Tuesday, November 27, 2012

SITAISAHAU facebook 10



MTUNZI: Emmy John P

MAWASILIANO: 0654 960040


SEHEMU YA KUMI



ILIPOISHIA

Nilitaka kumuita jina lake kwa sababu nilihisi ninalijua jina hilo. Hata sura mbona nilikuwa nimewahi kuiona hapo kabla? Lakini kabla sijajua anaitwa nani. Teksi ilipigiwa honi ikapisha njia ikaondoka zake.
“Ah!! Huenda aliwahi kunibeba hapo kabla.” Nilijipa moyo.
Nikafungua pochi yangu na kuhifadhi hicho nilichookota.
“Mungu wangu!!!!” nilipiga kelele kwa nguvu sana. Nilikuwa nimesimama wima.
Kwa kuwa halikuwa eneo la watu wengi nilipata sekunde kumi za kuhakikisha nilichokiona.
Hakika kilikuwa chenyewe.
Kilikuwa kitambulisho cha chuo ni heri kingekuwa changu.
Kitambulisho cha John mikononi mwangu. Kitambulisho kinachoaminika kupotea ,msibani huko Iringa , kitambulisho nilichokiona ndotoni.
Kitambulisho cha muuaji!!!
Ewe dunia funguka unimeze!!! Ni sala niliyoiomba kimyakimya.
Nilikuwa nimezizima siwezi kwenda mbele wala kurudi nyuma.
Harufu ya kifo!!!!

***NI jambo juu ya jambo…….ISABELA ISABELA ISABELA.
Lakini je ungekuwa wewe ungefanya nini sasa….John unampenda, John umeota akiwa anaua, kweli mtu kafa. Huyu mtu ni binamu wa John. John anapoteza kitambulisho. Na ndotoni muuaji anadondosha kitambulisho.
John na muuaji wa ndotoni wanafanana….Kabla ya kujua Isabela mimi nilifanya nini…je WEWE UNGEFANYA NINI HAPO.
Pagumu!!!!!

ENDELEA

ITAENDELEA.

Nilisahau ni jambo gani lilikuwa limenipeleka huko mjini. Yale mawazo niliyoamini nimeyapunguza kwa kunywa pombe sasa yalikuwa yamerudi kikamilifu. Tena mara mia zaidi.
Hofu ikatanda. Nikachukua teksi nyingine nikarejea nyumbani kwangu.
Nilikuwa natetemeka, na kila nilipoguswa na kitu nilishtuka. Hata nywele zangu za bandia kichwani ziliponigusa shingoni nilitetereka.
Nilipohakikisha kuwa nimeifunga milango vyema kabisa na ndani nilikuwa peke yangu. Nilifungua mkoba wangu nikakitoa kitambulisho.
Hapakuwa na mabadiliko. Kilikuwa kitambulisho rasmi cha chuo kikuu matakatifu Augustino. Mmiliki akiwa John Joseph.
Mpenzi wangu.
Nililazimisha akili yangu kutafuta kumbukumbu huenda siku moja aliwahi kunipatia kile kitambulisho. Hapana kitu kama hicho.
Au aliweka mwenyewe bahati mbaya akakisahau? Hilo swali walau kidogo liliamsha uhai na kunipunguzia hofu.
Akija nitamuuliza!!! Nilimaliza hivyo. Nikautua mzigo wa mawazo.
Nikaingia maliwatoni nikasafisha mwili wangu kijuu juu. Nikajitupa katika sofa iliyokuwa sebuleni. Ule uchovu wa ulevi jana usiku ukawa unanishawishi kusinzia.
Nikajifikiria kwenda kulala chumbani. Mara mlango ukagongwa.
Nikajikausha!! Ukagongwa tena.
Nikaenda kufungua. Alikuwa ni John.
Alilazimisha tabasamu!! Nami nikatabasamu. Hatukusalimiana.
Tayari kakereka jana sikulala nyumbani!!! Niliwaza, huku nikijiandaa kukabiliana na maswali atakayoniuliza kwa fujo.
Wanaume wana mikwara jamani!!!!
Akafika hadi katika lile sofa nililokuwa nimejilaza awali. Akajitupa hapo. Akazishusha pumzi kwa nguvu sana. Kisha akajishika kichwa. Mimi yangu macho nikawa nasubiri lawama.
“I hate this…..” Alisema huku akiwa kama anajisea mwenyewe.
Yaleyale!!! Nikajisemea.
“Uko ok!! John!!” Hatimaye nilimuuliza. Hakunijibu!!
“John jamani….” Nilibembeleza. Bado hakunijibu kitu. Nikaamini kuwa John amekerwa sana na kitendo changu cha kulala nje bila taarifa.
Wazo!!! Wazo likanijia. Nikasimama tena bila kumuaga nikatoweka pale hadi chumbani. Nikazama katika mkoba. Nikachomoa kile kitambulisho.
Nikakisokomeza katika sidiria niliyokuwa nimevaa. Kisha nikarejea sebuleni. Wanaume dawa yao ndogo tu!! Mfanyie kitu anachopenda kwa wakati!! Baaasi hakuna ujanja tena.
John akishaona kitambulisho chake ndo basi tena anasahau kuhusu suala langu la kulala nje. Najua mada itageuka na yatazaliana maswali.
Umekitoa wapi? Ilikuwaje? Dah!! Siamini.
Kwisha mchezo!! Nilijiaminisha.
Sasa nilikuwa mbele ya John. Bado alikuwa kama anayefikiria kitu kabla ya kuzungumza. Nikamsubiri labda atasema kitu hakusema. Nikamuita akaitika kwa kichwa chake kutingishika.
“I hate…my country (naichukia nchi yangu).” Alisema huku akitazama mbele. Nikaurudisha mkono uliokuwa umekamata kile kitambulisho tayari kwa kumshangaza. Nikakirudisha katika sidiria ili nipishe kwanza anachotaka kusema John.
“Nini tena mpenzi wangu jamani.” Tayari nilikuwa ubavuni mwake wakati anayasema haya. Hakujibu upesi bali alicheka kwanza. Kicheko cha kujilazimisha.
“Eti kile kitambulisho….kile kitambulisho kile.” Alianza kuzungumza, nikafarijika kusikia mada ni juu ya kitambulisho na sio wivu wowote wa kimapenzi. Kisha akamalizia, “kile kitambulisho eti kimeibiwa ama kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Serikali yetu bwana..haya sasa kuna haja gani ya kuipenda?” Alimalizia, bado alikuwa ametazama mbele tu. Akiyang’ata meno yake kukabiliana na pepo la hasira.
Mshtuko!! Nikatoa kelele ya kuogopa, lilikuwa yowe ambalo hata John aliyekuwa anatazama mbele lilimshtua akapata nafasi ya kuniangalia.
Nilikuwa wima!!! Mikono kichwani mara kiunoni, wakati mwingine najiziba uso. Mithili ya mwendawazimu.
John alidhani nasikitika kwa jinsi alivyonitazama lakini sikuwa katika kusikitika, nilikuwa naogopa sana. Kitambulisho kilichoibiwa si ndio hichi katikati ya maziwa yangu ama!!! La haula!!
Ndio hiki kitambulisho cha muuaji. Muuaji mwenyewe si ndio huyu mbele yangu. John ndiye muuaji anayejitafuta mwenyewe.
Mbiombio nikakimbilia chumbani. Sikujiamini tena kuwa mbele ya John. Sikuwa na uwezo wa kumueleza chochote juu ya kitambulisho chake. Kitambulisho kile kilikuwa na utata mkubwa.
Nilipokuwa natimua mbio kwenda chumbani, John naye nyuma akanifuata. Muuaji nyuma yangu, lengo langu nifike chumbani niwahi kujifungia mlango. Maziwa yakaruka kwa fujo wakati nakimbia, kitambulisho kikazidiwa ujanja kikakosa pa kujificha. Upesi kikachoropoka.
Kitambulisho haramu kikadondoka katika marumaru.
Nikasita kuendelea mbele. Sikutaka John akione kile kitambulisho.
Niliweza kusimama nikageuka. John huyo anakuja mbiombio. Macho ya John kwangu. Macho yangu katika kitambulisho kilichokuwa katika marumaru. Kila mmoja na wazo lake.
Kitambulisho sasa kikawa katikati yetu. John na moka zake modeli ya ‘wanchoma kumoyo’ akakikanyaga bila kutambua kile kitambulisho wakati ananikimbilia. Kitambulisho ni manira laini sana, kikaisikia kero ya kukanyagwa na bwana John. Zilikuwa zimebaki hatua moja na nusu niweze kukichukua ndipo nikakumbana na wakati mwingine matata ambao nisipousimulia utanilaumu mwisho wa simulizi. Mi sitaki lawama!!!
John akateleza, baada ya kukanyaga kile kitambulisho. Marumaru ikampokea kwa shangwe, kisogo kikatoa mlio kama chuma kilichogongana na chuma kingine. Kitambulisho kikaachana na kile kiatu kikawa mbele yangu.
Shida yangu ilikuwa kukiwahi kitambulisho. Sasa kitambulisho kimetulia na John ametulia tuli sakafuni.
Mamaaaa!!! Niliita tena, mama mwingine nani sasa zaidi ya mwalimu Nchimbi huko Makambako? Atanisikiaje sasa wakati nipo Mwanza. Ujinga!!
Nikimbie!!! Nilijiuliza huku nikitetemeka.
Kwenda wapi sasa?? Ujinga mwingine.
Mara damu nzito nyuma ya kisogo cha John. Macho yamefumbwa kistaarabu. Mdomo wazi.
Nikahisi kuchanganyikiwa sasa. Damu ikazidi kusambaa katika marumaru ile nyeupe.
“Atakufia huyu Isabella shtuka fanya kitu.” Sauti ikaniambia. Sasa hapo nikashtuka, nikainama nikakwapua kitambulisho chenye utata. Nikakimbia nje.
Taksiii!! Nikapiga kelele. Ikasimama, ikaanza kurudi nyuma. Macho ya dereva taksi badala ya kunitazama usoni na kunisikiliza shida yangu, yakawa yananitazama huku mapajani. Nilipojitazama, mbio nyingine mpya kurudi ndani. Nilikuwa nimevaa kinguo kifupi sana. Hakina tofauti na chupi. Kanga iliyokuwa inanisitiri ilikuwa imedondoka huko ndani.
Dereva teksi alinisubiri. Nikarejea nikiwa nimeegesha kanga kiunoni.
Nina mgonjwa!! Ni mume wangu. Ameanguka!!! Nilimsihi huku nikimvuta. Akanifuata. Tulipofika ndani bado John alikuwa ametulia tuli vilevile.
“Ameanguka!!.” Nilijibu bila kuulizwa. Dereva akafanya jitihada za kumnyanyua John. Wapi haikuwezekana. Kila aliposhikwa ili anyanyuliwe alilegea na kuangukia upande mwingine.
Mimi nilikuwa mtazamaji na nilikuwa namuogopa sana John.
“Hebu ngoja nakuja!!!.” Aliniaga dereva. Nikaamini anaenda kuleta msaada zaidi. Nikangoja kwa muda fulani dereva hakurudi!! Nilipotoka nje hapakuwa na dereva wala teksi.
Nilitamani kupiga kelele. Nikahaha huku na huko. Baada ya robo saa nikaona teksi. Ilikuwa inakuja pale kwangu. Iliposimama alikuwa ni yule dereva. Nyuma yake ikafuatia Ambulance.
Wakashuka wataalamu. Wakamtwaa John asiyejitambua.
Bahati nzuri walikuwa wananitambua. Ukarimu ukaongezeka maradufu.
John akafikishwa hospitali. Agha Khan.

Hakuwa amepasuka sana. Ulikuwa ni mpasuko wa kawaida. Akashonwa. Lakini akatakiwa kupumzika. Fahamu zilimrejea baadaye. Hakuwa msumbufu, alielewa upesi nini kinachoendelea.
Siku iliyofuata ndio siku ambayo John alitakiwa kutoka.
Nililazimika kurejea nyumbani kuchukua pesa kwa ajili ya malipo.
Nikiwa katika teksi, niliwaza juu ya kile kitambulisho. Nikahisi kitaniletea matatizo iwapo nitaendelea kukishikilia, tayari kilitaka kuutwaa uhai wa John. Sasa kitazua mengine.
Sasa nimpatie ama vipi? Nilijiuliza. Sikupata majibu.
Ile ndoto ya muuaji anadondosha kitambulisho ilikuwa inanikera maana haikutaka kufutika kabisa. Haikuwa ndoto kama ndoto nyingine maana sasa niliiona sura ya muuaji. Muuaji alikuwa John.
Nguvu ya penzi lake ikanikwamisha kumwambia mtu yeyote ukweli huu. Hata yeye pia sikumwambia.
“Hichi kitambulisho simpatii.” Niliamua kusimamia upande huo.

SITAISAHAU facebook

MTUNZI: Emmy John P.

CONTACTS: 0654 960040



SEHEMU YA TISA


                                                                                           ILIPOISHIA

Pasipokutegemea John alisukumwa chini, akapinduka, lakini yule bwana alijaribu kukimbia tayari mguu wake ulikuwa umekamatwa.

John alipogeuka ile alama ya kuchanwa na kisu ikaonekana. Nikabaki kama zoba siwezi kupiga kelele wala kutoa msaada wowote.

