Tuesday, October 30, 2012

HATIA---- 10

 Na GEORGE IRON

“Zawadi kwa lipi kaka nililofanya”
“Jana umetumia muda wako mwingi sana kuzungumza na Matha nimeyaona mabadiliko leo mabadiliko makubwa nilikuwa na Matha asubuhi ya leo hapa!!” John alizungumza huku tabasamu likichanua katika mdomo wake.
“Aaah!! Amakweli leo nimelala sana”
“Kwa suala hilo nahitaji kukupongeza!!!”
“Usijali wewe ni kaka yangu” Michael alisema huku hasira zikiwa zimemtawala ndani ya nafsi yake pepo wa wivu akaanza kumtafuna taratibu, akaanza kuhisi Matha ni mali yake peke yake.
“Hata kama lakini unastahili zawadi” alisisitiza John. Michael hakupinga zaidi ya kukubali kwa shingo upande hiyo zawadi.
“Matha amekuja??? Muda gani na saa ngapi ameondoka?? Au mtego huu?? Eeh!! Mungu nisaidie” baada ya muda mrefu sana kupita Michael alikumbuka kupiga dua.
Au wananichora hawa kasha wanitoe kafara! Alijiuliza.



****


Hali ya utulivu ilitawala eneo hili la Nyegezi jirani kabisa na chuo kikuu cha mtakatifu Augustino maarufu kama SAUT. Pumzi na mapigo ya moyo ya wawili hawa yalisikika, mmoja akiwa anajiamini na mwingine akiwa ametekwa na uoga. Ilikuwa saa sita na nusu usiku, sauti za ndege wasiojua ubora wa nyimbo zao zilisikika kwa mbali na mara chache kuingiliwa na sauti mbaya za popo. Maumbo yao yalikuwa yanaendana walikuwa wamesimama kama vile kuna jambo flani walikuwa wanazungumza kwa siri kutokana na ukaribu wao.
Majira ya saa saba usiku mmoja alisogea na kujificha mahali na kumwacha mwenzake akivuta sigara na kupuliza moshi hewani. Michael alikuwa ameachwa na John eneo lile, uoga ulipitiliza kipimo hadi akaizoea hali ile kwa kuamini kuwa kama John angekuwa ameamua kumuua angeweza kufanya hivyo mapema na si lazima kutumia mbinu zote hizo. Lakini licha ya kujiaminisha sana, suala la kupewa zawadi eneo kama hili halikuwa la kawaida. Zawadi yangu ni kifo!!! Alijiuliza. Alitamani kumpigia simu Matha lakini akakumbuka alikuwa amepewa onyo kali juu ya kuwasha simu.
“Shika huu waya, nitakuamuru uuvute!!!!” John alimuelekeza Michael kwa sauti ya chini. Michael akatii. John akawasha sigara na kuanza kuvuta. Mara ghafla akamuamuru Michael kuuvuta ule waya hadi kwenye ki-mti kidogo kilichokuwa jirani kabisa na njia hiyo ya uchochoroni baada ya kuufunga waya huo Michael alisikia muziki kwa mbali ukizidi kusogea karibu. Kufumba na kufumbua Michael aliuzuia mdomo wake usiweze kupiga kelele. Pikipiki ilikuwa imeachana na dereva aliyekuwa anaiongoza kama hiyo haitoshi kichwa kilikuwa kinakaribia kuachana na kiwiliwili. John alikuwa ameua kwa kumtegea waya dereva wa pikipiki.
“Panda twende…” John alimwambia Michael ambaye bado alikuwa amezubaa asijue la kufanya. Kwa sauti kali ya John akawa amerejewa na ufahamu akapanda katika pikipiki.
“Bila shaka itakufaa kwa safari za hapa na pale, kifo hiki kinanikumbusha enzi hizo naanza maisha ya ujambazi!!” John alizungumza kwa sauti ya juu ili Michael aweze kumsikia, hakuwa na wasiwasi hata kidogo. Michael hakujibu kitu.
Mnamo saa nane na nusu kila mmoja alikuwa amejichukulia nafasi katika sebule kubwa kabisa. Michael hakuwa na amani lakini John alikuwa mzoefu sana.
“Zawadi yangu!!!!!! Oooops!!! Nilikuwa nimesahau” John alikumbuka zawadi aliyoahidiwa na Matha kupitia Michael.
“Mh!! Hiyo mpaka pakuche tena” alijibu Michael.
“Hapana twende hiyo pikipiki ina mafuta ya kutosha” alitoa hoja John, Michael kwa kumuhofia John akakubali.
Mwendo wa dakika kumi tayari walikuwa Buzuluga. Kama kawaida John akamwacha Michael aende mwenyewe. Siku hii hakukaa sana alirejea na bahasha na kumpatia John kisha wakaondoka kurudi nyumbani. Ilikuwa ni nguo ya ndani ya kiume!!
Asubuhi sana aliwasili mtu asiyefahamika machoni pa Michael alikuwa maalum kwa ajili ya kubadilisha namba za pikipiki ile. Zoezi lilifanyika kwa umakini na kufikia jioni John kwa uhuru wote alitoka na pikipiki ile nje akiyapita kama hayaoni magazeti yanayozungumzia kifo cha muendesha bodaboda mitaa ya Nyegezi.
John alifika nyumbani kwa Matha majira ya saa tatu usiku baada ya mizunguko mingi ya kujaribu ubora wa pikipiki ile.
Matha alitegemea ujio huo hivyo chumba kilikuwa kinanukia sana kutokana na maandalizi ya uhakika. John alipokelewa kwa upendo wa hali ya juu sana, mabusu kadhaa ya hapa na pale yalikonga sana nyoyo zao lakini hasahasa John aliyekuwa hana la kusema mbele ya Matha.
“Nakupenda Jo!!”
“Sina la kusema nadhani unajua kuwa nakupenda”
“Asante sana” alisema Matha kinafiki, huku akijua fika ana hatia ya kumsaliti John tena kwa mtu wake wa karibu Michael. Matha alimkaribisha mezani John ili wapate kwa pamoja chakula alichokuwa amekiandaa. Walijumuika kwa pamoja na baada ya hapo wakahamishia mashambulizi kitandani. John alikuwa anampenda sana Matha!!.
Vurugu hizo zilitwaliwa na usingizi baadaye hadi John alipokuja kushtuka alfajiri. Alikuwa na miadi mida ya saa nne hivyo alivaa nguo zake bila hata kuoga kwani hapakuwa na choo wala bafu la ndani kwa ndani katika chumba cha Matha.
“Mh!! Kuoga usioge yaani na Suruali unavaa hiyo hiyo??”
“He! Sasa nitavaa ipi nyingine?? Unaota nini!!”
“Subiri” Matha alisema huku akiinuka kizembezembe, umbo lake zuri lilijihifadhi katika nguo hii ya kulalia John alipatwa na matamanio wakati Matha amegeukia upande wa kabati, John hakujua ni nini anatafuta mawazo yake yote yalikuwa katika maungo ya Matha.
“Mh!! Na wewe kunichungulia tu loh!! Mwanaume huna haya wewe, usiku mzima hujaridhika tu!!” alitania Matha na kumkurupua John aliyezuga kwa kucheka. Matha alimshangaza John kwa kumpatia suruali ambayo ilimkaa na kumpendeza vyema.
“Asante mke wangu!!!” alishukuru John na kisha akahamishia vitu kadhaa kutoka katika suruali aliyoivua na kuvitia katika hii aliyokua ameivaa.
“Umenipatia hadi kiuno” alisifu John huku akijitazama. Matha akajibu kwa tabasamu. Baada ya kujitathmini akambusu Matha katika papi za midomo yake na kuondoka. Pikipiki bado ilikuwa na mafuta ya kutosha. John alipofika nyumbani aliingia moja kwa moja bafuni akaoga kisha akavaa suruali aliyopewa na Matha na juu akaweka shati jingine halafu akachomekea, uchaguzi wa kiatu ukamshinda akaamua kuvaa viatu vya wazi. Tayari ilikuwa saa mbili na nusu asubuhi. Michael alikuwa hajaamka bado, Bruno ndiye aliamka kumfungulia geti John kisha akalala tena hivyo hata wakati (John) alipokuwa anatoka hakuweza kumsikia tena. Wakati huu alitoka na gari ndogo Toyota Corolla. John alikuwa anawahi miadi ya kwenda kuzungumza na wenzake juu ya ‘dili’ la kuvamia mahali.


****
Kituo cha mafuta kilichopo maeneo ya Miti mirefu karibu na shule ya sekondari ya Pamba ndipo John alijijengea mazoea ya kwenda kujaza mafuta hivyo alikuwa anafahamiana na wafanyakazi wengi wa pale. Siku hii pia alikwenda na gari yake hadi katika kituo hicho. Alichangamkiwa na muhudumu ambaye pia alikuwa anamfahamu japo hawakuwa karibu sana.
“Weka ya elfu thelathini” aliamuru John huku akimkabidhi pesa kijana huyo aliyeonekana kutamani sana mazoea na John lakini ikawa inashindikana, John alikuwa bize sana na simu yake. Baada ya kuhudumiwa John alimpatia kijana huyo shilingi elfu tano kama malipo ya uchangamfu wake (bakhishishi) tangu John anafika hapo.
“Akhsante sana bosi”
“Kwa heri” aliaga John.

