Friday, November 2, 2012

CHOZI LA FUKARA

Na 

DEARNA MAROTER

 3

Maria alikuwa na uwezo kiasi fulani “aha Karibu shostito wangu” maria alimkaribisha “asante yaani nimekumisi shost” “aha wewe si utaki kuja kunitembelea na unakaa hapahapa mjini, utadhani tumegombana” maria aliongea na kisha kwenda kumchukulia juice ya matunda “ehe nipe mastory” maria aliongea kisha kuketi kwenye kochi “nina story gani bwana zaidi ya kuja kukusalimia na unipe ela ya mboga maana leo hata sijui nita kula nini” aliongea Mercy

“Mhh!! Ahaa, hivi Mercy rafiki yangu mbona hujielewi elewi” 


 SASA ENDELEA

Maria aliongea kwa kejeli “kwanini” mercy alihoji “kwahiyo yule ndo unataka kuniambia ni mume wako mtarariwa au wakuzugia” “Maria sina utani wala!! Jordan ndiye chaguo la moyo wangu na sidhani kama nitamwacha” Mercy alimjibu “aha nikikumbuka zamani ulivyokuwa unang’aa na sasa ulivyo pauka? Mhh uzuri wako wote ahaa!! Shost umepotea njia, mbona wanaume wa kukuoa wako wengi na ulivyo tia timu tu hapa wenye pesa zao, watakao kutunza, wanaokupenda, wenye kukuhitaji na kukutimizia mahitaji uonekane wa kung’aa walinifuata lakini nikashindwa kuwajibu ila mmmh” maria aliongea utazani mama wa mipasho “sikiza Maria ninachotaka ni penzi la dhati na siyo pesa” Mercy alimjibu “umdhaniae ndiye huwa siye, mtazichuma kwa shida lakini mwisho atakuja kukusaliti nakwambia kwa sababu ni rafiki yangu na sipendia uwe ombaomba, kwani utakuwa ombaomba mpaka lini relax maisha ni ujana bwana shauri lako its up to you na nisingependa uje tena eti kuniomba ela ya mboga aha hii ni mara ya mwisho kuombaomba kama utaki kukiacha hicho kimasikini chako utajua mwenyewe mtu ninakuonyesha njia ya maisha alafu unajishaua unajua kupenda utakufa masikini kwa kukitegemea hicho ki Jordan”  Maria alimpatia ushauri kisha alimpatia fedha kidogo na Mercy aliondoka kuelekea kwake. Siku zilizidi kusogea na Mercy alikuwa ni mwenye mawazo “hata siku moja sijawahi kwenda saluni sijui hata nitaenda lini mhuuu” aliwaza kichwani mwake “hali hii ngumu sana na niyazingatia maneno ya zafiki yangu da!! Lakini moyo umezimia kwa Jordan sijui amenipa dawa gani” aliwaza sana na ghafla simu yake iliita na ilikuwa namba ngeni kwake. Alipokea na kumsikiliza kisha mtu huyo alimsihi wakutane muda wowote lakini Mercy hakumjibu. Kwa upande wa Jordan alizidi kutafuta na kwa bidii na siku iliyofuata alipanga aende nyumbani kuwataarifu ndugu na mama yake kuwa anatarajia kumtambulisha wenza wake wa maisha ili wajiandae na kumsalimia mama yake aliye kijijini bariadi.
Jordan: “mpenzi wangu mimi kesho nitakwenda kumsalimia mama pamoja na ndugu pamoja na jamaa pia kuwataarifu kuwa tutakwenda wote kujitambulisha hivyo niandalie nguo pamoja na kazawadi kadogo nilichokuja nacho kwa ajili ya kesho”
Mercy: sawa mpenzi wangu ila usikawie kurudi kwani nitakuwa mpweke sana” alijibu kisha kuandaa baadhi ya vitu alivyoagizwa kuandaa na usiku walikula kisha kwenda kitandani ambapo walipiga story nyingi na walizidi kuwekeana ahadi. Usiku ulikuwa mwema na asubuhi tayari ndege walishangilia mawiwo ya jua ndipo walisindikizana hadi kituo cha mabasi huku wakiongea na kumpatia salamu nyingi ndipo Jordan aliweka begi chini na kumkumbatia mercy huku akiimba
Jordan: “mpenzi ninakwenda safari, Mpenzi ninakwenda safari penzi letu lilinde”
Mercy: oho! usiwe na shaka mpenzi, usiwe na shaka mpenziii penzi nitalilinda”. Walikubatiana kwa muda kisha gari lilikuwa limewasili na Jordan alipada na kupunga mkono ishara ya kuaga kisha gari lilipotelea kwenye barabarani  ya lami kwa mwendo kasi. Mercy alirudi nyumbani akiendelaea na shughuli zake za kila siku, baada ya shughuli zake alijipumzisha huku akionekana ni mtu mwenye mawazo mengi ndani ya kichwa chake kwani.