Huyu naye akageuzwa shingo, kisha ghafla pakawa giza sikuweza kuona mbele. Lakini nilihisi kama napoteza fahamu hivi.

Macho yalipopatra ujasiri na kufunguka nilikuwa nimezungukwa na watu wenye nguo nyeupe.

Kila jicho likinitazama mimi.

Hofu mpya ikaanza.

***ISABELA katika mtihani mwingine!!!!


ENDELEA


******

Watu hawa walitabasamu vizuri lakini sikujua kwa nini wanatabasamu.

“Pole sana!!.” Mmoja wao aliniambia.

“Nini kwani…eeh!! Hapa ni wapi.”

“Hospitali ulipoteza fahamu.” Mwanaume aliniambia.

Sasa akili ilianza kuunganika upya nikawatambua kuwa wale ni madaktari. Kilichonisibu nikashindwa kukielewa vyema. Nikavuta kumbukumbuku nikakumbuka kuwa ni ndoto. Ndoto nyingine ya maajabu. Ndoto iliyonifanya nizimie dah!! Hii ilikuwa hatari zaidi ya kawaida.

Nikatamani kumshirikisha mtu yeyote kati ya wale madaktari lakini nikaamini kuwa hawataelewa.

Mtu sahihi wa kumueleza ni John. Huu ni wakati muafaka wa kumueleza kila kitu kinachotokea. Ni John pekee ambaye anaweza kunielewa juu ya shida hii. Sikuona mtu mwingine wa kumueleza.

Nilipumzika kwa masaa kadhaa kisha John akaruhusiwa kuondoka na mimi. Ni yeye aliyenileta pale hospitali baada ya kugundua kuwa nilikuwa nimezimia.

Ilikuwa ni tukio la kawaida mtu kuzimia lakini lilikuwa si la kawaida kwa sababu aliyezimia ni Isabela. Mtu mwenye heshima zake pale chuoni. Kila mtu alitaka kujua nini kimenisibu. Nashukuru John alikuwa akiwajibu kwa niaba yangu.

Sasa tulikuwa chumbani. John alinikorogea uji wa ulezi akatia maziwa na pilipili manga. Alijua kuwa ninaupenda sana uji wa aina hiyo.

Nilipomaliza kunywa kikombe cha kwanza. Nilitaka kuanzisha ile mada juu ya nini kilinitokea ndotoni.

Maajabu!! Nilipomuita naye aliniita ndani ya sekunde hiyo hiyo. Tukajikuta tunacheka.

“Nani sasa aitike ya mwenzake.”

“Ladies first.” John alidakia. Basi sikuwa na ujanja mimi nikaitika nimsikilize John anasema nini.

“CR (Class representative) wa PR (Public relation)….”

“Amekufa??.” Niliuliza hata kabla John hajamaliza kunieleza. Tayari picha ilianza kuja kichwani.

“Yeah! Umejuaje kwani?.” Aliniuliza.

“Ni yule alikuwa ndugu yako au sio..”

“Ni yeye Michael ndio jina lake. Binamu yangu.” Alisema kwa masikitiko makubwa sana John kisha akainama. Hapakuwa na haja ya kuuliza kama alikuwa anajizuia kutoa machozi.

“Pole John.” Nilimwambia kwa sauti ya chinichini.

“Wamemnyonga binamu yangu wameona kumuua Jesca haitoshi aaah!!.” Alilalamika mwisho akashindwa kuendelea akaanza kulia kwa sauti ya juu. Nikawa katika hali mbili ghafla. Kwanza hofu kubwa kwani alichozungumza John sasa kilitaka kuwa kile ambacho nilikiota. Pili nikawa katika kumbembeleza Michael kwa juhudi zote. Huku nafsi ikiniambia ninambembeleza muuaji.

Lakini muuaji gani huyu sasa asiyejitambua kuwa ameua? Nilijiuliza.

Nikahisi kuchanganyikiwa.

“Isabela.” Aliniita.

“Bee!!.”

“Nitahakikisha namfahamu huyo muuaji…kitambulisho chake kilidondoka na polisi wamedai wanafanya upelelezi.” John alitoa kauli nyingine. Kauli ambayo ilinishtua upya. Niliona kitambulisho kwenye ndoto. Lakini mwenye hicho kitambulisho alikuwa ni John mwenyewe na muuaji ni John.

Ina maana John anaapa kujitafuta mwenyewe ama!!

Nilichanganyikiwa!!!

Nilitamani kumweleza John juu ya ile ndoto lakini sasa hamu yote ilikuwa imetoweka. Sikuwa na haja ya kumweleza, ataniamini vipi. Kwamba ni yeye aliyemuua binamu yake kwa kumnyonga na kuwa hicho kitambulisho ni cha kwake.

Hapana hawezi kuniamini hata kidogo!! John ataniona mjinga na ataidharau ndoto yangu.

Nikaghairi kumweleza. Siri hiyo ikajikita na kuanza kuutesa moyo wangu. Mateso makali.

Baada ya maziko hayo. Sasa chuo kilikuwa kimesimamia kidete juu ya upelelezi juu ya vifo mfululizo vya wanafunzi katika chuo cha mtakatifu Augustino. Kitambulisho kilichookotwa eneo la tukio kilikuwa kimeamsha hamasa ya kumjua muuaji. Polisi walikuwa makini sana katika hili na walikuwa watulivu wakiendelea na upelelezi kimya kimya.

Alipotoka msibani John alikuwa na jingine jipya. Alikuwa amepoteza kitambulisho cha chuo.

“Yaani sijui hata kimepoteaje. Maana kilikuwa kwenye Wallet yangu. Sasa ah!!” Alinieleza John. Sasa ndoto ikawa imekamilika kabisa.

Ni John alikuwa muuaji. Lakini muuaji wa ndotoni.

Ndani ya siku saba nilikuwa nimekonda sana. Uzito ulikuwa umepungua. Ni serikali ya ubongo wangu pekee iliyojua ni nini kinanisibu.

Si John wala mtu mwingine aliyejua nini kinanisibu.

Nilikuwa nawaza juu ya usalama wa John. Niliona kama anaenda kukutana na hatia kubwa sana ambayo hawezi kuikwepa. Lakini kosa lile alilifanya katika ndoto yangu mimi pekee!!!

Kivipi niwe na hofu!!

Nilijifariji kuwa ile ilikuwa ni ndoto tu lakini hapana bado nilikuwa hoi bin taabani

Suala la kupoteza kitambulisho chake lilinipagawisha.kimawazo.

HATIA------- 15


MTUNZI: George Iron

CONTACTS: 0655 727325


SEHEMU YA KUMI NA TATU


Matha bila kujua kuwa anafuatiliwa alielekea barabarani akaangaza hapa na pale akanyanyua mkono wake wa kuume akaita taksi, haraka haraka dereva aliyekuwa amemuona Matha aliifikisha gari yake Matha akaingia ndani.

John akasubiri ile teksi ilivyoanza kuondoka naye akaingia katika teksi aliyokuwa amekodi.

“Fuata gari hiyo!!” alitoa maelekezo hayo John, dereva akafuata maelekezo. Gari mbili zikawa zinafuatana bila gari ya mbele kuwa na habari juu ya hilo, John alikuwa amevaa miwani nyekundu kuziba macho yake yaliyokuwa mekundu sana, hakutaka kumtisha dereva.


*****

Adrian alikuwa amekaa nje ya duka kubwa la kuuza nguo maeneo ya Makoroboi, umeme ulikuwa umekatika na biashara haikuwa nzuri sana siku hiyo. Adrian alikuwa anaperuzi katika gazeti la michezo alilokuwa amenunua muda mrefu uliopita.
Ubovu wa biashara wa siku hiyo haukumshtua sana Adrian kwani alikuwa na uhakika kuwa maduka mengine matano yaliyokuwa yamezagaa jijini Mwanza yangekuwa na biashara nzuri siku hiyo.
Mzee Mhina Mboje alikuwa amemuamini sana kijana wake huyu wa pili kuzaliwa, japo aliwahi kuikataa shule alipokuwa kidato cha tatu lakini akili yake katika kutafuta maisha ilikuwa inavutia wengi sana na kuwapa wivu. Adrian sasa alikuwa anasimamia maduka yote ya baba yake huku lile la Makoroboi likiwa mali yake binafsi. Adrian aliwahi sana kujipanga kimaisha kwani tayari alikuwa ameondoka nyumbani miaka mingi iliyopita na kuamua kufanya maisha ya kupanga.
Mwanzoni alikuwa anakaa na mdogo wake wa kiume lakini baada ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi aliamua kumrudisha mdogo wake nyumbani kwa wazazi ili aupate uhuru zaidi wa kujivinjari na binti huyu. Kwa kuwa ulikuwa upendo wake wa kwanza alikuwa akimsikiliza sana binti huyo ambaye alikuwa bado ni bikra, mapenzi yao ya kitoto toto waliyajua wao wenyewe. Adrian hakuruhusiwa kufanya lolote katika mwili wa huyu binti zaidi ya kumbusu shavuni tu na kuishia kucheza cheza.
Adrian hakuruhusiwa pia kutangaza kwa mtu yeyote juu ya uhusiano huu eti kisa tu baba yake binti alikuwa mkali sana. Upendo wa dhati ukawa umejijenga.
Ile hali ya Adrian kuukana uhusiano wake mbele ya watu ili kumfurahisha mpenzi wake huyo ilikuja kumgharimu sana. Akatokea mwanaume aliyekubuhu akamlaghai huyu binti ambaye ni Matha, alikuwa ni John Mapulu aliyemnyang’anya Adrian Mhina tonge mdomoni. Matha akahamishia upendo wake kwa John ambaye alikuwa ameitoa bikra yake. Adrian akabaki kama zezeta asijue la kufanya lakini hatimaye akazoea baada ya wawili hawa kuhamia sehemu nyingine kabisa mbali na yeye.
Kumbukumbu juu ya Matha zikasahaulika pia kutokana na mchumba wake ambaye walikuwa wanatarajia kuoana baada ya mwezi mmoja kwani walikuwa na mwaka mzima tangu waishi maisha ya uchumba huyu alikuwa ni Monica Lewis, dada zake walikuwa wakimpenda sana na hii ndio ilikuwa chachu ya kumshawishi Adrian kuoa.
Mara kwa mara Monica alikuwa analala nyumbani kwa Adrian, na hata kabla ya kutambulishana kwa wazazi tayari Monica alikuwa ameshiriki katika tendo la ndoa na Adrian, ujanja aliofanyiwa na Matha miaka iliyopita hakutaka tena kumwamini mwanamke.
Mwezi mmoja kabla ya ndoa tayari Monica alikuwa mjamzito, jambo hilo walilitambua wao peke yao, hawakutaka wazazi watambue hali hiyo ya wao kupata mtoto nje ya ndoa.
“Mambo vipi kaka” alisalimiwa Adrian akiwa bado ameinamia gazeti lake.
“Poa karibu!!” alijibu huku akiunyanyua uso wake. Hakutaka sana kumuangalia mtu aliyekuwa mbele yake kwa sababu alikuwa ameficha uso wake.
“Unanikaribisha unanijua kwani??” aliuliza yule binti ndani ya baibui, Adrian akacheka.
“Adrian!!! Za siku!!”
“Mh!! Kwani we nani”
“Matha!!! Jamani” alijitambulisha. Kumbukumbu ya sauti ile ya kupendeza ikarejea katika kichwa cha Adrian. Kabla hajajua la kufanya, Matha alimsogelea na kumkumbatia. Adrian hakuamini alichokuwa anakiona mbele yake, Matha akasikika kama analia, kilio hicho kikafuta hasira zote alizokuwanazo Adrian, joto lililopenya katika baibui na kumuingia Adrian likaibua hisia za upendo.
Walikumbatiana kwa dakika nzima. Kisha baada ya kuachiana Matha alijifunua kidogo, Adrian akaona vishimo katika mashavu ya Matha.
Upendo maradufu ukamvaa!!!
Matha akawa katika majuto ya hatia iliyokuwa inamkabili kwa yote aliyomtendea Adrian miaka iliyopita. Kwa mbaali akausikia mguso wa kimapenzi kutoka kwa Adrian. Akaanza kupatwa na hofu huenda Adrian bado ana hasira, lakini haikuwa hivyo!!!!
Walizungumza kwa dakika kadhaa kisha Matha akamwachia namba yake kijana huyu mwenyeji wa Tanga aliyekulia jijini Mwanza.
Yote hayo yaliyokuwa yanatokea yalishuhudiwa na jicho kali lililokuwa nyuma ya miwani, jicho la John Mapulu. Alitamani kumfyatua palepale yule mwanaume lakini alijikaza, akauzuia wivu usipitilize. Akawa amemtambua mwizi wake akapanda teksi na kuondoka, wakati huo na wawili hawa walikuwa wameagana.
Laiti kama angesubiri kidogo tu angepata kufahamu kuwa mpenzi wake huyo anakwenda kukutana na Minja anayeaminika kuwa alikufa usiku uliopita.
Lakini John Mapulu hakuwa na subira.

John alirejea nyumbani kwake, hakutaka tena kwenda kwenye tukio la ujambazi akili yake ilikuwa imechanganyikiwa kabisa. Uchungu alioupata Adrian miaka mitatu iliyopita sasa ulikuwa umemgeukia yeye.
Wakati anamnyakua Matha mikononi mwa Adrian alijiona kidume sasa na yeye alikuwa katika majaribu ya namna ya kipekee.
“Kama mwanzoni nilimchukulia Matha wake sasa wakati huu naitwaa roho yake, mshamba kama yule hawezi kumchukua Matha kirahisi hivyo, nitamuua!!!” aliapa John kwa sauti ya juu.
Alikuwa kama amechanganyikiwa!!!
Wivu ukawa unamtesa!!!