John alikuwa wa mwisho kuingia katika mkutano huo wa siri, ulikuwa ni mkutano wa watu sita wakiwa na lengo la kuvamia na kupora katika Supermarket ya Imalaseko jijini Mwanza, mpango ulikuwa umewekwa tayari kabisa kilichokuwa kimebakia ni kutekeleza. Kikao kiliendeshwa kwa sauti za chini sana katika hotel ya Mwanza (New Mwanza Hotel). Wakati kikao kinaendelea simu ya John iliyokuwa katika mlio wa kimya (silent mode) iliita, ilikuwa namba mpya John akapuuzia. Ikaita tena kwa mara ya pili na ya tatu hadi ya nne.
“Naingia uwani dakika sifuri” aliomba ruhusa John.
“Uwahi kurudi” mwenyekiti wa kikao alijibu.
Alipofika chooni simu iliita tena.
“We nani??” aliuliza kwa jazba John
“Samahani bosi….”
“Nimeuliza wewe nani??” aliendelea kusihi
“Bosi ni mimi Minja, wa hapa sheli”
“Tatizo!!”
“Bosi kuna kikadi cha hospitali hapa nadhani kilikuwa katika pesa zako ulizolipia hapa”
“Kikadi gani, sidhani kama ni mimi” alipinga John
“Aaah!! Bosi ni cha kwako, angalia bwana kikipotea hiki itakulazimu kupima upya..??” upande wa pili ulilazimisha uchangamfu ambao haukupokelewa na John. Sauti ilikuwa imemkumbusha John kuwa anayezungumza ni kijana aliyemjazia mafuta kwenye gari asubuhi hiyo
“Mbona sikuelewi”
“Matha Mwakipesile ndio mkeo!!!”
“Ndio kwani nini mbona husomeki jombaa” John alizungumza kwa jazba hakupenda jinsi alivyozungushwa zungushwa.
“Basi kuna kikadi chake hapa cha hospitali….”
“Haya nitakupigia baadaye nipo kwenye kikao” alisema John na kukata simu, alihofia kuwaudhi wenzake waliokuwa wanamsubiri.
Laiti kama angeendeleza mazungumzo japo kidogo tu yangekuwa mengine.

****

Mapigo ya moyo ya Matha yalikuwa yakienda kasi tofauti na siku zote maishani mwake. Kabati la nguo halikuwa na kitu chochote ndani yake, kila kitu kilikuwa shaghalabaghala. Matha alikuwa anatokwa na jasho jingi. Kwa mara ya kwanza tangu aingie katika suala zima la ujambazi alijihisi kutingishika na kushikwa na uoga wa hali ya juu. Kadi iliyokuwa na majibu kwamba yeye ni mjamzito ilikuwa haionekani, kila kona alipojaribu kugusa hapakuwa na chochote, tegemeo la mwisho na aliloliamini zaidi ilikuwa ni katika suruali aliyomzawadia John asubuhi hiyo. Matha alitamani kurudisha muda nyuma lakini muda ulizidi kwenda mbele. Amani ikatoweka, giza likatanda, kizunguzungu kikamtwaa akakaa kitandani, alilazimisha kilio ili kuondoa donge la wasiwasi na karaha kooni, kilio hakikutoka akawa kama anakoroma, akaligundua hilo akanyamaza kimya. Akatamani aizime simu yake bado hakuona tija. Hatia ikaanza kumtafuna, hatia ikaanza kuipasha joto damu ya mlimbwende huyu.

Matha alichukua simu yake na kutaka kumpigia Michael lakini kabla ya kupiga alisita. Hofu ikamkumba Matha, Michael angeweza kukimbia. Nguvu za Hatia ziliendelea kumtafuna kwa kasi Matha aliamua kumpigia simu John japo hakuwa amejiandaa nini cha kumuuliza. Mikono yake ilikuwa inatetemeka wakati simu inaanza kuita, simu iliita bila kupokelewa.
"Tayari amekiona!!" alitahayari Matha, wakati akizipiga tena namba za John. Wakati huu iliita mara mbili kabla ya kukatwa. Wasiwasi ukatanda. Nimelikoroga!! kwa mara ya kwanza Matha alijikuta anamuogopa John. Huku akijitazama kwenye kioo, mikono yake ikiwa imekishika kiuno chake chembamba.


*****

Akiwa amewakera wenzake katika kikao hicho cha watu wachache japo chenye mpango wa kuumiza wengi John Mapulu hakuumizwa sana na hilo ila ile hali ya kupigiwa simu na Matha kisha hakuzipokea ndio ilimtia mawazo. Kengere za tahadhari zilipiga masikioni mwake, huenda Matha yupo matatani, ama ana shida ya msingi sana. Akafikiria kuomba ruhusa tena lakini nyuso zilizojaa chuki zilikuwa zikimtazama yeye, akahairisha! lakini kwa kujificha akatuma ujumbe.
'Nipo kwenye kikao honey! kuna nini?' baada ya kutuma ujumbe ule akahifadhi simu yake, punde wakati akijiweka sawa kuendelea na kikao akaisikia simu yake inatoa mlio, akaichomoa tena.
"Message sending failed" alijilaumu John kwani alikuwa hana salio kwenye simu yake hivyo ujumbe haukufika, kwa ujasiri akaomba ruhusa.
"Dakika moja ni 'waifu' sijui kuna nini" alijieleza John. Hakuna aliyemjibu. Alijua wamekasirika lakini hakujali, alimpenda sana Matha. Alipofika chooni akambip Matha. Punde akapigiwa.

"Yes sweet heart nambie"
"Kwani vipi?...kwema huko, nimekukumbuka wewe" alijiumauma Matha.
"Huku poa tu sijui hapo nyumbani"
"Poa tu upo kwenye kikao eeh!...nimekusumbua" alijishaua huku sauti yake ikitawaliwa na mawimbi mawimbi ya hofu
"Hujanisumbua hata kidogo" alijibu John
"Haya endelea na kikao mume wangu" Matha alitoa neno hilo ambalo lilimlegeza John akauhisi upendo wa Matha ulioanza kupotea ukirejea kwa kasi.
"Asante 'waifu' ehe! unatoka saa ngapi leo ulisema?"
“N’taenda baadaye mjini mpenzi wangu kuna mahitaji nitafuata supermarket"
Suala la Matha kuelekea mjini likaifungua akili ya John akakumbuka kitu, ilikuwa ni simu aliyopigiwa kutoka sheli. Upuuzi wa kimaamuzi alioufanya haustahili kusamehewa. John Mapulu akamgusia suala hilo Matha 'mkewe'
"Tena afadhali pitia hapo sheli hapo kuna jamaa mmoja mchaga hivi anafanya hapo kazi amesema sijui kuna kidude gani nimempa kimakosa hebu kaanga.. . . . ." kabla hajamalizia kuongea simu ilikatwa na kuzimwa, mwenyekiti wa kikao alikuwa amemfuata John huko huko chooni, kwa hasira akaitwaa simu na kuizimisha, John akasonya kwa ghadhabu lakini hakufanya lolote zaidi ya kurejea kwenye kikao.

Matha alikuwa anatetemeka tangu anaongea na John neno la kwanza kwenye simu, alikuwa anajaribu kuzichanga karata zake aweze kufahamu kama John alikuwa anafahamu juu ya uwepo wa kikaratasi kinachoonyesha majibu yake siku alipoenda kupima ujauzito. Hofu ilikuwa imetanda lakini aliamua kujaribu. John hajui lolote! ndio mshangao alioupata Matha baada ya kuisikia sauti ya John ikiwa tulivu na iliyojaa mahaba.
"Sheli...kidude. . . Mchaga hivi vitu vinahusiana kweli na hicho kikaratasi" alijiuliza Matha baada ya mawasiliano kukatika. Alikodolea macho simu yake huwenda John atampigia, hakupigiwa, akaamua kupiga tena, simu ikawa haipatikani. Sentensi isiyonyooka na isiyomaliziwa kutoka kwa John ilimuacha Matha katika jitimai la nafsi. Hakuelewa John alimaanisha nini.
Matha hakuelewa kama John alimaanisha hicho kikadi alichokuwa akikiwaza yeye ama la! . Akili ya Matha ilikumbwa na zizimo, muda ulikuwa unasogea bila maamuzi sahihi kupita katika halmashauri ya ubongo wake.
Aliingia bafuni akaoga akavaa nguo zake alizokuwa amevaa siku iliyopita. Kama vile mtu anavyoitwa na wachawi usiku wa manane kutokea usingizini ndivyo Matha alivyotoka chumbani kwake na kuanza kutelemsha ngazi hadi akafika chini.
Sheli!! lilimjia hilo wazo ghafla baada ya kugundua hakuwa na mahali rasmi pa kwenda.
"Sheli gani sasa??" lilikuwa swali lililofuata. Hakika lilikuwa swali gumu sana kwa maana sheli zilikuwa nyingi mno. Matha aliweka kituo kisichokuwa rasmi katika banda linalouza magazeti, akawa kama anasoma vichwa vya magazeti mbalimbali kwa umakini mkubwa sana lakini hakuna alichokielewa, mawazo yake hayakuwa hapo.

"Naomba KIU" Matha alitoa pesa na kumlipa muuzaji akapewa gazeti alilohitaji. Macho yake yakakutana na sheli upande wake wa kushoto alipogeuka. Bila kujiuliza mara mbilimbili akawa ameamua kuifuata baada ya kuhakikisha upande wa kushoto na kulia mwa barabara usalama ulikuwepo. Pale sheli palikuwa na mgahawa, Matha akapenyeza hadi karibu na huo mgahawa, walipita watu kadhaa akaishia kubadilishana nao salamu, mara aanze yeye ama wao, hakuongeza neno.

Niulize mchaga au? huu ni upuuzi!! Matha akajifanyia mahojiano mafupi na kugundua alikuwa anajidanganya. Alipiga hatua kadhaa kuuacha mgahawa kwa ghadhabu lakini mara upepo ukavumia usawa wa pua yake, harufu nzuri ya chai ya maziwa, donati, sambusa, chapati na mayai ya kukaangwa mchanganyiko na eggchop vyote vikaungana na kupenya katika pua yake. Minyoo ikashtuka usingizini, tumbo likaunguruma Njaa!! Matha akabadili uelekeo akaurejea mlango wa mgahawa, akachukua nafasi yake.
"Maziwa ya moto, donati na egg chop" aliagiza kwa utulivu Matha huku macho yake yakizipitia kurasa za gazeti alilonunua, simulizi ya Beka Mfaume ya WIVU ambayo siku zote ilikuwa inateka akili yake leo hii alikuwa anaiona kama makala mbovu ya siasa za ughaibuni tena iliyoandikwa katika lugha ya kigeni.
Chai ilipoletwa ukawa mwisho wa kusoma gazeti. Tumbo lake ambalo halikuwa na chochote tangu kupambazuke lilikuwa linafurahia maziwa ya moto yaliyopenya katika kinywa kisichopatwa na ladha yoyote. Mfululizo wa matukio yasiyokuwa katika mtiririko maalum uliisumbua akili yake hatimaye akaiona sura ya Michael, akajutia kukutana naye lakini akajilaumu kwani yeye ndiye alimwendesha hadi akafikia kuwa mpenzi wake wa siri. Hakujua alitumia muda gani kufikiri lakini alipokumbuka tena kupeleka kikombe cha maziwa mdomoni yalikuwa yamepoa hakuendelea kunywa.
Akalipa akaondoka!!
Kelele za mpiga debe zilimvuta akapanda daladala inayoelekea Nyegezi ikitokea Igoma. Matha alipanda kwa msukumo wa mpiga debe hakuwa amenuia rasmi kwenda huko Nyegezi.
Muziki mkubwa ndani ya gari hiyo ulimtia ghadhabu, alitamani kushuka lakini alikuwa siti ya nyuma akahofia kufanya usumbufu.
"Tuache hapo Natta!" abiria mmoja aliyekuwa jirani na Matha alimkumbusha kondakta ambaye naye aligonga bodi dereva akasimamisha. Aliposimama kuanza kushuka Matha naye akaamua kushuka, baada ya kulipa nauli alishangaa hapa na pale na kujiangalia amepungukiwa nini ndipo alipogundua ameacha gazeti ndani ya gari, bila uelekeo maalum Matha alianza kukaza Mwendo.
"Mh! au ile sheli ya Mitimirefu??" swali la ghafla likanasa katika ubongo wake likisubiri jawabu.


