.”
“We mtoto umekuwaje lakini.”
“Nijibu mama.”
“Mbona kila kitu kipo wazi..ukoo wako ni huu wa baba yako, na jina hilo ni mimi na baba yako tulikupatia.” Alinijibu.
Niliondoka sebuleni nikaenda chumba cha wasichana nikajinyoosha. Nikapitiwa na na usingizi.
Nilikuja kushtuka nikiwa na njaa kali.
Nikaliendea jiko.
Nikajihudumia vilivyokuwepo, kisha nikareje chumbani.
Majibu ya mama yalikuwa hayajaniridhisha hata kidogo.
Nitamuuliza baba pia!! Huenda kuna kitu anajua.
Kwa nini aliniita Isabela.
Nikasinzia huku nikiwa nimejiahidi hivyo kichwani mwangu.
*****
Asubuhi na mapema nilikuwa wa kwanza kuamka. Nilihitaji kumuwahi baba akiwa katika akili zake vyema kabisa.
Kabla hajalewa!!
Niliwahi na kujifanya naosha vyombo.
Hatimaye nikasikia mlango wa chumbani unafunguliwa. Baba akatoka.
“Aaah!! Bela mwanangu…lini tena umetuvamia wewe…umemaliza mitihani lakini.”
“Nimemaliza..shkamoo baba….”
`aliijibu salamu. Tukabadilishana mawazo na hatimaye kama kawaida yake akaniomba pesa.
“baba kabla ya hilo…nahitaji kukuuliza kitu.”
Alinisikiliza kwa makini, nikamueleza kile nilichomueleza mama. Baba
alionekana kushtushwa na habari hiyo. Alijaribu kujiweka sawa lakini
nilikuwa nimemsoma.
“Fanya hivi…nipatie hiyo pesa nikirejea
tutaongea ni stori ndefu kidogo..si unataka kujua maana ya Isabela na
kwanini tulikuita hivyo..nifanyie kwanza nienda kupata supu kidogo.”
Alijaribu kukwepesha mada.
Niliheshimu maamuzi yake. Nikaingia ndani nikarejea na pesa kidogo nikampatia. Akatoweka.
Moyoni nilipata matumaini makubwa sana!! Niliyaamini yale maneno ya yule mzee.
Sasa mimi ni nani kama sio Isabela? Na kuna siri gani inazunguka hapa. Nilijiuliza. Wa kunijibu alikuwa ni baba.
Nilisubiri sana. Hadi pale ilipokuja taarifa kuwa baba amekutwa
mtaroni. Hana jedraha lakini haijafahamika bado kama anapumua ama
amekufa!!
Hii ilikuwa ni habari ya kushtua sana.
Mimi na mama tukakimbia kuelekea hospitali ambayo tulielezwa kuwa amelazwa.
Bahati mbaya zilikuwa mbio za kuwahi upepo.
Baba yangu hatukuwa naye tena!! Kifo cha utata. Hakuwa amelewa. Alikutwa na ile pesa niliyompa.
Hakika mimi sio Isabela, na kuna siri mzee wangu amekufa nayo!! Nilizungumza na nafsi yangu.
Jina langu ni nani sasa? Na kwa nini waliniita Isabela?
***Najua wengi watafadhaishwa na hili……lakini hakuna jinsi lazima iwe hivi.
***ISABELA katika wakati mwingine mgumu…amehakikishiwa kuwa Isabela si jina lake. Na hicho ndio chanzo ncha matatizo.
***JINA lake hasa ni nani? Na kama baba amekufa na siri hiyo atafanya nini kujikomboa na kuwakomboa wengine???
***JOHN, BASU, DAVIS, OSMAN…nini hatma yao viumbe hawa???
KWA HAPA uwanjani SITAISAHAU facebook inaishia hapa.
MTUNZI: Emmy John p.
MAWASILIANO: 0654 960040
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
...
Maskini yule dada bila kujua kwamba ameambiwa anipatie kinga. Akadhani
yule mbongo amemaanisha ule mkoba. Akaniomba msamaha kwa kila namna
kisha kwa ukarimu kabisa akanipatia ule mkoba. Ulikuwa mzito kiasi.
Nilipotaka kuondoka yule dada aliyekuwa amejikita katika kutafuta
anachojua yeye, aliniita, nikageuka na kumshangaa kidogo.
“Unatakiwa kuweka sahihi.” Alinielezea kwa ukarimu.
Nikaona kama huyu binti ana nia mbaya na mimi. Nikabaki wima najiuliza
iwapo niende mbele ama nirudi. Tukatazamana kwa sekunde kadhaa. Nikaona
isiwe tabu. Nikarejea nikachukua kalamu niweze kuweka sahihi. Mara
nikasikia fujo za mlango kufunguliwa.
Nikaomba Mungu usiwe mlango wa yule jamaa mbongo. Kisha nikasikia hatua kubwa kubwa zikitambaa.
“How long does it take to…to…..hell..” (Inachukua muda gani ku…ku…. ).
Ilisikika sauti yenye kitetemeshi cha hasira. Alikuwa yule mbongo.
Sasa badala ya kuweka sahihi nikabaki kulishikashika tu lile daftari na
kalamu. Mkojo ukatoka safari yange ya mbali na sasa ulikuwa unahitaji
kutoka. Nikabana miguu yangu!! Mkoba mkononi.
Ninafumaniwa Isabela mimi!!
Nikataka nikimbie!! Miguu ikawa mizito. Sikuwahi kufanya kitendo cha wizi hivyo lazima hali kama hii ingenitokea.
“Iam sorry boss..i have already given her (samahani mkuu..nimempatia
tayari.)” yule dada wa mapokezi alijitetea kwa uoga. Mara vile vishindo
vikasita.
Yakafululiza matusi ya nguoni kutoka kwa yule mlevi wa kibongo.
Hapo sasa nikaangusha saini yangu.
Narudi vipi na ule mkoba sasa!! Nikajikaza nikaanza kuondoka.
Nilipogeuka nikakutana na kosa ambalo nililitegemea. Yule dada wa mapokezi alikuwa amebonyea chini tena.
Asante! Nilimshukuru kwa kitendo hicho.
Ghafla nikabadili uelekeo. Nikaelekea katika vyoo.
Upande huu, nikaambaa na korido hadi nikaufikia mlango wa kutokea.
Nikamuachia tabasamu mlinzi aliyekua kwa nje na yeye akatabasamu.
Tabasamuu la kizee. Kisha nikatoweka. Nikapiga hatua kwa hatua hadi
nikalifikia geti kuu la kutokea. Hapa nilitakiwa kuandika jina.
Nikaandika jina lililokuja kichwani mwangu lakini sio jina sahihi.
Geti likafunguliwa. Mimi na mkoba wangu. Nikatoka.
Nilipogeuka nyuma nikakutana na maneno mazuri ya kupendeza.
The Savoy Hotel
12 Buteko Avenue
Ndola
Zambia
Haya hayakuwa yananihusu. Niligeuka na kutazama mbele. Nikaanza kutokomea. Nikashtuliwa kwa kuguswa begani.
Nikageuka upesi nikaikuta amani ambayo nilikuwa naihitaji.
Samson…jemedari wa kisukuma.
Akanikumbatia kunipongeza. Lile joto lake likanikumbusha mengi. Nikapuuzia.
Oparesheni ilikuwa imekamilika.
****
Pesa zilikuwa kwa mafungu yanayolingana. Zilikuwa zinang’ara kuonyesha kwamba hazikuwa zimepitia mikono mingi.
Ilikuwa saa kumi alfajiri. Sasa nikiwa pamoja na Samson tulipita katika
vijiwe ambavyo wenzetu walikuwa wanalala. Wote wakaamshwa. Hatimaye
tukawa na mkutaniko wa pamoja wa kwanza tangu tuwe katika ardhi ile.
Niliwakumbusha juu ya ahadi yangu!! Sasa ilikuwa imetimia.
Hakuna aliyekuwa anafahamu thamani ya kwacha ya Zambia katika shilingi
ya kitanzania. Hilo halikutupatia shida. Nikawachukua wenzangu watano wa
kwanza. Nikaliendea basi linalotoka Ndolla kuelekea Mbeya mjini.
“Kwacha ngapi?” niliuliza. Akanijibu. Nikalipia nafasi za watu watano.
Wakaingia garini. Kiongozi wao akiwa Jesca
Nikarejea na kuwachukua wengine. Hawa kiongozi wao akawa Jenipher.
Kundi la nne nikalikabidhi kwa Samson.
Kisha nikabakisha kundi lililosalia mikononi mwangu.
John!! Akiwa ameambatana nami!! Nilichukua siti ya watu wawili. Nikamuweka John kisha nikambebesha mfuko fulani.
Hakuruhusiwa mtu kukaa pale.
Safari ikaanza huku maelekezo yota ya tunakutana vipi yakiwa kwa viongozi wa msafara.
Hatimaye tukaiacha Ndolla majira ya saa kumi na mbili. Safari ya kurejea Tanzania.
*****
Pesa zilibaki nyingi sana. Hivyo tuliamini kabisa hakuna
kitakachoharibika. Jesca alikuwa na akiba yake, Jenipher na Samson
vilevile.
TUNDUMA, Mbeya.
Mji ulikuwa umetulia sana. Hapakuwa na harakati za hapa na pale. Ilinishangaza sana kwa boda kama hii kuwa katika utulivu huu.
Tulikuwa tukihangaika kutafuta mahali pa kulala. Nyumba za kulala
jirani na kituo cha mabasi zilikuwa zimejaa. Hivyo ilitulazimu kidogo
kuzunguka. Hatukupata mahali pa kulala kwa wingi tuliokuwa nao. Sasa
tuliamua kuishi maisha yetu ya Zambia. Tukaamua kulala katika stendi ya
mabasi.
Baada ya kufikia uamuzi huo. Sasa mwenye kutafuta chakula
aliruhusiwa lakini pa kulala tulikuwa tumeamua kabisa ni hapo hapo
stendi.
Wanaume watatu waliamua kusindikizana kwenda kutafuta chakula.
Mkuu wa msafara huo Jesca aliwapatia pesa wakatoweka kwa ahadi ya kurudi upesi.
Ahadi ikavunjwa maradufu!! Hawakurudi.
Hadi tuliposinzia. Haikuwa kama yaliyomkuta Samson kule Ndola. Hawa hawakurudi kabisa.
Kesho yake. Tulipotoa taarifa polisi tulikutana na taarifa ya vifo vya watu watatu kwa kukatwa na mapanga.
Waliukuwa wenzetu!! Lakini hatukukiri!! Hatukuhitaji kuwa karibu kabisa
na polisi. Kwa kifupi hatukuwa tunajua hatma yetu. Hasahasa mimi ambaye
nilikuwa na siri nzito.
Baada ya taarifa hizo kutapakaa.
Tukajua nini kinachoendelea ndani ya mji wa Tunduma. Majambazi wa ajabu
walikuwa wameuvamia mji. Hawa walikuwa na hadhi ya kuitwa majambazi
wastaarabu. Walibandika matangazo kabisa kuwa kama mwanaume anatembea
usiku basi awe na tahadhari aidha simu ama kiasi cha pesa shilingi. Elfu
hamsini lakini bila hilo wakikutana ama zao ama zake.
Kumbe ndicho kimewasibu wenzetu!! Nilisikitika kuzipoteza roho hizi.
Asubuhi hiyo nilitaka kwenda kubadili pesa. Lakini bahati mbaya sikuwa
na kitambulisho chochote. Nikaitupa kazi hiyo kwa Samson. Akazunguka
mtaani kuzibadili baada ya kugundua kuwa Kwacha moja ni sawa na shilingi
0.3 ya kitanzania.
Baada ya zoezi lile kukamilika na kupata
pesa ya kutosha sasa kila mmoja alitakiwa kuubeba mzigo wake mwenyewe.
Aliyesema kuwa anaishi Dar alipewa nauli aondoke zake, wa Arusha naye
vilevile. Na pesa ya ziada kila mmoja alipewa.
“Muutangaze ushuhuda
huu bila kuipunguza wala kuongeza neno!” niliwaambia wakati tunaagana.
Kila mmoja alikuwa na furaha huku wakiniona mimi kama Mungu wao.
Sikujali sana!!
Safari ya Mwanza tukabaki watano. Mimi, Jesca, John, Jenipher na Samson.
MAUZAUZA MAPYA TANZANIA
Siku ya safari kama ilivyo kawaida nikalipia siti ya watu wawili, Jesca
na Jenipher wakakaa siti moja huku Samson akikaa peke yake.
Alama ya John shingoni ilinikwaza sana. Nilitamani aweze kutuona. Lakini alikuwa anauona ulimwengu wake mwenyewe.
Safari nzima ilikuwa tulivu sana. Nilikuwa natafakari mambo mengi sana.
Nilitamani kwenda Makambako kwa mama lakini niliamini haukuwa wakati
sahihi.
Nilihitaji nkujua kitu kuhusu Maria. Maana alinitokea kule porini siku ya kwanza kabisa na kamwe sikumuona tena.
Nini kilimsibu? Nilijiuliza.
Tulipita miji mbali mbali. Tukaipita Makambako, nikainama nikajifuta
machozi, tukaiacha Mafinga, tukaingia Iringa mjini. Na hapa hatukusimama
sana tukaendelea na safari.
Sasa gari lilisimama!! Hatukushangaa sana. Tulidhani ni kwa madhumuni ya kuchimba dawa. Lakini hatukuiona dalili hiyo.
Dereva akateremka. Akaangaza gari lake bila kuona tatizo.
Akaangaza tena. Hakuna tatizo.,
Msaidizi wake naye akashuka. Hakuna msaada!!
Wakashuka mafundi wakajaribu kugusa hapa na pale. Gari lilikuwa limezima.