******


“Tukutane hapo nje ya chuo cha biashara (CBE)”
“Sawa dada” alijibu Minja. Matha akapiga hatua kadhaa akawa amefika hapo chuoni. Minja alikuwa ameanza kukasirika baada ya kuwa anapiga simu ya Matha halafu haipokelewi.
“Ingia ndani!!!” Matha alimuamrisha Minja bila kumuangalia usoni. Hiyo ilikuwa ni mbinu ya kuepusha kama yupo mtu anawafuatilia asiweze kugundua lolote. Laiti kama angejua aliyekuwa anawafatilia tayari amepata jibu na kuondoka hata asingeweza kujihangaisha hivyo.
Minja aliingia akaa katika meza moja, baada ya dakika mbili Matha naye akafika.
“Samahani kaka naweza kukaa hapa?” alizuga, Minja akashangaa. Matha akajiongeza akakaa.
“Chooni wapi kaka samahani” aliuliza kwa sauti ya juu ili majirani waweze kumsikia.
Minja akashangaa tena.
Matha akamuuliza mtu mwingine akaelekezwa akaenda uani.
Aliporejea alikaa alipokuwa Minja. Aliamini kuwa tayari amewapoteza baadhi ya watu.
“Ehee!! Kuna tatizo gani?”
“Yaani sijui nisemeje”
“Umeniita kufanya nini kama hujui la kusema” aliunguruma Matha, Minja akaogopa.
“Usiku kuna mtu ameuwawa ndani kwangu” alijitutumua na kumueleza kila kitu kilivyokuwa. Matha akawa ameelewa kuwa dhumuni lilikuwa ni kuuwawa kwa Minja.
“Laiti kama John angempata jana basi najua mambo yangekuwa mabaya……” aliwaza Matha huku walau hofu ya John kugundua tatizo hilo ikianza kupungua, lakini uwepo wa Minja jijini Mwanza ungekuwa bado ni tatizo. Matha hakuona tena haja ya kumuua Minja kwani alimuona kama hana hatia yoyote ile tena.
“Unatakiwa uondoke haraka hapa Mwanza”
“Sasa naenda wapi dadangu nisaidie”
“Hujui pa kwenda, basi utaenda jela” alisema Matha, Minja akatetemeka kusikia hivyo.
“Chukua hii, kesho uondoke!!!” Matha alimkabidhi Minja shilingi laki moja.
Laiti kama angejua kuwa Minja kuna jambo zito analifahamu wala asingekubali aondoke hai jijini Mwanza.
Asubuhi iliyofuata Minja akaondoka kuelekea Singida, alitegemea kufikia kwa rafiki yake ambaye waliwahi kufanya shughuli za udalali pamoja jijini Dar es salaam. Amani ikarejea moyoni mwake, akajihisi kuwa hana hatia tena. Akawa amesahau kuwa hatia humfuata muhusika popote atakapoenda.
Hatia ilipanda naye katika basi kuelekea Singida!!!!
Hatia haimuachi muhusika mpaka mwisho wa uhai wake, hatia huingia na mtu wake kaburini!!!

CHOMBEZO: GUBERI LA KIMANYEMA

MTUNZI: INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)

SIMU: 0713 59 35 46/0755 04 05 20


SEHEMU YA KWANZA


ALIPOCHEKA, alipendeza. Tabasamu lake zuri, tabasamu linaloshawishi na kusisimua, huwafanya watu hususan wanawake, wamsogelee na kumsalimia. Baadhi ya wanawake hao husisimkwa miili pindi tu waisikiapo sauti yake. Alikuwa na sauti ya kipekee, sauti iliyogusa hisia zao na kuamsha gharika la maraha kwenye michipuo ya fahamu zao.
Alikuwa ni kijana wa kiume, mwenye sura ya ucheshi na macho ya upole. Hakuwa mwoga wa kutazamana na mtu, lakini hakupenda kutazamana na mwanamume mwenzake. Kwake, macho ya mwanamume mwenzake yalikuwa na kitu asichokijua, kitu kisichopendeza.
Hali hiyo ilikuwa kwa wanaume tu, siyo kwa macho ya wanawake. Aliyapenda macho ya wanawake na ilipotokea akakutanisha macho na kiumbe yeyote wa kike, katu hakuyabandua macho yake. Ndani ya mboni za mwanamke yeyote kulikuwa na kitu fulani kisichoelezeka, lakini kilichomvutia na kumsisimua.

*****

ALIPOZALIWA wazazi wake walimpa jina la Maftah, jina ambalo baada ya miaka kadhaa lilipotea na kuzaliwa kwa jina jingine, Kiwembe, ambalo alipachikwa kutokana na yale ayapendayo na ayatendayo, yale aliyokwishayageuza sheria badala ya kawaida.
Ni katika kitongoji cha Ujiji mjini Kigoma ambako Kiwembe alizaliwa. Wazazi wake walikuwa na nyumba katika Kata ya Kasingirima, na katika ndoa yao walibahatika kupata mtoto mmoja tu, huyo Kiwembe.
Kiwembe hakubahatika kufaidi vilivyo malezi ya baba na mama. Mwaka 1978 mji wa Kigoma ulitikiswa na maradhi ya kipindupindu, maradhi yaliyowakumba wakazi wengi, na wengi wao wakafariki dunia. Wazazi wa Kiwembe walikuwa miongoni mwa waliofariki kwa maradhi hayo. Walimwacha Kiwembe akiwa na umri wa miaka kumi na miwili.
Mzigo wa kumlea mtoto Kiwembe ulihamia kwa mama yake mdogo ambaye aliishi mtaa wa tatu kutoka kwao Kiwembe. Hayakuwa maisha yaliyostahili kwa mtoto wa rika la Kiwembe. Huyo mama yake mdogo hakujali kuwa Kiwembe kala nini au kama anahudhuria masomo ipasavyo. Hivyo, mara nyingi Kiwembe akawa anazurura mitaani.
Akiwa ni mtoto ambaye alijaaliwa kukua harakaharaka, Kiwembe alikadiriwa na wengi kuwa ana umri wa miaka kumi na minane au ishirini.
Ni umbo lake hilo kubwa ndilo lililomfanya Mama Kadala wa mtaa wa pili amtazame mtoto wa watu kwa macho yenye kila dalili ya njaa dhidi yake. Mama huyo aliyekuwa na umri wa kutosha kuwazaa akina Kiwembe wengine kama watatu, hakuwa mtu wa kujali eti huyu ni kijana aliyekwishabalehe au bado.

Alichopenda yeye ni ‘kupakata dogodogo.’ Na baada ya kumwona mtoto Kiwembe akiwa hana uangalizi mkubwa, akaamua kumwinda taratibu. Jimama hilo tipwatipwa likawa haliishi kujipitishapitisha jirani alikoishi mtoto Kiwembe.
Jimama hilo lilimpenda Kiwembe na likawa tayari kufanya jambo lolote na mtoto huyo potelea mbali hayo matokeo yake yatakavyokuwa. Na hata kama matokeo hayo yatakuwa ya kumfedhehesha, hakujali. Aliapa kuwa ni lazima ‘aanguke naye kisahani.’
Ndipo ikaja siku ambayo Kiwembe alijikuta akiingia kwenye anga za Mama Kadala. Walikutana njiani, saa 12 jioni, Mama Kadala akamwomba Kiwembe msaada wa kumbebea kijifurushi kidogo hadi kwake. Kilikuwa kijifurushi kilichosheheni vitunguu, nyanya na vikorombwezo vingine vya kutayarishia mboga.
Kiwembe hakuwa na hiyana, kwa heshima zote akamsaidia mama huyo mzigo huo mdogo hadi kwake. Ni hicho alichokihitaji mama huyo asiyejua soni au heshima ni kitu gani.
“Karibu Kiwembe,” Mama Kadala alisema huku akimtazama Kiwembe kwa macho yaliyoongezwa utaalamu wa kutazama kimapenzi.
Umri wa Kiwembe haukuwa wa kumfanya aweze kutambua kuwa Mama Kadala ana maana gani kumtazama kwa namna ile. Yeye alitii ile ‘karibu’ kwa kuingia na kijifurushi kile hadi ndani na kukitua sebuleni

Hapo Mama Kadala akavuta kigoda na kumkabidhi Kiwembe kisha naye akavuta kingine na kujibweteka puu!
Wakatazamana.
Ukaaji wa Mama Kadala ukampeleka mbali kimawazo mtoto Kiwembe. Akazidi kumkodolea macho jinsi alivyokuwa ameketi pale kwenye kigoda; kiti kidogo cha jikoni. Alionyesha kushangaza mama huyo jinsi alivyokaa huku tako moja tu likiwa limekijaza kigoda kile, tako jingine likiwa kando, kama vile likining’inia.
Jimama la nguvu!
Jimama tipwatipwa!
Ndiyo, Mama Kadala alikuwa amejaaliwa umbo kubwa na teketeke, umbo jeupe, lililonawiri na kunang’anika. Kwa ukubwa wa umbo lile, alionyesha dhahiri kuwa anakionea tu kigoda kile. Lakini yeye hakujali wala hakukihurumia. Alianza kutayarisha mlo huku wakiwa hapohapo, uso kwa uso na mtoto Kiwembe.
Mama Kadala akazidi kuchuchumia na kukifanya kile kitenge alichojifunga mwilini mwake kianze kuuachia wazi mwili kutokana na hekaheka za mwiko na sufuria. Wala hakujali Mama Kadala, kwamba yule mtoto anamkodolea macho.
Zaidi, alijiachia kwa uwazi, labda akitaka mtoto huyo akishuhudie kile anachosikia au ambacho aliwahi kukisikia. Mama mtu mzima huyo hakujali kuwa macho ya mtoto Kiwembe hayakuwa na pazia. Yeye aliithamini ile methali isemayo “MTOTO USIYEMZAA NI MKUBWA MWENZIO…”
Ni ile nguo pekee, ndogo, laini ya ndani ndiyo iliyomkinga na macho ya Kiwembe, asione vyote. ‘Sukari ndani, sukari nje!’ Lakini macho ya Kiwembe yalikuwa shahidi wa yote, yakaona kisichostahili kuonwa.
Punde Mama Kadala aliuachia mwiko ule, akashika sehemu ya pindo la kitenge alichojifunga, akajipangusa jasho usoni. Kitendo hicho kilimfanya awe mtupu, kama aliyedhamiria kumuumbua mtoto wa mwenzie.
Macho ya Kiwembe yalitazama kwa ukomo wa fahamu zake. Akayatembeza macho hayo taratibu, kutoka kwenye unyayo wa mama yule, unyayo uliokolea hina, akayapeleka hadi kwenye shina la mapaja; alichokiona hapo akakiundia taswira isiyoelezeka wala kueleweka akilini mwake. Akahisi ibilisi akimnyemelea kichwani. Kizunguzungu kikamvaa ghafla.
Fahamu zikamtoka!
Alizinduka muda mrefu baadaye, usiku ukiwa umeshaingia. Akajikuta kalala kwenye kitanda cha Mama Kadala, mwenzi wake katika kitanda hicho akiwa ni yuleyule Mama Kadala, na wote wakiwa tupu kama walivyozaliwa, wamejifunika shuka moja!
“Haa! Mama Kadala! Hapana! Unaniwangia Mama Kadala,” Kiwembe alinong’ona kwa sauti iliyoonyesha woga. Akakurupuka kutoka, hakuweza.
“Tulia…tulia mtoto…tulia mtoto mzuri,” Mama Kadala alimbembeleza huku akimkumbatia na kumpapasapapasa. “Tulia, usihofu… wasiwasi wa nini?”
Kiwembe akaishiwa kauli. Na huo ukawa mwanzo wa kijana mdogo, Kiwembe kulijua penzi. Tangu siku hiyo penzi lao likawa penzi la siri. Siri ikawa siri hadi siku alipojikuta akibalehe kifuani pa Mama Kadala, mwanamke mwenye mwili mkubwa, asiye na haya wala staha.
Wakazidi kupendana. Kiwembe akapikiwa ‘wali wa tako moja na chai ya maandazi ya sukari ndani, sukari nje’ na michuzi ya mapaja wazi. Ujiji ikamfanya mtoto Kiwembe abalehe kabla ya wakati!

Thursday, November 22, 2012

HATIA--- 14

MTUNZI: George Iron.

CONT: 0655 727325


SEHEMU YA KUMI NA NNE

"Hapana sivyo!!! ila huyo John huyo John Mapulu namfahamu hana uwezo wa kuzaa iweje useme mkewe ana ujauzito?" aliuliza kwa sauti ya chini Rashid, macho yakamtoka Minja akabakia na pande la nyama mdomoni bila kutafuna, kauli ile ilikuwa imefungua akili yake kwa kiasi kikubwa.

Akatulia hivyo kwa sekunde kadhaa bila kusema lolote. Kisha akatikisa kichwa kumaanisha kuwa ametambua jambo. Akili yake ilifanya kazi harakaharaka tamaa ya pesa ya kichaga ikamwingia, ikamtuma kumchenga Rashid ili aweze kula peke yake.

