Tuesday, October 16, 2012

HATIA--07

Na George Iron

Moshi wa bangi na sigara vilianza kuizoea damu yake, sumu ya maneno aliyokuwa akilishwa na John Mapulu sasa ilikuwa imesambaa ndani ya damu yake, aliwaona watu wote wanaomzunguka kuwa ni maadui hasa hasa askari.
John alimwelezea Michael jinsi polisi wanavyoua raia wema hovyohovyo, alimpa mikasa mbalimbali ya kutisha hivyo kuikoleza hoja yake kuelekea kwenye ukweli. Taratibu Michael akaanza na sigara hatimaye akajiunga katika mkumbo wa wavuta bangi, kwa jitihada zote aliyapinga matumizi ya unga hilo pekee ndilo alilipigania hadi mwisho.
Mwanzoni alikuwa msindikizaji katika shughuli walizokuwa wakienda kufanya akina John sehemu mbalimbali katika jiji la Mwanza kila baada ya shughuli alipewa nafasi ya kuuliza maswali mawili matatu. Kwa kuwa Michael alikuwa mwingi wa maswali hii ilimuwezesha kuelewa mambo mengi sana katika kipindi kifupi mno.
Tayari alijua mbinu za kuvunja maduka, kuiba magari, na mbaya na kubwa somo la matumizi ya silaha lilikuwa limemkolea.
John Mapulu hakuwa mtu wa masihala linapokuja suala linalomuhusu moja kwa moja, jambo hili hata Michael alilitambua upesi sana kadri alivyokuwa akiishi naye karibu. Mahusiano yaliyokuwepo kati yake na Matha (mpenzi wa John) katika kufundishwa jinsi ya kutumia bunduki yalikuwa yameanza kuvuka kiwango, nafsi ya Michael baada ya kumtamani Joyce Keto bila mafanikio ya kumpata, Joyce mwingine aliyefariki bila kuwa ameelewa azma ya Michael, sasa Michael alikuwa anamtamani Matha japo pia alikuwa hajamwambia, kila siku alikuwa akijizuia na kuuonya mdomo wake usije ukamponza.
Aliamini kwa kumtamkia Matha kuwa anampenda ni sawa na kuanzisha vita na John Mapulu, vita kubwa ambayo wala hakuwa na ubavu wa kuicheza. Wakati fulani Michael aliamini Matha amewekwa karibu yake ili kumchunguza tabia zake hivyo alikuwa makini sana asiweze kuzionyesha hisia zake kwa mrembo huyu.
Matha hakuisha kumvalia nguo za mitego Michael kila wanapokuwa wawili katika chumba maalumu cha mafundisho hayo.
Siku hii jioni tulivu kabisa John na wenzake wakiwa wameingia katika tukio la kuiba pesa benki ambapo hawakutaka kuandamana na Michael kwa sababu ya uchanga wake katika masuala ya uharifu pia hawakuwa na mtaalamu wao wa kike Matha Mwakipesile aliyedai kwamba akili yake haikuwa barabara siku hiyo. Michael kama kawaida akiwa katika burudani yake ya kuangalia filamu, mwilini akiwa na pensi fupi na fulana iliyokatwa mikono alishtuliwa ghafla na ujio wa Matha pale ndani.
“He!! Mwalimu vipi….pole aisee nasikia unaumwa??.” Michael alimuanza Matha ambaye kwa sasa walikuwa wamezoeana sana.
“Mh!! Kakwambia nani??”
“Ah!! Nimesikia tu!!!” alijibu huku akisimamisha hiyo filamu kupisha maongezi yake na Matha.
“Ok!! Twende darasani” Matha alimwomba Michael naye akafuata bila ubishi, darasa alilokuwa akipewa na Matha lilimvutia kuipenda bunduki. Walipofika chumba hicho maalumu somo lilianza kama kawaida lakini hawakuchukua muda mrefu Matha akabadili hali ya hewa ya hapo ndani, ni wakati akimfundisha Michael jinsi ya kulenga shabaha akiwa kwa nyuma yake mkono wake wa kushoto ukiwa umekizunguka kiuno cha Michael, zoezi lilisimama ghafla baada ya wawili hawa kujikuta hawaitazami bunduki ila wanatazamana machoni wakiwa wametwaliwa na dalili zote za mahaba mazito.
Mapigo ya moyo ya kila mmoja yalikuwa juu sana, taratibu bunduki ikatuliwa chini, Matha kwa kuutambua uoga wa Michael yeye mwenyewe akajitoa muhanga kusogeza papi (lips) za mdomo wake hadi zikagusana na za Michael, akaupenyeza ulimi wake katikati ya papi za Michael na yeye akaupokea taratibu. Michael alikuwa anatetemeka sana lakini baada ya ndimi zao kukutana akauvaa ujasiri, hapakuwa na godoro pale ndani hivyo wakajikuta katika sakafu iliyokuwa na vigaye, kivazi alichovaa Matha ni kama alimaanisha kitu kwani baada ya kuanguka chini alikigusa nacho mara moja mikanda ikaachia wawili hawa wakawa katika ulimwengu wa mahaba mazito.
Matha yule ambaye ana uwezo wa kuua binadamu dakika yoyote ile katika mapambano sasa alikuwa amelala chali mshindi akiwa ni Michael katika kifua chake. Raha walizozipata waliweza kuzielezea wao peke yao maana hapakuwa na shahidi pale ndani zaidi ya mtutu wa bunduki. Hiyo ilikuwa ndiyo siku ambayo Michael kamwe hataisahau kwani ile hali ya kujiamni mbele ya John alihisi inapungua huku akihofia siri hiyo iwapo itavuja ni jinsi gani John atakisambaratisha kichwa chake.
Kwa upande wa Matha hakuonyesha mabadiliko yoyote, hakuwa na uoga hata chembe, na siku iliyofuata alifika hapo nyumbani kwa ajili ya kumfundisha Michael. Darasa likageuka ukumbi wa ngono, Michael alipewa onyo kali.