Walijaribu kufanya kila wanaloweza lakini hapakuwa na matumaini. Dakika zikaanza kwenda. Masaa yakaenda. Hatimaye jioni.
Abiria wakashindwa kuvumilia. Wakatoa matusi mengi lakini haikusaidia. Gari halikuweza kuwaka.
Duh! Leo tunalala njiani!! Nilimweleza John japo hakunisikia.
John alichoweza kuona ni chakula na mengineyo lakini si watu!! Na watu halisi pia hawakuweza kumuona yeye.
Simu ilipigwa ili gari jingine liweze kuja kutuchukua. Basi lilifika
likiwa na abiria wengine. Likazimishwa ili tuweze kubananishwa wote
twende Dodoma. Abiria walilaani kitendo kile kwa lugha zote, huku
wakilalamikia usalama wao.
“Kama hutaki basi hili hapa lala
utasafiri kesho!!.” Zilikuwa kauli ngumu kutoka kwa mpigadebe. Hakuna
aliyependezwa na kauli hiyo. Wakati huu sikuweza kukaa na John badala
yake tulikuwa tumesimama. Ni Jesca pekee aliyepata nafasi ya kukaa.
Yalikuwa mateso.
Walipofanikiwa kutubananisha kama viroba. Dereva akisifiwa na wapambe wake akaingia garini aweze kuendesha tuondoke.
Ikaanza tena kama utani, akachokonoa kwa mara ya kwanza likagoma, akajaribu mara ya pili bado hali ileile.
Akajaribu tena na tena. Injini haikuweza kuwaka. Kila mmoja akawaza lake.
Watu wakakimbilia kwenye imani za kishirikina.
Lakini huyo mshirikina ni nani? Hakuna aliyejua.
Abiria wakashuka. Kila mmoja akarejea kwenye basi alilokuwa amepanda awali. Hapakuwa na safari tena.
Usiku ukafika wanakijiji wakapika chakula na kutuuzia kwa bei mbaya sana. Hatukuwa na ujanja tukanunua.
Saa nne usiku mambo yakananza kubadilika. Hali ya hewa ilibadilika na
kuwa ya kushangaza hata wanakijiji walikiri kuwa hiyo haijawahi kutokea.
Badala ya baridi kali la Iringa sasa lilitanda joto.
Joto hilo ni
kama lilimshtua John. John akasimama akataka kuondoka. Nikamzuia. Akawa
anatumia nguvu!! Nikamzuia John, John akanitazama kwa jicho la hasira.
Macho yake yakiwa mekundu sana.
John alikuwa ananiona? Nilijiuliza.
Lile joto likazidi. Abiria wakashuka garini.
Kuna kitu hapa!! Mapambano mapya!! Nikajisemea huku nikiendelea kumzuia John.
John sasa akanizidi nguvu.
Akanitoka. Akashuka chini. Nikajaribu kumkimbilia.
Huko nikamkuta akiwa anafanya jambo la ajabu. John alikuwa anajarfibu kuisukuma gari kwa kuitikisa.
Ajabu! Ikaanza kutikisika kweli. Mtikisiko ule ukawashtua wengi. Sasa vilio vikaanza kusikika. Kila mtu kuitetea nafsi yake.
Watu wakashuka upesi kwa kugombania mlango. Basi likaanguka.
Lilipoanguka John akatazama mahali. Na mimi nikageuza jicho kutazama. Yalikuwa ni makaburi mawili.
Makaburi yaliyo na historia ya kushangaza. Makaburi ambayo yalimtoa
nishai mchina alipojaribu kupitisha umeme juu yake. Umeme ukagoma
kuwaka.
Haya yalikuwa makaburi ya Kiyeyeu.
Yalikuwa yanafuka moshi wa dhahabu!!
Vita!!
***BADO haijawa salama kwa ISABELA ni vita nyingine tena.
***Nani huyu ameyaleta haya tena…
MTUNZI: Emmy John P.
MAWASILIANO: 0654 960040
... SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
Nilimchukua Jenipher, Jesca na Samson. Kikawekwa kikao cha dharula. Mada kuu ikiwa tunatoka vipi.
Nilimpatia Jenipher na Jesca baadhi ya nguo. Wakajihifadhi.
Mazungumzo yalikuwa marefu sana na pambazuko lilikuwa linakaribia.
Mengi yalizungumzwa na sasa tukawa tumefikia katika maamuzi mawili.
Kubwa kabisa likawa kukimbilia ubalozini kupata msaada.
Wazo la
kupata simu tuweze kufanya mawasiliano nyumbani pia lilitujia vichwani!!
Lakini hatukulitilia sana maanani katika nchi za kigeni. Tulitaka
tufike kwanza Tanzania ndipo tufanye mawasiliano.
Ubalozini!! Hiyo ndio ikawa mada.
Lakini swali likaja kwa John ambaye bado alikuwa na alama 666 na hakuwa
akionekana. Lakini kama hiyo haitoshi, tukapata hofu ya usumbufu wa
maswali mengi kutoka kwa chombo husika kitakachokuwa kinahusika na mambo
ya uhamiaji.
Kwa jinsi tulivyokuwa wengi tuliamini kuwa itatuwia
ngumu sana kupata msaada upesi. Pia ubalozi wa Tanzania katika nchi ya
Zambia ulikuwa una makao yake Lusaka. Mji mkuu wa Zambia.
Hilo lilikuwa gumu sana. Tulikuwa tunahitaji pesa. Pesa!!
Kama tukipata pesa tunaweza kupanda mabasi yatakayotufikisha Mbeya.
Hapo sasa tutakuwa katika ardhi salama ambayo tunaweza kupata msaada.
Pesa tutaitoa wapi? Hilo likawa swali.
Tukakubaliana kuingia katika mapambano ugenini. Mimi, Jesca, Jenipher na Samson. Tukafunga mjadala.
Asubuhi ikazidi kujongea. Hapa sasa nikachukua maamuzi. Nikatembelea
kundi moja baada ya jingine. Nikawapatia chakula kidogo kidogo
nilichonunua kwa kutumia pesa niliyopewa na kaka yule wa kitanzania.
Huku katika kila kundi nikiwapa moyo kuwa tumekaribia kuondoka kurejea
nyumbani.
Siku iliyofuata kila mtu alikaa kwa tahadhari bila kuzungumza na raia wa Zambia.
*****
Majira ya saa nne asubuhi nilikuwa katika ofisi ya yule mwanaume wa
kitanzania aliyeahidi kunisaidia niweze kufia Mbeya. Nilimkuta akiwa
amebanana kulingana na majukumu. Nikatulia mpaka alipomaliza. Nikaingia.
Alinichangamkia sana. Akamkabidhi mwenzake ofisi akanipeleka mgahawani. Chai ya maziwa na chapatti nzito kabisa.
Mazungumzo yakiendelea!!!
Akanielezea mpango wake huku akinisihi niwe mvumilivu katika safari
maana patakuwa na tatizo la kuhamishwa siti na wakati mwingine kukosa
kabisa pa kukaa maa nitasafiri kama ‘staff’. Hilo halikuniumiza kichwa
sana, maana niliamini naweza kusimama cha msingi nia yangu kutimia.
Kilichoniumiza kichwa ni hawa wenzangu. Itakuwaje!!
Nilimshukuru yule bwana. Akanipatia namba yake ya simu. Ni hapo nilimtambusa jina lake aliitwa Saidi.
“Ukinipigia simu we niite Side boy.” Aliniambia wakati ananiaga.
Alinipatia kiasi kingine cha pesa.
Nilishukuru kwa kuzaliwa mwanamke maana bila hivyo sidhani kama ningepata msaada.
Jioni ilipofika. Jesca hakuwa ameambulia lolote. Na Sam hadi wakati huo
hakuwa amerejea. Tukajipa moyo kuwa huenda amefanikiwa kupata kibarua
chochote huko alipo. Ikafika giza nab ado Sam hakuwa amerejea. Hofu
ikaanza kutuingia na kuamini kuwa Sam anaweza kuwa aliongea Kiswahili na
kugundulika kuwa ni mtanzania asiyekuwa na uhalali wa kuishi Zambia.
Hatukujua kuwa ni wapi tuanzie kumtafuta. Kama tukisema twende polisi na sisi tutakuwa matatani. Tatizo jipya!!
Jesca na Jenipher wakawa wananisikiliza mimi.
Kimya kikatanda!! Makundi mengine hayakujua nini kinaendelea.
Nilijiuliza maswali mengi sana bila kupata majibu. Samson amefanya jambo gani la kitofauti hadi wakati huu hajarejea.
Au amerejea tena katika kijiji cha Dokta Davis. Niliwaza peke yangu bila kumshirikisha mtu yeyote hisia zangu.
Saa nne usiku nilikuwa nimepitiwa usingizi.
Nilisikia kama natikiswa nikadhani ni Jesca amejigeza lakini nilikuwa
naendelea kubughuziwa. Japokwa nilikuwa nimelala chini niliutamani
usingizi.
Nilijikaza nikafumbua macho.
Usingizi ukakatika palepale. Alikuwa ni Sam!!
“Bella!! Bella!!” alinong’oneza. Nikamtazama usoni nikahisi kuna nhali ya tahadhari. Nikajipa utulivu wa lazima.
Akanishika mkono akaninyanyua. Akanivuta pembeni kidogo.
“Ulikuwa wapi Sam.”
“Bwana Mkubwa!!.”
“Kafanyaje…ndio nani?” nilitaharuki.
“Sio mtu ni sehemu inaitwa hivyo.”
“Pamekuwaje…”
“Nimekutana na mtu!! Aah!! Nimemuona mtu….amepata madini.”
Bado sikuweza kumuelewa Sam anamaana gani. Nikamuomba anielezee kwa kirefu.
Akanieleza juu ya mgodi wa Bwana Mkubwa ambao upon je kidogo ya mji wa
Ndolla. Mgodi huu alipoutaja tu! Sikuwa na swali lolote. Nilikumbuka
somo la Historia kidato cha pili hadi cha tatu. Mgodi huo ukanikumbusha
madini hadimu ya Risasi (Copper) ambayo hupatikana kwa wingi katika
nchi ya Zambia. Hasahasa Ndolla.
Sam akaendelea kunielewesha. Na sasa akanigusia juu ya bwana ambaye amepata madini hayo siku hiyo.
“Kwa hiyo ulikuwa huko.”
Akanijibu kwa kutikisa kichwa juu na chini akimaanisha kuwa ni kweli alienda ‘Bwana Mkubwa’.
Samson alikuwa amekuja na habari ambayo mwanzoni nilikuwa ninapingana
nayo lakini hatimaye kulingana na shida tuliyokuwanayo nikaamua
kukubaliana naye. Wizi!
Samson alinihakikishia huyo bwana ana pesa nyingi sana. Amefuatilia nyendo zake hadi alipofanikisha kuyauza yale madini.
“Alinipa lifti kwenye gari yake. Nilijifanya sijui lolote lile. Aliponishusha mjini nikamfatilia na kumuona aliyauza.”
“Sasa tunampata wapi?”
“Yupo anakunywa pombe sasa hivi. Ni hapo pekee pa kumkamatia.” Alinisisitiza.
“Nzuri zaidi ni mtanzania…” alinisisimua kwa kauli hiyo. Nikamwomba
Mungu huyo bwana asiwe na tabia za kitanzania bali awe mbongo.
Nilitulia kwa dakika chache kisha nikamuamsha Jesca. Hakunisikia.
Nikapekua huku na huko. Nikachukua mafuta. Nikaenda bafu za kulipia
nikaoga. Nikajipaka mafuta. Nikavaa kanga moja.
Samson akawa kioo changu akakiri kuwa kwa namna ile lazima anitamani.
Samson akaniongoza hadi nikafika eneo la tukio.
Jirani na bwana huyu palikuwa na kiti kipweke ambacho hakikuwa na mlevi aliyekikalia. Nilikitoa upweke nikajiweka juu yake.
Haraka akafika muhudumu wa kizambia, mweusi na mbaya kumtazama. Nikaagiza soda.
Meza yangu haikuwa mbali sana na yule bwana ambaye Samson
alinielekezea. Nilikunywa soda taratibu huku nikiisoma akili ya yule
bwana aliyepata bahati ya kupata madini Bwana mkubwa.
“Yaani
wahudumu wengine nao….ona sasa.” Nilizungumza kwa hasira. Kama
najiongelesha. Sauti ikamfikia mlengwa ambaye ni yule bwana anayekunywa
pombe.
Akajileta mtegoni.
Akasogeza kiti karibu nami.
“Wewe ni mtanzania kumbe..ama unaibiaibia Kiswahili. Nimefurahi kukusikia ukisema Kiswahili.”
Nikatabasamu, nikalegeza jicho kimaksudi.
“Yeah! Mtanzania halisi…..na wewe je?”
“Mimi ndio orijino kabisa.” Alijibu. Nikacheka tena.
“Dah!! Miezi miwili sijarudi nyumbani aisee. Maisha haya.” Nililalamika.
“Aaah! Mimi kila wiki huwa naenda aisee.”
Maongezi yakawa maongezi. Kama bahati alinipendelea vile. Yule bwana alikuwa na tabia za kibongo. Akaniingizia mada za mapenzi.
Sasa nane usiku tukawa tunatafuta chumba kwa ajili ya kutimiziana haja. Yeye akinitaka kimwili na mimi nikimtaka kipesa.
Alilipia chumba cha bei ghali sana. Nilimshuhudia wakati anauacha mkoba wake mapokezi. Nikagundua mchezo unataka kuharibika.
Nikajipa moyo. Nikaenda hadi chumbani!!
Hapakuwa na jipya huko. Mzee huyu mwenye matamanio. Alinivagaa na
kuanza kunisumbua huku na huko. Sikuwa na hisia hata kidogo. Niliwaza
pesa tu.