****MATHA amesahau kikadi kinachoonyesha majibu yake kuwa YU MJAMZITO.......katika Suruali aliyompatia JOHN MAPULU.......

***JOHN MAPULU bila kutambua anakitoa kikaratasi kile pamoja na pesa anazolipia sheli.....Anapigiwa simu kukumbushiwa juu ya alichosahau!!!
***MATHA naye anahaha kujitoa katika HATIA hii.....hatia ya usaliti......

***JE NANI ATAMUWAHI MWENZAKE????....na vipi ikifahamika...USALAMA WA MICHAEL UPO WAPI???
HATIA HATIA HATIA!!!!

Monday, October 29, 2012

HATIA 9


MTUNZI: George Iron Mosenya
CONT: 0655 727325

SEHEMU YA SABA

“Shiit!!! Nimeacha mguu wangu ndani ya gari!!!” John alijisonya baada ya kugundua amesahau bunduki yake garini, haukuwa utaratibu wake kutembea bila silaha. Lakini hakujisumbua kusimama na kuifuata. Kauli hiyo ilizidi kumtetemesha Michael.
Ina maana ndio amekuja kunifichulia maovu yangu na kuniua hapahapa!!!! Mungu wangu, lakini nilimwambia Matha kila siku kuwa ananitia matatani ona sasa!!! Aah!! Ona sasa Matha!! Aliwaza Michael kwa uchungu na kuzitupa lawama kwa Matha kabla John hajaendelea kuzungumza
“Eeeh!! Umeuliza kuwa nina maana gani, ujue Michael kuna wakati unafika lazima kila ukweli uwe wazi na uamuzi ufanyike mara moja, na uamuzi mgumu ni ule unaomuumiza aliyeuamua!!!” John aliendelea Michael akawa kimya, alikuwa amekodoa macho funda la mate alilotaka kumeza ni kama lilikuwa linataka kumshinda, koromeo lilionekana kuwa dogo lakini akajilazimisha likapita.
“Michael nakupenda sana lakini………” hakuweza kuendelea John muhudumu akawa amefika na vinywaji, akawafungulia , Michael akapiga mafunda mawili kulainisha koo lake, John hakupiga funda lolote bali alitia kiasi fulani kwenye glasi yake, wakati muhudumu huyu anaondoka kupisha faragha ya Michael na John, muhudumu wa kiume kutoka jikoni naye akafika kuwasikiliza.
Paja la mbuzi, weka pilipili, tenganisha sahani, ndizi nne zikaushe vizuri, mwambie huyu aongeze bia. Ni baadhi ya maneno mengi waliyozungumza na hatimaye mada ikawa imesahaulika!!! John hakuendelea na maelezo. Simu aliyopigiwa na Bruno ikawa imeingilia kati.
Michael akapata ahueni!!

*******

Joyce Keto alionekana kuwa kikwazo pekee kwa John Mapulu katika mipango yake ya kujipanga upya katika shughuli zake. Alitambua ni kiasi gani wasichana ni dhaifu. Hivyo kuwa mikononi mwake lilikuwa jambo salama sana.
Iwapo Joyce angetiwa mikononi mwa polisi, lazima angesema lolote analojua kuhusu Michael hali ambayo ingemuweka matatani Michael, kijana ambaye ametokea kushibana naye.
Sasa Joyce alikuwa mikononi mwake katika nyumba ya mafichoni nje kidogo ya mji wa Mwanza. Kama ilivyokuwa kwa Michael. Joyce naye alijazwa chuki na kujihisi yupo hatiani. Hasahasa baada ya kuelezwa kuwa Michael anakabiliwa na kesi ya mauaji.
“Kuonekana kwako tu pale kituoni..unatafutwa sasa ukasaidie upelelezi. Maana Michael alitoroka.” John alimwogopesha Joyce. Kisha akamalizia kwa kumueleza juu ya Michael kumkimbia.
“Kwa hiyo mlivyotoroka, amekutoroka na wewe.”
John akakubali kwa kutikisa kichwa juu na chini.
Sumu pandikizi ikapenya katika akili ya Joyce. Akawa mtumwa wa kifikra.,
Uhusiano wa kimapenzi ambao Joyce alimueleza John kati yake na Michael haswa ndio ulimfanya John asipendezwe na kitendo cha wawili hao kukutana mapema. Alihofia kusalitiwa. Hivyo alijionya kuwa muangalifu sana.
Akaamua kumuweka Joyce mbali na Michael hadi wakati stahili utakapowadia.



KILICHOJIRI BAADA YA WATUHUMIWA KUTOROKA

Askari wa zamu usiku wa tukio la mauaji na kutoroka mahabusu wa kituo kikuu cha polisi wapatao kumi kwa kulinda maisha yao waliificha siri ya kutoroka kwa mahabusu wanne katika mazingira tatanishi. Pia mauaji ya askari usiku huo huo. Kwa uzembe huo kama wangethubutu kubaki, kifungo cha maisha ilikuwa halali yao kwani watuhumiwa wote wanne waliofanikiwa kutoroka walikuwa wanahusika na mauaji, John akiwa mkongwe anayefahamika kwa kesi hizo, Michael akiwa amesingiziwa lakini ushahidi ukimuhitaji sana kwa upelelezi na wengine wawili wakiwa na kesi ya kuiba na kuua kwa kutumia bunduki.
Kwa watuhumiwa wa kesi nzito kama hizo ni nani angepona kwa kusema kuwa hajui wanne wametoroka toroka vipi??? Bila kushirikishana lakini kila mmoja akijua lake moyoni, wanne kati yao wakaamua kutoroka wawili wakajiua na wanne waliojisalimisha wakaanza kusota rumande na baadaye gerezani Butimba kwa kesi ya kuwasaidia mahabusu kutoroka pia kuhusika katika kuua askari mmoja. Wema waliodhani ni silaha ukawa umewaponza, upelelezi unaendelea ndio kauli pekee iliyosalia wakati wanazidi kuteketea mahabusu. Mmoja baada ya mwingine wakaanza kupoteza maisha kutokana na mateso makali na msongo wa mawazo huku wengine wakigeuzwa wake za watu angali walikuwa mahabusu.
Akabakia askari mmoja huyo alikuja kutoka kwa msamaha wa raisi miezi miwili baadaye baada ya kesi yake kukosa ushahidi wa kutosha, huyu aliweza kuona na kutembea kama aliyekamilika lakini hakuwa na uwezo tena wa kuzaa, mateso aliyopitia tayari yalikuwa yamemvuruga uzazi lakini kubwa zaidi ni kuingiliwa kimwili mara kadhaa na wafungwa wazoefu wakati yupo gerezani akisubiri hukumu yake. Hakurudishwa kazini baada ya msamaha hakuwa na vigezo tena. Uaskari wake ukawa umeishia katika simulizi mbaya na ya kuumiza kama hiyo. Huyu aliyepona aliyebahatika kurejea uraiani alikuwa ni Sajenti Kindo Malugu, hakuwa sajenti tena alibakia kuwa mzee Malugu.
Siku chache kabla ya kukamatwa kwake alipokea taarifa ya mwanae mpendwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha, ni baada ya kukumbana na unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa baba yake mdogo aliyekuwa amechukua jukumu la kumlea baada ya mzee Kindo kuhamishwa kikazi kutoka Singida na kuhamishiwa Mwanza.
Baada ya mwanae huyo wa pekee wa kike aliyezungukwa na wenzake wawili wa kiume ambao walikuwa wameathirika na matumizi ya madawa ya kulevya ndio kwanza alikuwa amejitahidi na kumaliza kidato cha sita.
Hakuwa tayari kuolewa bali alitaka kundelea na masomo yake ya chuo kikuu. Mateso, kejeli na dharau kubwa kutoka kwa baba yake mdogo pamoja na mkewe zilikuwa zimemsukuma kutoroka katika mji huo na kwenda mahali alipopajua mwenyewe. Baada ya kupata taarifa hiyo mzee Kindo alinuia kuchukua ruhusa na kurejea nyumbani kushughulikia suala hilo, halikuwa suala dogo hata kidogo ile ilikuwa ni damu yake inatangatanga. Lakini akiwa katika kusubiri ruhusa yake ipitishwe ndipo linatokea tukio la mauaji katika nyumba ya kulala wageni jijini Mwanza.
Hakuwa mmoja kati ya askari walioenda kwenye tukio kwani alikuwa anahangaikia ruhusa lakini alikuwa ni yeye aliyeandika maelezo mafupi ya awali kuhusu mali alizonazo mtuhumiwa kwa wakati ule yaani PPR baada ya Michael kukamatwa. Ruhusa ilizidi kumchelewesha hadi linapotokea tatizo jingine kubwa la kuuwawa kwa askari aliyekuwa lindoni na kutoroka kwa watuhumiwa wanne wa kesi za mauaji, hata siku hii pia alichelewa sana kuingia kazini kwani suala la ruhusa yake lilikuwa bado gumu. Siku hiyo alikuwa zamu, hivyo alikuwa anahusika katika kujibu kitakachoulizwa.
Mwanzoni alikubaliana na wenzake kuhusu kutoroka lakini alipompigia mkewe simu na kumuomba ushauri alipinga vikali na kumsihi asijaribu kutoroka kwani alikuwa na mtihani mwingine wa kumtafuta mwanae je angeuweza vipi huu mtihani wakati asingekuwa huru tena??? Maneno hayo makali yaliyosindikizwa na kilio kisha meseji kadhaa za kumsisitiza asifanye alichokusudia zilibadili mawazo ya Sajenti Kindo, yeye pamoja na askari wengine watatu wakajisalimisha, siku hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kwake kuwa huru hadi alipotoka kwa msamaha wa raisi.
“Vua gwanda, vua mkanda, saa na hiyo kofia” haya yalikuwa maneno yaliyowaamrisha siku wanaingia mahabusu, ilikuwa kama utani lakini miaka miwili ikathibitisha si utani ule.
“Mwanangu Joyce, sijui alipatikana???” ni swali la kwanza alilojiuliza mzee huyu, punde tu baada ya kuambiwa yuko huru.
“Poti!! Poti!!....” Kindo alisikia sauti ikimuita wakati akiondoka katika mahakama hiyo ambapo alikuwa amemaliza hatua zote za kuachiwa huru kutokana na msamaha wa Raisi, hakugeuka mara moja kwani aliamini kuwa si yeye aliyekuwa anaitwa. Sauti ile ilipoendelea kusisitiza alisimama na kugeuka. Sura haikuwa ngeni sana machoni mwake lakini hakutaka kuonyesha dalili zozote za kuikumbuka sura hiyo.
“Poti!! Pole sana kaka….nafurahi kukuona mtaani tena dah!! Ya Mungu mengi” mtu huyo mfupi mnene aliyekuwa ananyemelewa na kitambi alizungumza kwa furaha.
“Sijakukumbuka ujue!!!” Kindo alinyanyua mdomo wake na kuzungumza. Bwana yule alifuta tabasamu lake usoni na kuvaa huzuni alimsikitikia Kindo kwani aliamini ni maisha ya kukosa uhuru yalikuwa yamemsababishia hali hiyo ya kukosa kumbukumbu.
“Kura tumekura pakurara je!!!!” badala ya kujibu alitoa kauli hiyo, Sajenti Kindo akashtuka sana kisha akamkumbatia kwa nguvu zake zote mzee huyo, machozi yakawa urembo katika nyuso za wawili hawa.
“Poti Magembe ni wewe kaka???” aliuliza Kindo pasipo kuamini macho yake.
“Ni mimi poti!!! Pole sana kaka, tuliumia sana kukupoteza uraiani” alizungumza kwa huzuni huku akimkagua Kindo kwa macho jinsi alivyozeeka ghafla ndani ya miezi ishirini na nne (24). Walizungumza mengi wakiwa wamesimama wima, Kindo bado alikuwa mkakamavu kiasi licha ya masumbufu ya maisha ya mahabusu bado alikuwa imara. Walikumbushana mengi sana yakiwemo maisha yao ya uaskari tangu wakutane Singida na baadaye Kindo akahamishwa kwenda Mwanza.
“Vipi na wewe ulihamishwa nini??” aliuliza Kindo.
“Ndio hivyo kaka, yaani baada ya wewe kutupwa huko ndani wiki mbili baadaye nikahamishiwa hapa, hivyo niliipata stori yako punde tu baada ya kuhamia hapa. Mazungumzo yalikuwa mengi sana lakini hasahasa kumbukumbu ndio zilitawala.
“Poti hapa nilipo ni kama nashuhudia muujiza nimeachiwa, sina kazi nimefukuzwa tayari, hapa nilikuwa natembea kwenda nisipopajua nashukuru nimekuona, huu mji ninauchukia sana nahitaji sana kurudi nyumbani kwangu huko Singida hapa Mwanza hapana, ngoja nirudi nyumbani…lakini poti!! Mi hapa sina hata nauli, tusizungumzie njaa ninayoisikia hapa hii nitaivumilia…suala ni nauli” alijieleza Kindo kwa sauti ya chini. Magembe akawa amemuelewa.
Kitu cha kwanza walipata chakula ambacho Kindo hakikukifurahia sana, baada ya hapo wakaelekea nyumbani kwa Magembe maeneo ya National housing. Alipumzika kwa siku mbili pale wakati Magembe akihangaika huku na huko hatimaye akapata kiasi cha pesa akampatia Surgent Kindo, akashukuru akaaga na kuondoka.
Siku iliyofuata akaiacha ardhi ya Mwanza.