"Ah!! wanawake wa mjini hao, hebu achana naye" alisema Minja. Rashid akaafiki, baada ya nusu saa wakaagana. Safari hii kila mmoja aliondoka kivyake.

ENDELEA>>>>>>



****

Matha baada ya kumhadaa Minja na kumsimamisha kazi aliamua kutokuwa mbinafsi na kumshirikisha suala hilo Michael ambaye mara nyingi alikuwa msikilizaji. Lakini katika maongezi ya siku hiyo hakuwa ameridhia maamuzi hayo yaliyotaka kufanywa na Matha, yaani kumtafutia kazi nyingine Minja ili kumuweka mbali na John.
"Na vipi siku akikutana na John, au akimpigia simu???" aliuliza Michael, Matha akakiri kuwa hali bado ni tete.
"Minja sio mropokaji ni muelewa sana" alijaribu kutetea Matha, Michael akakubali kwa shingo upande.
"Akithubutu kunichezea nitamuua!!!" alijisemea kwa sauti ya chini lakini Michael aliweza kumsikia.
"Kuliko kuua ni heri tutoroke Matha!!" alishauri Michael, Matha akamkazia macho, Michael akawahi kukwepesha macho yake. Matha akaaga na kuondoka, John na Bruno hawakuwa nyumbani.
Huo ni uoga wa kunguru!!! Akawaza Matha juu ya kauli ya Michael kuhusu kutoroka.

****

Ukaidi wa Minja mbele ya John ilikuwa dharau kubwa sana, John alijua lazima kuna kitu, hisia za kwamba Minja anaweza kuwa 'informer' na huenda ameishtukia dili yao ya kwenda kuiba Supermarket. John akawaeleza wasiwasi huo wenzake, hisia za John zikawashtua wenzake, mara moja msako Minja ukaanza. Sehemu ya kwanza kabisa ilikuwa kazini kwa Minja yaani sheli ambapo hakuwepo. Msako haukuishia hapo lilikuwa jeshi la watu wanne wenye mioyo ya kuua.
Minja alikuwa katika hatia asiyoitambua.
John alikuwa amekerwa sana na dharau aliyofanyiwa. Msako huu kwa upande wa John ulikuwa kwa faida ya Matha, alitaka kujua kuwa ni kwa jinsi gani Minja amemfahamu Matha tena kwa majina yote mawili kiufasaha.
"Au Matha ana uhusiano naye jamaa ananifanyia jeuri!!!" alihisi John, wivu ukachukua nafasi yake ukaanza kuikwaruza nafsi ya John, hasira ikajikaribisha katika kiti kilichokuwa wazi katika moyo wake.
"Nitamuua kwa mkono wangu!!!" aliapiza baada ya kumkosa pale sheli kwa mara ya tatu.
Wenzake na John walichukulia kuwa hizo ni hasira za kawaida ambazo John alikuwanazo lakini haikuwa hivyo ni wivu wa mapenzi ulikuwa unamshambulia tena shambulio la nguvu na la ghafla.
Msako ukatoka pale sheli na kuhamia nyumbani kwake, ramani ilikuwa tayari mkononi mwa kundi hili.
Wakashauriana waende usiku!!!!

*****

Kitanda kilikuwa hakilaliki, si kwa sababu ya godoro lililokuwa limechakaa sana bali kutokana na mgogoro wa nafsi, mke wa Rashid aliigundua hali hiyo kwa mumewe ambaye siku hiyo alipendezesha chumba kwa harufu ya bia tofauti na siku nyingine ambazo hunuka pombe za kienyeji.
"Baba Karim!!!....vipi mbona hulali"
"Sina tu usingizi mke wangu" alijibu kwa sauti ya kukwaruza.
Rashid alikuwa katika dimbwi kubwa la mawazo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Minja. Umasikini ulikuwa unamtia katika fedheha kubwa, alidharauliwa na wala hakupendwa na mtu yeyote maana hakuwa na msaada wowote kwao. Wazo la utajiri kupitia kuusema ukweli unaomuhusu mke wa John lilimwingia lakini kisu kilikuwa kimeshikiliwa na Minja. Tamaa ikamwingia Rashid akatamani akishike yeye kisu hicho.
"Nitamweleza Minja na kama akikataa je?" alijiuliza.
"Akikataa nitaenda mwenyewe kwa John Mapulu" alijipatia jibu.
Mgogoro mkubwa wa nafsi ukautwaa usingizi wake, maumivu ya kichwa yakayeyusha usingizi wake. Rashid akaamua kuamka na kukaa kitandani, wakati huo mke wake alikuwa amelala tayari.
Nimeuchoka umasikini!!! alisema kwa nguvu kisha akajaribu tena kuutafuta usingizi.
Safari hii usingizi ulimchukua.
Siku iliyofuata akaamua iwe siku ya vitendo hakutaka kuchelewa zaidi. Kwa kuwa alipajua nyumbani kwa Minja aliamua kwenda usiku baada ya kuwa ametoka lindoni majira ya saa kumi na mbili jioni.
Siku nzima lindoni Rashid alikuwa anatazama vitu vya thamani huku akiamini kuwa iwapo Minja atakubaliana naye basi baada ya muda mfupi atakuwa na uwezo wa kuvinunua.
Ujio wa Minja nyumbani kwake siku moja iliyopita ulimzidishia tamaa zaidi ya kuipata pesa, miaka yake 40 aliyokuwanayo bado ilimruhusu kuwa na tamaa za kimwili, Rashid aliwatamani wanawake waliokuwa wakipishana katika maduka mbalimbali kununua vitu vya gharama.
"Nikizipata hawa watakuwa wananiheshimu na pia watakuwa wakinisalimia, hebu tazama wanavyonipita kama hawanioni vile!!!" Aliwaza Rashid, donge la hasira likamkaa kooni akajilazimisha kumeza mate lakini hayakupita. Akasonya!!
Alitamani jioni iweze kufika aijaribu bahati yake ya kupata pesa.
Jioni ilifika akaaga na kurejea nyumbani, hapo pia hakukaa sana alimuaga mkewe kuwa anatoka kisha akatoweka!! Hakusema anakwenda wapi.



*****


Chumba cha Minja kilikuwa kimya sana wakati anaingia, alijaribu kuita lakini hakupewa jibu lolote, lile giza lilimlazimu kutumia simu yake ya tochi kuweza kuona vyema ndani.
Chumba kilikuwa na harufu nzuri za manukato jambo ambalo halikuwa kawaida hata kidogo.
Jeuri ya pesa!!! aliwaza Rashid huku akichukua nafasi na kukaa.
Baada ya dakika kadhaa pakiwa na giza hivyo hivyo alisikia vishindo vya watu vikiingia ndani. Miale mikali ya tochi ilitua katika macho yake, alitumia viganja vyake kujikinga.
Maumivu makali katika paji la uso wake aliyasikilizia huku mwili wake ukiwa ardhini.
"Kwa nini leo hujaingia kazini??, kwa nini umeacha kazi tangu tufike siku zile??" Alisikia maswali yakimuelekea.
"Ni juzi tu ndio sijaenda jamani!!! sijaacha kazi, hata leo mchana nilikuwepo" alijitetea.
John alipatwa na ghadhabu akiwa nje ya chumba kile akiangalia hali ya usalama.huku akipuliza sigara yake.
"Fala huyo anawadanganya!!!" alikoroma kwa sauti ya hasira tena yenye kisilani, wivu juu ya mpenzi wake ulimtwaa kwa kiasi kikubwa. Aliamini kuwa yule ndani ya chumba kile alikuwa ni Minja.
Waliokuwa wameingia ndani waliposikia kauli inayoitwa kudanganywa moja kwa moja wakajua kuwa aliyekuwa mbele yao ni adui.
Dakika tano pekee zilitosha kumbadilisha Rashid na kuwa tayari kwa kuhamia kaburini. Ilikuwa ni kabali baabkubwa iliyomzidi nguvu mlinzi huyu ambaye hata chakula cha usiku alikuwa hajapata.
Timu nzima ya John ikajua kuwa imemuangamiza Minja.
Tamaa zikawa zimemponza Rashid, utajiri alioutaka ukawa umeingia shubiri. Mchezo asioujua mwanzo wake ukawa umetwaa uhai wake.
Rashid akatokomea na tamaa yake!!

******


Minja akiwa na jeuri ya pesa ambayo sasa ilikuwa imebaki kama shilingi elfu sitini. Aliichukia sana hali ya chumba chake kutokuwa na umeme, siku hiyo hakutaka kuuvuta moshi mkali wa kibatari, giza lilivyoanza kuwa totoro akaamua kutoka, kwa kuwa hakuwa na chochote cha thamani kinachoweza kuwavutia wezi aliurudishia mlango wa chumba chake na kutoweka, alikuwa amevalia nguo mpya alizokuwa amenunua siku hiyo, aliamini kuwa alikuwa amependeza sana. Pesa zile kidogo zilikuwa zinamuwasha, taratibu huku akiepuka kuchafua kiatu chake kilichokuwa kimeng'arishwa haswa alizipiga hatua hadi akafika katika 'bar' maarufu pande za Mabatini iliyokwenda kwa jina la 'Corner bar', akachagua meza ambayo ilikuwa tupu ikiwa imepambwa na viti vinne visivyokuwa na watu.
"We mwanamke!!!" alikoroma Minja, muhudumu akajikimbiza mara moja akasimama mbele ya Minja.
"Kasto laga (Castle lagger)" alibwatuka.
Muhudumu akachukua pesa na kuondoka kisha akarejea na kinywaji, Minja alianza kunywa taratibu kama mwanaume asiyekuwa na hofu ya pesa kumuishia. Baada ya pombe kumkaa sawa kichwani alipata ujasiri wa kwenda kumhadaa muhudumu ambaye alikuwa anashangaa shangaa huku na kule kutazama kama kuna mteja atamuita kwa ajili ya kutoa huduma.
"Njoo saa nne!!" yule muhudumu alimpa ahadi hiyo Minja. Minja hakutaka kurejea katika kijumba chake alichokuwa anakichukia kwa siku hiyo kutokana na giza lililokuwepo. Alichofanya ni kuhamia 'bar' nyingine huku akienda sawa na muda.
Saa nne kamili alikuwa amerejea 'Corner bar', muhudumu alikuwa tayari amevua sare zake. Akatokomea na Minja kama mpenzi wake wa siku nyingi sana.
Safari yao ikaishia nyumba ya kulala wageni.
"Mi silali lakini mwisho saa saba"
"Usijali" alijibu Minja huku akizivua nguo zake haraka haraka.
"Kwanza nipe pesa yangu kabisa!!"
"Shilingi ngapi??"
"Elfu tano"
Minja akatoa elfu kumi akampatia.
"Sihitaji chenji baki nayo" alisema kwa ujivuni Minja baada ya yule binti kuulizia kama Minja anayo 5000 iliyoshikana.
Binti akatabasamu na yeye akaanza kuzipunguza nguo zake mwilini. Tayari kwa kutoa huduma.
Hakuna aliyekumbuka suala la kutumia kinga, na hakuna aliyejutia baada ya tendo.
Saa sita usiku Minja alikuwa anarejea nyumbani kwake, alijihisi mwepesi na aliyechangamka sana baada ya tendo hilo alilokuwa amelikosa kwa siku nyingi sana.

Alipokikaribia kibanda chake furaha yake ilianza kupungua kwa kasi, alilitambua joto lililokuwa linamnyanyasa katika kijumba chake ambacho hakikuwa na 'sealingboard'. Alitamani kurejea katika nyumba ya kulala wageni ila akakumbuka kuwa alilipia kwa masaa kadhaa tu na wala si kulala hadi asubuhi.
Akapiga kite cha hasira kisha akaingia katika kijumba chake cha kupanga kama amelazimishwa hivi. Giza lilimpokea, lakini kwa kutumia uzoefu wa eneo hilo alipapasa hadi akakifikia kitanda chake akajibwaga bila kushusha neti. Usingizi haukumpitia kwa wepesi alipanga mipango kabambe ya siku inayofuata.
"Hivi nianzie na John ama nile pesa za Matha!!!" Alijiuliza huku akijipiga bega lake kupambana na mbu waliokuwa wanamzengea. Minja alikuwa katika wakati mgumu wa kufanya maamuzi, kauli aliyokuwa amepewa na rafiki yake Rashid juu ya tatizo la John la kutozaa na kijitambulisho cha ujauzito wa Matha vitu hivi vilimtia kizunguzungu, akajiuliza ni nini cha kufanya. Hakika alikuwa masikini na hii kwake aliiona kama bahati ya walau kuukwaa huu ugonjwa unaotawala Tanzania, ugonjwa wa umasikini, ugonjwa uliokosa tiba ya kudumu.