Nilipomtazama umri wake nikagundua huyu hana lolote la
kuweza kunishinda. Akili ya maajabu ikanivaa, nikajikuta nimevamiwa na
wazo kuwa kama nisipokuwa makini naweza kutumika kimwili na nisipate
chochote kile.
Nikaamua kutumia nafasi moja tu kusawazisha mambo haya!!!
Pata potea!!
“Mh!! Hauna kinga?” nilimuuliza baada ya kuwa nimempelekesha akalegea
kabisa macho yake na nikajua kuwa alikuwa anahitaji mwili wangu.
Ni hapa nilikuwa napahitaji.
“Sina mpenzi wangu…njooo tu hivyo hivyo” akajibu. Nikamtukania mama yake kimoyomoyo kwa ujinga aliozaa.
Nikasimama. Nikamtazama kwa jicho la kimapenzi huku moyo wa chuki
ukimtusi. Ubongo unaohitaji pesa nao ukifanya kazi kwa bidii kubwa.
“Ngoja niende kuchukua mpenzi wangu, naogopa mimba mwenzako, ujue
nimeolewa eeh!!” nilimlaghai. Akaingia mkenge. Nikachukua upande wangu
wa kanga, nikashusha ngazi mpaka mapokezi.
Nikamkuta mwanadada mweupe akiwa ameuchapa usingizi.
“Nipatie mkoba wa mzee!!” nilimwambia huku nikiwa nimetega mkono!! Moyo ukiwa hauamini kama nitafanikiwa.
“Mmm. Hapana mwambie aje mwenyewe dada, hajaturuhusu kumkabidhi yeyote
zaidi yake.” Alinipinga yule dada kwa kingereza chake kibovu kisha
akaendelea kuuchapa usingizi. Nilitamani sana kumrukia nimkabe. Lakini
alikuwa ametenganishwa na nondo. Nisingeweza hata kumgusa.
Niliondoka pale nikiwa nimetaharuki sana, mpango ulikuwa unakaribia
kushindikana sasa, na asubuhi inayofuata nilitakiwa kusafiri kuelekea
Mbeya.
Nikapanda hadi juu kule chumbani nikaufungua mlango kwa ghadhabu kubwa.
Yule bwana akashtuka.
“Ndio ujinga gani huu huku Zambia I hate such embarrassment!!” nililalamika.
“Nini tena mamito.” Aliniita kimapenzi akiwa amelegea.
“Yaani hadi kuchukua kinga I need to go with you!!”
“He!! Wamekunyima?” aliponiuliza swali hilo, nikajikuta Napata nafasi ya mwisho.
“Fanya hivi naomba umpigie umwambie anipe!! No discussion!!” niliwaka,
zile hasira za kutaka kuikosa pesa ile zilikuwa zimenipanda.
Mbongo akachukua simu akainyanyua. Nikaomba mizimu yote asije akasemam maneno mengi kwenye simu.
“Halo!! Chumba namba 12….mpe huyo dada nilichomuagiza…na muache mambo
ya kipumbavu” akakoroma kwa kiingereza kilichonyooka. Kisha akakata simu
kwa hasira.
Sikusema neno!! Nikafungua mlango, nikatoka.
Nikiwa nimeukunja uso kwa ghadhabu nikafika mapokezi. Yule dada usingizi ulikuwa umekatika!! Tukatazamana!!
Yeye anaogopa na mimi naogopa!!!
***Je? ISABELA ataichukua hiyo pochi anayoamini kuwa ina pesa??
***Vipi safari itawezekanika????
MTUNZI: Emmy John P.
MAWASILIANO: 0654 960040
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
...
Nikafadhaishwa baada ya yule Davis ambaye sasa niliamini naenda
kummalizia alipogeuka kuwa joka kubwa la kijania. Haraka nikawahi
kujitoa lakini nilikuwa nimechelewa sana. Joka lile likawahi
kujiviringisha kuanzia kiunoni likawa linapanda juu. Sasa lilikuwa
limenifunga hadi kifuani.
Ajabu!! Lilikuwa linawasha sana.nilitamani kujikuna lakini haikuwezekana na mikono ilikuwa imefungwa tayari.
Nililiamuru liniachie lakini halikuiheshimu amri yangu. Nikazidi
kuwashwa, nikajaribu kujigalagaza, haikuwezekana. Sasa likaanza
kujikaza, muwasho ukaenda likizo, maumivu yakaingia kati. Lilizidi
kukaza, mara likaongeza kujiviringisha hadi likaniziba usoni. Kifo
kikanukia harufu ya kukera.
Nikabaki jicho moja tu kuona nje!!
Viungo vingine vyote vilikuwa vimefunikwa. Sikuwa na ujanja. Jicho langu
likamuona John akiwa ameshangaa kama tahira. Nilijaribu kutoa sauti
haikutoka, nilikuwa namwomba John kwa mara ya mwisho aweze kuniokoa.
Hakuweza kunisikia.
Nikatazama juu nikakutana na mawingu yenye rangi
inayoshabihiana na buluu, nikaikumbuka rangi ya mtandao wa kijamii. Ni
huku nilikutana na Dokta Davis. Akanipa zawadi ya utajiri, akanipatia
kazi nyepesi inayonipatia kipato kikubwa. Nikamuamini sana. Sasa alikuwa
amegeuka joka kubwa na lilikuwa linaniua.
Hakika lazima nife!! Jitihada zangu zote hazikuwa na maana tena.
John hakuwa msaada wowote kwangu. Na hakuwepo mwingine wa kunipa msaada.
Nilipofikiria ni nani mwingine wa kunisaidia akili yangu ikaejea kwa
mwalimu Nchimbi. Mama yangu mzazi. Nikajaribu kuita sauti haikutoka.
Mama naye hakuwa na msaada katika hali hii.
Nikayakumbuka maneno ya mama. Miaka mingi sana nikiwa mdogo aliwahi kunikambia maneno.
“Yupo mtu anakusikia hata usipotoa sauti.” Hili lilikuwa jibu alilonipa
baada ya kumuuliza iwapo mabubu na viziwi wanaweza kuzungumza na Mungu.
Jibu lake hadi ukubwani halikunitoka.
Nami sasa nilikuwa bubu.
Jaribio la mwisho kabisa ni kuzungumza na yule anayesikia wakati wote.
Ajuaye unachokiwaza. Kila wakati, mahali popote.
Mungu!
“Eeh!
Baba sijui kama nilistahili adhabu hii. Na kama ilikuwa stahili yangu
baba. Nichukue kwako sasa. Nimeumia na IMETOSHA.” Nilizungumza katika
nafsi yangu. Kisha nikasubiri kuiaga dunia hii chungu.
Nilitua chini
kama mzigo mzito, bahati nzuri nilitua katika majani. Sikuumia.
Nilipumua kwa fujo sana, nilikuwa nimerejewa na uhai tena.
Nikalishuhudia lile joka likihangaika huku na huko, hatimaye likatoweka.
Maajabu makubwa ambayo sijapata kuyaona na yalikuwa yanastahili kutolea ushuhuda.
Sikuwahi kuwa na imani katika miujiza lakini sasa ilinitokea ili
niiamini. John naye alikuwa anashangaa kama awali. Na bado hakuweza
kuniona. Sikupoteza muda nikamshika mkono. Tukaanza kuondoka. Sikukiacha
kisu changu.
Nilijikuta naifuatilie ile njia tuliyopita awali hadi nikaufikia ule mlango. Nikamtanguliza John nami nikatoka.
Maajabu mengine. Niliwakuta wale waliotangulia wakiwa katika sintofahamu wasijue nini cha kufanya.
Kwa kukadiria muda ilikuwa saa sita mchana. Na tulikuwa katika ulimwengu halisi lakini hatukutambua ni wapi hapo tulipo.
Magu, Bariadi, Sumbawanga, Songea!! Kila mtgu alifanya utabiri wake.
Hatukuendelea kukaa pale. Tukaanza safari kuelekea tunapoelekea bila kutambua ni wapi.
Baada ya kilometa takribani sita tukaingia kijijini.
Mimi nikiwa na upande wa kanga pekee. Wenzangu wakiwa na nguo
zilizochakaa sana. Tukakiona kijiji. Baadaye tukaanza kukutana na watu.
Kila mtu akiwa na lake la kufanya. Hakuna aliyetuuliza swali. Walikuwa
weusi sana, wengine walifanana na nyani huku wanawake wengi wakiwa na
maziwa makubwa.
Ni wapi sasa hapa? Nilijiuliza.
Tulitamani sana kuzungumza na watu hawa lakini hawakuwa wakarimu.
Njaa iliuvunja uamuzi wetu wa kusubiri watuanze. Njaa ilituuma na hatukuwa na chochote cha kuweka tumboni.
“Ha…habari..”
“Nkesuu…” asijui kama aliniuliza ama alinijibu salamu.
Lugha ya wapi hii!! Niliwahi kusikia mahali, ni wapi vile. Niliumiza
kichwa. Kila mmoja alikuwa ananitazama mimi kama mwokozi katika
mapambano haya.
“Me come great…” nilizungumza kiingereza kibovu ili
nipate kujua wanazungumza lugha gani na ni watu wa wapi. Hakunijibu
akanikazia jicho kwa shari. Ni hapo nikapata jawabu sura hizi nimewahi
kuziona wapi. Ni kwenye basi. Siku ya safari yangu kuelekea Ndolla
Zambia kwa Dokta Davis kusaini mkataba ule ulionifikisha hapa nilipo.
“Sam…it’s either Congo or Ndolla….(Sam ni aidha Kongo ama Ndolla)” nilimnong’oneza yule msukuma.
“Ndolla??”
“Yes! Ndolla Zambia..” nikamjibu. Akashangaa. Yule bwana tuliyemuuliza akawa amesonya na kutoweka.
Watu hawa sio wazuri hata kidogo. Wameathiriwa na vita za wao kwa wao.
Wakitugundua ni hatari. Naamuru!! Hakuna mtu kuzungumza na mgeni yeyote,
I WILL!!! Nilitoa tamko kama amiri jeshi mkuu wa mapambano hayo.
Kila mmoja akanielewa.
Safari ikaendelea, tulikuwa tumechoka lakini tuliuhitaji sana ukombozi, tulihitaji uhuru wetu.
NDOLLA TOWN 40 KM AHEAD. Kilisoma hivyo kibao kigumu cha chuma. Nikajipongeza katika nafsi yangu kwa kuwa na kumbukumbu nzuri.
Jesca alikuwa mtu wa mawazo mazito. Hakuwa akiongea na ule urembo wake
wa enzi zile haukuwa na nafasi hapa. Pia ugomvi wetu wa kumuwania John
kimapenzi haukupewa nafasi pia. Kila mmoja alitazama anajikomboa vipi.
Tulitembea kimafungu mafungu. Jumla tulikuwa watgu ishirini na moja
lakini, tulikuwa kama hatufahamiani. Kila mmoja na lake. Likitokea la
kuzungumza nilikuwa nachukua nafasi hiyo.
Tulipoufikia mto, kila
mmoja aliyatumia maji anavyoweza, wengi walikunywa na wachache walioga.
Pumziko la dakika ishirini kisha tukaendelea mbele. Tukaufikia mti wa
maembe. Hapa sasa kila mtu alikula kulingana na ukubwa wa tumbo lake.
Angekuwa mjinga ambaye angeacha kubeba akiba ya maembe matamu ya Zambia.
Sasa kasi ikaongezeka na mazungumzo yakaibuka. Njaa kitu kibaya sana.
Mimi na John tulikuwa tumeambatana. Ile hali ya yeye kutoniona iliniumiza sana lakini sikuwa na namna.
Kilometa zikazidi kukatika, tulitembea hadi usiku, kwa kukadiria tulitumia masaa yanayozidi kumi. Kuzikamilisha zile kilometa.
Mji wa Ndolla ukatukaribisha. Ulikuwa mara yangu ya pili kuja katika mji huu na mara ya kwanza kufika nikiwa katika matatizo.
Nilijipongeza tena kwa tabia yangu niliyoionyesha siku ya kwanza. Tabia
ya kushangaa shangaa. Hivyo kuna baadhi ya vitu nilivikumbuka. Hadi
tukaipata stendi.
Kama nilivyoamuru kila mmoja alijitenga kama
hatujuani. Kanga yangu ikiwa imefungwa vyema. Ni hiyo pekee ilikuwa ngao
yangu. Nikaingia katika stendi ile ambayo ilikuwa inazidiwa hadhi na
stendi ya Ubungo jijini Dar es salaam katika nchi yangu ya Tanzania.
Nilizunguka hapa na pale. Nikaiona ofisi ya magari amabyo nilikuwa naitaka.
“Mambo vi wewe…inakuwaje…mishemishe vipi…oya acha kuzingua…” maneno haya yalikuwa yanazungumzwa katika ofisi hizi.
Nikainama chini jicho langu la kulia likatangulia kumwaga chozi la
kushoto nalo kwa uchungu likamwaga chozi. Nikajiinamia chini nikalia kwa
uchungu mkubwa. Uchungu wa kuikumbuka nchi yangu Tanzania. Kilio
hichohichoi kwa namna ya kipekee kilikuwa kilio cha furaha. Ndio lazima
nifurahi. Sasa ningeweza kumvuta mtu na kuzungumza naye Kiswahili.
Ni hivyo nilifanya. Mwanaume kipande cha mtu akavutika kunisikiliza.
Kwanza sikutaka kumuelezea kuwa tupo wengi. Niliitetea nafsi yangu.
Nilikuwa natetemeka kwa baridi. Akanipatia sweta zito nikajistiri.
Nikajielezea kuwa nimepotezana na bwana aliyenileta Zambia.
“Umesema wewe mwenyeji wa Makambako.”