*****

Maongezi kati ya Michael na John yaliendelea baada ya John kumaliza mazungumzo yake kwenye simu na Bruno mazungumzo yaliyochukua takribani nusu saa huku John akizungumza kwa makini na utulivu asiweze kusikiwa na mtu yeyote. Hali hiyo ilizidi kumtia Michael katika jitimai la nafsi. John aliporejea mezani tayari huduma kutoka jikoni ilikuwa tayari, wakaanza kula na kunywa baada ya hamu kuanza kuwaisha ndipo maongezi yakaendelea.
“Michael naamini una ukaribu flani na Matha!!!” John alisema, lilikuwa shambulizi kubwa sana lililomzidi ujanja Michael akayumba kimawazo lakini hakuanguka, wasiwasi wake ulikuwa wazi sana lakini bahati ilikuwa kwake kwani John alikuwa ameinama akichezea vipande vya mifupa vilivyosalia katika sahani.
“Ndio kwa sasa nipo naye karibu tofauti na mwanzo wakati sijamzoea” alijaribu kujibu mashambulizi Michael.
“Unamchukuliaje kwa jinsi alivyo sasa na kipindi cha nyuma”
Mimba!! Mimba!! Mimba!! Kengere za hatari zililia kichwani mwake.
“Sijaona mabadiliko sana” alijibu huku akiwaza juu ya uwezekano wa swali hilo kuhusisha mimba.
“Michael natamani sana ungejua ni kiasi gani mimi nampenda Matha na nilivyohangaika naye hadi hapa tulipo, ungelijua hilo nadhani ungenionea huruma” aliongea kwa huzuni sana John. Michael akaanza kutetemeka miguu alitamani amtumie ujumbe Matha lakini alihofia huenda tayari simu yake ipo mikononi mwa John hivyo kwa kitendo cha kutuma ujumbe angeongeza maradufu hasira za John.
“Michael Msombe!!!! Nisaidie kitu kimoja tu!! Naamini unakiweza”
“Ni kipi hicho??”
“Unapafahamu kwa Matha??”
Mtego!!!! Alishtuka Michael
“Hapana sipafahamu, sijawahi kwenda” alidanganya Michael kwani aliwahi kukitumia kitanda cha Matha kwa masaa kadhaa kufanya mapenzi na binti huyu mpenzi wa John Mapulu. John alimtazama Michael usoni kwa muda huku akiwa kama anasoma kitu fulani.
“Ok!! Nitakuelekeza….au nitakupeleka…nahitaji msaada wako, wewe ni mwanaume kama mimi” alizungumza John, pombe ilikuwa kidogo imemchangamsha.
“Nimekuelewa kaka” alijibu huku akimeza funda la bia na kukunja sura yake ili kuupokea ukali wake tumboni.
Kimya kikuu kilitawala kwa muda kila mtu alikuwa anawaza na kutenda la kwake hadi walipomaliza na kulipia huduma walizofanyiwa kisha wakaondoka baada ya kuwa wamechukua makopo kadhaa yaliyojazwa bia.
“Endesha!!!!” John alimwomba Michael.
“Sina uzoefu na hizi left hand kaka” alijitetea Michael.
“Ah!! Madereva wa VETA na nyie mna matatizo kweli” alitania John huku akiingia katika kiti cha dereva, safari nyingine ikaanza. Muziki wa hip hop ndio ulitawala ndani ya gari, John aliweza kuimba mistari aliyoifahamu na Michael akijiumauma pale anapoweza hadi gari iliposimama maeneo ya Buzuruga jirani na stendi ya mabasi yaendayo mikoani, ni ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya Nyegezi.
“Unaona lile ghorofa pale, acha hilo linalomeremeta hiyo ni bar, hili la pembeni yake, chumba cha tatu juu, hapo ndipo anakaa Matha, fanya kama surprise sawa” alielekeza John.
“Sasa naenda kufanya nini???” aliuliza Michael. John alijigongesha kichwa chake katika usukani na kusababisha gari ipige honi isiyo na maana, John alikuwa anajishangaa kwani alikuwa hajampa maelekezo yoyote yale Michael.
“Dah!! Mapenzi haya, ok!! Michael kwa maneno yako yote yaliyo kichwani naomba ukamweleze Matha kuwa ninammpenda sana” John alisema kisha akatulia kidogo.
“Najua hakuna rafiki yangu mwingine ambaye ataeleweka kwa Matha lakini wewe naamini atakuelewa, naamini hivyo Michael” John akatulia akamwangalia Michael, macho yake yalikuwa mekundu sana dalili zote za kutaka kulia.
“Ni kitu gani simpi mimi?? Najua amepata kimwanaume kinamzuzua lakini mwambie akumbuke tulipotoka!!!!” alishindwa kuendelea akaanza kulia, Michael akashuka garini akaupunga mkono ishara ya kuaga na kutokomea.

