Alistaajabu alipofungua nakuingia kwani hakukuta nguo zake yaani begi lake la nguo halikuwepo Jordan alijiuliza maswali mengi sana bila kupata jibu hakupata usingizi kwa usiku huo alitoka nje akichunguliachungulia labda angemuona au alichelewa kurudi lakini alikumbuka hata begi lake halikuwako. Jordan alisononeka sana moyoni mwake roho ilimuuma sana kwani alijua tayari amempoteza mpenzi wake ila hakutambua wapi amekwenda hivyo alikaa tu ndani akilala akiwaza na kulia kwani alimpenda sana.
Wiki mbili zilipita bila ya kumwona mpenzi wake ndipo akapata barua, aliichukua
Na kuifungua haraka haraka Ili ajue kilichopo ndani ya barua hiyo ghafla
machozi yakaanza kumtoka alilia Sana, alisononeka moyoni Na aliwaza kupita
maelezo, alikumbuka alivyomwimbia siku akiondoka pia alikumbuka promise
waliyowekeana ndipo moyo ulizidi kumuuma. Mchana kutwa hakula wala kufanya kazi
bali alishinda nyumbani tu akiwa na mawazo pia majonzi ndipo rafiki yake ambaye
walifanya kazi pamoja ya kuzoa taka alikuja kumsalimia baada ya kuona aonekani
kijiweni “aha vipi mshikaji mbona upo hivi unaonekana kama moyoni unamajonzi
niambie mbona huonekani kijiweni, niambie basi au kunakitu kimekugasi” rafiki
yake alimuuliza baada ya kumkuta akiwa ameshika tama “aha we acha tu ndugu
yangu kwa mkasa ulionikuta kwani ahaahh” Jordan alimueleza tangu alivyo ondoka
na kwenda kijiji kuwataarifu wazazi juu ya kwenda kumtambulisha mpenzi wake na
alivyo rudi hali aliyoikuta pia alimpatia barua iliasome iliyotoka kwa mpenzi
wake wa rohoni ambayo aliipokea baada ya wiki kadhaa kupita. Ndipo rafiki yake
huyo aitwaye Juma alichukuana kuanza kuisoma na ilikuwa imeandikwa hivi
“ikufikie wangu mpenzi wa enzi mie kiafyai ni mzima natumaini nawe u mzima, dhumuni
la barua hii ni kutaka nawe kujua ni nini hasa kisa na mkasa kilicho nishawishi
mbali nawe kwenda kuishi siyo siri sikupenda kuishi hali ya umasikini ya chini
sana kumbuka ufukara ndiyo umechangia hivyo ninatarajia kufunga pingu za maisha
ili niishi maisha bora mazuri kama almasi na nimeweka kadi ya mualiko niyako
fanya ima harusini uhudhurie ukipata nafasi”
Juma alisoma barua hiyo naye machozi
yalimlenga lenga kwa huzuni kwani aliumia sana moyoni akijihisi ni yeye,
alimfariji rafiki yake akimuondoa mawazo lakini Jordan
akuacha kuwaza juu ya tukio hilo
lililotekea katika maisha yake. Siku zilisonga mbele na na hatimaye siku ya
harusi ikawadia, Mercy and Moses wakiwa mbele ya kanisa Pembeni Mchungaji na
watumishi pamoja na wapambe wa maharusi ambao ni Maria na Maico. Jordan
alihudhuria bila kukosa Kwa uchungu alilia Sana alipomuona Mercy akimvisha Pete
mwanaume huyo ambaye alionekana kigogo yaani tajiri Wakutupa, roho yake
ilimuuma Sana alitoka nje Na kuzunguka nyuma ya kanisa kisha akaanza kulia,
alijikaza kiume asitoe chozi lakini wapi alijikuta akilia kama
mtoto mdogo. Baada ya ibada watu walitoka wakishangilia na kuanza kuelekea
ukumbini, ndipo Jordani alipata muda wa kuongea na Mercy kwani alikuwa
hajaingia bado kwenye gari. “Why Mercy? Ok ni uamuzi wako, basi naomba unipatie
pete yangu niliyokuvisha wakati wa uchumba wetu” jordani aliongea kwa uchungu sana “ehee wewe usinitie
majonzi saa hizi kaitafute mule ndani kwenye maboksi” alimjibu kwa dharau kisha
alipanda gari na kuondoka zake. Jordan
alirudi nyumbani akiwa na mawazo sana hivyo
alipanda kitandani na kulala lakini hakupata usingizi kwa ajili ya mawazo
aliyokuwa nayo aliwaza mengi sana
ila alimuomba mungu ampatie roho ya kumsahau mwanamke huyo lakini pia aliwaza
kuwa asingeweza kumsahau maisha yake yote. Aliendele na kazi zake za hapa na
pale ndipo alijipati fedha kidogo na kuamua aende kumsalimu mama yake kipenzi.