“Ndio kaka.”
“Makambako sehemu gani hiyo?”
“Ni karibia na stendi kuu. Hapa Magegele …..”
“Alaa Magegele napafahamu sana huko…kabla ya kuhamia huku nilikuwa
naenda na mabasi ya Dodoma Mbeya…sasa hapo Magegele kuna mgahawa
tulikuwa tunakula tulimzoea sana yule mama kiukweli..hata wewe nikutajia
lazima utakuwa unamjua..”
“Mama Kesho.” Niliwahi kumjibu. Akacheka sana, hakuna mtu wa Makambako ambaye hakumjua mama huyu. Alikuwa mkarimu sana.
Tulizungumza mambo mengi usiku ule. Alizungumza nami kwa ukarimu. Ni nani alikwambia kuwa watanzania sio wakarimu.
Kuna tofauti kubwa kati ya mtanzania na mbongo!! Mtanzania ana utu
lakini mbongo anajifanya mjanja mjanja. Huyu bwana alikuwa mtanzania
haswaa.
Upesi nikapata chakula. Kisha akaingia ndani akatoka na nguo. Zilikuwa za kike.
Akanieleza abiria huwa wanasahau nguo zao na kamwe hawarudi tena
kuzichukua. Nikamshukuru. Akanipatia na kiasi cha pesa. Akaniomba
nirejee majira ya saa tano asubuhi aweze kunifanyia utaratibu wa
kunisafirisha kurejea Mbeya kisha Makambako Iringa.
Ilikuwa bahati
ya kipekee sana kupata msaada huu. Lakini hapo hapo ilikuwa bahati mbaya
sana maana nisingeweza kusafiri peke yangu. Na yule bwana sikumueleza
tupo wengi zaidi ya kikosi cha timu ya mpira wa miguu.
Ubarikiwe sana!! Nilimpa Baraka hizo.
Kisha nikiwa na mavazi kamili sasa. Nikapiga hatua kwa hatua. Kigiza
giza kikanifanya nionekane kama kivuli. Mkono mmoja mfukoni kuzilinda
Kwacha (Pesa halali kwa matumizi ya Zambia) nilizopewa, mkono mwingine
ukiwa umeshika kiroba cha nguo nilizopewa na yule bwana. Isabela nikiwa
na raba nyepesi miguuni. Nikatoweka huku nikiamini nina mzigo mkubwa wa
kuwaokoa rafiki zangu ambao walinitazama kwa jicho la huruma.
Nilijihesabu kama mshindi wa vita ya 666. Lakini bado nilikuwa na vita nyingine ya kurejea nyumbani.
Mshindi akifia ugenini huyo ni mshindwa lakini akirejea nyumbani hata kama amejeruhiwa vipi bado ataitwa mshindi.
Mapambano yameanza rasmi!!! Nilikiri huku nikiwa nayatamani hayo
mapambano ambayo niliamini hayawezi kuwa magumu kushinda vita ya joka
kuu la msituni.
***HAYA SASA KAMANDA ISABELA OPARESHENI UKOMBOZI imefikia Ndolla Zambia. Nini kitaendelea katia nchi hii ya kigeni??
*** Je Davis amekufa?? Vipi kuhusu chata ya 666 katika shingo la John!!!!
MTUNZI: Emmy John P.
CONTACTS: 0654 960040
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
...
Joka lilijinyanyua juu. Sote tukawa chini yake. Joka lenye rangi ya
dhahabu!! Sasa ikawa patashika kila mtu analazimisha kujificha nyuma ya
mwenzake. Hakuna aliyetaka kufa. Mimi, Jenipher na wale wengine
waliokuwa wanatambua yule nyoka amekuja kufanya nini pale tulijiweka
mbali na vile vipande vya zile nya
ma zenye namba 666.
Joka
likavimba kama linataka kutema sumu. Likavimba zaidi kama linataka
kupasuka. Hatimaye likautoa ulimi nje. Likatanua mdomo kama linataka
kutumeza sote. Kisu chan gu bado kilikuwa mkononi.
Mara likajirusha
na kujizungusha kama pangaboi. Hapa hakuna kitu kilichosalia. Kila mmoja
wetu alirushwa mbali kabisa. Mimi sikuumia lakini wenzangu waliumizwa.
Nilipogeuka nilimwona kiumbe akiwa amelowa damu akiwa na jambia
mkononi. Alikuwa akikimbia mahali ambapo joka lipo. Alikuwa ni Samson
yule jasiri wa kisukuma.
Macho yako yalifumba kisha yalipofumbua
alikuwa ameingia mzimamzima katika kinywa cha yule nyoka. Jambia na yeye
wakawa wamemezwa.
Hali ya hatari!! Nilijitahadharisha.
Joka
lilikuwa linameza vile vipande vya mabaki ya nyama yenye chapa ya 666.
Ndipo hapa nilimuona tena yule Osmani aliyetambuliwa kama waziri wa
miundombinu. Nikakumbuka kuwa ni huyu bwana nimeambiwa kuwa anazijua
njia zote za kutoka katika mji huu wa kishetani. Nikamnyemelea huku
nikiwa makini na yule joka na pia nikiwa makini asiweze kuhisi chochote
kile.
Nikamfikia nikamkaba shingoni. Nilikuwa na nguvu za ajabu sana. Nikamvuta hadi katika kichaka nilichokuwa nimejihifadhi hapo.
Hakuwa ananiona!! Jambo hilo lilinipa nafasi nzuri ya kumtawala. Kwa
ukombozi wa wengi na kujitoa katika adha ya kufia katika mji huo.
Nikanyanyua kisu changu nikazamisha katika paja lake. Akatoa kilio
kikubwa sana. Kilio kile kikasababisha lile joka linyanyuke mara moja.
Likaanza kuangaza huku na huko. Nami nikatulia tulii kuangalia nini
kinatokea. Joka likanyanyuka kisha likatanua midomo yake. Kisha
likionekana dhahiri kuwa na hasira lilitapika. Maajabu!! Samson yule
jasiri katika vita hiyo akatangulia kisha jambia lake likafuata.
“Njia ya kutoka hapa ni ipi?” nilimuuliza Osman huku bado akiwa katika himaya yangu.
“Sijui.” Akanijibu kwa jeuri. Nikamchoma tena kisu katika sehemu ileile kilipopitia awali.
“Nasemaaaaa!” akapiga kelele.
“Dakika moja tu nakupa sema upesi.”
Osman akaanza kutoa maelekezo ya namna gani ya kutoka katika kijiji hicho cha maajabu!!
Maelezo yalikuwa yamenyooka!! Japo yalikuwa na masharti. Sikuwa na budi kuendelea kumshikilia. Ni huyu angetuwezesha kutoka.
Joka lilizidi kuhangaika.
Sasa lilitazama mahali alipokuwa Osmani na mimi. Likatambaa kwa hasira
kali sana likawa linatufuata. Nikajikuta namuiachia Osmani. Nikaanza
kukimbia. Joka likawa linaufuata uelekeo wangu.
Mungu wangu!! Kumbe linaniona sasa hivi. Nimekwisha.
Nilizidi kutimua mbio. Hatimaye mbio za sakafuni zikaishia ukingoni! Nikaanguka chini. Joka nalo hilo likanifikia.
Likaachama mdomo wake mkubwa.
Sasa nakufa! Nilikubali yaishe.
Achaaaaaa!! Nilipiga kelele za mwisho za kutokwa na roho. Huku
nikitegemea zitakuwa kelele za mwisho. Haikuwa hivyo. Niliweza kuwa hai
tena. Joka lilikuwa limeufumba mdomo wake. Likatulia tuli.
Nikaduwaa kulikoni nyoka huyu hajanimeza. Au! Au! …nikakosa majibu.
Joka likaendelea kutulia kama lina urafiki na mimi. Kwa uoga nikasimama
na kuanza kutambaa taratibu. Joka limetulia halina habari. Nikasimama.
Bado tuli! Nikaanza kuondoka hadi nikatokomea! Nyoka ametulia.
Maajabu makubwa sana haya!!
*****
Nilirejea hadi kule walipokuwa wanakijiji wenzangu. Osmani alikuwa
amehitisha mkutano tena. Alionekana mwenye furaha sana na ni kama
alikuwa anatoa karipio kali.
Samson niliyedhani amekufa kumbe
alikuwa amezimia tu baada ya kutemwa na yule nyoka. Nilimkuta akiwa
amefungwa kamba nyingi sana. Bila shaka adhabu yake ilikuwa imewadia.
Nilimuona Jesca pia. Lakini John pekee ndio nilikuwa sijamuona.
Nilikuwa na hasira. Nikatumia ule mwanya wa joka kutulia. Nikamvamia
Osmani. Nikamkaba tena. Safari hii sikutaka mambo mengi sana, nilihitaji
njia ya kutokea.
“Wakati wa kuwa watumwa wa shetani umekwisha.
Tunatakiwa kusihi maisha yetu tuliyoshi awali. Manyanyaso haya yote na
yasiendelee. Tusikubali kabisa uonevu huu. Sasa tunatoka humu. Kila
mwenye nia na aungane nami sasa. Tunatokaa!!” niliunguruma kwa sauti
kuu. Wale wasiokuwa na Chapa walinisikia na kuniona. Wale waliokuwanayo
waliduwaa wasijue kinachoendelea.
Samson alifunguliwa kamba alizokuwa amefungwa. Sasa Osmani akawa anatuongoza kuielekea njia ya kutokea.
Chapa ya 666 ilikuwa katika mkono wake wa kuume.
Kijiji kilikuwa kikubwa sana. Tulipenyeza njia hadi njia bado hatukufika tulipokuwa tunahitaji.
Sasa tulifika mahali palipokuwa na majani makavu lakini laini sana.
Tulipokuwa pale. Osmani akaniponyoka. Kisha akapiga mluzi fulani hivi.
Wakatokeza kenge wa ajabu. Wakubwa kama mamba. Walikuwa wanne. Na
dhahiri walikuwa na njaa. Walishambulia katika namna yha ajabu na upesi
sana.
Waliua! Watu kumi wakaanguka chini. Mamba wale badala ya kula nyama wakawa wananyonya damu.
Ilikuwa zamu yangu sasa. Osmani alikuwa pembeni akitucheka. Kuna unga fulani alijipaka usoni, sasa aliweza kuniona vizuri.
“Achaaaa!!” nilijikuta natamka neno lililoniokoa midomoni mwa joka lile
kuu. Kenge hawa wa ajabu wakatulia palepale wakafunga vinywa vyao.
Osmani akashangaa na mimi pia nikashangaa.
Samson ambaye naye alikuwa amekata tamaa alishangaa.
Nikawahi kuipoteza hali yangu ya kushangaa. Nikamwendea Osmani. Nikamkaba tena. Nikampiga makofi mawili akaanza kutema damu.
“Njia ya kutokea!!” niliamuru.
Akageuka, akatunyooshea mkono. Palikuwa na mlango mdogo wa mbao
zilizooza. Nikawaamuru wanakijiji wsaliosalia wapite. Wakapita!!
Hadi walipomalizika ndipo mimi na Osmani tulipita. Kabla hatujamaliza
kupitia nilisikia kilio kikubwa. Kuna mtu alikuwa akiniita.
Sauti ile ilikuwa ya John!
Nikasita kutoka. Nikarejea nyuma niweze kuchungulia.
John alikuwa anagalagazwa na lile joka kubwa.
Huruma ya mapenzi yangu kwa John ikanijia. Nikaweka kando yote
aliyowahi kunitendea. Nikarudi kwa kasi. Neno acha likiwa mdomoni
mwangu. N ilipofika nikaamuru kwa sauti kuu. Joka lile likatii kwa
nidhamu. Nikaduwaa. Nikamchukua John na kuanza tena kuitafuta njia ya
kutokea.
Kosa kubwa! Nilimuacha mbali waziri wa miundombinu!
Osmani akawa amepotea! Sikujua ni wapi pa kupita.
John hakuwa akiniona wala kunisikia. Nilitamani ajue ni mimi nipo naye. Lakini haikuwa hivyo.
Nilifanikiwa kukipata kisu. Nikaamini sasa nitaiondoa alama ya 666 katika mwili wake na ataweza tena kuona.\
Hofu! Na kukata tamaa. John alikuwa na alama ile shingoni mwake. Mwili ukafadhaika.
Siwezi kumchinja John!! Siwezi!! Niliapa.
Lakini nitafanya nini sasa.
Kitu kama tetemeko la ardhi likatwaa mawazo yangu. Nikamvuta John
asiyejielewa nikamkumbatia. Tetemeko hilo lilivyopita hapakuwa tena na
lile joka.
Lakini kitu kipya kikajitokeza. Ulikuwa mwanga mkali kama jua vile!! Nikatafakari ni kitu gani hicho. Sikuweza kutambua.
Mara ule mwanga ukapotea. Nikasja kushtuka nimepigwa kibao katika shavu langu. Nikaanguka.
Niliposimama nikapigwa tena, na sikumjuona kiumbe aliyekuwa ananifanyia hivyo.
Mapigo yakaongezeka. Nikawa navuja damu.
Sikuweza kusimama tena.
Sauti ya Jenipher ikanijia kichwani, “Ukinywa damu unakuwa kama wao!!”
Maneno hayo yakanifanya nipatwe na ari mpya. Nikatambaa nikamfikia John.
Badala ya kumchinja! Nitamnyonya damu walau kidogo tu.
Nikamfikia. Nikamkamata. Akaanguka chini, nikajirusha shingoni mwake.
Nilipoifikia shingo yake nikamkumbuka yule mganga wa kinaijeria. Hapo
sasa nikakumbuka sio mara yangu ya kwanza kunywa damu. Nikapenyeza meno
yangu pale pale kwenye alama ya 666 aliyopigwa shingoni.