Michael aliamini yupo katika mtego mkubwa kuliko yote maishani mwake, suala la kuagizwa usiku wa saa tano kwenda nyumbani kwa Matha aliamini kuwa ni mpango wa kumtia katika hatia yenye ushahidi wa kutosha ili kuhalalisha hukumu yake. Alitamani sana kumpigia simu Matha lakini bado nafsi yake ilikuwa na mashaka.
“Hapana sipigi simu yoyote ile…nitawapa uhakika mapema sana” alizungumza peke yake. Akiwa na simu yake mkononi badala ya kumpigia Matha alimpigia John, simu yake ikawa inatumika. Akakata baada ya dakika tano John akapiga.
“Vipi mdogo wangu umepotea nini??”
“Umejuaje?? Umesema chumba namba??” alizuga Michael
“Namba tatu upande wa kulia, pembeni yake kuna jiko” alielekeza John baada ya kujilazimisha kucheka kidogo.
“Poa kaka nimeuona mlango, haya baadae” aliaga.
Kwa tahadhari kubwa sana aliufikia mlango, palikuwa kimya sana lakini hilo halikumtisha haikuwa mara ya kwanza kwenda mahali usiku, mara nyingi akiwasindikiza akina John huwa ni usiku. Mlango ulikuwa umerudishiwa kidogo bila shaka muhusika alikuwa hajalala bado. Michael aligonga mlango kwa utaratibu sana. Sauti kutoka usingizini ilimuuliza yeye ni nani hakujibu akausukuma mlango na kuingia ndani.
“Matha!!! U hali gani??”
“Michael!!!!” aliita kwa mshangao mkubwa Matha huku miguu yake tayari ikiwa sakafuni, mikono ikiyapikicha macho yake yaweze kupambana na giza lililokuwa limetanda.
“Upo na nani??”
“Peke yangu kwani vipi???” alihoji Matha kwa sauti ya chini sana huku akiuendea mshumaa na kuuwasha, chumba kikapata mwanga.
“Matha umemfanya nini John”
“Hamna kitu kwani vipi??”
“Una uhakika upo peke yako??”
“Nipo peke yangu jamani sasa haka kachumba na wewe huoni au??” alisema kwa ghadhabu kidogo.
“John ameanza kutushtukia” Michael alisema kisha akaelezea stori yote ya siku hiyo wakiwa na John, Matha alionekana msikivu sana na ambaye huenda angeuliza maswali mengi sana baada ya hiyo simulizi lakini haikuwa hivyo.
“Ujue Michael, huyu John huyu anataka kuchanganyikiwa yule John yule niachie mimi, wewe haumuwezi hata kidogo, yaani yule John….” Matha akiwa anayazungumza hayo alikuwa mbele ya Michael, akiyabinyabinya mabega yake, punde akawa amemkumbatia kabisa, joto kali kutoka kwa Matha, pombe alizokunywa Michael zikaungana kwa pamoja kumshabikia shetani, mapepo yakaruhusiwa kuamka Michael akawa ameagizwa na John kwenda kuzini na Matha, Michael akakisahau kilio cha mwanaume jasiri kama John. Michael akatumia masaa manne kumbembeleza Matha, wakaoga pamoja kwa mara ya kwanza. Walisahau hata mimba iliyokuwa inakua taratibu katika nyumba ya uzazi ya Matha.
“Mwambie John asante sana kwa zawadi eeh!!..mwambie awe anakuagiza kila siku tena usiku ndo inapendeza” Matha alimtania Michael wakati anaondoka. Michael akatikisa kichwa akatabasamu akaondoka. Tayari ilikuwa saa kumi adhuhuri. Kutoka Buzuruga kwenda Mecco ni mbali kiasi lakini Michael aliamua kutembea kwa miguu. Wakati akiwa kwa Matha hofu haikuwepo lakini alipokaribia Mecco, hofu ikamtwaa upya akaanza kumuogopa John, kitendo alichotoka kufanya na Matha kikamtia hatiani tena, hatia ikainyanyasa nafsi yake akaukosa uhuru wa nafsi.
“Hujalala mpaka sasa hivi kaka??” aliuliza Michael baada ya kumkuta John sebuleni akiwa macho anaangalia luninga.
“aaah!! Nilale wakati askari wangu hujarejea bwana!!!” alijibu kwa furaha John .
“Dah!! Nimekuja kwa miguu, si unajua tena daladala hazijaamka bado” alisema kwa utulivu huku naye akichukua nafasi.
“Mh!! Una mambo kaka, nadhani shughuli ilikuwa nzito sana”
“Aah!! Kiasi chake lakini kawaida”
“Si kawaida yaani hadi kufikia suala la kuoga si mchezo ati!!!” alisema John, kauli iliyovunjavunja ujasiri wa Michael, almanusura apige goti kuomba msamaha kwa aliyoyafanya muda mfupi uliopita lakini alisita akabaaki kushangaa.
“Mh!! Aaah!!! Umejuaje kaka” alijipa ujasiri wa bandia na kuuliza.
“Marashi gani ya Matha nisiyoyajua mimi???? Sabuni uliyotumia ni Candy na marashi ni Halloween uongo uongo!!!” alisema kwa utani John ili kumdhihirishia Michael kuwa anamfahamu Matha nje ndani.
“Dah!! Na Matha kanambia hivyo hivyo nikakataa kumuamini mh!! Mnajuana nyie watu si kitoto” alipata uongo wa kujibu Michael.
“Hah!! Matha kakwambia ehee ilikuwaje??” John alikaa vizuri aweze kumsikia Michael vyema.
“Siwawezi nyie…hamuwezi kuibiana kama mnajuana hivyo” alijibu pasipo imani hata kidogo kwani alijua kila kitu tayari John anajua. Michael hakuelewa kuwa kuendelea kusema uwongo ndio yupo sahihi ama auseme ukweli aujue mwisho wa mchezo.
“Nimezungumza na Matha, kwanza amestushwa na imani yako ndogo na amesema kesho niende anipe kitu nikuletee na amesema asante sana kwa Surprise!!!!!” alijilazimisha kufurahi Michael lakini hatia yake iliimeza furaha yote.
“Hata mimi kanitumia meseji!!! Kashtuka sana najua kukuona usiku huu??” aliongezea John. Michael bado hakuelewa kama John alikuwa hajashtukia kinachoendelea ama la!!!
“Vipi kesho muibukie basi au vipi, mi ntakutoa za viroba na nyama choma” kwa sauti iliyojaa ubembelezi John alimsihi Michael.
“Ngoja nikalale maana nimechoka mie, shem kanidekeza hadi nimeoga dah!! Sijui alijuaje kuwa sikuoga wakati natoka” Michael alisema, John akamuunga mkono kwa kicheko kikali cha furaha. Siku ikaisha hivyo tena walakini ukiwa bado umetawala.

Michael aliingia chumbani kwake, hakuamini kama siku hiyo inakatika bila John Mapulu kuusema ukweli wote juu ya uovu aliougundua dhidi yake. Usingizi ulimchukua mapema sana kutokana na uchovu na ulevi wa siku hiyo. Alijilazimisha kuwa na amani ilhali moyoni haikuwepo hata chembe. Michael aliamini kuwa alikuwa mtegoni.
“Mh!! Sijui kama patakucha salama!!” ni wazo la mwisho kichwani mwa Michael kabla hajapitiwa na usingizi mzito.
Majira ya saa nne asubuhi ndipo alishtuka kutoka usingizini lakini alitumia nusu saa nyingine kuuruhusu mwili wake ubanduke kitandani. Njaa ilikuwa inamuuma lakini hakuwa na hamu na kitu kingine zaidi ya supu. Hang over zilikuwa zimemtawala!!
“Oyo!! Huoni au mbwembwe tu!!!” sauti ya John ilimsimamisha Michael aliyekuwa anataka kutoka nje huku akipiga mluzi bila hata kutoa salamu. Michael alisimama na kumwangalia John kwa hofu.
“Ah! Sijakuona wala nini, nawaza tumbo tu hapa nataka nikarekebishe kiaina si unajua tena!!!” alijibu Michael huku akijiegemeza kwenye mlango ambao ulikuwa nusu wazi nusu umefungwa.
“Nilikuchukulia supu na chapati nenda ukacheki jikoni!!” John alimwambia Michael kwa sauti ya upole sana. Kengele za hatari zikalia kichwani mwa Michael. Sumu!!! Aliwaza mara moja kabla ya kushukuru na kujongea jikoni kwa ajili ya hicho alichohifadhiwa.
“Ukimaliza kula uniambie kuna jambo nahitaji tuzungumze!!” John alimwambia Michael ambaye aliupokea ujumbe huu akiwa anakaribia kulifikia jiko. Uoga ulikuwa umeitwaa nafsi yake, kila jambo alilofanyiwa na John alitia walakini ndani yake Hatia iliyokuwa inamkabili ndiyo ilimhangaisha. Kwa mwendo wa kunyata kama mwizi wa njiwa Michael alichukua kipande kidogo cha nyama iliyokuwa katika supu na kurushia paka aliyekuwa akifugwa hapo kwao. Paka alikitafuna kipande kile kwa shangwe zote hata kabla hakijatua chini vizuri kisha akajilambalamba ulimi na kutoa mlio wa nyauuu!!! Huku jicho lake likimtazama Michael kwa matamanio ya kupewa tena kipande cha nyama. Michael alisubiri kwa dakika kadhaa na yule paka naye akisubiri kuongezwa kipande kingine. Paka hakukumbwa na mushkeli yoyote ile. Chakula kilikuwa salama!! Michael alikuwa katika maisha ya mashaka sana!!
“Ah!! Kama ameniwekea sumu juu kwa juu bwana maisha gani haya ya wasiwasi? Bora nife!” alijisemea kwa sauti ya chini Michael huku akiivamia supu ile ambayo ilikuwa ya moto bado, hakujiandalia chakula mezani alimaliza kila kitu pale pale jikoni.
“Asante sana braza maana mh!!!” Michael akiwa na glasi ya maji ya kunywa baridi kabisa alimshukuru John.
“Hapo sasa safiiiiiii!!!!” alizungumza John kwa furaha.
“Ah!! Hapa hata nisipouona mchana poa tu” Michael alijibu huku akichukua nafasi yake katika sofa iliyokuwa ikiangaliana na sofa aliyokalia John.
“Michael nina zawadi yako nahitaji nikupe leo nadhani utafurahia”
“Zawadi kwa lipi kaka nililofanya”
“Jana umetumia muda wako mwingi sana kuzungumza na Matha nimeyaona mabadiliko leo mabadiliko makubwa nilikuwa na Matha asubuhi ya leo hapa!!” John alizungumza huku tabasamu likichanua katika mdomo wake.
“Aaah!! Amakweli leo nimelala sana”
“Kwa suala hilo nahitaji kukupongeza!!!”
“Usijali wewe ni kaka yangu” Michael alisema huku hasira zikiwa zimemtawala ndani ya nafsi yake pepo wa wivu akaanza kumtafuna taratibu, akaanza kuhisi Matha ni mali yake peke yake.
“Hata kama lakini unastahili zawadi” alisisitiza John. Michael hakupinga zaidi ya kukubali kwa shingo upande hiyo zawadi.
“Matha amekuja??? Muda gani na saa ngapi ameondoka?? Au mtego huu?? Eeh!! Mungu nisaidie” baada ya muda mrefu sana kupita Michael alikumbuka kupiga dua.
Au wananichora hawa kasha wanitoe kafara! Alijiuliza.
****

***MICHAEL anazidi kujikita katika penzi la MATHA.
***JOHN hajaushtukia mchezo...anamuamini sana Michael.....
***NINI KITATOKEA SIKU AMBAYO JOHN ATAGUNDUA KUWA MICHAEL ANAMZUNGUKA.
KUMBUKA JOHN NI MTU KATILI NA ANAUA ANAVYOTAKA.

