Saturday, October 20, 2012

SITAISAHAU facebook


MTUNZI: Emmy John P

CONT: 0654960040

           2
SEHEMU YA PILI

Baada ya dakika mbili nilikuwa nimemaliza kuusoma ujumbe mrefu wa Dokta Davis. Nilikuwa natetemeka, mapigo ya moyo yalikuwa katika mwendokasi wa kutisha sana. Macho yalikuwa hayafumbi bali yanaitazama simu yangu!!! Nilikuwa simuoni Dokta Davis lakini nilikuwa katika TAHARUKI!!!!!

SIKUAMINI!!!!!


*Ni kitu gani Isabella amekisoma hadi kumtisha hivyo…

**Je ni biashara gani hiyo ya mtandao.

*** Na kipi kilimsibu Isabellla baadaye!!!!


ENDELEA.


Kilichonishangaza zaidi ni faida iliyoandikwa na Dokta Davis. Sikuipinga lakini mtaji wake haukuonekana kabisa, swali likawa ni biashara gani hii isiyohitaji mtaji lakini ina faida kubwa kiasi hichi??
Nilitaka kumuuliza lakini nikakumbuka kuwa tayari aliita biashara ya mtandao.
Shida zilizokuwa zikinikabili sikutegemea kuwa naweza kumruhusu roho wa kukataa anitawale.
Mara moja nikakubaliana na Davis kuwa naweza kuifanya biashara ya mtandao. Sikutaka hata kidogo kukumbuka kuwa katika biashara huwa kuna faida na hasara.
“Lakini tunatakiwa kuonana sasa itakuwaje!!! Au hakuna mkataba?” nilimuhoji.
“Keshokutwa kama ukiwa na nafasi njoo unipokee Airport, haitakuwa mbaya kama utakuja na rafiki yako mmoja anayejua kuongea kiingereza kiasi.” Alinijibu.
Siku hiyo ikapita, lakini haikumalizika bila maajabu mengine.
Ilikuwa saa moja jioni. Sikuwa na mpango wowote wa kupata pesa, ujumbe ukaingia kwenye simu yangu.
“Nitumie namba yako ya akaunti kuna kipesa kidogo nataka nikuwekee ili mtumie kama nauli kuja uwanja wa ndege kunipokea. Nilishangazwa na meseji hiyo kutoka katika namba ambayo hakika haikuwa ya mtandao wa Afrika mashariki. Bila kuuliza nikajibu ujumbe ule lakini haukuweza kwenda, simu yangu haikuwa na salio la kutosha.
Ni kama vile upande wa pili ulitambua hilo. Simu ikaanza kuita nikapokea. Alikuwa Dokta Davis, nilimtajia namba za akaunti yangu kwa ufasaha. Ilikuwa mara ya kwanza kusikia sauti yake.
Sio siri dakika kumi zilikuwa nyingi ukaingia ujumbe kuwa pesa tayari imewekwa. Sikukumbuka kufunga mlango nilikaza mwendo hadi ‘ATM’ nikaiweka kadi yangu huku nikiwa siamini kama ni kweli ama la.
“Salio lako ni 666,666” macho yalisoma tarakimu hizo, nilitumia mkono wangu kuzihesabu moja baada ya nyingine huku nikijiuliza kuwa hiyo ni elfu sitini ama laki sita? Jibu lilikuwa laki sita. Kijasho!!
Niliondoka ATM na shilingi laki mbili. Kinyago gani angenibabaisha pale chuoni? Mimi ndio mimi.
Usiku mzima nilikuwa naitafakari pesa na kazi niliyoahidiwa na Dokta Davis. Nilianza kujiuliza ni nani ambaye anafaa kuwa nami katika msafara wa kwenda kumpokea mtu huyu muhimu, Dokta Davis. Niliwachambua marafiki zangu mmoja baada ya mwingine, hatimaye nikamchagua Mariana. Huyu alikuwa ni rafiki yangu hasa, lakini tatizo kiingereza kilikuwa kinampiga chenga..nikamsikitikia sana kwa kuikosa nafasi hii hadimu. Mwishowe nikamchagua Happy ambaye hatukuwa karibu kivile lakini alikuwa ana vigezo. Vigezo alivyotaka Davis