Damu ikaanza kutoka. Nikaimeza huku nikiwa nimeikunja sura yangu.
Nguvu za ajabu zikaniijia. Sasa niliweza kumuona adui yangu aliporejea
tena. Alikuwa ni Dokta tuliyekutana katika mtandao, alikuwa ni Dokta
Davis.
Alikuwa ananisogelea tena aweze kunipiga. Nikaudaka
mkono wake. Akataka kujitoa hakuweza. Nikaweka sawa kisu changu
nilichokuwa nimekificha kwa nyuma. Nikazamisha katika sehemu zake za
siri huku nikipiga kelele.
Akaanguka chini na kuanza kujirusharusha.
Nikamkumbuka yule ninja wa kisukuma, Samson ambavyo hakuwa na huruma.
Na mimi nikamuiga. Nikamrukia Davis na kuanza kumchoma visu.
Nilipoanza tu kumchoma kisu cha kwanza mambo yakawa tofauti na yule
ninja wa kisukuma aliyekuwa akichoma kisu anaua hapo hapo...nikakumbwa
na mfadhaiko mkubwa.
Oparesheni ukombozi ikaingia doa jingine!!
***ISABELA katika mapambano ana kwa ana na Davis. Je nini hatma!! na ni kipi kimetokea mbona amefadhaika
***Je? John ndio amekufa baada ya kung’atwa na Isabela.
MTUNZI: Emmy John P.
MAWASILIANO: 0654 960040
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
Sasa tukazidi kufunguka akili kuwa yule nyoka anawaona watu wenye
alama. Na yawezekana ni nyoka huyu yupo katika kuwamiliki wanadamu kwa
chapa yake ya hatari.
Swali kuu likabaki. Tunatoka vipi katika pori hilo.
Mwanaume yule hakuzimia, alikuwa na timamu zake. Tukamweleza kwa kifupi
naye akajieleza kuwa, tamaa ya utajiri imemtupia katika shimo hili
baya.
Yule mwanaume alijitambulisha kwa jina la Samson
alikumbuka vyema kuwa kabla ya kufika hapo alikuwa mkazi wa jijini
Mwanza na alikuwa mwanafunzi katika chuo cha biashara (CBE) tawi dogo la
jijini Mwanza.
Huyu alikuwa Samson kweli maana alikuwa ni mbabe
sana. Lile kovu lake la kwenye paja halikumsumbua. Tulitembea kidogo
akachuma majani fulani akayasagasaga akayaweka katika lile kovu. Hapa
sasa aligumia kwa maumivu. Bila shaka ile dawa ilikuwa kali sana.
Akaniwekea na mimi katika kovu langu. Nikapiga mayowe. Akanikamata
imara. Hadi maumivu yalipotulia kidogo. Jenipher hakutaka kovu lake la
sikioni liguswe aliweza kuyakadiria maumivu makali ya dawa ile.
Siku mbili zilipita. Kovu lilikuwa linakauka kwa kasi. Nilimshangaa kijana huyu.
Siku hiyo ya pili harakati za kujikomboa zilianza rasmi. Jeshi letu bado lilikuwa dogo. Tulihitaji jeshi kubwa zaidi.
Samson alituongoza hadi katika ngome ambayo yeye alikuwa akishi hapo
kabla. Walioishi katika ngome hii ni wanaume wababe wanaoweza kufanya
kazi ngumu. Tuliindia hapa na kuwakuta wanaume sita waliojaa haswahaswa.
Kama ilivyo kawaida hawakuweza kutuona japo kila mmoja alikumbwa na
hisia za namna yake mwenyewe.
Mimi kisu mkononi. Samsoni panga kubwa mkononi, Jenipher kazi yake kukaba kwa bidii zote. Sisi wawili tukawa tunakata tu!!
Iwe sikioni hiyo alama. Sikio sio lako tena!!
Iwe kwenye mkono. Samsoni anaushusha mzima mzima.
Kama ni kiganja. Mimi naondoka nacho kwa kutumia kisu changu. Ikishindikana tu, panga kubwa la Samson linatimiza wajibu.
Waliokuwa wamewekewa alama katika vifua vyao hawa walitupa wakati mgumu
sana na tulilazimika kuwaacha wanaume wawili. Wanne tukaungana nao.
“Sam kwani we kabila gani?” nilimuuliza wakati tunaondoka.
“Msukuma wa Bariadi!!” alinijibu huku akijaribu kutabasamu.
Amakweli!! Hana huruma mtu huyu kama vile…kama kabila gani vileee…..
Nilipotea katika mawazo nikarejea katika uhalisia. Joka kuu tukapishana
nalo. Wenzangu wakakumbwa na uoga. Mimi sikuogopa tena. Nilijua kazi
gani linaenda kufanya.
Jeshi lilikuwa kubwa sasa na kila mmoja alikuwa na nia ya kuwa huru hivyo tulipambana kwa bidii sana.
Mapambano yalikolea sana kwani kila siku tuliongeza timu ya ukombozi.
Kilichotutatiza ni kuijua njia ya kutokea. Sasa tukiwa tunajiamini
kabisa siku hii hatukutembea kwa kundi kubwa bali kila mmoja alienda
njia yake huku akijiamini kabisa kuwa hawezi kuonekana. Nia ikiwa
kutafuta njia.
Shughuli hii ilianza asubuhi kabisa. Mimi na Jenipher tulienda njia yetu. Huku jeshi jingine nalo likienda njia tofauti.
Masaa yakapita na jioni ikawadia. Ile jioni ambayo tulikuwa tumekubaliana tukutane.
Tulingoja kwa muda mrefu lile eneo tulilokubaliana tukutane lakini wenzetu hawakutokea.
Tulisubiri sana, hatimaye giza likaanza kuiingia. Nikaingiwa na
wasiwasi, huenda wenzetu waliipata njia na sasa wapo huru wametusahau
sisi. Nilijilaani kwa kuruhusu hali hii ya kila mmoja aende kivyake.
“Jenny”
“Bela” aliitika.
“Unaweza kuwa unajua lolote kuhusu hawa watu.”
“Mh!! Kwakweli hata mimi nipo katika mashaka.”
“Wanaweza wakawa wamepata njia na kutoroka?” nilimuuliza.
“Kama hawajatoroka basi kwenye kambi ya usiku lazima watakuwepo.”
“Kambi ya usiku ndio nini?”
“Kila usiku wanachama ama wananchi wa mji huu huwa wanaitishwa kitu kama gwaride hivi, tena leo ni gwaride kuu.”
“Linafanyika wapi.”
“Nitakupeleka Bela. Lakini panatisha sana huko. Na sijui kama patakuwa salama.”
“Jenny pawe salama ama pasiwe salama..kwa sasa haina maana ujue bora kufa sasa..maisha gani haya unadhani.”
Jenny alikubaliana na mimi, akaniongoza kwenda katika kambi kuu. Kila
mtu alikuwa kimya sana. Nilikuwa namfuata Jenny anapoelekea. Hadi
tulipoona mahali panafuka moshi
“Huko wanakula nyama…na damu pia.”
“Kwa mifugo gani sasa?” nilihoji kwa sauti ya chini.
“Wananchi wanaotaka kutoroka huwa wananyonywa damu.” Nilishtuka sana kuisikia kauli hiyo.
“Na leo kuna mwananchi alitumwa damu kutoka Naijeria, ndio leo anaileta sasa.”
“Na wewe umekula nyama ya mtu?” nilimuuliza.
“Hapana hizo wanakula viongozi wakubwa tu. Mwananchi ukila ama kunywa
damu wanasema unakuwa kama wao. Kwa hiyo hairuhusiwi hata kidogo”
Alinieleza kwa utulivu mkubwa.
Tukaifikia KAMBI YA USIKU.
Shangwe zilikuwa kubwa na watu takribani hamsini walikuwa wakisheherekea.
“Ndio watu wote hawa ama kuna wengine?”
“Ni hawa tu!! Ujue hii ardhi ndio kwanza ilikuwa imeanzishwa.”
Nilikuwa kimya nikiwatazama watu kwa mbali tulipojificha. Nilimuona
John, nikamtambua na Jesca. Baadaye kila mmoja akatulia kuna mtu alitaka
kuzungumza neno.
“Leo raisi atakuwa amekuja. Isabela tuyondoke hapa.”
“Raisi ndio nani?” niliuliza kwa jeuri. Kuna kitu kama hasira kilikuwa kimenikaba kooni na sikuhisi uoga hata kidogo.
“Mkuu wa Nchi hii. Huwa haoneshi sura yake lakini anaitwa mtukufu raisi.”
“Na yule anayeonekana ni nani?”
“Yule tulitambulishwa kwake kama waziri wa miundombinu…njia zote anazifahamu yeye.”
Niliposikia hivyo nikatamani sana kumtia mikononi, mtu yule aliyeitwa
waziri wakati namfahamu kwa jina la Osmani!! Huyu alikuwa ni Osmani
mwanaume aliyenipatia namba ya simu 6666666. Na ni huyu huyu aliyenijia
ndotoni akiwa na John wakimkwapua mama yangu mzazi.
Sikuwa na uoga. Nilipiga hatua sasa nikawa nimejichanganya na watu hawa wachache waliokuwa wakimtumikia shetani.
Osmani alikuwa akiongea kwa maringo na kutumia amri sana.
Kila mtu alikuwa anamsikiliza.
“Leo damu ipo nyingi, nyama za kusaza.”
“Manson, Fanson, Rinzon, Wenton, Zeiron.” Alitaja vitu nisivyovijua na
kila alipotaja kuna mtu aliitika na kwenda mbele. Walikuwa wanaume
watano waliojaa vyema.
Bila shaka walikuwa wanaujua wajibu wao. Niliwaona wakizichukua kamba nene kabisa. Pamoja na visu.
Walitulia kwa dakika kadhaa, mara wakaletwa mbele yao watu ambao walionekana wazi kuwa walikuwa wamechoka sana.
Nilimuona Samson akiwa amevimba sana kutokanaq na kipigo. Hasira ikanipanda. Nikatulia tuli!!
Wanaume wale walioitwa kwa majina ya ajabu wakatumia kamba zile kutengeneza namna ya vitanza, kisha wakavitundika mtini.
Mwanaume mmoja akamchukua mvulana kutoka katika lile kundi. Mvulana
yule hakuwa na sikio. Nikamkumbuka ni mimi niliyemkata ili kumtoa katika
ulimwengu huu wa giza.
Nikiwa sijatafakari nini cha kufanya,
nikashuhudia damu ikikingwa kutokea shingoni. Kisha akatupwa katika
kitanzi. Alikuwa maiti!!
Samsoni akavutwa akataka kuleta ukorofi.
Akachapwa na mjeledi akapiga yowe kubwa huku akitukana matusi mazito
maziro kwa kabila la kisukuma.
Alipotukana akanikumbusha wakati aliokuwa ananiambia jina lake. Nikajisikia uchungu.
Liwalo na liwe!! Nikaanza kusogea mbele. Bado Samson alikuwa
akiwasumbua. Maajabu nikafika mbele ya hawa wanaume hawakuweza kuniona.
Nikajaribu kumsukuma mmoja aliyekuwa na kisu tayari kwa kumchoma Samson.
Haya yakawa maajabu makubwa. Isabela mimi namsukuma mwanaume mkubwa
kama yule anaanguka kwa kishindo hivyo. Samson mwamba wa kisukuma,
msukuma kutoka Bariadi akafanya jambo ambalo hadi leo ni kumbukumbu
kwangu. Haraka akaokota visu viwili, akavimba kwa hasira kifua chake
kikaweka mfereji mkubwa. Samsoni alikuwa amevimba kama mcheza mieleka.
Bila shaka zilikuwa ni hasira kali za nusu mwanadamu na nusu mfu. Maana
bila jitihada zangu angeuwawa.
Nikabaki kushangaa. Akamrukia mwanaume mmoja sijui ndio Frazon, Manson ama vipi. Kisu kimoja. Mwisho wa uhai.
Akakichomoa akamrukia yule ambaye alikuwa chini baada ya mimi
kumsukuma. Visu viwili vikazama katika sehemu zake za siri. Damu
ikaruka. Nikasisimka sana!! Samson hakujali.
Sasa yule Osman akawa
ametaharuki. Hajui nini kinatokea. Na yeye hakuwa ananiona. Nikamwona
akimjaribu kumfuata Samsoni huku akiwa na jambia. Samson hakuwa
anamuona.
“Saaam!! Saam!! Nilimuita.” Maskini hakunisikia.
Osmani na jambia. Akalichomoa mahali ambapo linahifadhiwa.
Akalielekezea alipo Samson. Alipoanza kukimbia na mimi nikashtuka
nikaanza kukimbia. Kabla hajamfikia. Mimi nikamfikia. Nikafanya
kumsukuma. Akapepea kama karatasi. Takribani mita arobaini kutoka pale
nilipokuwa. Samson alipogeuka, hakunitazama mimi bali alitazama chini.
Akakumbana na jambia.
Msukuma huyu mkali kabisa wa mapambano akatupa visu chini akatwaa jambia.
Ilimchukua dakika chache. Manson, Fanson, Rinzon, Wenton, Zeiron. Wote
wakawa tayari kwa kuzikwa kama hiyo nchi yao ina huo utaratibu wa
kuzika.
Samson alikuwa kidume!! Nilikiri.
Kidume yule ambaye
hakuzisikia sifa nilizokuwa nampa. Alizidi kunidhihirishia kuwa kile
kifo cha yule mvulana cha kuchomwa kisu shingoni kilimuuma. Aliendelea
na zoezi la kuwaondoa wananchi kadhaa kwa fujo zile alama za 666 popote
zilipo katika miili yao. Ilimradi tu hakuwaua.
Nia ikiwa kukuza jeshi letu!!