“Ukikataa tusiendelee kufanya nitamwambia John kuwa unanisumbua kimapenzi, usidhani kuwa atakuhoji kama ni kweli ama la…atakachofanya atachukua bunduki kama hivi na kukufyatua kichwa chako, kama akiwa na huruma sana atakuwekea sumu ufe usingizini….vipi upo tayari kufa??” Matha alimwambia Michael kwa sauti iliyojaa majivuno. Michael hakuwa tayari kufa hivyo akaingia rasmi katika utumwa wa ngono na mpenzi wa muuaji hatari, tena katika nyumba ya muuaji. Raha alizokuwa akizipata wakati wakipashana miili yao joto ilikuwa inayeyuka kila alipokuwa akimfikiria John siku akiugundua huo mchezo mchafu unaoendelea.

*****

“John leo nitampeleka huyu dogo kwa mafunzo ya shabaha kule pori!!! Usiku” Matha alimweleza John Mapulu ikiwa majira ya asubuhi baada ya kuwasili pale nyumbani kwa John.

“Vipi lakini uelewa wake anaweza kuingia mzigoni???” Badala ya kujibu naye aliuliza

“Kiaina lakini si wa kuingia mzigoni kwa sasa. Ni moto wa kuotea mbali akishaiva vizuri” Matha alimsifia Michael. Wakati huo na Michael naye alikuwepo pale sebuleni, hakutaka kumwangalia John wala Matha. John alianza kudhani Michael ameogopa sana kusikia habari za porini usiku, wakati Matha alijua kwa nini Michael hakutaka kuwatazama usoni.
Msichana gani huyu hana hata chembe ya aibu!!! Aliwaza Michael.

“Kwa hiyo twende wote ama utaenda na Bruno!!!” aliuliza John

“Mwenyewe ninatosha hata usijali hatutachukua wakati sana, isitoshe Michael si mkorofi” alipanga maneno yake Matha kama karata na yakakubaliwa bila chembe ya wasiwasi na John.