ITAENDELEA

CHOZI LA FUKARA

  

 
                   NA  DEARNA MAROTA
2
ILIPOISHIA>>>>>>>>

 Ilikuwa ni jumapili jioni ambapo jordani siku hiyo hakufanya kazi yoyote kwani ilikuwa siku ya kumcha bwana hivyo aliiheshimu. Baada ya kutoka katika ibada ya jioni alikuwa ameketi tu barabarani ambapo kulikuwa na kijiwe chake alichopumzikia pindi atokapo kwenye miangaiko ya hapa na pale, ndipo alikiwa kwenye dibwi la mawazo jinsi ya kukabiliana na hali ngumu ya maisha alishtushwa na sauti nyororo ya mrembo kwa nyuma yake “za jumapili kaka”


SASA ENDELEA

“aha salama tu Karibu dada yangu” aliitikia na kumkaribisha kisha aliketi “mbona una mawazo sana kaka yangu” dada huyo alihoji “aha ni maisha tu dada sijui unaitwa nani?” alijibu kisha alimuuliza swali “naitwa Mercy na wewe je waitwaje? Mrembo alihoji “naitwa Jordan ukiniita fukara haukosei” “ahaa usiseme hivyo Jordan kwanini unajiita fukara na umejaaliwa nguvu na uwezo wa kuifanya kazi  so usijali ipo siku mungu atakupa uwezo” Mercy alimfariji nao walibadilishana mawazo ya hapa na pale kwa na hapo ndipo ukawa mwanzo wa mahusiano yao na mwanadada huyo. Kwa uzuri Mercy alijaaliwa na mwenyezi kitu ambacho Jordan aliwaza moyoni kuwa ataweza kumtunza. Siku zilizidi kwenda na Mercy alishapajua nyumbani kwa jordani ambapo alikuwa amepangisha na mara kwa mara alilala hapo na Jordan. Kadri siku zilivyozidi kwenda ndipo mapenzi ya wawili hao yalishamiri na walipendana kupita maelezo. Lakini kwa upande wa Jordan hakuacha kumkumbuka mama yake kwani ndiye alimpenda kuliko kitu chochote. Waliishi hivyo hivyo kwa kubangaiza kwa chakula, na matumizi madogo madogo na siku nyingine walikosa na waliishia kunywa maji.

Jordan:  mpenzi wangu maisha yangu ni ya shida sana tuvumilie naamini ipo siku mungu atatujalia moyo wangu umekuchangua wewe angalia usije kunisaliti, ukaniacha nikateseka katika nafsi yangu kwani ni wewe tu uliyemoyoni mwangu, vumilia mpenzi kwa leo tulale hivihivi ila kesho nitajitahidi tupate kitu japo cha kutafuna.
Mercy:  usijali mpenzi wangu hatakama nisipokula nikiwa na wewe najihisi nimeshiba ala tu nahitaji upendo wako kutoka moyoni mwako  nami naamini Mungu ndiye aliyekuchagua uwe mume wangu wa ndoa na endapo utanisaliti sitaona umuhimu wa kuishi katika dunia hii ya sasa kwani bila wewe najihisi bado sijakamilika hivyo promise me kama hutaniacha na niwe wako wa milele mpaka pale kifo kitakapo tutenganisha
Jordan: I promise mpenzi wangu nitakupenda milele daima katika maisha yangu
Mercy: I promise
       Maisha yao yalizidi kusonga mbele na upendo wao ulizidi kipimo kwani walipendana kupita maelezo siku walipokosa nao walilala na njaa na siku waliyo pata nao walimshukuru Mungu kwa alicho wapatia. Jordan aliangaika mno ili kujikimu na ugumu huo wa maisha na kwa kipindi hivyo fedha ilimsaliti kabisa hadi alikosa kodi ya nyumba na walijikuta wakifukuza wasijue pa kwenda
Jordan: mpenzi wangu angalia hali tuliyo nayo tutakwenda wapi sasa” Jordan aliongea kwa unyonge akiwa amemkumbatia mpenzi wake wakiwa nje na mizigo ilikuwa imewazunguka wakishauriana wataelekea wapi. Walishauriana na wakaamua kwenda mjini kutafuta maisha yao nako walifikia kwa rafiki yake Mercy aitwaye Maria
  Walikaa hapo kwa wiki moja huku Jordan akijitafutia vibarua vya hapa na pale na baada ya wiki moja tayari alikuwa ameshapata fedha kidigo hivyo walipangisha chumba chao kama ilivyokuwa awali.
          Waliendelea kuishi kwa upendo usio na kifani na kila aliye waona mjini hapo aliwaonea vivu. Kwa kipindi chote hiki jordani hakuwahi kumtambulisha Mercy kwa mama yake wala ndugu yeyote kwani bado alikuwa hajajipanga na wakati anaondoka alimuaga mama yake kuwa hatamtupa bali kumkumbuka daima na angerudi kila mara kuangalia hali yake kwani kaka yake (Kelvin) alikuwa bize na miangaiko yake hivyo alimkumbuka kwa nadra sana. Waliishi kwa muda mrefu na hali yao kimaisha ilikuwa palepale. Wakati Jordan alienda kwenye miangaiko yake na Mercy alibaki nyumbani kwa usafi wa mazingira na shughuli ndogondogo za nyumbani hapo lakini siku ya jumamosi aliamua kwenda kwa rafiki yake Maria kumtembelea. Maria alikuwa na uwezo kiasi fulani “aha Karibu shostito wangu” maria alimkaribisha “asante yaani nimekumisi shost” “aha wewe si utaki kuja kunitembelea na unakaa hapahapa mjini, utadhani tumegombana” maria aliongea na kisha kwenda kumchukulia juice ya matunda “ehe nipe mastory” maria aliongea kisha kuketi kwenye kochi “nina story gani bwana zaidi ya kuja kukusalimia na unipe ela ya mboga maana leo hata sijui nita kula nini” aliongea Mercy
“Mhh!! Ahaa, hivi Mercy rafiki yangu mbona hujielewi elewi” Maria aliongea kwa kejeli “kwanini” mercy alihoji

Je Rafiki yake Mercy anamshangaa nini Mecry?? fuatiolia .............

Saturday, October 27, 2012

CHAGUA MOJA YA LOVE SMS HIZI UMTUMIE MPENZI WAKO LEO

If people came with labels, yours would say:
100j PURE,
25% loving,
25% caring,
25% smart,
25% loyal,
COLOUR: cheerful,
SIZE: huggable,
TYPE: one of a kind!!!

My love 4u is unconditional
My love 4u is real
My love 4u is something
so incredible to feel
Holding u on those summer nights
Feeling ur soft kiss with the sun
My love for u is something
that never once had to be won
I love u with the passing days
and with those we have not seen
ur the one in all my thoughts
in all my living dreams
ur the one whose hand is in mine
Whose lips I can't ignore
u are my life, my world, my love
ur all that I adore.


I awake each day with a smile
& greet it with a laugh;
The world is a treasure to me
Because of u.
Every time I think of something sad,
I replace the thought- with u!
My mind is instantly changed
& my heart is filled with gladness.
Every breath I take is meant for u,
I live this life surrounded in joy
& I bathe in the promise of ur love,
My soul belongs to u.
Each time I see something beautiful
I want to take it and bring it to u;
My life has so much meaning now
All because of u.

Even through tears,
The sun shines through.
Without your warmth,
What would I do?

it 4 u, dont drop it on d ground, cos u may not find it again,dont kip it on d air, cos it may fly away. give it a place in ur heart. i mean ma luv.


Do u knw d relation btwn 2 eyes? De blink 2gther, de mov 2gether, de cry 2gether, de c things 2gether n de sleep 2gether BT STIL DE NVR C EACH OTHER . Its TRU RELATION.
life

if each leaf of a tree is ur smile. then i promise u i will water it through out my life so i can seeur ever green smile forever!

Sending u 1000 smiles.take one 4 now and remaining 999 under u,r pillow.pick out 1 every time u think of me because i want 2 see u smiling always

its not the presence of someone that brings meaning to life but its the way someone touches your heart that gives life a beautiful meaning


Let me start by saying that I thank to Allah every night since I found you. You came into my life when everything seemed so dark but you provided the light to find my way. I've never been so certain of anything in my life like I am of us. You have totally changed my outlook in life and I thank you for that. I feel as if I'm walking over clouds just thinking about you. You make my life complete. I know you've said we could do foolish things


You're eyes are soft en tender,as sweet as they can be.There's one thing you must remember, you are the one for me!!!




It's hard to find someone whom you truly love, much less to find someone who loves you as much. When the chance comes, don't ever let go.

You showed me how it is to be loved. Now I know what really love is. 1 day we will be together forever. I can't wait to hold you in my arms again.

LoVe iS LiKe QuiCkSanD - ThE DeEpEr yOu FaLL iN iT ThE HaRdeR iT iS tO GeT OuT

Trying to forget someone you loved is like trying to remember someone you never knew.


Love is like a cloud... love is like a dream... love is 1 word and everything in between... love is a fairytale come true... Coz I found love when I found U.

"24 Sweet hours make 1 Sweet day"!
"7 Sweet days make 1 Sweet week"!
"4 Sweet week make 1 Sweet month"!
but... " 1 sweet person like "U" makes entire life sweet!

As days go by, my feelings get stronger,
To be in ur arms, I can't wait any longer.
Look into my eyes & u'll see that it's true,
Day & night my thoughts r of U

5 Lovable
words- "I
am alone
without u",
4 pleasant
words- "I
care 4 u",
3 sweet
words- "i
like u",
2 special
words
"Miss U",
1 important
word- "U"



Liking u is my nature, missing u mydisapointment,fightin wit u my fast-time but 4geting u is never on mymind ..ur un4getabl


She's da one who broke my heart...
She's da reason why my world fell apart....
She's da one who makes me cry.....
Yet I still luv her....n I don't no why...

sea full of water, sky full of
star's tree full of leaf's
garden full of flower's
But i think my heart
full of you 

Messages are not for time pass
They silently say that I'm thinking of "U" right now
& also making "U" & think of ME 4 a moment 

Gateway of memories will never close. How much i miss u no one knows. Days will in years & i will remember u in my silent tears

I want to share everything with you, your sadness, your happy moments, every single second of the day.
Do your feet never hurt ???? ... You are wondering around my thoughts all day long....