Nami nikamuunga mkono!! Jenny naye huyo akaokota kisu kikubwa kaanza kufanya kazi.
Tulilolifanya hapo lilikuwa kosa kubwa sana. Alama za 666 zilizokuwa
zinaanguka katika mfumo wa vipande v ya nyama. Ukaleta balaa.
Joka kubwa kuliko lile la awali likaibuka. Joka hili sasa lilikuwa halijulikani wapi mbele na wapi nyuma.
Lilikuwa na vichwa viwili. Mbele na nyuma.
Halikujulikana linatambaa kwenda kaskazini ama kusini, magharibi wala mashariki.
Yule bingwa wa mapambano Samson akajikuta analiachia jambia lake, Jenny
aliyekuwa anaanza kunogewa na shughuli ya kukata nyama za watu naye
akatulia tuli. Alikuwa anatetemeka
Nami nikakumbwa na uoga na nikakiona kifo kikibisha hodi.
Isabela nakufa!! Nakufa nikiwa katika u…”
Kabla sijamaliza kuwazua. Ghafla……..Ghafla!!!!!
Ilikuwa ghafla sana!!!!
****JOKA KUBWA linaingilia harakati za ukombozi huu. Lina vichwa viwili.
**Si Isabela wala yule msukuma bingwa wa kupambana anayejiamini tena.
***Nani wa kuwakomboa viumbe hawa???? Iwapo Isabela anaogopa???
***Nini hatma yao.
MTUNZI: Emmy John P.
CONTACTS: 0654 960040
SEHEMU YA ISHIRINI
...
Ikiwa bado sijaweza kusimama. Lile joka lililopotea njia sasa lilionekana tena. Safari hii lilikuwa linakuja kwangu tena.
Bora nife!! Nilijiapiza. Sasa nikaanza kutambaa kumfuata huyo nyoka.
Mkononi nikiwa na kisu ambacho nilikiokota, bila shaka ni kile
kilichotumika kunikata nyama.
Nikawa natambaa kama joka lile linavyotambaa. Sikuwa naijua nia yangu. Lakini nilihisi ni vyema kufa kuliko mateso haya.
Lile joka likazidi kunisogelea, macho yake makali yakiangaza huku na
huko. Urefu wa joka lile la dhahabu likiwa na kipande cha nyama mdomoni
ulinitia kwenye hofu. Nikajiuliza iwapo kisu changu kinaweza kupenya
katika ngozi yake, nikajipuuza maana kisu changu kilikuwa kidogo sana.
Nikasita kutambaa. Nikatulia tuli, huku nikiamini kuwa ni heri linimeze
kistaarabu kuliko kunimeza likiwa na hasira baada ya mimi kujaribu
kupambana nalo. Nikafumba macho nikakitupa kisu changu chini,
nikajinyoosha tayari kwa kumezwa.
Haikuwa ndoto kwamba nikifumbua
macho nikutane na mashuka yangu masafi ya kuvutia yakinibembeleza kulala
badala yake nilipofumbua macho. Joka kuu hili hapa!!
Ubaridi wake ukapenyeza sasa, lilikuwa juu ya mwili wangu, pumzi zikawa zinaniishia. Ndio ninamezwa au? Nilijiuliza.
Nikaanza kugalagazwa kadri lilivyokuwa linajivuta. Sasa ile hamu ya
kufa ikatoweka baada ya lile kovu langu makalioni kupatwa maumivu
makali. Maumivu yaliyosimamisha misuli yangu. Nilipogeuka kujitazama
nikakuta kuna mwiba umezama nikajivika ujasiri nikauchomoa. Sikuwa
navutwa tena. Nilitazama mbele nikalishuhudia lile joka likienda zake.
Inamaana huyu nyoka hakuniona ama!! Nilitafakari. Nikashangaa.
Damu zilikuwa zikinitoka tena, sasa haikuwa katika kovu tu, bali na
sehemu nyingine. Lile joka lilikuwa limenivuta hadi katika mti wa miiba
na ni hapo nilipojitonesha.
Pori likatulia kimya, kimya kikawa
kirefu sana. Nikawa nahisi kiu kikali. Lakini hapakuwa na maji. Usingizi
ukanisaidia kuikwepa karaha hii. Nikasinzia.
Mwanga wa jua ndio
ulionishtua. Nikakurupuka. Ni uchi!! Nikajishangaa kisha nikawahi
kujiziba lakini bahati mbaya hakuwepo ambaye alikuwa ananichungulia.
Nilikuwa peke yangu katika pori lile.
Hakuna mnyama, hakuna mmea ninaoufahamu, hakuna hata mdudu!! Lilikuwa pori la maajabu, pori la mateso makali kwa kiumbe hai.
Nilisimama wima, nikajisikia dhaifu sana lakini sikutakiwa kuendelea
kuwa lelemama, nikiwa nachechemea nilianza kuzunguka huku na kule
niangalie uwezekano wa kupata msaada. Harakati zangu sasa zikazaa
matunda, kwa mbali nilimuona mtu akiwa analima. Alhamdulilah!!
Lilikuwa jambo maalumu kwa wakati maalumu. Nikajongea kwa kujikaza hadi
nikalifikia lile shamba. Hakika mtu huyu alikuwa mchapakazi. Alikuwa
peke yake na shamba lilikuwa kubwa sana.
“Kaka!!....Kaka…” Sauti ilitoka kwa taabu, nadhani hakuweza kunisikia.
Nikataka nimsogelee. Lakini ghafla akageuka. Ni kama aliuhisi uwepo wangu pale.
Japo alikuwa amechakaa sana. Nguo zikiwa zimeraruka, lakini niliweza
kumtambua. Huyu mtu alikuwa ni marehemu. Zaidi ya kuwa marehemu, kifo
chake niliwahi kukiota. Basu!!
Hakusema neno alipogeuka na wala
hakunitazama, ni mimi niliyeiona alama ya 666 kifuani pake. He!
Anamilikiwa!! Nilitafakari. Nikatimua mbio. Mbio za kuchecheme
ziliniumiza lakini nitafanyaje??
Akili yangu ilikuwa sawa kabisa.
Nilikuwa namkumbuka vyema Davis. Nilijuta kukutana na bwana huyu katika
mtandao na kumuamini sana. Nilijutia na pesa alizokuwa akinipatia.
Mara nikaanguka!! Nilikuwa nimegongana na kitu kigumu. Ajabu na kweli
haukuwa mti bali mtu. Jesca! Jesca na urembo wake alikuwa amebeba ndoo
kubwa ya maji, alikuwa peku na alikuwa amepauka sana. Hata Jesca naye
hakunitazama, badala yake aliendelea na safari zake huku akinipa nafasi
ya kuitazama alama ya 666 katika mkono wake.
“Jesca!! Jesca!!” hakunijibu na dhani hakunisikia. Akatoweka.
Sasa sikukimbia tena, ina maana hawa watu hawanioni. Na kama hawanioni hata lile joka halinioni. Nilijiuliza.
Kwani kuna kitu gani sifanani nao? Nilipojiuliza hivyo. Nikaikumbuka
alama ya ‘666’ iliyokuwa imetolewa katika upande mmoja wa makalio yangu.
Alama hii ni ile ninayoijua ama kuna utofauti? Nilitafakari. Jesca huyo
akawa ametoweka. Nilipoendelea mbele kidogo nikakutana na kile kisu
nilichokitupa. Nikakitwaa. Nikazunguka huku na huko nikiwa uchi
nikaipata ile kanga yangu, nikaivaa, wakati naivaa ndipo nilikumbuka juu
ya watu wawili niliokuja nao huku katika kujisafisha na alama hiyo
mbaya.
Nilipowakumbuka nikalikumbuka na kaburi lililokuwa wazi.
Nikazungukazunguka na sasa nilikumbana nalo. Huenda walikuwa
wamejichimbia kaburi hili. R.I.P na mwenzake walikuwa wamejizika huko.
RIP yule bwana mwenye mbwembwe, mwingi wa maneno mtaalamu wa kucheka
alikuwa ametlia tuli katika kaburi akisubiri kufukiwa!!!
Amakweli
wewe ni Roho Iliyo Potea!!! Nilikiri kimoyomoyo baada ya kugundua kuwa
sasa RIP amepotea kweli kama jina lake lilivyokuwa. Nilisikitika kuwa
hakuwa amenieleza mambo mengi juu ya alama hizi za maajabu.
Jambo
moja la muhimu alilonieleza ni kwamba nilikuwa namilikiwa. Kuna mtu
alikuwa ananimiliki. Ili nisimilikiwe ilikuwa lazima alama hiyo ifutwe.
Sasa nilikuwa nimekatwa kipande cha nyama. Damu hainitoki tena na
sihisi kichefuchefu cha mimba. Ina maana ndio similikiwi tena?
Nilishangaa.
Lakini sasa mbona siwezi kutoka humu porini? Nilijiuliza sikupata jawabu.
Mawazo yangu yalikatishwa na sura ya mtu mwingine aliyekatisha mbele
yangu. Huyu alikuwa ni marehemu mwingine ambaye tulisoma chuo kimoja
enzi za uhai wake.
Hivi niko peponi ama jehanamu? Kwa nini sasa nakutana na maiti tu.
Huyu naye hakuonekana kunifahamu. Alikuwa na alama yake sikioni.
Nikakumbwa na moyo wa kujaribu. Kama mimi nimekatwa kipande cha nyama na
alama imetoweka, nikaamua kujaribu kutumia mbinu ya RIP ambaye sasa ni
marehemu.
Nikamnyatia yule binti. Nikakiweka kisu changu tayari
nikamkaba. Bila kukumbuka maumivu atakayoyapata nikafyeka sikio lake.
Nikasisimuka lakini katika nafsi nikikiri kuwa kile kisu kilikuwa kikali
sana. Sikio chini!! Yule binti naye chini, akawa anatoa kilio kikubwa
sana. Kitu cha ajabu hakuna msaada alioupata. Mimi nikajiweka mbali
niweze kuwa shahidi wa nini kitakachotokea.
Mara upepo mkali ukaanza
kuvuma. Miti ikayumba, pori likatulia na sasa alitokeza nyoka mkubwa,
ni yule yule wa awali. Nikataka kukimbia, nikakosa ujasiri nikaendelea
kujificha, joka lile likatambaa hadi katika ule mwili unaogalagala,
kisha likakwapua lile sikio na kisha kuanza kuzurura huku na huko hadi
lilipotoweka ndipo nilipomsogelea yule binti. Alikuwa ametulia tuli na
damu haikuwa ikivuja sana.
Nikamgusa. Akajigeuza, akanitazama. Mungu wangu!! Tiba inafanya kazi ile. Aliniita jina langu. Akakaa kitako.
Sikuwa nikiamini lakini sasa nikampongeza RIP yule tahira niliyemdharau sasa alikuwa njia.
“Na wewe umejiua?”
“Nimejiua?” nilimuuliza.
“Isabela kwa nini uliniua?” alinihoji. Nikashangaa.
“Mimi nilikuua wewe.”
Yule binti alinieleza kila kitu, akanisimulia alivyouwawa akiwa
ndotoni. Akakiri kuniona mimi nikimmaliza huku ninacheka. Akanielezea
juu ya sauti alizozisikia. Ni sauti zile zile na mimi nilizisikia katika
kifo chake na pia katika mazishi ya yake, hata Jesca alipokufa
zilisikika.
Niliamini tena kauli ya RIP kuwa kuna mtu ananimiliki na
ananifanya anavyotaka yeye kwa wakati wake. Huyu mtu ni nani?
Nilijiuliza huku tuhuma za kwanza nikizitupia kwa Dokta Davis.
******
OPARESHENI UKOMBOZI
Jenipher alinieleza mambo mengi huku akinisaidia kupata chakula na
maji. Chakula kilikuwa kizuri na maji yalikuwa safi lakini namna ya
kuvipata ilikuwa ya namna yake. Wakati huo na yeye hakuweza kuonekana.
Chakula na maji pekee havikuwa vitu tulivyokuwa tukihitaji. Kikubwa
tuliuhitaji ukombozi wetu na wanadamu wengine wanaomilikiwa na watu
wabaya.
Sasa ilikuwa ni lazima kuuvaa moyo wa ujasiri ili kufanya
harakati za ukombozi. Tuliwahitaji wanaume wenye nguvu waweze kuungana
nasi.
Basu akawa chaguo la kwanza! Tulimtegea siku akiwa katika kulima shamba kubwa lisilotoa mazao.
Tulifanikiwa kumpata kwa wakati. Huku tukiwa tunajiamini kabisa.
Tulimvaa kwa nguvu akaanguka chini huku akiwa haoni lolote. Anaangaza
kushoto na kulia. Nikachomoa kisu.
Alama ipo kifuani!! Huu sasa ukawa mtihani. Nichome au nisichome..nikimchoma maana yake ninamuua. Nikabaki kujiuliza.
Hali hiyo ya kujiuliza, ikapoteza sekunde kadhaa. Ni katika sekende
hizo, nilimshuhudia Jenipher akirushwa mbali kisha nikamwona nyoka
akimshambulia. Nikajitoa katika mwili wa Basu nikiwa na kisu changu
nimesimama wima. Nilimshuhudia Jenny anavyohangaika. Na nyoka yule
alikuwa ni mdogo sana. Nikajitoa muhanga.
Bila kusita mbio mbio. Kisu mkononi huku nikipiga kelele nikamfikia yule nyoka nikamfyeka. Akagawanyika vipande viwili.
Jenny akasimama. Hakuwa amejeruhiwa. Tukatoweka mahali hapo. Tukamwacha Basu akiwa katika taharuki asijue nini kimetokea.