MCHEZO RASMI UKAANZA

Ndege ilitua muda ambao dokta Davis alikuwa amenieleza kabla, alitupigia simu baada ya kuwa ameshuka na tukafuata maelekezo ya jinsi ya kuonana naye.
Happy alikuwa mkimya sana kwani hakuwa akijua mengi hivyo aliniachia mimi majukumu yote.
Hatimaye tukaonana na Dokta Davis. Kwa jinsi alivyokuwa muonekano wake na sisi basi ilimpasa yeye aje kutupokea sisi na wala si sisi kwenda kumpokea yeye. Lakini ndio hivyo ni sisi tulienda kumpokea yeye.
Lafudhi yake ilikuwa na mchanganyiko wa kiingereza cha Afrika magharibi na Marekani. Alikuwa na mwili mdogo tu usiokuwa na chochote cha kuvutia sana. Hakuonekana kuwa mtu mwenye pesa.
“Happy, huyu ni rafiki yangu wa siku nyingi.” Nilimtambulisha Happy kwa Davis bila kumwambia kama tulikutana facebook. Nikamtambulisha na Happy huku tukienda kwenye taksi iliyotuleta.
“Nipeleke hoteli nzuri kabisa.” Alizungumza Dokta. Nami bila kusita nikamuelekeza dereva kwa kiswahili hoteli nzuri ya kifahari. Moyoni nilikuwa na wasiwasi bado kama Dokta Davis atazimudu gharama za hoteli hiyo. Muonekano wake bado ulikuwa kikwazo kwangu. Hakufanania kabisa kumiliki pesa nyingi!!
Alipolipa kwa mfumo wa dola bili za hoteli alinikata wasiwasi wangu!!!
Hapo kabla nilikuwa sijawahi kuingia hoteli yenye hadhi kama ile. Nilikuwa nashangaa shangaa tu pale ndani, sikujua ni wapi mlango unafunguliwa, sikuona mahali pa kuwashia taa baada ya kuingia ndani, na ilinishtua kengele iliyopiga kelele baada ya kuwa mlango haujafungwa vizuri. Hata Happy naye nilimwona akishangaa shangaa, lakini Davis alionekana mzoefu sana wa sehemu kama hizi. Heshima ikaanza kujengeka.
Tulizungumza mengi sana na Davis, alitawala maongezi kutokana na maswali aliyokuwa anatuuliza. Tulimweleza maisha magumu tunayopitia pale chuoni. Alisikitika sana na kuulaani umasikini.

