Monday, July 9, 2012

MALIPO YA UKARIMU-1

      Alex ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 22 tu lakini tayari alikuwa amepata nafasi ya kuingia chuo kikuu kwa mara ya kwanza katika maisha yaka. Akiwa mwenye furaha tele, Alex alivuta kumbukumbu ya yale yaliyowahi kumtokea huko nyuma, ambapo alikumbuka maisha machungu aliyoyapitia, ilikuwa ni vigumu kwake kuamini kama kweli siku moja angefika chuo kikuu. Mara nyingi kila akikumbuka ya nyuma machozi yalikuwa yakimlenga akitamani kulia lakini alijipa moyo, na kuona kama ni sehemu ya maisha ambayo hata wanadamu wengine wanayapitia. "thanks God leo nimeona jina langu kuwa naenda chuo kikuu, Duh siamini" hayo yalikuwa ni mawazo ya Alex akifikiria jinsi maisha yanvyobadilika. 
     
Baada ya muda wa mwezi mmoja tayari Alex alikuwa katika maandalizi muhimu ya kwenda chuoni, alikuwa amepangwa kwenye chuo cha St. Augustine University of Tanzania tawi la Tabora, hili lilikuwa ni tawi jipya ambalo lilikuwa limefunguliwa hapo Tabora. ilikuwa ni furaha isiyo na kifani. Safari yake ilianzia Moshi Mjini kuelekea Arusha tayari kwa kusafiri kwenda Tabora kwenda kuona kwa mara ya kwanza jinsi gani ambavyo maisha ya chuo kikuu, hali ilikuwa si ya kawaida ndani ya gari la kutoka Moshi. hata hivyo alifika Arusha mnamo saa 12 jioni, na alipofika tu alimpigia simu rafiki yake Omary ambaye alikuwa anasoma Arusha Technical College, akaungana na Omary pamoja na Rafiki yake aliyekuwa anasafiri kutoka Moshi kwenda Tabora. walilala hapo chuoni siku hiyo, ki uhalisia Alex hakupata hata lepe la usingizi usiku huo. Alipata shida usiku huo maana mawazo juu ya hali ambayo wangekutana nayo huko chuoni hakuijua wala hakuwahi kufahamu  watu huwa wanaishi vipi huko chuoni. kwa mawazo yake alifikiri kuwa pengine mtu akienda chuoni atakuwa anaishi kama mwanafunzi wa Boarding wa A-level, hayo yalikuwa ni mawazo tu ambayo yalikuwa yakimsumbua kijana wetu Alex.
      Asubuhi waliamka asubuhi na mapema kuwahi usafiri wa basi iliwasije wakachelewa kuelekea chuoni. Walipofika hapo stendi ya mabasi walipanda gari tayari kwa safari ya kuelekea Tabora, ambapo matumaini ya safari yake yalikuwa ni kuitimiza malengo yake ambayo alikuwa anayalilia kwa muda wa miaka mingi. Baada ya kuuacha mji wa Arusha aligeuka pembeni mwa siti yake, alishituka sana macho yalimtoka kwa taharuki ambayo hata mwenyewe hakujua kama ametaharuki namna ile,pamoja na kwamba Alex alikuwa anasikiliza mziki kwenye Ipod yake, lakini hakusikia tena huo mziki, ilikuwa ni kazi ngumu kuzuia hisia zake.

Je Alex ameona nini au ndio malipo yaukarimu, je ni ukarimu upi huu ambao Alex analipwa au analipa??

ungana na 
Meshack Jackson 
jumatano hii..................... Toa maoni juu ya Hadithi hii

No comments:

Post a Comment

Recent Posts