Hatukuwa tumezungumza lolote. Hadi pale tulipokutana na mwanaume
mwingine. Huyu alikuwa ametoka kukata kuni. Tulimpisha njia kisha
tukamfatya kwa nyuma tukamvamia, akapiga mweleka. Alipojaribu
kurusharusha miguu. Alama ile chafu ikaonekana katika paja lake. Bila
kujiuliza Isabela mimi nikafanya kama nachuna mbuzi. Nikaikata nyama ya
paja lake. Mwanaume huyu akalia kama mtoto.
Nilipoiondoa nikaitupia mbali. Baada ya muda akatokea yule nyoka akakichukua kile kipande.
Sasa tukazidi kufunguka akili kuwa yule nyoka anawaona watu wenye
alama. Na yawezekana ni nyoka huyu yupo katika kuwamiliki wanadamu kwa
chapa yake ya hatari.
Swali kuu likabaki. Tunatoka vipi katika pori hilo.
Mwanaume yule hakuzimia, alikuwa na timamu zake. Tukamweleza kwa kifupi
naye akajieleza kuwa, tamaa ya utajiri imemtupia katika shimo hili
baya.
***ISABELA ameanzisha OPARESHENI UKOMBOZI….je atafanikiwa??
***Vipi kuhusu mmiliki wake….je ndo mwisho wa enzi??
MTUNZI: Emmy John P.
CONTACTS: 0654 960040
SEHEMU YA KUMI NA TISA
...
R.I.P hakujali kama nilikuwa nimeshtuka ama la! Aliendelea kuongeaongea
huku akiwatukana matusi mazito ya nguoni wale maiti kama vile
wanamsikia. Hakika alifanana na mtu aliyerukwa akili. Kuishi na maiti
napo kazi sana huenda ndo maana amechanganyikiwa.
“Ulisema unaitwa nani vile.”
“Naitwa Isabela.”
“He!! Unaitwa Isabela, yupo mwenzako humu hebu njoo umuone.” Akanivuta
kwa kutumia nguvu sana hadi mkono ukashtuka. Yeye hakujali hayo.
Akanivuta vuta hadi tukafikia kabati jingine. Nikajiandaa kushuhudia
maluweluwe mengine.
“Hili nalo lilikuwa linakula nini sijui
likanenepa hivi. Majitu mengine mapumbavu sana ujue. Heri yako wewe
haujanenepa sana.” Alizungumza peke yake.
Akatumia mikono miwili akavuta. Likatoka bonge la mwanamke. R.I.P akaanza kucheka, kicheko kikubwa hadi akatoa machozi.
“Anaitwa Isabela huyu, mpumbavu sana huyu alienda kunenepeana huko.
Amewasumbua sana siku ya kumleta humu ndani. Kuna vindugu vyake,
vyembamba hivyo basi likawa linawaponyoka. Linaanguka puu!!” alisimulia
huku anacheka. Mimi sikuwa namuelewa.
Kisha tukarejea tena mahali tulipokuwa nikalazimika kukaa juu ya lile jokofu la kuhifadhia maiti.
“Au nimlete Isabela make nae, Isabela bonge.” Aliniuliza. Mimi nikawa namshangaa. Yaani alikuwa kamna mpumbavu fulani.
“Isabela….umewahi kufa wewe?” aliniuliza.
Swali gani sasa hili la kijinga!! Nikawaza.
“Bado”
“Mwenzako niliwahi kufa. Na wewe una hamu ya kufa.”
He!! Umewahi kufa….kivipi.”
“Kwani mtu akifa anakuwaje?” aliniuliza, sikujibu.
Akaendelea, “hebu tuachane na hayo..msichana mdogo kama wewe ukifa sio vizuri ujue.”
“Kama ukiwa makini hautakufa. Tena wewe hautakufa, nitakusaidia usife sawa!!”
“Sawa!!” nilijibu kwa nidhamu kubwa.
“Njoo huku…”
Nikamfuata hadi mahali patulivu kabisa. Sasa hii ilikuwa ofisi kweli.
R.I.P akanipokea. Akaniacha ofisini kwa muda, kisha akaingia tena baada
ya dakika kadhaa.
Hakuwa yule tahira, hakuwa mchafumchafu kama
nilivyokueleza mwanzoni. Huyu alikuwa na hadhi ya yule mvulana
ninayemuhitaji. Alikuwa mtanashati.
Hakuwa akicheka hovyo! Alikuwa makini na mtaratibu.
Roho Iliyo Potea (R.I.P). Alianza kwa kujitambulisha jina lake halisi.
Kisha akaniupongeza sana kwa ujasiri wangu hadi kufika hapo.
Akajieleza kwa ufupi maisha yake ya utafutaji huku na kule hadi
alipojikuta akitafuta kwa njia za mashetani. Ni katika maelezo haya
alinieleza juu ya namba 666. Nilishangazwa sana na maelezo yake lakini
nilipiga moyo konde nikiamini tiba ipo.
Baadaye akanieleza jinsi
alivyojitoa katika harakati hizo za kumtumikia shetani. Haikuwa njia
rahisi. Aliwapoteza ndugu zake kadhaa lakini mwisho akawa amejikomboa.
"Hiyo chapa uliyopigwa lazima ifutwe! Ni njia hiyo tu ya kukukomboa
kutoka ufalme huo. Wewe unamilikiwa na mtu kuna mtu wewe ni mtu
wake..anakutumia anavyotaka" alinieleza kwa sauti iliyomaanisha
msisitizo
Nilikuwa makini nikimsikiliza.!
USIKU MNENE
Safari ya kuelekea kuitoa ilea lama ilikuwa imewadia. Pesa taslimu
milioni moja ilikuwa imenitoka tayari ili kufanikisha jambo hili.
Tulitumia usafiri wa gari binafsi. Tulikuwa watatu. Mimi, RIP na
mwenzake ambaye sikuwa namjua jina. Yeye alikuwa anaendesha gari.
Sasa gari ilisimama. Tukashuka garini. Nilikuwa nimevaa upande wa kanga
kama RIP alivyoniagiza. Tulitembea kwa muda hadi tukakifikia kichaka.
Hapakuwa na vibuyu wala dawa za kienyeji lakini tulikuwa mbele ta
kaburi, hilo kaburi lilikuwa likimsubiri mtu limmeza. Yaani lilikuwa
wazi.
Mara akachomoa kisu, akachomoa na kisahani.
Nikaamuriwa kuvua nguo!! Nikavua. Nikawa uchi mbele ya wanaume hawa wawili. Sikuwa na aibu!!
R.I.P akatoa sindano akavuta dawa. Akanigeuza, nikageuka.
Akanidunga sindano. Hii ya sasa ilipenya. Nikaisikilizia maumivu yake
kisha taratibu nikasikia mguu wangu wa kulia unakufa ganzi.
Kisu kikatwaliwa upesi. Ilikuwa saa sita kasoro dakika sita. Hii ni kwa mujibu wa RIP.
Sikujua kinachoendelea lakini nilipotazama chini niliona kitu kama maji
vile. Ghafla ikasikika sauti. Sauti ya kike ikiniita kwa mbali. Sauti
ile ilikuwa inanisihi sana nikimbie.
Nikimbie kwenda wapi sasa.
RIP na mwenzake walikuwa wameshikilia kile kisahani. Sasa niliweza kuona
kipande cha nyama. 666 zilionekana zikiwa katika mng’aro wa dhahabu.
Nikiwa sijajua lolote linaloendelea. Mara ghafla ile sauti sasa iliweza kusogea zaidi na zaidi.
Hatimaye aliyekuwa anaita kwa juhudi zile nikamuona. Alikuwa ni Maria,
yule rafiki yangu tunayeishi naye. Alikuwa yu uchi wa mnyama. Alikuwa
akikimbia kwa juhudi zote lakini hakuwa akikimbia bure kuna kitu ama mtu
alikuwa anamfukuza.
Nikajaribu kupiga kelele. RIP na mwenzake hawakunisikia.
Maria alikuwa anakimbizwa na nyoka. Nyoka mkubwa alikuwa anang’ara sana. Nashangaa wenzangu hakumuona.
Nikajikuta natimua mbio uchi. Na nilikuwa kitendo cha sekunde chache
yule nyoka akavamia eneo lile. Sikushuhudia sana kilichowatokea
wenzangu. Sasa nikaanza kuhangaika huku na huko katika pori hilo ambalo
sikuwa nalifahamu.
Mguu mmoja ukiwa umekufa ganzi. Ningeweza vipi
kukimbia mbio ndefu. Isabela mimi nikaanguka chini. Sasa nikawa najivuta
kama nyoka. Nalia kama mtoto. Sikuwa na uelewa bado kwa nini mguu wangu
ulikufa ganzi. Lakini kumbukumbu za kuchomwa sindano ile kali zilikuwa
kichwani mwangu.
Nikiwa bado sijapata jibu sahihi. Lile joka la
maajabu sasa likatokeza mbele yangu. Mdomoni likiwa na kipande cha
nyama. Nyama ile yenye namba 666.
Nikajiinamia kwa uchungu.
Nikafanya dua fupi. Nikajilaani kwqa kila hatua ya maisha yangu
niliyopitia. Nikatamani ningekuwa na nguvu niweze kutimua mbio. Lakini
tayari nilikuwa nimelegea. Macho yakazidi kuhesabu hatua za yule nyoka
kunifikia. Sijawahi kuona nyoka mkubwqa kama huyu!!! Nakufa kwa kumezwa
na nyoka. Inauma sana!!
Joka likazidi kusogea!! Joka kuu likawa linatambaa!!!
Kabla joka halijanifikia. Lilibadilisha uelekeo. Ni kama kuna kitu
lilikuwa limehisi. Likaanza kutambaa kuelekea upande mwingine.
Joka linatoka mara sasa namuona John. John yule mpenzi wangu ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha pale chuoni.
“John…John!!” nilianza kumuita. Sauti ilikuwa imekauka. Haikutoka.
Joooooh!!! Nikajaribu tena, nikawa kama ninafanya mnong’ono. John akawa
anaenda zake. Nikalia sana kuikosa nafasi hii hadimu ya kusikiwa na
John!! Huenda angeweza kuwa msaada mkubwa kwangu.
Ubaridi
ulipenya katika mwili wangu. Mwanzoni niliuhisi kuwa wa kawaida lakini
baadaye nikahisi kama maumivu hivi. Nikajipapasa. Nilipoutazama mkono
wangu ulikuwa na damu. Nikageuka kujitazama sehemu zangu za nyuma.
Maajabu!! Nilikuwa na kovu kubwa sana!! Na palikuwa pamechimbika. He! Ina maana nilikatwa nyama yangu ya…..!! niliduwaa.
Maumivu yakazidi. Na sasa giza likazidi kuchukua nafasi yake baada ya
mbalamwezi kutoweka. Giza nene!! Hapo bado nilikuwa sijaweza kunyanyuka
imara. Nikajaribu kujikunjua nisimame. Maumivu makali katika makalio.
Nikaanguka kama mzigo. Nilipoanguka palikuwa na kisu kipya, kikiwa na
damu.
Nikaendelea kulia. Sauti haitoki.!! Nilikuwa katika jaribio kuu maishani.
Ikiwa bado sijaweza kusimama. Lile joka lililopotea njia sasa lilionekana tena. Safari hii lilikuwa linakuja kwangu tena.
Bora nife!! Nilijiapiza. Sasa nikaanza kutambaa kumfuata huyo nyoka.
Mkononi nikiwa na kisu ambacho nilikiokota, bila shaka ni kile
kilichotumika kunikata nyama.
Nikawa natambaa kama joka lile linavyotambaa. Sikuwa naijua nia yangu. Lakini nilihisi ni vyema kufa kuliko mateso haya.
***ISABELA katika msitu asioujua. Kisu mkononi anataka kukabiliana na JOKA KUU la rangi ya dhahabu.
***RIP na mwezake wako wapi. Maria naye vipi huko msituni amefikaje?...JOHN? vipi naye kumbe hakufa ama!!
MTUNZI: Emmy John P.
MAWASILIANO: 0654 960040
SEHEMU YA KUMI NA NANE
...
Ni kama daktari alikuwa haamini ambacho amekiona, katika mwili wangu na
alichokuwa akifanya pale ni kunitoa tu katika hofu. Mabadiliko ya mimba
yangu yalimfanya achanganyikiwe. Tulirejea katika chumba chake cha ofisi. Mazungumzo yaliyokuwepo ni juu ya kuitoa mimba ile.
Daktari alikataa kata kata akidai kuwa mimba ikifikisha miezi sita na
msichana akijaribu kuitoa basi lazima atapatwa na matatizo na kuna
uwezekano wa kufa. Maelekezo ya daktari yaliyoambatanishwa na neno
KUFA yalinipa ahueni ya nafsi kwa sababu nilikuwa nataka kufa. Sikuwa na
ujasiri wa kujiua na hakika nilikuwa naogopa kufa. Lakini kufa kwa
namna anayoitaja daktari hata hakunipa hofu badala yake nikavutika na
kumsihi anisaidie kuitoa ile mimba. Mazungumzo yalikosa kabisa
muafaka. Daktari yule alikuwa mbishi sana hakutaka kushiriki katika
utoaji mimba huu. Nilipoona daktari huyu amekuwa na msimamo sana
niliamua kutumia njia fulani ambayo hugeuza ukweli kuwa uongo na uongo
kuwa ukweli. Nikaangusha mezani shilingi laki mbili. Akazikataa, nikaaga
nikatoka. Niliporejea niliziongeza zikafika laki nne. Daktari
akazikodolea macho, kisha akatazama kushoto na kulia. “Umekuja na nani?” akaniuliza.
“Mwenyewe!” nikamjibu. Akatazama tena kushoto na kulia kisha
akazikwapua zile pesa akazizamisha katika sehemu zake za siri.