Sometimes
my HEART asks:
Why I miss you?
Why I like you?
Why I SMS you?
Then my mind answered,
Its bcoz..
"sweet" people NEED more CARE

DO U want 2 know how much I Love U,ASK the Butterflies flying in at the river bank, un4tunatly they can't talk 2 U but their Beautiful colors will tell U thousand words. I MISS U

HATIA---08



“Matha Mwakipesile ndo wewe eeh!!!.”
“Ndio ni mimi dokta vipi malaria nini??.” alifanya utabiri usiokuwa sahihi.
“Hapana hauna Malaria mwanangu..”
“Mh!! Nini sasa hichi Mungu wangu.”
“U mjamzito Matha!!!....mwezi mmoja.”
“Dokta!!! Be serious!!!”
“Ninamaanisha, vipi kwani hukutegemea au??.”
“Yaani siamini maana ni wakati muafaka hii zawadi imekuja.” alijibu kwa uchangamfu Matha. Akaaga akaondoka!!!
Alimanusra apate ajali njiani kwa papara alizokuwa nazo katika kuendesha gari kwa mwendo kasi ili awahi mahali. Hakuwa akienda kwa John lakini alikuwa akielekea kwa Michael aliamini kwa namna kubwa sana yeye ndiye muhusika wa hiyo mimba maana hawakuwahi kutumia kinga hata siku moja. Sijui walikuwa wakijiamini vipi!!!!
Matha alikuwa na furaha tele kwani ni mwaka wa nne tangu awe na uhusiano na John Mapulu bila dalili zozote za kupata mtoto. Tangu amtoe usichana wake walipokutana katika msiba wa mama yake mzazi na Matha, uhusiano uliokomaa na kudumu kwa miaka hiyo tele, miaka iliyomhamisha Matha kutoka shuleni na kuingia rasmi katika ujambazi. Akiwa kama kipenzi cha John hakumjua mwanaume mwingine hadi anapoingia kati Michael Msombe.
“Kumbe John hazai!!!” alisema kwa sauti ya chini kama vile kuna mtu pembeni yake alikuwa anamsikiliza.
“Mbona sasa amekuwa mbinafsi kiasi hicho??? Kwa nini hakunambia kuwa ana matatizo, nimejihisi mpweke na kumlaani mama yangu kwa kunizaa mgumba!!! Namchukia John. Kama alinipenda kwa nini ameificha siri hii??” alilalama Matha bila kupata msaada wowote. Breki za gari yake zikafanya kazi yake alipolikaribia geti kisha injini ikazimwa baada ya gari kuwa limeingia maeneo ya Mecco ndani ya nyumba ya John aliyoishi na Bruno!!! John hakuwepo!!! Lakini Michael alikuwepo.
“Michael!!!!.”
“Nambie mpenzi wangu.” Kwa mara ya kwanza Michael akamwita Matha jina hilo kwa kujiamini. Matha akambusu shingoni kimahaba, wakati huo walikuwa katika chumba chao cha mafunzo ya kutumia bunduki.
“Michael asante sana!!!!.”
“Asante kwa lipi huishiwi visa wewe mke wa bosi!!”
“Ah!! Sitaki mie hilo jina utaniudhi sasa hivi!!!” alilalamika kwa sauti ya chini Matha.
“Basi samahani kipetito” Michael alimwambia Matha huku akichukua kichwa chake na kukilaza mapajani mwa Matha.
“Michael nina ujauzito.” kama vile aliyepigwa shoti alijikuta akiruka kutoka mapajani mwa Matha na kusimama mlangoni kama anayetaka kukimbia. Matha akaubetua mdomo wake.
“Matha unasemaaje??.”
“Kwani ulikuwa unatumia kinga wakati tunafanya??.” Swali la Matha likamfadhaisha Michael akawa kama anayetaka kulia lakini chozi lilikuwa mbali sana, sura yake ikawa kama amepigwa ngumi.
“Michael nimekwambia nina mimba yako!!!”
“Sasa Matha hapo mimi nafanyaje unadhani??” alizungumza kwa upole Michael.
“Nakusikiliza wewe!!!.”
“Una uhakika kuwa ni ya kwangu???.”
“Asilimia zote!!!! John hana uwezo wa kuzalisha” alijibu Matha kwa ujasiri
“Fikiria kwa makini halafu utaniambia tunafanya nini???” alisema Matha kisha akambusu Michael katika papi za mdomo na kumwacha solemba. Mara akarejea na kumkuta Michael akiwa bado amesimama
“Katika mawazo yako yote sahau kuhusu kufanya arbotion, I won’t!!!”

*****
Suala la Matha kumkumbusha Michael kuwa sahau kuhusu kitu kinaitwa utoaji mimba lilimchanganya zaidi Michael. Kila alipofikiria kuhusu tatizo la John la kutokuwa na uwezo wa kuzaa Michael alizidi kuchanganyikiwa kwani aliamini kuwa endapo John ataigundua mimba aliyonayo mpenzi wake (Matha) basi mshukiwa wa kwanza kabisa ni yeye (Michael) hilo halikuwa na kipingamizi chochote.
“Na ikiwa hivyo basi nimekwisha mie!!!” Michael alisema kwa sauti ya chini huku kijasho kikipenya katika vinyweleo vya mwili wake kutokea kichwani na kuweka michirizi katika mashavu yake.
Michael hakutafakari na kupata jawabu lolote la maana akaingia chumbani kwake akajiegesha kitandani. Akapitiwa na usingizi!!!
Majira ya saa mbili usiku ndipo alishtuka, mang’amung’amu ya usingizi yalikuwa yakimyumbisha alikuwa akiyapikicha macho yake ili aweze kuona mbele vizuri wakati huo alikuwa anauendea mlango wa chumba chake aweze kuufungua na kutoka nje kiu kilikuwa kimemshika. Alipoufungua mlango ni kama alikuwa amemfungulia mtu ambaye bado alikuwa hajaomba kufunguliwa, Michael alikurupuka kama aliyekuwa amekabwa na jinamizi kisha ghafla akawa ameachiwa. Alikuwa ni John!!
“Vipi dogo….” John aliuliza
“Ahh!! Ni usingizi tu kaka vipi…aah!! Nilikuwa nimelala si unajua” alijibu pasipo kujiamini kijana huyu.
“Jiandae tutoke!!!..nakupa kama dakika kumi na tano fanya fasta” John alimuamuru Michael. Wasiwasi ukamuandama Michael, hakujua huo mtoko ulikuwa wa kwenda wapi. John hakuwa katika mavazi ya kikazi, bali alikuwa ameitundika suti yake nyeusi iliyombana kiasi na kuonyesha kifua chake kilivyoachana katikati, kwa ndani alikuwa na shati jeupe, kiatu cheusi chini kilihitimisha kumfananisha John na bwana harusi na wala si jambazi mzoefu. Hivi tutakuwa tunaenda wapi?? Alijiuliza Michael.
Hakuwa na wa kumpa jibu akaghairi kuliendea jokofu ili apate maji akapiga hatua kadhaa bafuni ili aweze kuoga, hata hivyo ubaridi wa maji ulimsababisha ajijengee hoja kwamba alikuwa msafi na kuhalalisha maamuzi ya kuacha kuoga. Badala yake akanawa uso kujitoa ile ladha ya usingizi usoni mwake, kisha akaliendea sanduku lake lililozuia zipu isijifunge kutokana na wingi wa nguo akatwaa jinsi ya bluu na fulana nyeupe akazitua katika mwili wake baada ya kuwa ametanguliza singlendi nyeupe kwa ndani, kisha akamalizia na raba iliyotawaliwa na weusi kiasi kikubwa na weupe ukichukua nafasi ndogo. Miwani aliyoivaa ilikuwa imempendeza sana kwani ilirandana na kiatu lakini usiku haukuwa wakati muafaka wa kuvaa miwani hiyo, baada ya kugundua hilo aliivua na kuirejesha mahali pake. Marashi!! Alikumbuka wakati anataka kutoka, haraka haraka alirejea na kupulizia kwa chati, aliporidhika akatoka na kuelekea sebuleni.
Hakuwa na haja ya kujitazama kwenye kioo, alikuwa amependeza!!
“Umejiandaa fasta sikutegemea maana nimekushtua sana!!!”
“Nimekacha kuoga!!! Ndo maana nimewahi” alijibu Michael huku akikaa katika ncha ya sofa.
“Twende zetu, huyu Bruno sijui atakuwa wapi muda huu??”
“Hata sijui maana tangu nimelala dah!! Wewe wakati unakuja pale ndo na mimi nilikua naamka, masaa kama manne hivi nilikuwa mfu”
“Shwari…tutampigia simu.” alijibu John huku akitangulia na Michael aliyetawaliwa na walakini akimfuata kwa nyuma hadi kwenye gari. Michael hakuingia kwanza alifungua geti gari ikatoka kisha akafunga ndipo akalifuata gari na kupanda.
“Aaah!! Tafadhali bwana mdogo yaani mi nimekuwa dereva wako!!!” alizungumza John kimasikhara baada ya Michael kukaa siti ya nyuma, haikuwa mara ya kwanza Michael kumsikia John akisema hivyo, mara moja akahamia siti ya mbele. Kabla hajakaa John aliondosha pakiti ya sigara iliyokuwa imebakiwa na sigara tatu ndani yake, hiyo ilimaanisha kuwa sigara takribani kumi na saba zilikuwa zimezama na kutoka katika mapafu ya John. Alipenda sana sigara bwana John!! Michael bila kuomba alitwaa naye sigara moja akaiwasha na kuanza kupuliza moshi ndani na nje. Na yeye tayari alikuwa ameathirika japo sio sana na utumwa huu wa sigara.
John alikuwa makini na usukani, kutokea pale Mecco alipinda kushoto kuifuata hoteli na bar ya Cheers kisha akakata kulia akiipita stendi ya Mecco na kuifuata barabara iendayo Nyakato sokoni, hapakuwa na masumbufu ya foleni za hapa na pale hivyo waliwahi sana kufika, baada ya kufika Nyakato sokoni gari ilikata kushoto baada ya kuwa imeingia barabara kuu ya Mwanza maarufu kama Nyerere road, gari liliondoka kwa mwendo mkali lakini salama kuelekea Igoma, NDAMA HOTELS ndipo kilikuwa kituo cha mwisho ambacho John alisimamisha gari lao dogo aina ya corolla. Wakati huo Michael alikuwa anamalizia kipisi kidogo cha sigara ya mwisho wakati wanashuka garini. John hakuwa katika hali ya uchangamfu hali hii ilizidi kumtia mashaka Michael.
“Vipi ina maana amegundua kinachoendelea ama kuna jambo gani linaendelea hapa??” alijiuliza Michael wakati huo John alikuwa akiangaza ni wapi wanaweza kukaa kwa utulivu. Walipata mahali palipokuwa na utulivu walioutaka wakaketi.
“Karibuni!! Karibuni sana” sauti ya muhudumu wa kike aliyetawaliwa na tabasamu bandia usoni maalum kwa ajili ya kazi aliwalaki wawili hawa.
“Asante sana…tutakuita tukikuhitaji!!!” alijibu John bila kumuangalia binti huyu usoni. Binti hakujibu kitu bali tabasamu lake liliyeyuka ghafla akaanza kuondoka.
“Hey!!....Mimi niletee Kilimanjaro, iwe ya moto tafadhali” aliamuru Michael
“Naomba 1800….” Alijibu yule dada ambaye sasa lile tabasamu lililopotea ghafla baada ya kuambiwa ataitwa baadaye sasa lilikuwa limerejea maradufu. Michael hakujibu akamtazama John aliyekuwa ameinama, muhudumu akailewa maana hiyo akamsogelea John bila shaka ni yeye alikuwa na jukumu la kulipia bili.
“Na mimi niletee Castle lite baridi, leta mbili kabisa.” John aliagiza huku akitoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi yule binti, akaondoka kwa furaha!! Bila shaka walipokea posho kutokana na idadi ya wateja walioweza kuwahudumia kwa siku.
“Michael unamuonaje huyu binti!!!.”
“Kivipi yaani.”
“Muonekano wake tu!! Ni mrembo eeh!!.”
“Kiasi chake, namaanisha yupo katikati!!” alijibu Michael huku akimtazama John na kulazimisha tabasamu ambalo halikujibiwa na John.
“Wasichana wana mambo sana…..” kauli hiyo ikamgutua Michael kimawazo.
“Kwanini wasema hivyo….” Aliuliza huku akijiweka sawa kwenye kiti chake, viwiko vya mikono yake vikiegemea mezani
“Unajua unaweza kumpenda sana mtu halafu asitambue upendo wako, akatumia upendo huo kukuadhibu……lakini bado unaendelea kumpenda” alianza kujieleza John
“Yeah!! Hiyo inawezekana lakini sijaelewa maana ya kauli yako ” aliuliza kwa hofu Michael wakati huu alitoa mikono yake mezani na kuifunga kifuani kwake
“Michael si unajua kuwa wewe ni rafiki yangu sana?”
“Naelewa hilo na ni kaka yangu pia kwani kuna nini??” Michael aliuliza huku akijutia kuuliza vile kwani hakutaka kusikia jibu litakalotoka, hatia iliusaga moyo wake, aliamini kwa maongezi hayo John kuna kitu alikuwa kama hajakigundua basi alikuwa amekihisi kati ya yeye (Michael) na Matha. Mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi, fulana yake iliyombana ilimwezesha mtu ambaye hata kama si mchunguzi wa masuala ya afya kuligundua hili.
“Shiit!!! Nimeacha mguu wangu ndani ya gari!!!” John alijisonya baada ya kugundua amesahau bunduki yake garini, haukuwa utaratibu wake kutembea bila silaha. Lakini hakujisumbua kusimama na kuifuata. Kauli hiyo ilizidi kumtetemesha Michael.
Ina maana ndio amekuja kunifichulia maovu yangu na kuniua hapahapa!!!! Mungu wangu, lakini nilimwambia Matha kila siku kuwa ananitia matatani ona sasa!!! Aah!! Ona sasa Matha!! Aliwaza Michael kwa uchungu na kuzitupa lawama kwa Matha kabla John hajaendelea kuzungumza
“Eeeh!! Umeuliza kuwa nina maana gani, ujue Michael kuna wakati unafika lazima kila ukweli uwe wazi na uamuzi ufanyike mara moja, na uamuzi mgumu ni ule unaomuumiza aliyeuamua!!!” John aliendelea Michael akawa kimya, alikuwa amekodoa macho funda la mate alilotaka kumeza ni kama lilikuwa linataka kumshinda, koromeo lilionekana kuwa dogo lakini akajilazimisha likapita.
“Michael nakupenda sana lakini………” hakuweza kuendelea John muhudumu akawa amefika na vinywaji, akawafungulia , Michael akapiga mafunda mawili kulainisha koo lake, John hakupiga funda lolote bali alitia kiasi fulani kwenye glasi yake, wakati muhudumu huyu anaondoka kupisha faragha ya Michael na John, muhudumu wa kiume kutoka jikoni naye akafika kuwasikiliza.
Paja la mbuzi, weka pilipili, tenganisha sahani, ndizi nne zikaushe vizuri, mwambie huyu aongeze bia. Ni baadhi ya maneno mengi waliyozungumza na hatimaye mada ikawa imesahaulika!!! John hakuendelea na maelezo. Simu aliyopigiwa na Bruno ikawa imeingilia kati.

