Friday, July 15, 2011

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka inayosimamia Mifuko ya Maendeleo ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (kulia) na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Lightness Mauki kwenye ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu, Bungeni Mjini Dodoma Julai 14,2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akijadiliana jambo na baadhi wa wabunge mara baada ya kuwasilisha hotuba yake ya Makadirio ya Matiumizi ya Fedha za wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012 Bungeni leo mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika(kulia), ambaye pia ni Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Wizara ya Nishati na Madini akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Bunda, Ester Bulaya leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) akijadiliana na Mbunge wa Jimbo la Sumve Richard Ndassa (kulia) na Kushoto ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Anan leo mjini Dodoma

No comments:

Post a Comment

Recent Posts