Nikakwepesha macho. Akanifanyia ishara ya mkono. Nikamfuata hadi
katika chumba kilichokuwa na harufu kali ya madawa. Akakifunga na funguo
tukabaki wawili tu! Kimya. Daktari alikuwa na hofu. Nililitambua hilo. Sikutaka kuuliza chochote.
“Toa nguo zote.” Aliniamuru. Kauli yake ikanikumbusha kauli ya yule
Mnaijeria aliyetaka kunibaka kwa kujifanya ananifanyia tiba ya asili.
Huyu sasa alikuwa daktari, nikaamua kucheza pata potea. Kwanza nilikuwa
natokwa damu. Sidhani kama angeweza kujaribu kunibaka. Nikaziondoa
zote, wakati huo yeye alikuwa amejikita katika kuchanganya madawa yake
ambayo sikuelewa kazi yake ni ipi. Nikabaki kumsubiri. Njoo hapa!! Aliniamuru huku akinielekezea kitandani. Geuka hivi!! Nataka kukuchochoma sindano. Nikageuka huku nikiwa katika uoga. Kifo! Nilikuwa naogopa kufa.
Nikahisi kitu cha baridi kikinipapasa. Nikauma meno yangu kungoja
uchungu wa sindano. Nilingoja huo uchungu lakini hamna nilichohisi.
“Acha kujikaza wewe sindano itakatikia ndani.” Alinigombeza daktari.
Nikashangaa hizo lawama zinatoka wapi wakati mimi hata sijajibana.
Alipoona simjibu kitu akanichapa kibao. Nikashtuka. “Mkubwa hivyo unaogopa sindano alaa!!” alinigombeza. Sikumjibu!! Nikatega tena aweze kunichoma!! Hali ikawa vile vile. “Sasa mimi nakuchoma hivyo hivyo.” Alichukua maamuzi yake binafsi. Nikageuka. Nikayasubiri maumivu!!
Badala ya maumivu nikakumbana nay owe kubwa kutoka kwa daktari.
Nilipogeuka na mimi nikiwa na hofu nikamkuta amekaa chini. Mbali na
mimi. Alikuwa ana hofu!! Jasho likimtoka. “Daktari!!.” Nilimuita. Hakunijibu, alikuwa katika mshangao. Alikuwa akinitazama kwa wasiwasi.
Nilikuwa siijui tena thamani ya kuwa na mavazi na aibu ya kuwa uchi.
Nilitapatapa hivyohivyo pale ndani. Daktari akiwa bado ananishangaa. “Vaa nguo!” aliniamuru kwa sauti ya chinichini. Nikaziendea nguo zangu na kuzivaa. Kisha nikamfuata hadi ofisini! “Chukua pesa zako!!” alinikabidhi pesa zile. Nilisita kuzichukua akanisihi nizichukue. Nikatii!! Nini kimetokea daktari? Nilimuuliza. Hakunijibu bali alisikitika.
Kisha akaanza kunielezea juu ya nini alichokiona. Ilikuwa ni alama ya
maajabu katika mwili wangu sehemu za makalio. Mwili wangu ulikuwa
umetoboka na matundu hayoyaliweza kuonyesha alama ya ‘666’. Mungu wangu!! Nikashangaa, daktari yeye akawa ni wa kusikitika tu! “Usipokuwa mkweli utakufa wewe na familia yako nzima kama wenzako.” “Wenzangu? Wapi” “Mnaomtumikia” “Nani?” nilihoji kwa hofu. “Mmiliki wa hiyo alama. Kwani siku wanakuwekea hawakukuambia.” Alinihoji kwa utulivu mkubwa. Nikawa kama mwendawazimu na sikuwa na lolote ninalojua kuhusu hiyo alama katika makalio yangu. “Daktari sijui lolote mbona.”
“Haya shauri zako, atakufa mama, baba, mdogo wako, dada, shangazi,
mjomba, wifi, na marafiki ikibidi kisha watakumalizia wewe tena kwa
uchungu mkubwa.” Daktari alinieleza haya kama simulizi ya kawaida huku
akinitajia orodha ya watakaokufa. Kwa lugha nyepesi alikuwa kama babu
anayemsimulia mjukuu simulizi ya kutisha. Nikatetemeka sana!! Vifo!!
“Sasa daktari jamani mimi ninakuficha nini. Mimi sijui kitu.”
Nilishindwa kuendelea kuongea nikaanza kulia. Nililia sana maana
nilikuwa nimekata tamaa. Mbaya zaidi nilikuwa nimepigwa chapa ya 666.
“Ndio maana nimejishangaa sana, iweje leo nikubali kuchukua rushwa,
nikubali kutoa mimba msichana. Ama kweli kila mwenye alama hii
hatakataliwa na dunia kwa lolote.” Daktari alinong’ona kama anasema
mwenyewe vile. Nilisikia kila kitu. Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa! “Nitakusaidia.” Alinyanyua uso daktari akanieleza huku akinitazama vyema usoni.
Nilifarijika sana kusikia maneno yale. Kisha akaendelea, “Lakini uwe
mkweli kwa kila kitu. Ukijaribu tu kuficha lolote lile. Nasema ukijaribu
kuficha lolote lile. Wewe, marafiki na ukoo wako wote utatokomea. Mimi
nakueleza haya kama mzee wako, katika kipindi changu cha miaka ishirini
ya udaktari nakutana na matukio mengi. Lakini hili ni la tatu katika
maisha yangu. Wenzako wawili, mmoja miaka saba imepita na mwingine mwaka
juzi, nilitaka kuwasaidia lakini wakaleta ujanja ujan ja. Tuliwazika!!
Aah!! Hatukuwazika insearch labda niseme tuliyafukia mabaki yao.”
Alimaliza kunielezea kisha akashusha pumzi kali sana. Macho yangu
nilihisi kama yanajilazimisha kutazama mbele. Machozi yalikuwa yamezidi.
Mapigo ya moyo yalikuwa juu, sasa nikaanza kuamini niliyokuwa
nayatazama katika filamu za kinaijeria. Kumbe uchawi upo? Hakika uchawi
upo!! “Kesho njoo!!” alinipa ahadi hiyo. “Kwa hiyo sitatokwa damu tena?” niliuliza swali la kijinga. “Kwani mimi ndiye niliyekuwekea” Daktari naye akanipa jibu la kijinga kama nilivyotegemea. “Usimwambie mtu yeyote kuhusu maongezi haya.” alinionya Nikaaga! Kiguu na njia hadi nikaipata taksi.
Njia nzima nilikuwa nawaza na kuwazua. Zile ndoto zangu za kumjengea
mama nyumba nzuri, wadogo zangu kusoma shule za kimataifa, mimi kuwa
maarufu zaidi chuoni, ndoto za kwamba nataka kuwa mtakatifu! Zote
zilikuwa zimekufa. Sasa nilikuwa nahangahika huku na huko huku
nikisurubika na mateso ya nafsi. Swali likajengeka katika kichwa
changu. Dokta Davius linizuia nisimueleze mtu kuhusu mambo haya. Sasa
daktari ananisihi nisifiche kitu. Hapa sasa nimuamini nani? Nilijiuliza. “Kata kushoto!!” nilimuelekeza dereva. Mawazo yangu yakawa yameishia hapo. Maria aliniona kuanzia mbali. Akanikimbilia, akafika akanikumbatia. “Da Bela jamani. Mbona mnyonge hivyo!.” “Nimemkumbuka sana John.” Nilidanganya, huku siri kubwa nikiwa nayo mwenyewe.
Maria akaniongoza hadi ndani. Nikajibweteka kwenye sofa sebuleni. Maria
akaniletea maji ya matunda niliyokuwa nayapenda, nikayagida kwa fujo
kisha nikagundua kuwa nilikuwa na njaa. Chakula kilikuwa tayari!! Maria
akanihudumia. Sasa niliweza kupumzika!! Sikutaka kwenda chumbani.
Nililala sebuleni. Kila baada ya masaa kadhaa nilikuwa naamka na
kubadilisha pedi na nguo ya ndani kisha kuoga. Hali hii japo ilikuwa
haijatimiza hata mwezi kwangu ilikuwa mateso makubwa. Sasa sikuweza
kwenda kwa marafiki wala nisingeweza kwenda. Nilijihisi ninanuka, japo
Maria hakuwa ameniambia hata siku moja lakini nilijijua mwenyewew kuwa
sikuwa kawaida hata kidogo. Siku hii ikamaliza bila tatizo!!
Asubuhi ya siku iliyofuata niliwahi sana kuamka. Badala ya kumuomba
Mungu anijalie uzima na aniepushe na matatizo haya mimi niliwekeza imani
yangu yote iliyosalia kwa daktari yule ambaye hadi sasa sikuwa
namfahamu jina lake. Saa nne kamili asubuhi. Nilikuwa katika mlango
wa kuingia ofisini kwake. Japo kulikuwa na watu kadhaa waliohitaji
kuonana naye. Mimi nilipewa kipaumbele, nikawapita nikaingia ndani. Ahaaa!! Binti! Vipi kwema? Alinichangamkia sana. Nikamjibu salamu yake. Nikakaa kitako kumsikiliza.
“Ngoja niwaondoe hawa watu hapo nje. Wewe nitakupigia simu uje mahali.”
Alininong’oneza. Nikamuelewa nikampatia namba yangu ya simu kisha
nikaaga. **** Sikuchoka kusubiria. Japo alichukua muda
sana. Baada ya masaa mawili na nusu. Aliniita odisini kwake. Nikaenda
upesi nikamkuta akiwa pamoja na mwanaume ambaye laiti kama ningekutana
naye wakati ule ambao nilikuwa na jeuri ya pesa sidhani kama alikuwa na
hadhi ya kupokea salamu yangu. Nilimsalimia kwa kuwa tu alikuwa pamoja
na daktari. Nilipomsalimia badala ya kunijibu, akanikonyeza!! Nikataka kusonya nikasita.
Kwa ncha za macho yangu nikamtazama mwanaume huyu, kuanzia mavazi
yalivyochoka, amechakaa nywele zake na hata ngozi ilikuwa imepauka.
Nikaamini hata akili yake haiku sawa. Nilipokumbuka jambo hili la akili
kutokuwa sawasawa nikaamini atakuwa ni mgonjwa wa akili. Na daktari
huyu alikuwa katika kumpa tiba. Kimoyomoyo nikamsamehe kwa kosa la jinai
alilofanya la kunikonyeza. “Binti..kama nilivyokueleza jana!!
Usisite kuusema ukweli wote. Ukificha haitakusaidia kitu zaidi ya
kuuangamiza ukoo wako wote.” Alinieleza kwa utulivu. Yule tahira
akacheka. “Sawa daktari.” Nilimjibu. Tahira akacheka tena!! Akaanza kunikera.
“R.I.P mtu wako niliyekwambia ndio huyu.” Sasa daktari hakuwa
akizungumza na mimi, bali alikuwa akisemezana na yule tahira.
Nikashtushwa na hali ile, ina maana ananikabidhi mimi kwa yule chizi au
alikuwa anamtania. Niliomba iwe hivyo lakini haikuwa. Alimaanisha. Sasa tahira akanivagaa akanishika mikono. Nikajitoa mikononi mwake akacheka!! “Nenda naye ofisini kwake huyo akakupe maelekezo. Anaitwa R.I.P” “Na yeye anaitwa nani.” Yule mtu niliyedhani ni tahira sasa aliuliza.
“Jitambulishe binti.” Tahira alinieleza huku akinishika makalio. Kidogo
nimtukane. Nikasita baada ya kuona daktari hakushtushwa na jambo hilo.
Nitafanya nini sasa!! Nikaanza kufuata uelekeo alionipeleka. Mara kwa
mara alikuwa anacheka. Tulipishana na watu wengi lakini hakuna
aliyemshangaa. Huyu sio tahira!! Nililazimika kuamini Mlango ukafunguliwa nikaingia ndani!! Ofisi yake ilikuwa na hewa nzito sana ya madawa lakini yeye aliifurahia. Karibu ukae…aaah!! Usikae kwanza hebu njoo huku.” Akanivuta kwa nguvu, nikamfuata. Akafungua kabati moja kwa fujo. Mungu wangu!! Maiti!! Nikaruka pembeni, akacheka!! “Binti hawa nao walikuwa wajing wajinga tazama….njoo..njoo” akaniita. Nikasogea. Akavuta kabati jingine likafunguka.
Maiti ya mwanamke. Akamgeuza. Alikuwa na alama ya 666 katika makalio
yake. Maiti huyu nilikiri kuwa kabla ya kuwa hivi alikuwa mrembo sana. Sijui nini kilimuua maskini!!
Akanipeleka katika kabati jingine akavuta tena. Akatoka motto mdogo.
Hana kichwa nay eye ana alama ya 666..R.I.P kazi yake ilikuwa kucheka tu
kama tahira. Wakati mimi nilikuwa katika hofu kuu. Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa. Maiti karibia tano zilikuwa pamoja nasi, waziwazi. Amani ikatoweka moyoni. “Na wewe ukificha neno lolote tu!! Utakufa na vizazi vyote vitakavyofuata.” Aliongea bila kucheka sasa. Nilikuwa natetemeka. “Hata huyo uliyemkalia na yeye nadhani ni walewale..hebu funua.” “Wapi?” nilimuuliza, likiwa neno langu la kwanza hapo ndani. Akanionyesha kwa kidole. Ni pale nilipokuwa nimekaa. Nikafunua nikiwa natetemeka. “Mamaaa!!” nikapiga kelele. Kumbe nilikuwa nimekaa juu ya maiti. R.I.P akacheka sana!! Zile dharau zangu zikawa zimeishia hapa!! Nikamuheshimu!!! *** ISABELA ndani ya chumba cha kuhifadhi maiti…je kuna msaada gani hapa!!! ***Nini hatma ya mimba yake!!!!