*******

Je!! Siri imefichuka???
Nini hatma ya Michael na Matha.

ITAENDELEA

Friday, October 26, 2012

CHOZI LA FUKARA

NA  DEARNA MAROTA

Mungu mwenyezi ni mkuu aliyeweza kuwaumba binadamu kwa mfano wake lakini kwa wepesi na ugumu wa nafsi tofauti tofauti. Mwanadamu huweza kutoa chozi lake kwa hisia tofauti: - machozi ya furaha na machozi ya uchungu. Chozi litokalo kwa uchungu wa jambo fulani huwa ni pigo lililo na pengo ndani ya moyo wa mwanadamu, CHOZI LA FUKARA ni story ambayo inaelezea jinsi masikini anavyo nyanyaswa na penzi kutokana na UFUKARA wake, na kujihisi hana nafasi ya kueleza hisia zake kwa mtu ampendaye kutokana na umasikini wake.
   “mwanzo wa mapenzi huwa matamu zaidi ya asali na mwisho wa kulishamirisha huwa kama shubiri iliyotiwa pilipili kichaa iliyo mbichi haswaaaa, kwa fukara kama mimi kwani penzi limeweza kunitoa chozi na pia kuninyanyasa katika nafsi yangu pia nikatambua fukara hana sauti” maneno haya yalitoka kinywani mwa Jordan ambaye ni kijana apatae miaka 30 kwa sasa na anafamilia hivyo ameamua kuelezea mikasa ya maisha yake na misukosuko ya mapenzi aliyopitia pindi alipokuwa masikini lakini mungu alikuwa pamoja nae mpaka kufikia hapo alipo sasa ndipo anaelezea kwa uchungu huku akivuta hisia na kumbukumbu ya mapito yake
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@------------------------- na mtunzi wako -----------------------------------
***************** ############################### %%%%%%%%%%%%%
 “Subira huvuta heri na Baraka kwa kila asubirie kwa heri kwani mungu hamtupi mja wake hata siku moja bali ukimtendea mwanadamu ubaya na mungu hukurudishia, malipo ni hapa duniani”
    Jordani ni kijana wa pili katika familia ya kimasikini aliyeishi na mzazi wake katika kijiji cha Bariadi mkoani mwanza. Kutokana na ugumu wa maisha ulipelekea Jordan na kaka yake aitwaye Kelvin kutokupata elimu ya mwangaza wa maisha yao ya baadaye kwani katika familia yao mlo wa siku tu waliupata kwa manati. Baba yao aliwatelekeza tangu wakiwa wadogo hivyo mama ndiye alikuwa na jukumu la kifamilia hiyo kwa muda huu Jordan alikuwa ni mwenye umri wa miaka 18 na Kelvin alikuwa na miaka 20. walifanya vibarua vya hapa na pale ili kupata fedha kwa ajili ya matumizi madogo madogo kama chakula, nguo za kubadili na vitu vinginevyo ili kumsaidia mama yao pia  ambaye alikuwa amedhoofika kiafya kutokana na mawazo aliyokuwa nayo kwa kipindi chote na misukosuko aliyopitia pindi alipokuwa akitafuta riziki kwa ajili ya watoto wake “kweli mama ni mama na hakuna mwingine kama mama” Jordan aliongea kisha aliendelea. Miaka ilizidi kusogea ndipo jordani alikuwa ni mwenye miaka 20 na alikuwa akifanya kazi ya kubeba taka na kupeleka katika dampo kuu la jijini mwaza pia alipokuwa na nafasi alichukua vibarua vya kuosha magari pindi alipoitajika na kazi hiyo ilimfanya apate vijisent kwa chakula chake mwenyewe na kidogo alimpelekea mama yake. Kwa kipindi hichi Jordan tayari alikuwa amepangisha chumba na alianza kujitegemea lakini kila siku alimwendea mama yake ili kumjulia hali. Mama yake aliwapenda sana tangu wakiwa wadogo lakini alizidisha upendo kwa Jordan kwani ndiye aliyemjali kuliko Kelvin lakini wote walimpenda mama yao sana kuliko kitu kingine.
Kwa upande wa Kelvin alipata marafiki ambao walikuwa wakifanya biashara za hapa na pale ili kujikomboa kimaisha.
       Ilikuwa ni jumapili jioni ambapo jordani siku hiyo hakufanya kazi yoyote kwani ilikuwa siku ya kumcha bwana hivyo aliiheshimu. Baada ya kutoka katika ibada ya jioni alikuwa ameketi tu barabarani ambapo kulikuwa na kijiwe chake alichopumzikia pindi atokapo kwenye miangaiko ya hapa na pale, ndipo alikiwa kwenye dibwi la mawazo jinsi ya kukabiliana na hali ngumu ya maisha alishtushwa na sauti nyororo ya mrembo kwa nyuma yake “za jumapili kaka” 
 
JE MREMBO HUYU NI NANI?? NA ANATAKA NINI??? ungana na mtunzi wako jumapili hii

Recent Posts