Tamaa za kuwa na mahusiano na Matha zilimtawala, roho mpenda sifa alimkaa mwilini akashindwa kubanduka.
"Matha atake asitake atakuwa mpenzi wangu wa siri....na kama akikataa namueleza John ukweli" Alijisemea Minja huku akizikumbuka raha alizozipata na yule muhudumu wa 'bar' katika nyumba ya kulala wageni. Aliamini kuwa sasa atakuwa akizipata raha hizo bila kulipia bali kulipwa.
Hali ya hewa ilibadilika taratibu, ulianza kuvuma upepo ambao ulipunguza joto kidogo pale ndani, kisha ikafuata miungurumo. Bila shaka ilikuwa dalili ya mvua.
Minja alikereka kutokana na hali hiyo kwani dari la chumba chake lilikuwa linavuja. Kwa mara nyingine alipiga tena kite cha hasira.
Miale ya radi za hapa na pale ilileta mwanga pale ndani, Minja akaona kitu ambacho hakukitilia maanani sana kwani aliamini yalikuwa mawazo tu.
Alikuwa ameiona sura ya Rashid mbele yake.
Rashi cha ulevi!! Huyu jamaa anakunywa pombe huyu!! Alisema kwa sauti ya juu kidogo kisha akacheka.
Akapuuzia akiamini ni mawazo tu, akaendelea kuwaza na kuwazua, mwanga wa radi ulipopiga tena, Minja akaamini hapakuwa na mawazo ya namna hiyo, kulikuwa na kitu chini ya kimeza chake.
Mara moja akaiwasha simu yake akapapasa kidogo akapata kiberiti akakiwasha kimshumaa kilichokuwa kinakaribia kuisha. Kama vile amesukumwa kwa mitambo maalum alijikuta anajibamiza kitandani akasimama tuli akiwa ameyakodoa macho yake.
Alikuwa ni Rashid akiwa amekodoa macho na kutoa ulimi nje!!! Hakuwa Rashid tena alikuwa hayati Rashid.
Minja alitamani kumeza mate kulainisha koo ili aweze kupiga kelele lakini kinywa kilikuwa kimekauka sana ikashindikana. Upepo ukavuma tena. Mshumaa ukazimika!!! Hofu ikaongezeka, haikuwa ndoto tena Minja alikuwa chumba kimoja na maiti. Alitamani kukimbia lakini akajivika ujasiri alikuwa anatetemeka akapapasa tena akakipata kiberiti akawasha tena mshumaa, ukawaka. Akapiga hatua, akafika mahali ulipokuwa mwili wa Rashid.
"Minja! Minja! usimguse!!! utaacha ushahidi" Sauti ya ndani (Conciousness) ikamwambia Minja, akashtuka akasimama wima akaanza kurudi nyuma, joto katika suruali yake mpya lilitoa jawabu la mkojo uliopita bila idhini maalumu kutoka kwa muhusika.
Upepo ulivuma tena, mshumaa ukazima Minja hakuuwasha tena.
Wazo la kukimbia likavamia ubongo wake, wazo hilo likaambatana na milango ya jela. Minja akatetereka kidogo aanguke akahimili kuendelea kusimama. Harufu ya kwenda jela ikamtuma kukimbia, hakuna kitu alichokiogopa kama polisi bila kuchukua chochote zaidi ya pesa alizokuwa amezihifadhi chini ya godoro lake Minja alitoka usiku uleule bila kumwambia yeyote.

SITAISAHAU facebook------- 8

MTUNZI: Emmy John P.

CONTACTS: 0654 960040


SEHEMU YA NANE


ILIPOISHIA


Akapoteza uelekeo kuniona naruka vile nikataka kukimbia nje.

Akanidaka kanga yangu. Kanga ikateleza ikauacha mwili.

Shanga nane za rangi tofauti zilizokishika vyema kiuno changu ndio pekee zilizosalia katika mwili wangu. Sasa John alikuwa amebaki na kanga mkononi mimi nikiwa nina shanga kiunoni. Nusu nilikuwa nje na nusu nilikuwa ndani.

Swali likavamia kichwa changu.

Nikimbie na shanga kiunoni kwenda nje ama nirudi chumbani kwa John huyu wa maajabu!!! John niliyemuhisi kuwa sasa ni ………….

Nikabaki katika kizungumkuti.


JE ISABELA ATAKIMBIA NA SHANGA KWENDA NJE AMA ATARUDI KWA JOHN???

NINI KINATOKEA HAPA!!!!!!!


ENDELEA

Nikiwa katika kujiuliza iwapo nirejee ndani ama nikimbie hivyo hivyo uchi na shanga kiunoni, mara John akaanza kunisogelea huku akiniomba mkono wangu.
Anauita akuue!!! Sauti iliniambia.
Hapohapo nikaamua kutimua mbio uchi. Ilikuwa ni kama bahati kwenye kamba ya kuanikia nguo nikakutana na kanga nikaikwapua nikawa nakimbia huku naifunga.
Ikawa kama ni muendelezo wa igizo. Wakati nadhani nipo peke yangu katika kukimbia mara nikashangaa tukiwa watatu. Wote wasichana. Mimi nilikuwa kimya. Wenzangu walikuwa wakipiga kelele za kuomba msaada. Msaada wa nini? Nilijiuliza.
John anatafuna watu!! Niliwaza. Nikaongeza mwendo zaidi. Sikuwa tayari kutafunwa. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa mwalimu Nchimbi. Anavyonitegemea!!! Atabaki na nani? Nikazidi kukaza mwendo. Kanga ikiwa imenikaa vizuri katika staili ya kupitia shingoni.
Mara mmoja akaanguka huku akipiga kelele. Ni hapo ndipo niligeuka, kutazama kulikoni. Niliamini kabisa kuwa ni John anatafuna mtu pale lakini ghafla nikashuhudia mbwa mkubwa akimgalagaza msichana mwingine. Nikatoa ukelele wa hofu kuu.
He!! John kageuka mbwa!!! Nimekwisha mimi. Ewe mwenyezi Mungu nisaidie. Sasa nilikumbuka kusali. Dalili za kupoteza matumaini.
Msikimbie nyie!!! Sauti kutoka nyuma ilitukanya. Haikuwa sauti ya John lakini ilikuwa sauti ya kiume.
“Spider acha!! Spider shenzi acha!!! Acha!!!.” Sauti ile ilikuwa inakanya kwa ghadhabu. Waliposimama na mimi nikasimama. Lakini nikiwa nimejiweka tayari tayari kukimbia iwapo itabidi.
Yule mbwa aliheshimu amri ile akaacha kumshambulia yule binti pale chini. Akaondoka kuifuata sauti ilipotokea. Baada ya yule mbwa kuondoka alitokeza yule kijana aliyekuwa anaamrisha. Alitutaka radhi wote kwa pamoja.
Mh!! Mimi sihusiki na hili lakini!! Nilijikanya.
Kumbe huyu mbwa sio John!!!
Au au au!! Ile ndoto imeniathiri akili!!!
Nilitaka kurudi chumbani ili niweze kuzungumza na John lakini wasiwasi ukanitawala zaidi.
Sikurudi, siku hiyo nililala kwa rafiki yangu.
Mbwa!! Hiyo ndio ikawa pointi ya kujitetea, hakuna aliyejua ni kipi kimenikimbiza kiasi kile.
Nikaoga, kisha nikalala na kuamka salama.

“HOFU YATAWALA CHUONI SAUT” Alizungumza kwa sauti kuu mtangazaji. Akaanza kuielezea habari hiyo. Mimi nilikuwa nimelala bado. Lakini sikio lilikuwa wazi.
“Kijana mwingine amekutwa amekufa kwa kugeuzwa shingo yake, amekutwa na kisu kikiwa na damu lakini hakuwa na kovu lolote mwilini mwake. Huenda alikuwa katika kupambana na muuaji kabla ya mauti kumkuta.”
Sijui hata ni muda gani niligeuka, na kukaa kitako. Habari ilikuwa imenishtua. Nilidhani kuwa ni ndoto tena imejirudia lakini haikuwa ndoto hii ilikuwa ni habari inaendelea.
Salma alikuwa ameshika tama akisikitika, hakupata nafasi ya kuniona jinsi nilivyokuwa katika mshtuko mkuu. Nilijilazimisha kulala tena lakini haikusaidia, taarifa hiyo ikanirudisha katika kumfikiria John.
Hapana John hawezi kuwa muuaji!!! Nilipingana na maono yangu ya usiku. Nikapuuzia.

*****

Jina langu lilikuwa limeanza kukua pale chuoni kutokana na elimu ya mahusiano niliyokuwa naitoa. Mwanzoni watu hawakujua ninamaanisha nini lakini mwishowe wakaanza kunielewa. Wasichana waliotendwa katika mapenzi walikuwa wanakuja kupata ushauri kwangu. Waliokuwa wakigombana na wapenzi wao nilihusika katika kusuluhisha. Isabela nikawa Isabela kweli.
Nilianzisha vikundi kadhaa vya kupinga unyanyasaji wa wanawake hasahasa katika suala la mapenzi. Kwa kuwa mapenzi yalikuwa yameteka asilimia kubwa ya mawazo ya watu basi nilieleweka kirahisi. Nikawapata wafuasi wa kutosha. Nikaipenda kazi yangu!!
Kwa kutumia pesa alizokuwa akituma Davis na kampuni yake niliweza kuandaa semina kadhaa huku nikialika wataalamu wa saikolojia. Masomo waliyotoa yaliwagusa wengi.
Sasa kila mtu aliweza kunifahamu walau kwa jina kama hajapata nafasi ya kujua sura yangu.
Kampuni iliyoniajiri ya SAVE THEM ilipotuma wajumbe wake kutoka marekani kufika chuoni kwetu kwa ajili ya tamasha kubwa kabisa lililohusisha mambo kadha wa kadha huku nikipandishwa cheo na kuwa muwakilishi wao katika vyuo vikuu vyote nchini ni hapo ndipo jina langu lilikuwa zaidi.
Vile vifo vya wanafunzi sita katika siku sita mfululizo vilikumbukwa kwa kusimama kimya dakika moja kabla ya ufunguzi wa tamasha lile.
Vifo vikasahaulika na mambo mengine yakaendelea.
Ile ndoto niliyoota kisha nikamfuma John na damu mgongoni niliamini kuwa yalikuwa ni mauzauza tu haukuwepo ukweli wowote.
John alikuwa amerejea kuwa mpenzi wangu rasmi na penzi lilikuwa moto sana. Jesca akasahaulika!!!
Isabella mimi sikushangaa sana sasa nilipoteuliwa katika baraza la mawaziri wa serikali ya wanafunzi. Nilikuwa naheshimika.
Malipo makubwa niliyokuwa napata yalibadilisha maisha ya nyumbani. Yote haya yalikuwa ndani ya miezi miwili.
Kila mara nilikuwa nikifikiria kuhusu hapa nilipo naishukuru facebook, kwani ni hii ilinikutanisha na dokta Davis na sasa nilikuwa mtu kati ya watu.

******

MAUZAUZA MENGINE UPYA

Ilikuwa siku ya sita ya juma yaani kuanzia jumatatu sasa ilikuwa jumamosi. Siku hii kimvua cha rasharash kilinikumbusha kulitafuta sweta langu ambalo lilikuwa chini kabisa ya kabati langu la nguo.
Licha ya kuwa na nguo nyingi nilikuwa na sweta moja. Mafua yalikuwa kidogo yananisumbua, uchovu wa siku iliyopita pia ulikuwa unanisumbua. Siku iliyopita ilikuwa siku ndefu sana, ilikuwa ijumaa ya kukumbukwa, kampuni ninayofanyia kazi ilikuwa imenihamishia katika nyumba kubwa kabisa ya vyumba vinne, sebule na mahala pa kulia chakula. Ilikuwa na geti na ua kubwa tu. Baada ya kujaza vitu ndani, nilialika watu kwa ajili ya uzinduzi rasmi. Nilialika marafiki wapatao sitini, akiwemo raisi wa chuo, watangazaji wa redio SAUT, marafiki wenye hadhi ya kuwa marafiki zangu, waalimu wenye heshima zao pale chuoni akiwemo ‘Dean of students’ aliyeitwa Mama Nasania, John naye alialika marafiki zake. Hapakuwa na michango wala kadi za michango. Na katika shrehe hiyo hapakuwa na kipengele cha kutoa zawadi.

Monday, November 19, 2012

SABABU ZINAZOSABABISHA WASICHANA KUINGIA KWENYE MAPENZI NA MTU ASIYEMPENDA

mara nyingi watu huwa wanajiuliza ni kwanini wasichana wengi ni rahisi kuingia kwenye mahusiano bila hata ya wao binafsi kupenda kuingia katika mahusiano hayo.

kwa uchunguzi wangu binafsi nimegundua sababu kuu nne ambazo wasichana hujikuta kwenye mahusiano ya mapenzi hata kama hawakupenda kuwa na huyo mtu aliyeko naye. katika sababu hizi haziaendani na sababu za kijamii, kiuchumi wala utamaduni wa eneo fulani bali ni sababu ambazo mara nyingi huwakuta wasichana wa rika na uwezo tofauti bila kujali kama ni masikini ama tajiri. Kwanza kabisa tuone sababu za msichana kutotaka kuwa kwenye mapenzi na mtu asiye mpenda.

1. UJASIRI

Msichana anaweza kuwa jasiri kuingia kwenye mahusiano ama kutoingia kwenye mahusiano. mara nyingi wasichana wanavaa ujasiri pale wanapokuwa wapo mbali na mvulana na kujiaminisha yakuwa akifika kwa mvulana na atamwambia kuwa sikutaki. Na mara nyingi kwa mtu ambaye hampendi na hatamani kuwa naye hata kidogo. hivyo anauvaa ujasiri wa kuongea kwa mvulana. kitendo cha msichana kuvaa ujasiri akiwa kwake I mean kabla ya kuonana na mvulana humpa sababu ya pili ambayo ni

2. KUJIAMINI

Msichana akiwa jasiri anaweza kujiamini ya kuwa akifika atamwambia ukweli na hivyo akiwa anaenda kukutana na huyo mvulana basi njia nzima anakuwa anajiamini kuwa akiwa jasri na kumweleza kuwa hampendi na hamtaki basi yule mvulana lazima atamwelewa. na sababu hiyo hata akiitwa kuwa aonane naye anakuwa anajiamini kuwa hiyo vita ataishinda.