****


Joyce Keto, alikuwa haelewi hata nini kilichokuwa kinaendelea ndani ya nyumba ile ambayo alikuwa hajafahamu wapi mlango wa kuingilia na kutokea licha ya watu kufika humo ndani na kuondoka, mwanzoni aliamini yupo katika mikono salama ya ndugu zake Michael lakini kadri siku zilivyosonga mbele ndipo akagundua kuwa alikuwa katika mazingira hatarishi sana. Siku hii jioni akiwa amepata tayari chakula chake alichokula bila kujua ni wapi kimetoka alipatwa na muwasho wa kuzunguka zunguka katika nyumba hiyo ambayo hakuijua tofauti na sebule na chumba chake cha kulala. Kiza kilikuwa kimeanza kuingia tayari lakini kutokana na taa kuwashwa mapema katika jengo hilo ilikuwa vigumu sana kugundua kwamba ni usiku. Joyce alizunguka sehemu mbalimbali bila mwongozo wa mtu yeyote hadi akaufikia mlango ambao ulikuwa umefungwa kidogo na kuachwa wazi kidogo, bila wasiwasi aliamua kuchungulia ndani.
Macho yake makavu yalikutana na tukio lililoizibua akili yake. Mwanaume mmoja alikuwa amefungwa kamba mikononi na miguuni, damu zilikuwa zinavuja kutoka katika paji la uso wake.

Joyce aliweza kumuona John, katika kundi la waliokuwa mbele ya mtu huyu, mapigo ya moyo yalipiga kwa kasi kubwa. Majambazi!!!! Ndivyo akili yake ilimtuma harakaharaka, akaondoka kutoka alipokuwa na kuelekea chumbani kwake. Aliwaza kukimbia lakini mgogoro wa nafsi ukamtawala hakuelewa kama alionekana wakati akichungulia ama la!! Alihofia kukimbia pia kwani hakujua njia sahihi ya kutoka nje ni ipi, nyumba ilikuwa kubwa sana. Akiwa bado hajaamua chochote mlango wake uligongwa alikuwa msichana wa kazi na alikuwaa amemletea kahawa ya jioni kama ilivyo ada. Alitamani kumuuliza juu ya alichokiona lakini hakumuamini hata kidogo akaizuia nafsi yake kufanya hivyo.