Hivyo siku iliyofuata alikuwa tayari amekwishafika jijini mwanza alipo mama
yake kwani alikuwa amemmis sana.
Alipofika alimkumbatia mama yake kwa furaha kisha kumpatia zawadia alizo
mpelekea na alikaribishwa pia mama yake alifurahi sana. Baada ya kuabdili nguo na kupata msosi
ndipo waliendelea na maongezi “yaani tulisubiri utuambie utakuja lini kutuletea
mkwe maana si unajua nimekwisha zeeka tena nahitaji mjukuu haya mbona umekuja
mwenyewe tena vipi?” “Yaliyo nisibu mama nayo makubwa kuliko, yalinisababisha
nikawa sili silali ila namuomba mungu anifanye niwe msahaulifu, Mercy
nilimpenda toka moyoni mwangu na naamini alinipenda ila jua mama tama ya pesa
ndiyo inayoharibu mapenzi ya watu na samaki mdogo mkunje kabla hajakuwa chatu,
pia nimeamini kuwa fukara hana sauti hana uwezo wa kueleza hisia zake tokana na
umasikini wake. Baada ya maongezi Jordan
alikwenda kujipumzisha kwani alikuwa amechoka kwa safari ya aliyokuwa ametoka.
Siku iliyofuata kaka Kelvin alikuja kuwasalimu na kwa bahati alimkuta Jordan
naye alikuwa amefika “ahha my young brother upo” “mie nipo tu kaka yangu
nitaenda wapi na maisha yenyewe ndo haya, Karibu tu kaka yangu” Jordan
alimkaribisha “vipi tena kaka si uliniambia utakuwa umerekebisha mambo baada ya
mwezi” “ahha nipe siku hizi mbili nitayakamata mapene kama sina akili nzuri”
Kelvin alimjibu. Siku iliyofuata Kelvin aliondoka asubuhi Na mapema kwani
alikuwa Na appointment Na rafiki yake ambapo waliongoza wote mpaka mahali
ambapo palijulikana Kama Kwa MTEMA NYOKA ambaye alikuwa Ni mganga, mchawi
aliyetokea Nigeria.
Waliingia hapo kwani walikuwa waeagiziwa kurudi siku hiyo “ahaaa!!! Kelvin Na
Joshua karibuni Sana ahaaa ahaaa shiiiii ahhaaa, siku ndiyo hii unataka pesa,
ahaaa utajiri ni wako ahhaaa Kelvin pesa sasa ni yako
Alisema mganga huyo
ambaye alikuwa ameshika njiwa mweupe mkononi na kitambaa cheupe na chekundu
mkononi mwake na sufuria nyenye maji yaliotiwa dawa kisha alimwambia Kelvin
atenganishe kichwa na kiwiliwili cha mnyama huyo na kelvini alifanya kama
alivyoambiwa na mganga huyo baada ya kutenganisha ndipo tone la damu
lilidondokea juu ya maji na ghafla Kelvin aliona sura ya mama yake kwenye
sufuria ile “what????
ITAENDELEA
No comments:
Post a Comment