mara nyingi watu huwa wanajiuliza ni kwanini wasichana wengi ni rahisi
kuingia kwenye mahusiano bila hata ya wao binafsi kupenda kuingia katika
mahusiano hayo.
kwa uchunguzi wangu binafsi nimegundua sababu
kuu nne ambazo wasichana hujikuta kwenye mahusiano ya mapenzi hata kama
hawakupenda kuwa na huyo mtu aliyeko naye. katika sababu hizi
haziaendani na sababu za kijamii, kiuchumi wala utamaduni wa eneo fulani
bali ni sababu ambazo mara nyingi huwakuta wasichana wa rika na uwezo
tofauti bila kujali kama ni masikini ama tajiri. Kwanza kabisa tuone
sababu za msichana kutotaka kuwa kwenye mapenzi na mtu asiye mpenda.
1. UJASIRI
Msichana anaweza kuwa jasiri kuingia kwenye mahusiano ama kutoingia
kwenye mahusiano. mara nyingi wasichana wanavaa ujasiri pale wanapokuwa
wapo mbali na mvulana na kujiaminisha yakuwa akifika kwa mvulana na
atamwambia kuwa sikutaki. Na mara nyingi kwa mtu ambaye hampendi na
hatamani kuwa naye hata kidogo. hivyo anauvaa ujasiri wa kuongea kwa
mvulana. kitendo cha msichana kuvaa ujasiri akiwa kwake I mean kabla ya
kuonana na mvulana humpa sababu ya pili ambayo ni
2. KUJIAMINI
Msichana akiwa jasiri anaweza kujiamini ya kuwa akifika atamwambia ukweli na
hivyo akiwa anaenda kukutana na huyo mvulana basi njia nzima anakuwa
anajiamini kuwa akiwa jasri na kumweleza kuwa hampendi na hamtaki basi
yule mvulana lazima atamwelewa. na sababu hiyo hata akiitwa kuwa aonane
naye anakuwa anajiamini kuwa hiyo vita ataishinda.
Lakini
tofauti na mategemeo, msichana hujikuta anaondokewa na ujasiri na
kujikuta yupo mikononi mwa mtu ambaye alidhani hapo mwanzo hatakuwa naye
na hii ni kwa sababu zifuatazo:
1. woga/fear
Msichana
anakuwa anaingiwa na dalili za kuogopa kusema kile alichokipanga
kukisema kwa mvulana na mara nyingi anapokutana naye uso kwa uso,
tofauti na hata angemtumia sms ama kumpigia simu. anapatwa na wasiwasi
mkubwa wa wapi aanzie kumweleza ya kuwa hampendi na hataki kuwa naye. na
hali mara nyingi hutokea pale mvulana anapomnyima nafasi ya kujieleza
msichana na kwa hiyo sababu huzaa zababu kubwa ambayo mara nyingi
imekuwa tatizo kwa watoto wa kike. sababu hiyo ni
2. HURUMA
Msichana
anapopatwa na woga anajikuta katika hali kumhurimia yule mvulana au
mwanume ambaye amejieleza kwake kwa kiasi gani anaumia kadri ambavyo
yeye msichana anavyoendelea kumkatalia ombi lake. na hii mara nyingi
hutokea pale mwanaume/mvulana anapotumia maneno yakuuchoma moyo wa
masichana. na point ya kuumia moyoni na kujiona ni mkosaji, msichana
hujikuta akiwa katika majaribu makubwa, ujasiri na kujiamini unaondoka
na woga na huruma huchukua nafasi na kujikuta yupo kwenye mikono ambayo
mwanzoni alifikiri si salama na hawezi kuwa na mtu kama yule ila sasa
tayri kazama.
MWISHO
kama kweli msichana huhitaji kuwa na mvulana fulani basi SIMAMIA HILO na usiruhusu woga wala huruma kuingia katikati.
No comments:
Post a Comment