Lakini tofauti na mategemeo, msichana hujikuta anaondokewa na ujasiri na kujikuta yupo mikononi mwa mtu ambaye alidhani hapo mwanzo hatakuwa naye na hii ni kwa sababu zifuatazo:

1. woga/fear

Msichana anakuwa anaingiwa na dalili za kuogopa kusema kile alichokipanga kukisema kwa mvulana na mara nyingi anapokutana naye uso kwa uso, tofauti na hata angemtumia sms ama kumpigia simu. anapatwa na wasiwasi mkubwa wa wapi aanzie kumweleza ya kuwa hampendi na hataki kuwa naye. na hali mara nyingi hutokea pale mvulana anapomnyima nafasi ya kujieleza msichana na kwa hiyo sababu huzaa zababu kubwa ambayo mara nyingi imekuwa tatizo kwa watoto wa kike. sababu hiyo ni

2. HURUMA


Msichana anapopatwa na woga anajikuta katika hali kumhurimia yule mvulana au mwanume ambaye amejieleza kwake kwa kiasi gani anaumia kadri ambavyo yeye msichana anavyoendelea kumkatalia ombi lake. na hii mara nyingi hutokea pale mwanaume/mvulana anapotumia maneno yakuuchoma moyo wa masichana. na point ya kuumia moyoni na kujiona ni mkosaji, msichana hujikuta akiwa katika majaribu makubwa, ujasiri na kujiamini unaondoka na woga na huruma huchukua nafasi na kujikuta yupo kwenye mikono ambayo mwanzoni alifikiri si salama na hawezi kuwa na mtu kama yule ila sasa tayri kazama.

MWISHO

kama kweli msichana huhitaji kuwa na mvulana fulani basi SIMAMIA HILO na usiruhusu woga wala huruma kuingia katikati.

Friday, November 16, 2012

SITAISAHAU facebook 7


MTUNZI: Emmy John P.

CONTACTS: 0654 960040

SEHEMU YA SABA

ILIPOISHIA

Au nataka kuwa mtakatifu??? Nilijiuliza. Huku nikiamini moja wapo ya dalili za kuwa mtakatifu ni kuyajua yanayokuja kupitia ndoto.

Mh!! Utakatifu gani huu lakini hata kanisani penyewe siendi?? Nilitengua mawazo yangu.

“Dada nakuita jamani!!.” Sauti ya yule muhudumu ilinishtua. Inavyoonekana alikuwa ameniita mara nyingi sana.

Nilikuwa sipo kawaida na niliombea sana wasiitambue hali hii.

Simu yangu ikaita nikaitoa kuitazama alikuwa ni Dokta Davis.

Nikapokea na kuiweka sikioni.

“Samahani nipo saluni.” Nilimsihi.

“Usijali nilikuwa nakutaarifu ukatazame salio katika akaunti yako.”

“Hamna shida.” Nilimjibu na kukata simu.

***ISABELLA katika mtihani mwingine…..Ndoto ya ajabu inayogeuka kuwa kweli.

Je kuna nini hapa??




ENDELEA


Nilipotoka pale saluni nilitaka niende kwanza nyumbani kwangu lakini nikaona kwanza nipitie benki kutazama salio.

“Laki sita elfu sitini na sita na mia sita sitini na sita.” Hichi ndio kiasi kilichokuwa kimeongezeka katika akaunti yangu. Sikushtuka sana safari hii, nilikuwa nimeanza kuizoea pesa hii kubwakubwa.

Sikuwa na haja yoyote ya kutoa pesa kwani bado nilikuwa na pesa nyingi ndani. Niliingia katika bajaji iliyokuwa imenileta nikamuamuru anipeleke Kijiweni, huku ndipo nilikuwa naishi.

Tulipoifikia kona ya kijiweni nilitelemka na kuliendea duka la madawa nikachukua dawa za kutuliza maumivu.

Nilipofika chumbani nikanywa na kujipumzisha kidogo kwa minajiri ya kuoga baada ya dakika kadhaa. Nilikuwa bado nawaza kuhusu kifo cha Basu kwa kung’atwa, lilikuwa jambo la kushangaza sana. Na kilikuwa kifo cha kustaajabisha, kivipi afe kama ndoto yangu ya usiku? Nilijiuliza sana. Sikupata jibu. Nikajitia imani kuwa hizo ni ndoto.


Suala la kwamba ninaandaliwa kuwa mtakatifu lilinisaidia kupungaza hofu.

Lakini utakatifu gani sasa huu wa kuupata bila kwenda kanisani??

Kwani watakatifu wote walikuwa wanaenda kanisani!! Nilijiuliza. Kisha nikaukatisha mgogoro huu wa nafsi kwa kumpigia simu John, nilizungumza naye kidogo akaniambia yupo njiani kuelekea Nyegezi kona kutazama maiti ya Basu.

Aliposema jina hilo nikashtuka lakini hakugundua kwa sababu hakuonyesha wasiwasi na wala hakuuliza swali.

“Basu…Basu amekufa?” Nilijifanya sijui lolote. John akanieleza stori ileile kama mama mnene wa kule saluni aliyosema.

Nikaingia katika fumbo, sikumjua mfumbuzi!!!

Nikapitiwa na usingizi!!!

****


Nilikuwa nautazama sasa umati wa watu ambao sikuelewa ni shughuli gani walikuwa wakiifanya. Sikuwatilia maanani sana na wala sikujua eneo lile ni wapi. Mara nikamuona mtu ambaye ninamfahamu. Nilitamani kumuita lakini niliamini kwa zile hekaheka alizokuwa nazo wala asingeweza kunisikia. Nikapuuzia!!

Sikujua nilikuwa nimejikita katika shughuli gani lakini kuna jambo nilikuwa nafanya.

Mara nikamwona tena yule mtu ambaye nilionekana kumfahamu, sasa alikuwa katika mtafaruku. Wenzake wote walikuwa wakimpigia kelele katika namna ya kupingana. Alikuwa peke yake na hakuna aliyemuunga mkono. Mara wenzake wakaanza kumzonga sasa hayakuwa mabishano tena bali ugomvi. Mtu mmoja anachangiwa na watu zaidi ya kumi. Ugomvi ukawa ugomvi. Kuna jambo walikuwa wanalazimisha. Jambo hilo huyo mmoja hakuunga mkono kabisa.


Baada ya kuzidiwa mara yule mtu akawaponyoka. Akaanza kukimbia. Alikuwa anakimbia huku akiangalia nyumba. Nilikuwa natabasamu nikimtazama maana alionekana kuwa na hofu kuu.

Alipogeuka mara ya kwanza lilikuwa kunndi la watu watano wakimfukuza, akazidi kukimbia, alipogeuka tena walikuwa watatu, akajitahidi kujitetea kwa kuendelea kukimbia, wakabaki wawili. Safari hii hakugeuka.

Alipokuja kugeuka sasa alikuwa amekaribia kukamatwa. Lakini cha kutia moyo alikuwa anakabiliwa na mtu mmoja tu. Japo alikuwa amechoka lakini hata huyu aliyekuwa anakabiliana naye alikuwa anahema juu juu. Walikuwa wanatazama kama majogoo yanayofanyiana ubabe.

Mara jogoo lililokuwa linamkimbiza jogoo mwenzake likamrukia yule mkimbizwa. Wakaanguka chini, ugomvi ukazuka.

Wakagalagana hapo chini kwa namna ya kuchekesha. Nami nikawa nacheka.


Mara yule mtu niliyekuwa namfahamu akaangusha vibaya. Halafu yule aliyemuangusha akachomoa kisu kidogo, upesi akamchana nacho mgongoni. Akatoa ukulele wa uchungu na hofu.

Kuchanwa huko kukawa kumemrejesha upya katika ugomvi. Sasa alikuwa na nguvu kamilifu. Yule aliyekuwa na kisu alipojaribu kumchana tena akawa amechelewa mkono wake ukadakwa, kisha kikafanyika kitendo cha sekunde kadhaa tu cha kuikamata shingo ya mwenye kisu na…na….na…


“Mamaaaaa!!!” Nikakurupuka usingizi!!

Nilikuwa nimelala masaa sita. Niliyapikicha macho yangu huku na huko niweze kuangalia vyema mbele.

Ukungu ulikuwa umetanda. Nikajipikicha zaidi nikaweza kuona, na sasa niliweza kusikia. Mlango ulikuwa unagongwa kwa nguvu. Fahamu zikanirejea vizuri, nikauendea bila hata kuulizia nikafungua. Alikuwa ni jirani yangu.

“Kakasirika kweli John dah!! Amegonga mlango, kapiga simu yako hupokei.” Alinieleza huku na yeye akionekana kukasirika.

Nilipiga mwayo mrefu kisha nikamuuliza kuwa alikuja saa ngapi. Akanijibu. Kisha akajieleza shida aliyokuwa nayo nikamsaidia . akaondoka!!!


*****


Sikuweza kuhudhuria msiba uliomuhusu Basu, akili yangu ilikuwa imechoka sana. Baada ya harakati za hapa na pale nilijipikia chakula kisha nilipomaliza nikalala tena.

Mara hii mlango ulipogongwa nilisikia vyema kabisa. Nikasimama na kwenda kumfungulia. Alikuwa John na ilikuwa saa tatu usiku.

John alikuwa amefanya mfano wa hasira usoni, nililitambua hilo na sikuwa na haja ya kumuuliza kwa nini amekasirika.

Baada ya kuzungumza naye dakika kama kumi hivi huku nikijiweka karibu naye. Alilainika na uso wake ukaunda tabasamu.

Tulizungumza mengi na mpenzi wangu huyu wa zamani. Na kama vile tulikuwa tumeambiana kwa pamoja tukageukiana tukakumbatiana kwa nguvu. John alikuwa analia.

Nilijua kuwa anamlilia Jesca, sikutaka kumuuliza najua angelia zaidi. Nilichofanya ni kuzidi kumkumbatia, viatu vikabaki sakafuni, sasa tukawa kitandani. Lugha iliyozungumza ilikuwa lugha ya mapenzi.

John alikuwa mtulivu kama aliyesafiri kwenda ulimwengu wa mbali. Nikaitoa shati yake akawa amebakiwa na singlendi. Nikataka kuitoa na ile.

“Ngoja nikaoge kwanza baby…” aliniambia kwa sauti nzito yenye kutamanisha.

Nikatulia nikamtazama naye akanitazama.

“Twende wote pliiz.” Nilimsihi. Hakujibu chochote nikajua kuwa maana yake ni kwamba twende.


Nikaziondoa nguo zangu, nikajivika upande wa kanga.


“He!! Sa na hiyo singlendi waipeleka bafuni kufanyaje tena!!!” Nilimuuliza John baada ya kumuona akiingia na ile singlendi bafuni.

“Si haujataka kunivua sa mi ntafanyaje?.” Aliniuliza kitoto. Nikatabasamu, nikamwendea, akakimbilia upande mwingine wa chumba nikamfata tukawa kama tunagombana. Japo hatukutumia nguvu sana!!!

“ukiweza kunivua nakubeba mgongoni!!” Alinipa motisha nikazidisha juhudi. Nikaitoa nikawa mshindi.

Mshindi kubebwa mgongoni!! Ikumbukwe hiyo.

Mimi ndiye mshindi, mgongo mali yangu.

John akachuchumaa nikawa nyuma yake.

Ile nataka kupanda mgongoni nikaona kitu cha ajabu.

Kovu!!! Kovu bichi!!! Kovu katika mgongo. Kovu la kuchanwa na kisu

“Mamaaaaa!!” nikapiga kelele. John akasimama. Tayari nilikuwa katika kona ya chumba nikiwa natetemeka sana!!!

“Sabe sabe!! Umekuwaje…” aliniuliza huku akinisogelea. Nikawa namkimbia, lakini wakati huu haukuwa mchezo tena nilikuwa katika hofu ya ukweli. Nilikuwa namuogopa John.

John alinisihi niache utani!!! Lakini sikuwa natania. Nilikuwa katika kumaanisha.

Hali ilikuwa tete. John alikuwa ananitisha.

Nikiwa katika kumkimbia John. Sasa aligundua kuwa kuna jambo limenisibu. Akanifata kwa kasi. Akanivagaa. Nikajilazimisha kujitoa mikononi mwake huku nikipiga kelele. Ghafla akaninasa vibao viwili.

Sasa hapo ndio nikachanganyikiwa mwenzenu na kuamini kuwa dunia imefika mwisho. Nililia huku nikimtaja mwalimu Nchimbi.

Lakini cha ajabu na kukera huyo mwalimu Nchimbi hata hakuwa akinisikia.

Iliniuma. John akaniongeza vibao vingine viwili. Sasa yale maumivu akili ikasogeleana.

“John una damu!! Una damu!!” nilipayuka

“Damu??” aliniuliza.

“Mgongoni umekuwaje wewe.”