*****

Pori kubwa na zito ambalo Michael aliyepelekwa huku akiwa amefunikwa kitambaa usoni, hakulitambua hata kama asingekuwa na kitambaa usoni kwani alikuwa mgeni Mwanza. Walifika porini Michael akiwa na wazo moja tu la kutoroka kabla mambo hayajawa mabaya kwa upande wake, azma ya kuchangia mwili mmoja na mtu mkatili kama John ilikuwa inamtafuna kwa fujo, mwili wake ulioanza kunawiri kutokana na mlo safi na kamili aliokuwa anaupata pale kwa John sasa ulikuwa unaanza kufifia tena.
Matha yeye ni kama raha hizo zilimkubali kwani alizidi kunawiri na kuongeza mvuto wake. Matha alisimamisha gari ndogo aina ya Cresta Michael akashuka na yeye akashuka, hakuwa na wasiwasi wowote juu ya Michael kwani alijiamini kupita maelezo katika suala la kujihami kwa kutumia viungo vya mwili mafunzo aliyoyapata kabla ya kuliasi jeshi la polisi miaka kadhaa nyuma. Nia ya Michael ilikuwa kutoroka lakini hakuona hata njia moja ya kuweza kumtoa pale katika lile pori.
Nitazua mengine hapa!! Aliwaza na kusubiri kuona kilichokuwa kinataka kuendelea.
“Michael!!!” Matha alimwita na kumtoa katika ndoto zake zisizo na mafanikio.
“Naam mama!!!” aliitika kwa nidhamu.
“Njoo huku mara moja!!!” Michael alitii amri, akamfuata Matha alipokuwa anaelekea, fikra zake ni kwamba alikuwa akienda kufundishwa huko kulenga shabaha. Alipokaribia aliamriwa kurudi kinyumenyume hivyo navyo akatii.
“Simama!!” Matha aliamrisha, Michael akatii. Matha akamsogelea Michael na kumtia kitambaa usoni.
“Vipi tena mama??.”
“Ndio masharti ya kujifunza shabaha” Matha alitoa sauti ya amri lakini isiyokuwa na kujiamini ndani yake. Kimya kilitanda kwa sekunde kadhaa kisha Michael bila kuwa amejiandaa alichotwa mtama na kujikuta yu katika fundo la majani lililokuwa katika mfumo wa kitanda, kisha akafunguliwa kitambaa usoni, kabla hajasema lolote ulimi wa matha ulipenya katikati ya papi za mdomo wake, ule ubaridi wa ulimi wa Matha ukaubembeleza uoga wa Michael hadi ukasinzia na ujasiri ukaamka. Matha alikuwa kama alivyozaliwa na baada ya dakika mbili Michael naye alikuwa hivyo hivyo. Hii siku ilikuwa ya kipekee kwao kwani walikaa porini masaa mengi sana huku bunduki zikiwa pembeni kama nguo zilivyosahaulika na miili yao ikiwa imenatana.
“Michael nataka uwe mpenzi wangu!!”
“Unasemaje Matha??” aliuliza kama vile hajalisikia swali. Matha hakusema tena aliamini Michael amesikia.
“Hivi unataka niuwawe ndio ufurahie???” Michael alisema kwa sauti iliyojaa hamaki.
“Hautakufa…akuue nani???”
“Matha unauliza aniue nani???...wewe umesema John anaua au sikukusikia??” alihoji Michael kwa ghadhabu, tayari alikuwa amejinasua kutoka mikononi mwa Matha.
“Kama nisipokulinda utauwawa, laini nitakulinda” alijitetea Matha kwa sauti iliyojaa uhitaji wa mahaba.
“Matha ujue unahatarisha maisha yangu, kwanini tusiuache mchezo huu, John hakupi nini kwani??” alilalamika Michael. Matha hakusema neno akaanza kulia, mwanga wa mbalamwezi ulimruhusu Michael kuishuhuda simanzi hii, hakuamini kama maneno yake ndo yamemkasirisha mrembo huyu, kosa kubwa!!! Alipojaribu kumbembeleza huku akisahau kuwa yu uchi alijikuta tena katika mahaba mazito ambayo baada ya hapo yalizaa tabia ya mara kwa mara kudanganya kuwa wanakuja kwa ajili ya mafunzo na kisha kuubadili uwanja wa mafunzo kuwa uwanja wa mahaba.
Nachezea sharubu za simba!!!! Aliwaza Michael.

******
Matha alikurupuka kutoka kitandani alipokuwa amelala na John kitandani, mbio mbio alikimbia kuelekea bafuni kuna jambo lilikuwa limemtatiza, lilikuwa jambo geni sana kwake. Alikuwa ana kichefuchefu cha ghafla, hakuwa anaumwa hapo kabla wala hakuwa amekula kitu kibaya usiku uliopita. Alifika na kutapika bafuni, kichefuchefu kikapungua hakutaka tena kurudi kitandani alioga kabisa na kuingia katika chumba kidogo cha mazoezi. Kichefuchefu kikamrudia tena safari hii hakutapika baada ya kukikabili kwa kulamba limao alilolitoa katika jokofu.
“Matha Mwakipesile ndo wewe eeh!!!.”
“Ndio ni mimi dokta vipi malaria nini??.” alifanya utabiri usiokuwa sahihi.
“Hapana hauna Malaria mwanangu..”
“Mh!! Nini sasa hichi Mungu wangu.”
“U mjamzito Matha!!!....mwezi mmoja.”
“Dokta!!! Be serious!!!”
“Ninamaanisha, vipi kwani hukutegemea au??.”

***MATHA ANA UJAUZITO......PABAYA HAPO

ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Recent Posts