Friday, July 15, 2011

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka inayosimamia Mifuko ya Maendeleo ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (kulia) na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Lightness Mauki kwenye ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu, Bungeni Mjini Dodoma Julai 14,2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akijadiliana jambo na baadhi wa wabunge mara baada ya kuwasilisha hotuba yake ya Makadirio ya Matiumizi ya Fedha za wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012 Bungeni leo mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika(kulia), ambaye pia ni Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Wizara ya Nishati na Madini akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Bunda, Ester Bulaya leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) akijadiliana na Mbunge wa Jimbo la Sumve Richard Ndassa (kulia) na Kushoto ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Anan leo mjini Dodoma

Wednesday, July 13, 2011

raisi ahutubiwa, wizara za pondwa

raisi wa serikali ya AUCTASO bw. DAUD BONIPHACE MBASA. alihutubiwa ijumaa iliyopita katika ukumbi wa masomo ( LECTURE HALL 1) hata hivyo katika hotuba yake rais huyo alisoma na kueleza baadhi ya mafanikio na changamoto iliyokutana nayo serikali yake katika kipindi cha kwanza cha uongozi wake.
          wakati alipo amliza kuhutubia aliruhusu maswali mbalimbali kutoka kwa wanachuo. na kwa utaratibu huo ndipo wanachuo walipopata muda wa kuanza kuzungumzia mabo muhimu yanayoihusu serikali na wizara zake. pia wanachuo hao waliwaponda wabunge wao kuwa ni watu ambao wapo kama mawaziri badala ya kutetea maslahi ya wanachuio wenzao. hata hivyo ahiyo haikuishia hapo pia wanachuo waliponda mfumo wa serikali nzima jinsi ulivyo ya kuwa haupo kwaajili ya maslahi ya wanachuo bali upande wa walimu. kama hiyo haitoshi baadhi ya wizara zilionekana kutokufanya kazi kabisa katika kipindi chote cha uongozi huu kwa awamu ya kwananza. pia mawaziri walikumbushwa kujituma kwa nguvu kwaajili ya kuwatetea wanachuo na sio administration. pia baadhi ya waanchuo walilalamikia itendo ya baadhi ya mawaziri kutokufahamika hapa chuoni na kutokuwa na umuhimu kabisa .
           Sisi kama wana AMUCTASO hatutachapisha hewani wizara ambazo zinalaumiwa

leo kusaini PH 102

wanafunzi WA amucta LEO TUTASAINI MACHAGIJA SAA 9 mchana. kwa taarifa za uhakika kutoka ndani ya ofisi ya makamu mkuu huyu wa chuo zinasema kuwa hali imechukua muda mrefu zaidi kufanyika kutokana na kuchelewa kusahihisha na hii inatokana na kuwa pekee yake katika.ktika idara hii hiyo ya falsafa.

Friday, July 8, 2011

wiki moja kabla ya UE.

  ni wiki moja sasa kabla ya wanachuo wa chuo wa chuo hiki cha amucta kuanza kufanya mitihan yao ya mwisho wa mwaka wa masomo. mitihani hiyo itaanza hapo ijumaa ya wiki ijayo ambapo kwa mujibu wa wanachuo hao  ni kwamba kila kitu kipo tayari na wanacho subiri ni paper tu. pia wanadai hawamwogopi tena yule mtunzi hatari NAMILEMBE.

Wednesday, July 6, 2011

AJA yaja amucta

  Na amucta team,
  
katika hali ya kutoa uhuru wa  habari hapa amucta, kimeanzishwa chama cha waandishi wa habari wa AMUCTA chama hicho ambacho kilizinduliwa juzi na katibu mkuu wawizara ya  habari, sayansi na teknolojia mh. NYANDA SYLVERY, katika uzinduzi huo chama hicho kilwachagua viongozi wao wa rasmi wa mwaka huu na viongozi hao walikuwa kama ifuatavyo
                     JACKSON MESHACK---- mwenyekiti
                     KIMOMWE  MARTHA--- katibu
                     ELIFURAHA JOHN ------- mharirimkuu
                     KALIMA  SALUM--------- mhariri msaidizi.
baada ya kupatikana uongozi huo, mwenyekiti aliyechaguliwa kushika nafasi mh. Meshack aliwataka wanachama wote wa chama hicho kushirikiana na kuaandaa jarida la mfano kwa mwaka huu. pia walikubaliana kuwa jarida hili litoke kabla ya watu kwenda field, pia walikubaliana kuwa jumamosi hii wakutane kuwasilisha habari walizo ziandaa ili zihaririwe na kuchapwa kwaajili kutoa jarida. chama hicho vha waandishi wa habari hapa AMUCTA kinaitwa AMUCTA JOURNALISTS ASSOCIATION (AJA)

kama wanahabari tunawakaribisha AJA kwenye tasnia ya habari.

Friday, July 1, 2011

mwisho wa NAMILEMBE LEO BAED B

yule mwalimu anayeogopwa na wanafunzi wengi hapa AMUCTA yaani madam NAMILEMBE raia wa Uganda leo anahitimisha module zake hapo lecture hall 1. wakizungumza kwa nyakati tofauti na blog hii pendwa ya wana AMUCTA, wanafunzi wa BAED B walisema yakuwa imekuwa heri ya kwake yeye kumaliza module maana amekuwa akiwakimbiza saana wanafunzi wa hapa. pia hawakusuita kumsifia kwa kuwa anafundisha vizuri japo kuwa ni mkali wa kutunga mitihani yake nja amekuwa mgumu kwa wnfunzi kwa kusainia wanafunzi waliochelewa kusaini. kila la heri madam NAMILEMBE  kwa kutufundisha vizuri na pia WELCOME NEXT ACADEMIC YEAR  if possible

Recent Posts