“Mgongoni pamekuwaje kwani…alilalamika huku akijipapasa”

Maajabu mengine jamani!. Mkono wake haukuwa na damu. Akanigeukia.

Nikatamani kuiaga dunia niende likizo mbinguni. Hakuwa na kovu.

Mgongo laini kabisa wa kiume ukatazama nami. Nikaruka mita kadhaa.

Akapoteza uelekeo kuniona naruka vile nikataka kukimbia nje.

Akanidaka kanga yangu. Kanga ikateleza ikauacha mwili.


Shanga nane za rangi tofauti zilizokishika vyema kiuno changu ndio pekee zilizosalia katika mwili wangu. Sasa John alikuwa amebaki na kanga mkononi mimi nikiwa nina shanga kiunoni. Nusu nilikuwa nje na nusu nilikuwa ndani.

Swali likavamia kichwa changu.

Nikimbie na shanga kiunoni kwenda nje ama nirudi chumbani kwa John huyu wa maajabu!!! John niliyemuhisi kuwa sasa ni ………….

Nikabaki katika kizungumkuti.


JE ISABELA ATAKIMBIA NA SHANGA KIUNONI KWENDA NJE AMA ATARUDI KWA JOHN ANAYETISHA??

NINI KINATOKEA HAPA!!!!!!!


ITAENDELEA!!!

HATIA ----- 13

"Nani Matha au....eeh!! upo Mwanza" alizungumza bila kujiamini, wakati huo yule Matha aliyekuwa anajidai amelewa chakari alikuwa amekaa kitako macho yamemtoka pima.

"Ndio nipo hapa maeneo jirani na nyumba yake dakika sifuri tu nafika ndani, we endelea kulewa si ushalijua jiji mi ntafanyaje??"

Tumekwisha Matha, tumekwisha!!!! alisema Michael huku akitapatapa pale ndani. Matha naye alikuwa wima, kanga ilikuwa imedondoka na alikuwa amesalia uchi lakini hata hakulitambua hilo.

Hatia ikaunda hofu katika mioyo yao!!!


******

Matha hakuonyesha kufurahia ujio wa John pale ndani, alijifanya kuwa amelewa sana ilimradi tu John aweze kuondoka mapema, ujanja wake ukafanikiwa John aliaga na kuondoka huku akiahidi kufika pale asubuhi.
"Na hiyo pikipiki ya nani hapo nje??." John alimuuliza Matha, hakujibiwa lolote Matha akajifanya amesinzia tayari. John akajikongoja akatoka nje, alijaribu kupiga simu ya Michael haikupatikana.
"Hili toto hili na wake za watu, shauri zake!!!" alijisemea John huku akiufungua mlango na kutoka nje.
Michael hakuwa na hali kabisa, mchezo uliokuwa unaendelea ni hatari sana kwa upande wake, hali ya kuwa katika chumba kimoja na John Mapulu ilimchanganya sana, japo alikuwa katika uvungu wa kitanda na John akiwa kitandani huo haukuwa umbali mkubwa sana kati yao, alisikia kila alilozungumza John, hisia alizomueleza Matha.
Hatia ikampa shambulizi kali akajikuta anatokwa machozi kimya kimya ni dhambi aliyokuwa akiifanya na Matha ni usaliti mkubwa sana ni zaidi ya hatia.
John alipotoka na kuhakikisha kweli ametoweka Michael alitoka uvunguni na kuvaa nguo zake vizuri kabla ya kuaga, safari hii hakukubali kutawaliwa kimawazo na Matha. Aliondoka!!!
"Naomba uiache pikipiki!!!" Matha alimwambia Michael, kidogo apinge lakini kwa shingo upande akakubaliana naye.


******


Asubuhi John aliamka akiwa amechelewa kiasi, majira ya saa nne. Simu yake ilikuwa inawakawaka kuonyesha kuwa kuna ujumbe ama simu imepigwa haijapokelewa. Ulikuwa ujumbe wa Matha. Ujumbe uliozidisha hofu ya John juu ya Michael. Matha alikuwa ameuelezea ukarimu wa Michael kwake.
"Tazama ameenda kwenye sherehe, tazama amemrudisha nyumbani na pikipiki, amehakikisha usalama wake upo kabisa, ni mashemeji wachache wanaweza kuwa kama Michael!!!" aliwaza John huku akirudia kuisoma meseji ile.
John alizidi kumchukia kijana aliyempa ujauzito Joyce Keto. "Isingekuwa mimba basi hiyo ndio ilikuwa zawadi ya kipekee kwake" alisema John peke yake.
Mawazo ya John dhidi ya Michael yaliipunguza furaha yake. Siku hiyohiyo jioni baada ya kumtembelea Matha alimtafuta Michael ambaye walikuwa hawajaonana ili waweze kuzungumza.
Kituo cha mafuta maeneo ya mitimirefu ndicho kilimkumbusha kuhusu kijana Minja. Alikumbuka simu yake ya mwisho na mazungumzo kati yao.
"Oyo niaje"
"Poa kaka karibu!!"
"Namuulizia Minja sijui yupo?" aliuliza John
"Yupo kaka yule pale anakuja" alijielezea bwana huyu aliyekuwa na sare za wafanyakazi wa pale sheli huku akielekeza mkono wake kwa Minja, kama vile tayari alikuwa ameitwa Minja alifika pale, mara moja alimtambua John Mapulu.
"Heshima yako mkurugenzi, heshima yako kaka" Minja alianza porojo zake. John hakujibu kitu
"Kulikuwa na nini siku ile kwani, uliponipigia simu" swali lile Minja hakulitegemea ghafla kiasi kile akajiweka sawa kwa kukohoa kidogo kisha akamtazama John, alikuwa amemkazia macho, sura ya Matha akiwa anamsisitiza asimwambie John ikatokeza na kumwambia tena.
"Aaah!! siku zile bosi wangu!! kilikuwa kikaratasi cha mtu mwingine tu nikadhani chako" alijaribu kudanganya.
"Matha Mwakipesile unamfahamu??" aliuliza John kama vile alikuwa akimtuhumu Minja.
"Matha.....Matha......" alijaribu kukumbuka
"Ni wewe uliniambia hilo jina kivipi leo humkumbuki???" aliuliza tena. Kijasho chembamba kikamkumba Minja, mzigo wa kuchukua pesa za Matha ili asiseme lolote ukawa unamzidia na sasa ulikuwa unamwangusha chini.
"Matha ni yule mkeo eeeh!!!" alijifanya kukumbuka Minja. Honi za magari yaliyokuwa yakihitaji kupita ndio ilikatisha maongezi yao, John aliondoa gari, alijaribu kutafuta wapi aweze kupaki lakini hakupata nafasi yoyote.
"Nitakupigia simu!!" alisema kwa sauti ya juu iliyomfikia Minja ambaye alikuwa anatetemeka hovyo. Alikuwa anawaogopa sana watu wenye pesa zao kama John Mapulu.
Njia nzima John alikuwa anamuwaza Minja Meri, alianza kuhisi kuna kitu anafahamu na ameamua kumuingiza mkenge, John alianza kuhisi kuna jambo la maana sana kama sio kitu cha thamani ambacho bwana Minja alikuwa anataka kumtapeli.
Haiwezekani siku ile amesema kuna kitu, leo hii anasema hakuna kitu!!! hapana!!! alisema kwa ghadhabu huku akiupiga kwa ngumi usukani wa gari lake mlio wa honi ukatoka, aliyekuwa na baiskeli mbele yake akapisha njia. John bado hakuwa na uhakika kama aweke kituo kwa Matha au aonane na Michael kwanza. Akaamua aanzie na Michael.


******


Watu hawakuwa wengi sana katika ukumbi wa 'If not why not' Igoma jijini Mwanza, Michael na John walikuwa na masaa mawili tangu wafike pale, baada ya maongezi ya kawaida ya hapa na pale ndipo John alipoleta mezani mada ambayo kwa upande wake ilikuwa ni sawa na kucheza bahati nasibu wakati kwa upande wa Michael ilikuwa ni kama kaa la moto katika kichwa cha mwanadamu.
"Michael mdogo wangu hivi hata wewe si huwa unapenda kwa dhati!" alianza John
"Ndio tena sana tu!!!"
"Sasa kwa mfano, namaanisha ni kwa mfano sawa!!!" alisita John akapiga funda moja la bia yake kisha akaendelea
"Mtu unayempenda unasikia kuwa.....kuwa ni...ni mjamzito" alizungumza kwa kusitasita John, Michael akahisi nguvu zote hakuna mwilini, pombe yake aliyokuwa anaifurahia ikageuka kuwa na ladha ya pilipili, na nyama choma ile iliyopendezesha meza yao ikawa inamzomea, HATIA ikaendelea kumuadhibu na sasa ilikuwa imefikia pabaya zaidi.

Michael sasa kila kitu aliamini kuwa kipo hadharani, sasa afanye nini hilo ndio likawa swali kuu.
"Mbona umeshtuka sana?? au swali limekuja wakati mbaya???" John alimuuliza Michael aliiyekuwa anajaribu kuushinda uoga uliokuwa umemtawala.
"Swali gumu sana kaka, kwani unamaanisha nini hapo???" na yeye Michael akauliza, John akacheka bila kusema lolote akachana pande la nyama akaanza kutafuna na kushushia na bia.
"Wewe ni mwanaume na mimi ni mwanaume, kwa sasa nawahi sehemu, hebu kaa ufikiri halafu unipe ushauri kuwa kwa mtu unayempenda ukigundua kuwa ana mimba unafanya nini???" aliuliza tena kwa sauti tulivu John, Michael akakubali kwa kutikisa kichwa.
John alimpatia nauli Michael kisha akamwacha pale na kuelekea nyumbani kwa Matha, tayari ilikuwa saa tatu usiku.
“Kumbuka kuwa hiyo mimba si ya kwako….” Alisisitiza John. Michael akabaki kumtazama.
John akatoweka!!! Safari ya kwenda kwav mpenzi wake. MATHA!!
Michael akabaki kimya huku akiona kifo chake kikimtongoza!!!


*****

Matha aliufungua mlango taratibu, John akaingia ndani bila kuvua viatu, Matha alivyoufunga mlango John akamkumbatia ishara ya kumjulia hali.
"Vipi unaumwa??" aliuliza Matha. John hakujibu, akamtazama Matha usoni.
"He!! vipi wewe??"
"Hata siumwi ila kuna tatizo nadhani"
"Usinambie kuwa umechezwa machale kuwa tukienda kuiba tutakamatwa? maana na wewe kwa hayo machale" alidakia Matha huku akimfungua John vishikizo vya shati lake.
"Matha hakuna kitu chako chochote kimepotea humu ndani??"
"Mbona wauliza hivyo kuna nini??"
"Kuna kitu umepoteza??" alirudia swali lake.
"Hapana sidhani!!!"
"Mimi nadhani na kuna mjinga mmoja anataka kutuchezea!!"
"Nani huyo??? na ni kitu gani??" Matha aliuliza kwa umakini mkubwa, sura ya kikatili ilikuwa imemuingia tayari.
"Anajiita sijui Minja sijui nani ni wa pale sheli Mitimirefu" Alijieleza awezavyo John, Matha moyo ukamshtuka kwa hofu kuu baada ya kusikia hilo jina Minja, kwa kuwa alizijua mbinu za John, hakutaka kukutanisha macho naye hivyo akainama chini. Alimfahamu fika Minja Meri, ni huyuhuyu aliyekuwa anaijua siri ya ujauzito wake, lakini haikuwa siri kiasi cha hatari iliyopo, aliamini kuwa Minja alichukulia kama kamchezo flani tu kati ya mtu na mpenzi wake. Hofu ikazidi kumtanda Matha alipomfikiria John, aliijua fika ghadhabu yake ikipanda juu ya mtu hatua ya chini kabisa ni kutesa hadi kuua kama si kuua mara moja.
"Vipi unamfahamu huyo jamaa"
"Jina sio geni sana!!" alijibu Matha akiwa bado na ameinama
"Utakuwa unamfahamu, ni bwege mmoja hivi, kesho nitakupitia ukamuone, anadhani mimi bwege, yaani asiposema kitu kesho namuua!!!" aliapiza John huku akiuma meno yake, Matha akatambua John yupo katika hasira kali juu ya Minja.
Taratibu akamsogelea na kuanza kumpepea kwa kutumia shati alilokuwa amemvua, jasho lilikuwa linamtoka. Matha alifanikiwa kuishusha jazba ya John, tatizo likabaki kwake ni nani wa kuishusha presha iliyokuwa inazidi kumpanda, hofu iliyokuwa ikimtawala. Ni nani wa kumsaidia kuibeba hatia hii, kama Minja atakutana na John katika faragha lazima atausema ukweli, na hata akisema bado atauwawa je itakuwaje kwa yeye Matha atakayesalia duniani kumkabili John, na vipi juu ya kijana Michael. Hayo yote yalimuumiza na kumkera Matha.
"Hata nikiitoa kwa sasa haina maana tena!!!" aliwaza Matha. John aliaga akaondoka na kuahidi kufika siku inayofuata muda wowote kwa ajili ya kwenda kwa Minja. Kuondoka kwa John kidogo kulimpa nafuu Matha, akaondoa nguo zake zote ili kukabiliana na joto, Matha alitamani sana iwe ndoto lakini hii ilikuwa hali halisi.
John atatuua!!!!
Wazo la kuuliwa na John, Matha hakutaka kulilazia damu kwani alimjua nje ndani. Baada ya kufikiria sana alipata wazo, wazo la kuonana na Michael ili waweke mipango sawa.