    Siku mbili zilipita tangu Jordan aondoke kwenda kijjini na alikuwa amefika salama kwani mungu alimlinda katika safari yake hiyo alifurahisana kumwona mama yake aliyeachana naye muda kwani alimpenda sana na mama yake pia alifurahi sana, alitembeatembea kuwasalimu ndugu jamaa na marafiki katika kijiji chao kwani alikuwa amewamiss sana. Jioni ilipofika walikuwa katika mazungumzo na mama yake pamoja na wazee walio Karibu na familia hiyo ambao walikuwa kama waangalizi na wazee wa kijiji pia na ndiyo walikuwa wakitoa muafaka wa mabo waliyoshirikishwa.
   “wazazi wangu mimi nimetoka mjini kwa malengo mawili, moja wapo ni kuwasalimu pia lengo kuu ambalo ni la pili ni kuja kuwapa taarifa kuwa mimi sasa nimefikia wakati wa kuwa na mwenza wa maisha na tayari nimekwisha mpata hivyo ningeomba mnipe ruhusa ya kuja kumtambulisha na ndiyo maana nimekuja ili kuwataarifu nisikie maneno yenu sababu neno la mzazi ndiyo njia kwa mwana” Jordan aliongea “ahaam uamuzi wako Jordan ni mzuri sana maana vijana wa siku hizi  huwa wanapelekapeleka mambo bila kuwashirikisha wazazi na wakubwa zake ambao wangempatia ushauri hivyo kwa upande wangu sijaona shaka sijui wazee wenzangu mnasemaje?” walishauriana wazee hao na wakakubali kuwa watawapokea kwa furaha “ila mwanangu angalia sana wasichana wa mjini huwa hawapendi wanaume wasio na uwezo kifedha je unaamini kuwa anakupenda kwa uhakika” Mama yake alimuuliza wakiwa wenyewe baada ya mazungumzo yao “nampenda sana na naamini ananipenda sababu nimeishi naye muda mrefu na tumepitia shida nyingi bila lakini yeye ndiye mfariji wangu pindi ninapokosa fedha na anaushauri sana kwangu juu ya mwangaza wa maisha yetu hivyo sidhani kama anaweza kunisaliti” Jordani alijibu nao waliendelea na maongezi. Wiki mbili zilikatika na safari ya Jordan kurudi mjini iliwadia hivyo alijiandaa vizuri kwa safari ya kesho yake “aha mama itabidi kesho niondoke na gari la asubuhi sana  ili niwahi” Jordan aliongea “ha humsubiri kaka yako Kelvin anakuja kesho hivyo humsubiri hata umsalimie?” mama aliuliza “dah kama atakuja itabidi nimsubiri kwani sijaonana naye siku nyingi sana na nimem miss sana”. Kaka na mdogo yaani Jordan na Kelvin walisalimiana na kuelezana mikakati ya maisha jinsi yanavyo kwenda “aha Jordani ndugu yangu yaani ninatarajia mwezi unaokuja nianze kukukaribisha nyumbani kwangu” Kelvin aliongea kwa shauku kidogo “aha usiniambie bwana kaka sikuizi mambo yako yatakuwa si mabaya” Jordan alimuuliza “kuna issue nafuatilia by wiki ijayo nitakuwa na mapene yaani we acha tu” Kelvin aliongezea tena “aya usinisahau na mimi mdogo wako” “siwezi kukusahau ndugu yangu wala sitamsahau mama yangu nakuahidi hilo ninavyo wapenda sidhani”. Waliongea sana na na siku iliyofuata Jordan alipanda gari kurudi mjini ghetto kwake, akiwa njiani aslimpigia mpenzi wake aje kumpokea lakini alikuwa apatikani. Alishuka stendi salama na kuenda nyumbani. Alipofika nyumbani hakumkuta mpenzi wake bali mlangoni kufuli alitafuta funguo akijisemea moyoni labda atakuwa ametoka kidogo pia alijaribisha tena kumpigia simu lakini ilikuwa haipatikani alikaa nje akimsubiri mpaka giza likaingia lakini hakutokea alijaribu tena kumpigia na alikuwa hapatikani ndipo aliwauliza majirani lakini hakuna aliyejua alipokwenda ndipo akaamua kuvunja kufuli ili aingie ndani kwani usiku ulikuwa tayari umeingia. Alistaajabu alipofungua nakuingia kwani hakukuta nguo zake yaani begi lake la nguo halikuwepo Jordan alijiuliza maswali mengi sana bila kupata jibu hakupata usingizi kwa usiku huo alitoka nje akichunguliachungulia labda angemuona au alichelewa kurudi lakini alikumbuka hata begi lake halikuwako

JE JORDAN ATAWEZA KUMPATA MERCY??? JE MERCE AMEENDA WAPI???

UNGANA NA MTUNZI WAKO TENA 

No comments:

Post a Comment

Recent Posts