****

Siku hiyo alitupatia shilingi laki moja kwa ajili ya nauli za kurudi chuoni kila mmoja ya kwake. Happy alipagawa nayo kila mara alirudia kusema asante huku Davis akimwambia asijali ni hali ya kawaida.
Nilipofika hostel niliyokuwa ninanishi nilitamani kila mtu anitambue Isabella nilikuwa nina shilingi ngapi mfukoni. Nilifika ndani na kujibweteka huku nikijisikia mwanamke mwenye bahati kupita wote. Nani wa kunisumbua!!
Nilimkumbuka John Paul, huyu alikuwa ni mpenzi wangu ambaye licha ya kuachana bado nilikuwa nampenda. John aliniacha kisa sikuwa na pesa, aliniacha kwa sababu umasikini ulikuwa damuni mwangu, huenda John alidhani naweza kumwambukiza umasikini, John akaniacha na kuunda uhusiano na msichana wa kitajiri, aliyekuwa anamiliki gari yake mwenyewe na kila mara alibadili nguo za bei ghari. Aliitwa Jesca.
Niliumizwa sana na hali ile ya kuachwa na John, nilijipa moyo kuwa siku moja nami nitapata bahati ya kupendwa tena. Lakini bahati mbaya kila aliyekuja alionekana kuwa ni mdanganyifu.
Yale matendo ya kejeli aliyonifanyia John, niliamini sio kwa kupenda kwake bali msukumo kutoka kwa Jesca yule binti wa kitajiri.
Hasira ikanipanda maradufu sasa nikauona ule wakati wa kulipiza kisasi ulikuwa umefika.
Wakati wa kumwonyesha John kuwa sasa nina pesa!!! Nikawaza kumiliki gari, nikawaza kuwa mwanadada asiyepitwa na vazi lolote jipya. Na kubwa zaidi nikamuwaza Dokta…..dokta Davis.
Nikamjengea picha kaka huyu iwapo atakuwa mpenzi wangu, kwanza nitakuwa na amri juu ya pesa zake, na pili nitakuwa Mrs. Davis. Lolote analofanya lazima nishirikishwe.
Mh!! Itawauma kweli Isabella nina mchumba kutoka Marekani. Nilijisemea huku nikitabasamu.
Zile picha za dokta Davis ambazo mwanzoni niliziona kuwa hazina mvuto sasa nikaziona kuwa hazina mfano dokta akawa dokta kweli. Uchafu gani mwingine wa kunisumbua humo facebook?? Nilijiuliza. Kisha nikagundua nilianza kujengeka kiburi kichwani!!!
Usingizi ulinipitia nikaja kushtuka saa kumi na mbili asubuhi.
Ni kama niliamka wakati sahihi. Dokta akapiga simu.
“Mchukue gari ya kukodi, mwambie dereva tutamtumia siku nzima.” Alitoa maelekezo hayo Davis. Nikafuata maelekezo.
Baada ya saa zima nilikuwa katika gari la kukodi.
Kabla ya kwenda kwa dokta nikaamua kwanza kulipa kisasi, nikamuamuru dereva twende chuo. Bahati ilikuwa upande wangu, ile nashuka kwenye gari kwa mbwembwe zote. Karibia wanafunzi kumi niliosoma nao darasa moja waliniona.
Macho yao yalionyesha kutoamini nami sikuwajali.
Nikajizungusha zungusha hapo kisha nikamwamrisha dereva, tukaenda kumchukua Happy. Huku nyuma najua niliacha gumzo!!!
Tulipofika nyumbani kwa Happy, Happy hakuwepo!!! Nikajaribu kupiga simu yake, haikupokelewa. Niliwauliza majirani wakadai kuwa alitoka lakini hawajui kama alirudi ama la.
Anachezea bahati huyu!! Nilijisemea.
 
Nikapanda ndani ya gari. Safari ya kwenda kwa dokta ikafuata.
Maajabu nilimkuta Happy akiwa amefika tayari!! Alikuwa na dokta wakinisubiri.
Mchomo wa wivu ukanishambulia na kunijeruhi moyoni, nikaanza kuhisi zile ndoto zangu zimeanza kufifishwa. Happy alinisalimia akiwa na tabasamu mwanana. Dokta akiungana naye kutabasamu. Nami nikajilazimisha nikatabasamu!!!
“Kesho nitarejea nyumbani mara moja….kuna dharula imejitokeza. Lakini kitu kimoja nahitaji mfanikiwe kupitia mimi.” Alianza kutueleza dokta, tukiwa ndani ya gari la kukodi. Kisha akaendelea, “Nitarejea hivi punde tu!! Na nikiwa huko nitakuwa nawasaidia, msisite kunieleza lolote nami nitawasaidia, hata mimi kufika hapa nilikuwa nasaidiwa kwa hiyo ni zamu yangu kusaidia.” Aliongea kwa ukarimu mkubwa.
Kwa mahesabu ya harakaharaka zile dola thamani yake ilikuwa milioni sita za kitanzania. Hizo ndizo Dokta alituachia tugawane.
Kwangu mimi ilikuwa kama ndoto ya mchana!!!
Siku iliyofuata dokta huyu wa ajabu akarejea huko anapojua yeye!! Hakutaka kusindikizwa uwanja wa ndege.


****

Dokta Davis ni nani???
Je? Mpango wa Isabella kuwa naye katika mapenzi utatimia??
Kwa nini…SITAISAHAU facebook???
TUKUTANE TENA

No comments:

Post a Comment

Recent Posts