Wazo hilo likapitishwa na asubuhi ya siku iliyofuata Matha akafanya ugeni wa ghafla nyumbani kwa John. John hakuutegemea.
"Mambo vipi Michael....darasani tafadhali" aliamuru Matha, John na Bruno wakavutiwa na amri ile wakamchukulia Matha kuwa ni mwanamke wa shoka. Michael alighairi kuendelea kunywa chai akamfuata Matha katika chumba cha mafunzo.
"Nakupenda sana Mic" Matha aliyeonekana mwanamke wa shoka mwenye amri sasa alikuwa amelegeza macho na kumwangukia Michael begani.
"Matha hali sio nzuri huyu jamaa amegundua kitu"
"Kitu gani???" aliuliza Matha huku akisimama imara na kumkazia macho Michael. Michael alimueleza swali zito alilopewa na John ili alifanyie tafakari.
"Kwa hiyo nani atakuwa amemwambia??" aliuliza Matha japo hakutegemea jibu lolote kutoka kwa Michael
"Au Minja amemwambia kilichopo katika kile kikaratasi"
"Minja ndo nani???" aliuliza Michael, ikawa zamu ya Matha kuelezea juu ya huyo Minja na wasiwasi wake juu yake.
"Atakuwa ni huyo hakuna mwingine!!!" alisema Michael huku akikaa kitako.
"Tukamtafute baadae" alitoa wazo Matha likakubaliwa na Michael. Hakuna mazoezi yoyote waliyofanya wawili hawa, Matha alikuwa anakwanguliwa na makali ya Hatia wakati Michael alikuwa kama mfu tayari. Matha alijaribu kumtia moyo Michael lakini ilikuwa sawa na bure hata yeye alilitambua hilo.
"Sasa tukishamuona tunamwambia nini?"
"Mbele kwa mbele itafahamika" alijibu Matha kisha akaendelea, "Akileta upuuzi atanijua mimi ni nani" Michael akawa kimya hakujazia neno.
Baada ya masaa mawili walitoka katika chumba cha mazoezi, Matha aliaga akaondoka Michael akaingia chumbani kwake. Hakuna ambaye aliwagundua kuwa walikuwa katika matatizo makubwa.

****


Minja Meri akiwa bado hajausahau ujio wa John Mapulu siku iliyopita. Siku iliyofuata akiwa kazini amehudumia magari mengi, lilikuja gari dogo aina ya Toyota Vitara, vioo vyake vilikuwa vimewekewa utando mweusi 'tinted' hivyo ilikuwa ni vigumu kuwaona walioko ndani.
"Ya shilingi ngapi bosi wangu???" Minja alimuuliza dereva ambaye alikuwa ameshusha kioo.
"Elfu ishirini....chukua pesa dirisha lile pale" alielekeza dereva, Minja kwa nidhamu akaelekea alipoelekezwa.
"Mambo vipi Minja??....sikia pesa hii hapa...unatoka kazini saa ngapi??" Minja alikutana na sura yenye uchangamfu ya Matha. Kwa kuwa walionekana kuwa na haraka naye Minja alijibu upesi.
"Ndio natoka sasa hivi hapa namalizia tu hizi gari mbili tatu, kuna ishu halafu nataka..."
"Poa nakuja muda si mrefu" Matha alimkatisha.
Baada ya kujizungusha kwa dakika kadhaa Matha alimpitia Minja wakaondoka eneo lile wakati huu alikuwa alikuwa anaendesha mwenyewe hivyo kwenye gari walikuwa wawili tu.
"Jana akaja mume wako bwana lakini hatukuweza kuzungumza vizuri....mh!!" Minja akaanza simulizi zake, Matha akawa kimya akijitwalia pointi mbili tatu.
"Minja unaipenda sana kazi ya sheli?" Matha alituliza swali hilo kwa Minja, walikuwa maeneo ya Mkuyuni tayari mezani pakiwa na vinywaji baridi.
Nitafanyaje sasa dadangu!!!" Minja hakuwa amejibu swali, lakini Matha alielewa.
"Nahitaji kukusaidia" alizungumza akasita kisha akaendelea, "nataka ufanye kazi nyingine tofauti na hii"
"Nitafurahi sana dadangu" alidakia.
"Unalipwa au unapata shilingi ngapi kwa siku??"
"Inategemea kuna siku napata elfu kumi siku nyingine hadi kumi na tano"
"Na una familia??"
"Naishi peke yangu maisha magumu sana!" alivutia kwake Minja.
"Pole sana!!" alisema Matha huku akimkazia jicho Minja.
Hisia za Minja zikaangukia katika mapenzi akaanza kuhisi kuwa Matha alikuwa amempenda tayari. Walipomaliza maongezi Matha alimkabidhi Minja shilingi laki moja na kumsihi asirejee tena kufanya kazi eneo lile. Minja alikuwa dhaifu katika pesa alipozipokea na amri aliifuata kama alivyotakiwa. Hakujua kuwa alikuwa kipofu anayepelekwa njia yenye miiba mikali, Minja akajihesabia kuwa ametoka kimaisha kwa kupendwa na mtoto mrembo sana tena mke wa tajiri.
Siku iliyofuata hakwenda kazini!!!
Na hata John alivyomchukua Matha jioni kwa ajili ya kwenda kumtambua na kumuadabisha Minja hawakumkuta. Matha akatabasamu ndani ya nafsi, kwake yeye ulikuwa ushindi wa chee!!! John akazikuza hasira zake juu ya Minja.
"Boya amekimbia ngoja!!!"
"Achana naye mjinga tu!!!" alidakia Matha
"Simuachi kirahisi hivyo......." alijibu John kisha akapiga kite cha hasira na kuondoa gari. Matha akazishusha pumzi zake na kumbusu John katika papi za midomo yake. Akawa amempumbaza!!!. ikabaki kazi ya kumtafutia kazi Minja Meri ambaye amebeba siri nzito bila kujijua kuwa ushahidi wake unahitajika ili dunia ipokee damu itakayomwagika.



*****


Usiku mzima Minja alikuwa akitafakari juu ya ukarimu aliotendewa na Matha, fikra zake bado zilikuwa bado katika mapenzi.
"Hivi nini kimemvutia kwangu mtoto mzuri kama yule jamani halafu kesho ananiletea jibu kama nimepata kazi ama la!!" Minja alijiuliza kwa sauti ya chini kama vile pembeni yake kuna mtu atampa jibu.
"Nikishakuwanaye najua hata haka kajumba nitahama...mbona akina Mussa watakoma" aliwakumbuka rafiki zake waliokuwa wanaishi maisha ya kufanana.
"Lakini kuhudumiwa na mwanamke mh!!!" aliendelea kuwaza. Usingizi ukampitia hatimaye. Asubuhi nayo ikachukua nafasi tena, Minja alikuwa amedamka mapema sana, tabasamu lilimtawala muda wote. Mara kwa mara alimfikiria Juma, huyu alikuwa ni jirani yake aliyekuwa anaishi nyumba ya vyumba viwili tena umeme na maji vilikuwepo, pia alimkumbuka mkewe Juma alivyokuwa mrembo aliyemtamanisha kila siku alipomtia machoni, dharau za mwanadada huyu aliyeitwa Husna zilikuwa zinamkera sana Minja lakini hakuwa na la kufanya. Minja aliamini kuwa karibu na Matha ndio kutawafunga mdomo wavimba macho wote mtaani, hisia za mapenzi zikamezwa na hisia za majivuno Minja akawa na ndoto ya kupata jina upesi upesi mtaani. Subira ikashindwa kutulia katika moyo wake, mguu na njia Minja akitembea mwondoko tofauti kabisa akaamua kwenda kumtangazia rafiki yake jambo hilo. Kwa kawaida huwa anatembea kwa miguu na kupita mikato ya hapa na pale hadi kufika nyumbani kwa Rashid, lakini siku hiyo aliamua kupanda gari la kukodi aina ya 'taksi'. Alifanya hivyo ili akajitwalie sifa mbele ya familia hiyo ya kimaskini maeneo ya Mbugani.
"Elfu tatu!!!"
"Twende!!!" alijibu kwa sauti iliyojaa ujivuni, Minja. Dereva akawasha injini gari likaondoka kwa mwendo wa kawaida hadi nyumbani kwa bwana Rashid, kabla ya kushuka kwa mbali kabisa aliwaona watoto wawili wa mzee Rashid wakikimbizana aliyetangulia alikuwa na hindi la kuchemshwa huku wa nyuma akiwa uchi na kilio kikimtawala. Rashid alikuwa akiwaangalia hakuwa na la kufanya bila shaka alikwishazoea maisha hayo.
"Hebu twende pale mara moja!!!, nitakuongezea malipo" Minja alimwamrisha dereva naye akatii bila kutia neno. Alisimamisha gari mahali ambapo palikuwa na duka kubwa kwa kiasi chake, Minja akatelemka na kuingia pale alitoa noti ya shilingi elfu kumi akanunua mikate na soda za kopo kisha akarejea garini.
"Simama mlangoni kabisa!!!" alielekeza Minja.
Kadri gari lilivyokuwa linasogea ndivyo watoto na mzee Rashid akishirikiana na mkewe walilikaribisha kwa macho yenye mshangao sana, haikuwa kawaida kabisa kupokea ugeni wa namna hiyo kwenye kibanda hicho cha mlinzi asiyekuwa na vyeti aliyeajiriwa kulinda duka la mtu binafsi.
Minja alishuka kwa madaha yote, akamwita yule dereva nje na kumlipa pesa yake umati wote umtazame, kisha akashusha mifuko ya mikate na vinywaji alivyokuja navyo. Heshima yake kwa siku hiyo ikawa juu sana, alifanikiwa kuwateka maskini wenzake.
Mtoto wa mwisho wa Rashid akamlilia Minja waondoke naye. Minja akambeba juu juu akampatia noti ya shilingi elfu tano. Kilio kikaishia pale.
Minja na Rashid wakatoka!!!! Rashid hakuisha kujichekesha kila mara mbele ya bosi wake wa siku hiyo. Kwa mwendo uleule wa kuchukua teksi Minja na Rashid walipotea mbele ya eneo hilo la kimaskini na kutua maeneo ya Nyegezi wakatafuta mgahawa mzuri wakakaa na kuanza kunywa taratibu. Kisha maongezi yakaingilia kati, Minja akamueleza kila kitu Rashid juu ya zali/bahati iliyomwangukia kupendwa na mke wa tajiri.
Maelezo ya Minja si tu kwamba yalimpa wivu uliokithiri Rashid lakini pia yalimuweka katika kizungumkuti, hakuelewa kama alikuwa sahihi ama la!!
"Umesema John Mapulu ndio mume wa huyo binti!!!!"
"Ndio lakini huwezi kumjua" alijibu Minja huku akipiga funda kubwa la bia.
"John Mapulu!!!" Rashid alifanya tafakari ya miaka miwili nyuma katika kazi yake ya ulinzi aliamini kuwa huyu mtu anayezungumziwa na swahiba wake aliwahi kuwa bosi wake tena si mara moja kwani aliwahi kupumzishwa na kurejeshwa tena, na baadaye bosi wake alitoweka katika mazingira ya ajabu hivyo akapewa chake na kuachishwa kazi. Hawezi kuwa amesahau zama hizo kwani alikuwa analipwa vizuri sana na familia yake ilikuwa inaneemeka na kazi ya baba yao, lakini baada ya kuachishwa kazi mambo yakawa magumu.
"Namfahamu lakini mbona...."
"Wewe humjui nakwambia cha msingi nipe ushauri!!!" aliingilia kati Minja. Rashid akakaa kimya kwa sekunde kadhaa akiikodolea macho sahani iliyokuwa imesheheni nyama ambazo ni kama zilikuwa zimekosa mlaji.
"Minja hapa kuna namna!!!"
"Namna gani, unadhani nimetumia juju" aliuliza Minja.
"Hapana sivyo!!! ila huyo John huyo John Mapulu namfahamu hana uwezo wa kuzaa iweje useme mkewe ana ujauzito?" aliuliza kwa sauti ya chini Rashid, macho yakamtoka Minja akabakia na pande la nyama mdomoni bila kutafuna, kauli ile ilikuwa imefungua akili yake kwa kiasi kikubwa.
Akatulia hivyo kwa sekunde kadhaa bila kusema lolote. Kisha akatikisa kichwa kumaanisha kuwa ametambua jambo. Akili yake ilifanya kazi harakaharaka tamaa ya pesa ya kichaga ikamwingia, ikamtuma kumchenga Rashid ili aweze kula peke yake.
"Ah!! wanawake wa mjini hao, hebu achana naye" alisema Minja. Rashid akaafiki, baada ya nusu saa wakaagana. Safari hii kila mmoja aliondoka kivyake.


****

***MINJA anahisi MATHA amempenda kimapenzi kwa wema aliotendewa......hajui kama anaingia HATIANI bila kujua......eeh! Mungu muepushe na janga hili.
***RASHID anajua kitu kuhusu John Mapulu!!! Na amemueleza MINJA je? Minja atatumia siri hjii kama chambo???
***HATIA ya mimba ya Joyce inamtesa na kumsulubisha JOHN MAPULU!!!!

HATIA INAZIDI KUSAMBAA....
TAFADHALI...

Recent Posts